Kiingereza cha Orest Kawau wa Magic FM

kabingo

Senior Member
Oct 16, 2015
115
118
Huyu jamaa kweli ni mwendeshaji mzuri wa kipindi cha Morning Magic akiwa na wenzake akina Kibwana Dachi Mkambala, na Mary Edward.

Tatizo lake ni kuongea maneno ya Kingereza kila baada ya sentensi mbili za Kiswahili. Hivi mbona wenzetu Wazungu wakiwa kwenye vipindi huwa hatusikii sentensi za lugha nyingine?

Sio kwamba hawajui lugha nyingine. Ila hawa watangazaji wa Kitanzania hadi kero. Mpe kipindi cha Kingereza uone wanavyochapia.
 
Ndio maana radio ziko nyingi siku hizi. Chagua watangazaji wanaokufurahisha.
 
Huyu jamaa kweli ni mwendeshaji mzuri wa kipindi cha Morning Magic akiwa na wenzake akina Kibwana Dachi Mkambala, na Mary Edward.

Tatizo lake ni kuongea maneno ya Kingereza kila baada ya sentensi mbili za Kiswahili. Hivi mbona wenzetu Wazungu wakiwa kwenye vipindi huwa hatusikii sentensi za lugha nyingine?

Sio kwamba hawajui lugha nyingine. Ila hawa watangazaji wa Kitanzania hadi kero. Mpe kipindi cha Kingereza uone wanavyochapia.

Kingereza=Kiingereza?
 
Orest ni form six leaver so lazima atumie kiingereza kuuthibitishia umma kwamba naye yuko juu kielimu wakati ni ujanja ujanja tu wa mjini
Hana utofauti Na Jiwe maana Na yeye sentensi moja Na kiingeza chake kibovu...sasa mwambie aongee kingeleza kitupu Na phd yake utacheka mpaka ufe
 
Huyu jamaa kweli ni mwendeshaji mzuri wa kipindi cha Morning Magic akiwa na wenzake akina Kibwana Dachi Mkambala, na Mary Edward.

Tatizo lake ni kuongea maneno ya Kingereza kila baada ya sentensi mbili za Kiswahili. Hivi mbona wenzetu Wazungu wakiwa kwenye vipindi huwa hatusikii sentensi za lugha nyingine?

Sio kwamba hawajui lugha nyingine. Ila hawa watangazaji wa Kitanzania hadi kero. Mpe kipindi cha Kingereza uone wanavyochapia.

Jamii Forums Buana:

Mimi sina tatizo na mtu ambaye anaongea lugha ambayo anaifahamu vizuri ili kuongeza mvuto wake katika jamii, aidha sina tatizo la mtu anayelazimishwa kuongea lugha ambayo haijui lakini analazimishwa na mazingira na mwisho sina matatizo na mtu ambaye anaongea lugha kwa kuchanganya kwa minajili ya kujifunza lugha husika.

Mdogo wangu Orest hadondoki kwenye chochote katika maelezo yangu hapo juu ambayo inanipelekea kuamini kwamba HUYU NI LIMBUKENI TU!

Mkuu haimaanishi kwamba wewe sio mtangazaji mzuri usinielewe vibaya!
 
Kuna dada alikuwa magic anaitwa somebody Mdoe alikuwa kama misss flani hivi,bado yupo? Pia alikuwa na vipindi channel 10 akiwa na Raph B Sijaona na Nick Ngonyani.
 
Katika mazingira ya soko huria, kama kuchanganya lugha ndiyo kitu ambacho walengwa wa redio wanakipenda, mtangazaji kuchanganya lugha inawezekana kuwa ni sehemu ya ufanisi wa kazi yake.

Na kwa kweli, kinachotakiwa kumhukumu ni jinsi anavyokubalika na kusikilizwa na jamii, si sheria za umaridadi na uadilifu wa kufuatilia lugha.

Kenya kuna lugha inaitwa "Sheng". Ni mchanyato wa Kiingereza, Kiswahili na maneno ya lugha za asili za Kenya.

Kama mtu anaweza kuanzisha stesheni ya redio ya kuongea "Sheng" na watu wakaikubali, kama wewe hupendi, usisikilize.

Jamaica wana "Patois", ambayo ni mchanganyiko wa Kiingereza na lugha nyingi ambazo watu wa Jamaica wana asili nazo. Watu wa daraja la juu Jamaica wanaiponda sana Patois, lakini ni lugha ambayo watu wa kawaida wanaitumia. Nilikuwa nasikiliza BBC World Service kama kawaida yangu, nikasikia wametafsiri Biblia kwenye Jamaican Patois, kwa sababu watu wanasema Biblia ya King James hawaielewi, kwa sababu hiyo si lugha wanayoongea kila siku.

The link is here

Sasa basi, kama huyo mtangazaji anachanganya lugha, na hivyo ndivyo wasikilizaji wake wanafurahia, muachieni afurahie uhuru wa soko huria.

Kama wasikilizaji hawafurahii, hawatasikiliza, redio itakosa wasikilizaji, itakosa matangazo, itakufa kifo cha asili kwa kutozingatia wanachotaka wasikilizaji.

Ndivyo biashara za soko huria zinavyotaka.

Unaweza kutangaza kwa Kiswahili cha Shaaban Robert, wasikilizaji wasikuelewe, ukawa hujafanya kazi inayotakiwa.

Kuongea lugha nyoofu si sawa na kuwasiliana na watu vilivyo.

Habari hii inanikumbusha habari ya hotuba ya Mfalme Hirohito wa Japan.

Baada ya Japan kupigwa mabomu ya Atomiki Hiroshima na Nagasaki, ilibidi Japan isalimu amri na kukubali kushindwa vita.

Mfalme Hirohito wa Japan alionekana kama Mungu kwa watu wake, na hawakuwahi hata kumsikia sauti yake kwenye redio.

Ila kwa sababu mabomu yalikuwa makubwa sana, na nchi ilitakiwa kukubali kushindwa, mfalme akawa na kazi ya kuwatangazia watu kuwa wanakubali kushindwa.

Mfalme akatoa hotuba kwa watu wake kwa njia ya redio. Wajapan karibu wote wakawa wamekusanyika kwenye redio zao wanamsikiliza mfalme.

Tatizo likawa, Mfalme alikuwa anatumia Kijapan cha hali ya juu sana (classic Japanese) kiasi kwamba, mpaka alivyomaliza kuhutubia, wananchi wakawa wanaulizana, hapo Mfalme kasema nini? Mbona hatujaambulia kitu?

Alikuwa amezingatia kuongea kijapani cha ndani na hali ya juu sana, kiasi kwamba hadhira yake haikumuelewa alikuwa anamaanisha nini. Wengine wanasema alifanya makusudi kuficha aibu, kama anakubali kushindwa vita kwa lugha isiyoeleweka vizuri ili asipate aibu ya kukubali kushindwa kwa lugha inayoeleweka.

Kwa hiyo, kuongea lugha sawia nikitu kimoja, kuwasiliana na hadhira unayotaka nikitu kingine.

Kwa habari zaidi kuhusu speech ya Hirohito, somahapa NPR Choice page
 
Kaka tatizo hata kingereza chenyewe anaongea mayai viza ndio shida inapokuja. Hata hivyo inawezekana ikawa ndio ile nitoke vipi, nitoke vipi na ukashangaaa katoka kweli.

Na Mungu anajua zaidi
 
Inawezekana Kiingereza mayai viza ndicho kinachoeleweka kwa hadhira yake, na akiongea Kiingereza fasaha atakuwa kama Mfalme Hirohito hapo juu nilivyotoa mfano.

Katika soko huria hili jambo utatuzi wake ni rahisi sana.

Kama mtu hampendi anavyotangaza, susieni kipindi au redio.

Kumuanika hapa JF pia ni sahihi kwa maana kama wanafuatilia maoni ya watu watasoma.

Ila kama watu wengi wanapenda hivyo, au hawajali, ataendelea hivyo tu.
 
Inawezekana Kiingereza mayai viza ndicho kinachoeleweka kwa hadhira yake, na akiongea Kiingeteza fasaha atakuwa kama Mfalme Hirohito hapo juu nilivyotoa mfano.

Katika soko huria hili jambo utatuzi wake ni rahisi sana.

Kama mtu hampendi anavyotangaza, susieni kipindi au redio.

Kumuanika hapa JF pia ni sahihi kwa maana kama wanafuatilia maoni ya watu watasoma.

Ila kama watu wengi wanapenda hivyo, au hawajali, ataendelea hivyo tu.

WACHA WAFU WAZIKANE WAO KWA WAO: CLOUDS FM WALILALAMIKIWA KWAMBA WANAKANDAMIZA WASANII HAWAKUSIKIA EFM WAMEKUJA SASA WANAHENYA KU RESTORE WALICHOPOTEZA NA KAMA HAIWEZEKANI VILE
 
Clouds bado ipo far miles kulinganisha na efm..
 
Mkuu Kiranga, inawezekana hujasikiliza hicho kipindi cha asubuhi cha magic fm - "Kupaka Rangi.." Kama unaweza ebu ckliza kwanza afu ulete mrejesho. Ni kipindi kizuri, kinakuwa na watangazaji 3 au 4 kwa wakati mmoja, ila kinachafuliwa na huyo jamaa kwa kuingiza kiingereza kibovu sana mara kwa mara. Baadhi yao kama Mr Dachi ni makini kwenye uchambuzi wa mambo, hivyo siyo vzr wasikilizaji kulazimika kuachana na kipindi sababu ya mmoja
 
Back
Top Bottom