Rais Magufuli awa kivutio nchi za Afrika

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,975
Rais Magufuli tangu aapishwe amezidi kuwa kivutio katika magazeti na mitandao mbalimbali ya kijamii katika nchi nyingi za Afrika.

Kwa kipindi cha takriban siku 20 alizokaa ofisini, Rais Magufuli amechochea utendaji katika utumishi wa umma na kupunguza gharama akianza kwa kukata safari za nje kwa watumishi wa umma, sherehe za uhuru na matumizi ya serikali na taasisi zake yasiyo ya lazima huku akiwafukuza wafanyakazi ambao ni wazembe.

Kutokana na utendaji huo, watumiaji wa mtandao wa Twitter walianza kutumia kwa kasi kiunganishi cha ''#Magufuli '' na ''#WhatMagufuliWouldDO'' huku kwa sehemu kubwa, raia wa Kenya wakiongoza mjadala.

Raia hao walionekana kuvutiwa na utendaji katika siku za awali za Dk Magufuli huku wakikosoa Serikali ya Rais Uhuru Kenyatta wakidai inazidi kukithiri kwa rushwa. 'Hello Tanzania, Kenya inataka imkodi #Magufuli kwa wikiendi moja,' aliandika kwa Kiingereza mtumiaji wa Twitter mwenye jina la Ezekiel Mogaka kutoka Kenya.

Lakini mtumiaji mwingine mwenye akaunti yenye utambulisho wa Chakkah Dan aliandika; 'Rais Magufuli bila shaka (Hayati Baba wa Taifa), Julius Nyerere anatazama chini kutoka peponi akiwa anajivunia utendaji wako. 'Watanzania wanaamka kila siku asubuhi wakiona jambo fulani limetekelezwa na #Magufuli lakini Wakenya wanakwenda kulala na jambo ambalo #Kenyatta kaahidi,' aliandika The Golden Voice.

Kwa mujibu wa mtandao unaofutilia mijadala kwenye Twitter nchini Kenya, #GURUS daily trend, tangu jana asubuhi, kiunganishi '#Magufuli ? kilikuwa ni miongoni mwa viunganishi vitano vilivyokuwa vinaongoza kwa kuchangiwa, vingine ni #WhatBalalaShouldDo , #YouDontKnowLifeStruggle , Welcome to Kenya, Turkey na #FagiaKenya.

Katika mijadala hiyo, Wakenya walikuwa wakijaribu kufananisha siku 19 za Rais Magufuli na miaka mitatu ya Rais Kenyatta na kutania kuwa iwapo Rais wa Tanzania angegombea mwaka 2017 nchini humo bila shaka wangemchagua.

Mijadala hiyo 'haijabamba' Kenya pekee, Burundi nao hawakuwa nyuma. Mwenye akaunti yenye jina Joseph Siboma aliandika. 'Wakati ukomo wa madaraka ukiheshimika Tanzania, namkaribisha #Magufuli atawale kwa vipindi visivyoisha #Burundi.'

Mhadhiri wa Sayansi ya Siasa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Richard Mbunda, alisema nchi nyingi za Afrika zinahitaji kuwa na viongozi wanaojali masilahi ya wananchi lakini historia inaonyesha sehemu kubwa ya viongozi waliopo madarakani ni watawala wasiojali watu wao na hawapendi kuharibiwa nafasi zao.

'Sasa inapotokea kuna kiongozi kama Rais Magufuli anayepunguza matumizi ya Serikali bila shaka atakonga nyoyo za wengi. Mtindo wa uongozi wa Rais ni mpya na katika mambo yote aliyoyafanya hakuna wanaopinga zaidi ya kuwapo wachache wanaoonya mwenendo huo uendelee bila kupungua kasi', alisema Mbunda.


Wengine wameenda mbali zaidi na kutaka jina la Magufuli liingizwe kwenye Kamusi ya Kiingereza kama inavyoelezwa hapa,

attachment.php

attachment.php
 

Attachments

  • Magufuli.jpg
    Magufuli.jpg
    58.1 KB · Views: 7,752
  • Magufuli 1.jpg
    Magufuli 1.jpg
    47.6 KB · Views: 7,620
Watawala wa kiafrika ndio wanatufanya waafrika hata tukiwa nje ya afrika kukosa kabisa kujiamini, wametufanya tudharaulike kwa ujinga wao, hatuna cha kujivunia katika nchi zetu tena, magufuli kaonyesha atakuwa tofauti na viongozi wengi tu wa afrika, kwakweli iko haja ya kumuunga mkono kwa kila hatua yake,
 
Wacha aendelee na moto huo huo na wala asikate tamaa, ingawa atakuwa na upinzani mkali sana toka kwa wahafidhina ambao hawajazoea kuona mambo yakienda kwny msitari!

Tumezoea kuona viongozi wengi wa Africa wakiahidi mambo mengi kwa wananchi lakini yanaishia kwny makabati ya ofisi zao#
 
Watawala wa kiafrika ndio wanatufanya waafrika hata tukiwa nje ya afrika kukosa kabisa kujiamini, wametufanya tudharaulike kwa ujinga wao, hatuna cha kujivunia katika nchi zetu tena, magufuli kaonyesha atakuwa tofauti na viongozi wengi tu wa afrika, kwakweli iko haja ya kumuunga mkono kwa kila hatua yake,
Tokea aapishwe mpaka sasa, hajanivunja moyo kwa utendaji wake na ninaamini hawezi kunivunja moyo kutokana na historia yake ya utendaji serikalini.
 
Wacha aendelee na moto huo huo na wala asikate tamaa, ingawa atakuwa na upinzani mkali sana toka kwa wahafidhina ambao hawajazoea kuona mambo yakienda kwny msitari!

Tumezoea kuona viongozi wengi wa Africa wakiahidi mambo mengi kwa wananchi lakini yanaishia kwny makabati ya ofisi zao#
Nadhani anafahamu kama kutakuwa na upinzani, ndiyo maana akasema ameamua kulitumbua jipu pamoja na kufahamu maumivu yake wakati wa kulitumbua.
 
Mkuu naona unausemea moyo,tusubiri muda utazungumza
Kuna baadhi ya watu wanaumia sana wanapoona Rais Magufuli anafanikiwa katika kazi zake za Urais.

Kuna wengine nadhani wanaomba kwa shetani ili asifanikiwe!
 
Kuna baadhi ya watu wanaumia sana wanapoona Rais Magufuli anafanikiwa katika kazi zake za Urais.

Kuna wengine nadhani wanaomba kwa shetani ili asifanikiwe!

Washindwe na walegee,hivi unaanzaje kuumia kwa kuona rais anafanya yale ambayo tulikuwa tunayaombea kila siku?

Me nadhan hao wote wanaoumia si bure watakuwa na hisa zao kwenye makampuni yaliyokithiri kwa kutolipia kodi
 
Back
Top Bottom