Dr. Magufuli acha kuwaonea dagaa mchele, anza na hawa nyangumi

tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
21,802
18,225
UTANGULIZI
Baada ya Mh Magufuli kutinga ndani ya Whitehouse ya Magogoni, hata angali hajamteua Waziri Mkuu, alifanya kitendo ambacho watanzania tulikuwa tunakitarajia kutoka kwa kiongozi yeyote makini na ambaye anazingatia viwango vya utendaji kazi. Dr Magufuli alitembea kwa miguu kutoka nyumba nyeupe hadi ofisi za BoT ambako alikutana na utoro wa watumishi wazembe wasiozingatia falsafa ya Hapa Kazi Tu!

Baada ya siku chache aliibukia ndani ya Muhimbili ambako alikutana na madudu ya ajabu sana....eti CT Scan na MRI zimeharibika kwa muda wa miezi sita iliyopita lakini hakuna anayejali. Kilichowapata wahusika kila mmoja anakijua.

MADA
Sasa nirejee kwenye mada......
Mh Dr Joseph John Magufuli Pombe, kila mtanzania ameona kazi yako na anaridhishwa na utendaji kazi wako uliotukuka, ijapokuwa hujakikalia sana kiti cha enzi cha Magogoni. Mh Rais nakuomba uache kudeal na vidagaa sasa uwageukie hawa nyangumi wanaolitafuna na kuliguguna taifa kama fisi mwenye njaa:

Mosi, kuna jamaa mmoja aliyekuwa akiishi hapo ulipo leo, aliwahi kutamka kwamba anawafahamu fika wauza sembe na mahali wanapokaa. Sasa nikuombe Rais wangu, kwa heshima na taadhima umtake huyu mtu atutajie hao wauza unga ni wepi na wapo mahali gani ili wapate kushughulikiwa na serikali yako makini. Hatuwezi kukubali kuona kizazi cha watanzania kikiangamia kuwa kubwia sembe wakati kuna mtanzania mmoja anawafahamu hao wauza sembe na hataki kuwataja. Nakuomba utumie mamlaka uliyonayo kumtaka huyu mtu atuoneshe walipo hawa wauza sembe ili kuokoa kizazi cha vijana wanaoangamizwa na sembe kila kukicha. Falsafa yako ya Hapa Kazi Tu haiwezi kuzaa matunda endapo tutaacha nguvukazi iharibiwe na sembe pasipo kuchukua hatua.

Mh Rais, umeingia ikulu na kukuta senti zote za watanzania zimekombwa na manyang'au hadi ukoko. Hadi harufu ya senti zilizokuwemo kwenye jungu kuu imenuswa yote na mafisadi hawa ili kuficha ushahidi. Hujakuta hata harufu ya senti kwenye jungu la watanzania. Kana kwamba hii haitoshi, kiongozi wa ukombaji wa senti hizo aliwahi kurejeshewa fedha za watanzania kutoka kwa wezi waliotukuka kisha akazichukua fedha zile akazitia mifukoni mwake na kuwaachia wezi waende zao. Mpaka leo hakuna mtanzania hata mmoja, ukiwamo wewe Mh Rais, anayejua mahali zile pesa zilipo na wale waizi waliozirejesha ni kina nani. Sasa kwa kuwa unalo rungu la madaraka Mh Rais, nakuomba umuamuru mhusika arejeshe fedha za watanzania na umshinikize awataje wale wezi ili uwashughulikie ipasavyo. Hayuwezi kukubali kuona hazina yetu imebaki tupu huku fedha zetu bado hazijarejeshwa.

Pili, Waswahili walisema ?Kikulacho ki nguoni mwako?. Hawakukosea hata kidogo. Mh Rais, kuna mtu mmoja mfupi hivi, mnene na mwenye upara. Huyu jamaa aliwahi kukalia kiti cha enzi ulichokalia sasa. Bwana huyu bila haya wala soni aliamua kwa makusudi kabisa kujitwalia mgodi wetu kwa bei ya thamani ya beberu moja la mbuzi. Hili suala sio siri hata kidogo. Linafahamika kwa watanzania wote, ukiwamo wewe. Ijapokuwa inasemekana mtu huyu ndiye aliyekuokotea dodo chini ya mwarobaini, nakuomba ufumbe macho, kama ilivyo kawaida yako, umuambie wazi wazi bila kificho arejeshe mgodi wa watanzania chini ya miliki yao. Huyu jamaa alipokuja hapo ulipo alijifanya mstaarabu sana kumbe ustaarabu wake si mali kitu. Mwambie arejeshe mgodi wetu wa nishati kwa wananchi haraka iwezekanavyo.

Tatu, kuna jitu moja linalojiita joka la kurembua macho, kwa ushirikiano wa karibu kabisa na yule mama yetu wa senti za matembele na waaizi wengine kibao waliohusika kukomba pesa zetu kutoka kwenye ile benki yetu ya kikristo. Huyu nyoka nasikia hata wewe sumu yake unaiogopa sana. Nimeambia kwamba wakati unapita huko porini, ulikwepa kusogelea kwenye shimo lake asije akakugonga na meno yake yenye sumu kali kama pilipili. Pia usisahau kwamba hili joka la mdimu liliwahi kuwatia hasara watanzania kwa kuchakachua fedha za kununulia ule mtambo wa kijeshi kutoka kule kwa malkia na kisha kuficha fedha zile haramu kwenye kisiwa cha mbali. Nakuomba Mh Rais, ushughulike na hili joka haraka iwezekanavyo kabla halijaliangamiza taifa na sumu kali. Zile senti lilizokomba kutoka kwenye shirika letu la stima na darabuni ya ndege kutoka kwa malkia zirejeshwe kwenye hazina yetu haraka iwezekanavyo. Haiwezekani kila siku hili joka liwe linatamba kwa ujuzi wake wa vifungu huku wananchi wakilia njaa. Ikiwezekana hivyo vifungu linavyoringia vitenguliwe ili litiwe hatiani misa ya kwanza.

Aidha wale waizi wote waliochota senti zetu kutoka kule kwa wamisionari nao washughulikiwe mara moja bila kuwaangalia usoni. Najua kwamba Mh Rais inakuuma sana na kukuumiza kichwa baada ya kukuta jungu kuu la watanzania halina chembe ya ukoko. Basi ni wakati muafaka wa kuwashugulikia hawa majambazi ili kurejesha heshima ya jungu kuu la taifa.

Nne, kuna watu fulani ambao walizembea uzembe wa makusudi na kuliingiza taifa hili hasara ya mabilioni ya shilingi. Hawa nao usiwaache. Unakumbuka ile monowali ya kichina iliyokuwa na kitoweo ulichokigawa kwa wananchi ili kuboresha afya zao? Baada ya wewe kutekeleza wajibu wako Mh Rais, kuna hawa wazembe ambao walikuwa wamekalia kiti cha maamuzi wakafanya uzembe na kutoa uamuzi kwamba jamhuri irejeshe ile monowari pamoja na kile kitoweo ulichotugawia kutoka kwa maharamia waliokuja kuvuna kitoweo kwenye shamba la bibi. Hawa wahusika wasakwe na wachukuliwe hatua kwa kulitia taifa hasara. Kila mtanzania ni shahidi. Wale maharamia hawakuwa na haki hata chembe ya kuingia shambani kwa bibi na kuvuna kitoweo kama watakavyo. Maharamia wale ilipaswa watupwe segerea ili liwe fundisho kwa wengine. Kwa bahati mbaya waamuzi waliohusika kuwapeleka segerea wanajua walichokifanya hadi kulitia taifa hasara badala ya kuwafunga maharamia wale.

HITIMISHO
Ndugu wanajukwa, nisiwachoshe sana na hadithi zangu za Alfu Lela Ulela. Sasa nirejeshe kikuza sauti kwenu. Je, nyie mwaona ni halali kwamba hawa nyagumi waachwe bila kushugulikiwa wakati mambo yakienda mrama? Mimi nasema hapana. Nataka hawa nyangumi tuwamulike kwa tochi kali ili nchi hii ipate heshima inayostahili. Kama kuna nyangumi mwingine niliyemshau kwenye orodha yangu, muweke humu tumumulike kwa tochi kali ili Mh Magufuli amuone na kumshughulikia ipsavyo.

Nawasilisha.
:yield:
 
JPM ana kazi kubwa, thats all. Nimecheka hadi basi ..... ..... ..... . .
 
Kuna watu mna muda....mnawezaje kusoma pumba zote hizo za mtoa post!? I don't believe if it's worth reading all that bunch of nonsense.
 
Kwa nini umesahau au umejifanya kusahau kuhusu Richmonduli?

Rais Magufuli lazima amshughurikie pia huyu Mzee aliyoota nywele nyeupe wakati bado akiwa kijana na kwa sasa anajiandaa kwenda kuchunga ng'ombe kijijini Monduli baada ya wewe kumstaafisha kwa manufaa ya umma kupitia sanduku la kura.

Huyu Mzee mwenye nywele nyeupe ni kinara wa mtandao ulizaa wezi na mafisadi ndani ya CCM na Serikali.

Badala ya kwenda kuchunga ng'ombe inafaa aende gerezani kuwa nyampala wa wafungwa.

Ni hayo tu Rais wetu unayefanya maamuzi makini na siyo maamuzi magumu!
 
Si alikupa chance ya kumpeleka mahakamani? Mbona hukumpeleka kama alikuwa na tatizo? Afadhali yake Lowassa kasema wazi huko hakufai na akajitoa huko kuliko Magufuli anayeifanyia kazi upinzani huku yuko ccm. Haya madudu yote mliyakubali, kuyashabikia, na kuyapigia makofi ya ndiyo bungeni. Leo Magufuli kawageuka kama nyoka badala ya kuketi chini mjiulize mlifikaje huko mnaanza kuwananga wapinzani. Hii ni aibu kubwa! Lowassa ni mtu mwadilifu kuliko mnavyofikiri. Mbona hamkumpaka mavi kabla hajatoka hiyo CCM. Sikumsikia Lowassa akimtukana mtu hata wakati wa kampeni. Alisema nipeni nchi hii niiongoze kwa speed ya 120 na nifanye maamuzi magumu. Hakutukana mtu Alijikubali akakana uvundo wa CCM na kuahidi kubadilika na kuleta mabadiliko. Tumpe credit kwa hilo na tuache kumnanga. Magufuli amekuwa ndani ya serikali muda wote anawajua fika wanaohitaji kuwanyoosha. Atawafanyia kazi. Usipoteze muda wako kumtukana Lowassa hapa. CCM wamemweka Magufuli kuwa raisi wakijua fika wanafanya nini. Bahati mbaya tuna elimu ndogo. Kama huna elimu unashabikia tu wala huwezi kuona mbali. Jikumbushe yale mambo ambayo upinzani waliyapigania sana bungeni. Jikumbushe kidogo jinsi wabunge wa CCM walivyokuwa tayari kupitisha chochote kinachifaidi CCM hata kama kinawamaliza watanzania na taifa lao. Lowassa ni mtu mmoja ambaye historia itambariki sana. Mwangalie Kikwete jinsi anavyumbuka na uaongozi wake sasa hivi. Fungua macho, kiri ukweli, angalia mambo kwa undani usishabikie tu upepo kwa kuwa sasa umebadilika na unaeelekea walipo wapinzani. Kama Mungu amepanga Lowassa atakuwa raisi wewe ngojea uone.
 
aturudishie na Home Shopping Center aje atulipe kodi yetu. amesamehewa kodi nyingi na swahiba wake na ameshafunga biashara zake tangu october wakt wa uchaguzi
 
Anshaghulikia Mahakama yao kwanza .. ! . Hawa amesema Ataingia Nao kwnye Vita ..mfano Wa NATO Vs KOSOVO ....chill and wait . ..ndio kwanza kipindi cha kwanza .

Kula mtori taratibu nyama Iko chini ..
 
Kwa nini umesahau au umejifanya kusahau kuhusu Richmonduli?

Rais Magufuli lazima amshughurikie pia huyu Mzee aliyoota nywele nyeupe wakati bado akiwa kijana na kwa sasa anajiandaa kwenda kuchunga ng'ombe kijijini Monduli baada ya wewe kumstaafisha kwa manufaa ya umma kupitia sanduku la kura.

Huyu Mzee mwenye nywele nyeupe ni kinara wa mtandao ulizaa wezi na mafisadi ndani ya CCM na Serikali.

Badala ya kwenda kuchunga ng'ombe inafaa aende gerezani kuwa nyampala wa wafungwa.

Ni hayo tu Rais wetu unayefanya maamuzi makini na siyo maamuzi magumu!

Nawe usiwe msahaulifu,mwambie arudishe nyumba zetu alizohonga kwa kimada wake Sundi Mlomo,na ile aliyomuuzia mdogo wake aitwaye Mussa,tunataka hayo maamuzi makini yaanzie kwake siyo kujitia "utakatifu" asiokuwa nao.
 
Kuna watu mna muda....mnawezaje kusoma pumba zote hizo za mtoa post!? I don't believe if it's worth reading all that bunch of nonsense.

Kama hukuisoma yote umejuaje kuwa ni pumba? Na kama umeisoma yote nawe ni pumba.
 
Nawe usiwe msahaulifu,mwambie arudishe nyumba zetu alizohonga kwa kimada wake Sundi Mlomo,na ile aliyomuuzia mdogo wake aitwaye Mussa,tunataka hayo maamuzi makini yaanzie kwake siyo kujitia "utakatifu" asiokuwa nao.

kumbe waliuziwa? Mie naona aanze kurudisha jengo letu la uvccm alilojitwalia na mamvi.
 
Si alikupa chance ya kumpeleka mahakamani? Mbona hukumpeleka kama alikuwa na tatizo? Afadhali yake Lowassa kasema wazi huko hakufai na akajitoa huko kuliko Magufuli anayeifanyia kazi upinzani huku yuko ccm. Haya madudu yote mliyakubali, kuyashabikia, na kuyapigia makofi ya ndiyo bungeni. Leo Magufuli kawageuka kama nyoka badala ya kuketi chini mjiulize mlifikaje huko mnaanza kuwananga wapinzani. Hii ni aibu kubwa! Lowassa ni mtu mwadilifu kuliko mnavyofikiri. Mbona hamkumpaka mavi kabla hajatoka hiyo CCM. Sikumsikia Lowassa akimtukana mtu hata wakati wa kampeni. Alisema nipeni nchi hii niiongoze kwa speed ya 120 na nifanye maamuzi magumu. Hakutukana mtu Alijikubali akakana uvundo wa CCM na kuahidi kubadilika na kuleta mabadiliko. Tumpe credit kwa hilo na tuache kumnanga. Magufuli amekuwa ndani ya serikali muda wote anawajua fika wanaohitaji kuwanyoosha. Atawafanyia kazi. Usipoteze muda wako kumtukana Lowassa hapa. CCM wamemweka Magufuli kuwa raisi wakijua fika wanafanya nini. Bahati mbaya tuna elimu ndogo. Kama huna elimu unashabikia tu wala huwezi kuona mbali. Jikumbushe yale mambo ambayo upinzani waliyapigania sana bungeni. Jikumbushe kidogo jinsi wabunge wa CCM walivyokuwa tayari kupitisha chochote kinachifaidi CCM hata kama kinawamaliza watanzania na taifa lao. Lowassa ni mtu mmoja ambaye historia itambariki sana. Mwangalie Kikwete jinsi anavyumbuka na uaongozi wake sasa hivi. Fungua macho, kiri ukweli, angalia mambo kwa undani usishabikie tu upepo kwa kuwa sasa umebadilika na unaeelekea walipo wapinzani. Kama Mungu amepanga Lowassa atakuwa raisi wewe ngojea uone.
Maelezo ni mengi ya kujaribu kumtetea Lowassa wakati andiko langu halikumtaja Lowassa!

Kwa kukusaidia zaidi, kama unadhani Rais Magufuli amechaguliwa kwa sababu ya hoja za wapinzani, kwa hoja hii huoni kuwa Lowassa alikuwa ni mzigo usiobebeka kwa sababu pamoja na kuuza Ilani ya CHADEMA ambayo unadai Rais Magufuli kwa sasa anaifanyia kazi, wananchi waliamua kutomchagua Lowassa na kumchagua Magufuli.

Kama Ilani ya CHADEMA ilikuwa ni nzuri, kwa nini aliyekuwa anainadi ambaye ni Lowassa hakuchaguliwa?

Lowassa kwa sasa hana nafasi tena katika siasa za Tanzania, He' suffering Mrema's political demise!
 
Back
Top Bottom