Waziri wa Nishati na Madini Prof. Muhongo agoma kusafiri kisa hana First Class ticket

BASIASI

JF-Expert Member
Sep 20, 2010
9,735
5,002
Hakia Mungu kweli hii nchi inatia aibu,wakati waziri wa uingereza akikata first class anaeleza sababu maalumu huku leo kimetokea kituko.

Waziri wenu wa nishati ambae anazidi kutulaza na joto na giza leo amewaacha hoi watanzania pale alipofika mpaka airport na akiwa anaboard akakuta anawekwa sehemu ya bussiness pax....baada ya kuwaambia hayuko first class akagoma na kutoka nje ya mlango
wakati hayo yakiendelea kumbe ana umati wa wenzake zaidi ya 9 wako economy na wawili bussiness class ...gafla nao wakaanza kushuka.

Hapo ndipo hekima za mmoja wa wahusika wa airline akamwomba hao waende then ye akabadilishe aje keshoo

Jamani kweliii kweliii first class inakushushia aibu hivi prof na bado unasema maisha.

Inaonekana zile buti za bora ulizivalia ukiwa form 5 haya ndio madhara yake mnapewa vyeoo wakati maisha yalishawapiga mnatafuta muafaka na yesu mkiwa madarakani.

Embu kuweni wastaarabu bana,sasa wale watu 9 ulitaka kuwashusha kwa nini na kama wamekwenda ulishindwa kuwambia wabaki mpaka mkaanza kuleta aibu uwanjani.

Inaonekena ndege m meanza kupanda uzeeni, najiuliza kivipi unaletewa tiketi hata kama na travel agency alafu unashindwa kuuliza ama kukagua mpaka unaenda uwanjani...unapewa bpass bado unashindwa kukagua ipi bussiness class bp..ipi first class loh so bad.
 
Kama hii ni kweli tunatakiwa tuwe na sheria ya kuwaongoza hawa wehu.
 
Nchi nyingi zina mwongozo viongozi wanatakiwa wapande madaraja gani sijui kwa nini Tanzania kila mtu anafanya apendavyo.
 
Ana haki. Tena namwomba asiamke asubuhi amkute huyo PS wake pale ofisini. Awe ameshakusanya kila kilicho chake aende makwao.
Prof. Muhongo ni mtu wa maana sana TZ. Ameombwa aje kushika wadhifa huo, yeye ana ofisi kulee Sauzi, we unampakia class gani eti. Sijui economy, economy gani wakati anaponda zake za mwisho wa Maccm? Unafikiri hajui ni za mwisho mwisho hizo?
Pengine alikuwa anaenda kuusaini mkataba wa vitalu kama 10 hivi kwa kabaila mmoja hukoo ni shs ngapi ataleta hazina. Pole sana Prof. Naomba tuwie radhi sisi tunaokaa huku uswazi tupe tu kaumeme kidogo kwa hisani yako. Hatujamtuma huyo PS wako akosee namna hiyo. Tusaidie tu baba sie Matonya wa huku uswazi tupate tone la umeme. Leo nakupa B/up Mhishimiwa, yule mgawaji kasahau huku kwetu hajakata tangu asubuhi. Huenda alifikiri ulisafiri.
MaSii sii eem Hoyeee 2015 is just very near. Mtayalamba matapishi yenu kwenye sanduku la kura tu
 
Ziku zote Baba ndiye anayekula firigisi na watoto kwa kawaida km ni kuku hula malenge/miguu.
 
Nchi nyingi zina mwongozo viongozi wanatakiwa wapande madaraja gani sijui kwa nini Tanzania kila mtu anafanya apendavyo.
Huyu kiongozi Hana sifa hata ya kupangiwa daraja gani ya ndege apande.ni kiongozi kwa domestic issue sio diplomatic so hata economy class angeweza kupanda km sio kujiona mungu mtu.
 
Lakini ungetuambia alilipia/alilipiwa class gani. Kama alilipiwa class ya juu kuliko ile ambayo wahudumu wa ndege wanamwonesha, naamini anayo haki ya "kulalamika"! Labda issue iwe ni namna ya "kulalamika"!
 
hawa ndo viongoz wanaojifanya miungu watu wa kibongo, next time watu kama hawa hawatufai hata kidogo
 
Aibu sana kwa mh. Kutaka kuspend kiasi hicho wakati huku tunateseka na lim'galo lisilo na kichwa wala miguuu.... sijui aliyekuchagua Kuwa waziri alikuwa anawaza nini..... shame on u
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom