Nilivyofunga "bao la mkono"...

Ramos

JF-Expert Member
May 13, 2010
498
130
Kiukweli mimi sio mtu wa kuonyesha haya 'makea artificial' kwa mke wangu, nikizingatia kuwa akiyazoe ntakuwa 'sina jipya' alafu atanchoka.

Sasa siku moja tulitinga harusini na my beloved wife, na kwa kuwa siku hiyo tuliunganisha functions, tulifika tukiwa tumechelewa kidogo. Ile kuingia ukumbini tukakuta inaporomoshwa misebene ya nguvu, na kwa kuwa sisi ni 'walevi' wa sebene, tulichofanya tuli-identify meza ya kukaa, tukakuta moja waliokuwa wamekaa famili friends wetu ina nafasi, wife akakabidhi kimkoba tukajimwaga jukwaani kusakata muziki. Tuliunganisha sebene kama tatu, kwa bahati mbaya kiatu kimoja cha mke wangu kikafyetuka soli, ikalazimika tukakae. Tulipofika tukakuta wale wenzetu pale mezani na meza za jirani wameshaenda kuchukua msosi pamoja na waliokuwa meza za jirani ambao wengi walikuwa office mates.

Kwa hiyo ikabidi kwenda kuchukua chakula, but kwa kuwa mke wangu kiatu kilishafyatuka, (watu walikuwa hawajagundua), nikamwambia "Kaa tu mamaa, umechoka, ngoja nikakuletee msosi"... Binafsi niliisema tu ile sentensi kiutani kwa kujua kuwa hataweza kwenda kuchukua chakula na kiatu chake kile. Kumbe nilipoenda huku nyuma nikaacha gumzo kwa watu wakifagilia 'nilivyo na makea'... kwamba ninavyomjali mke wangu nimeenda kumchukulia msosi..., kwamba kwa kuwa alikuwa amecheza amechoka (kweli mke wangu anayarudi masebene (ila hanizidi... ata ye anajua)), eti nimemuacha apumzike.. Niliporudi pale na sahani zangu mbili nikashangaa 'hongera' zinamiminwa kutoka kwa watu kadhaa, mi nikadhani ni kutokana na umahiri wa kusakata sebene. Naweza kusema lile tukio la kufyatuka kiatu lilinisababisha nikapewa misifa ambapo baadhi ya watu hasa office mates waliendelea kunichukulia hivyo (mtu wa makea) hata baada ya harusi. Ilikuwa haina tofauti na jinsi bao la mkono la Henry lilivyoipeleka France Sauz mwaka 2010...
 
Kuna mtu aliwahi kupost kuwa ana ugonjwa wa kupenda sifa, naona atakuwa amekuambukiza, tafuta dawa kabla haujapea
 
mie niliingia nikajua ulipiga bao wakati una dance sebene bana....kumbe wee mpenzi wa debe
 
Kwa hiyo bwanakaka unatakaje, tukupongeze kwa kumcare mkeo au tukupongeze kwa kumnunulia viatu vya "kagundua mchaga" vikamuumbua kwenye kadamnasi, tafadhali muombe radhi mkeo kwa kutomjali!!!
 
Me ulipofika hapo mmerudi mezani hakuna mtu me nilijua labda umepenyeza mkono chini ya meza kumpa raha hadi ukafunga bao ya mkono
Kumbe......patupi
 
wabongo bwana
mkeo na ww ni kitu kimoja tu
mimi nawashangaa hao waliokupa misifa.
unatakiwa uingie jikoni umpikie mkeo na pia mgawane shughuli hapo home kwenu
kuchukua chakule kumletea that is very minor issue kupewa sifa...
 
Kumchukulia chakula ni jambo la kawaida na kama walikupongeza kwa hilo ni tabia ya kibongo tu ya kupaka mafuta kwa mgongo wa chupa!kua makin na mbongo
 
bao la mkono? ulinichanganya sana mi nikajua ulimnawa bwana mpaka likatokea bao la mkono ah umenikata stimu
 
wabongo bwana
mkeo na ww ni kitu kimoja tu
mimi nawashangaa hao waliokupa misifa.
unatakiwa uingie jikoni umpikie mkeo na pia mgawane shughuli hapo home kwenu
kuchukua chakule kumletea that is very minor issue kupewa sifa...

labda wewe uko tofauti,
wanaume wengi wanachukulia kama udhaifu kumkea mtu
ila amekubali kuwa yeye yuko kny hilo kundi kubwa,lol
Ramos ukitaka ufurahi zaidi na mkeo,ongeza makea usione haya lol sema mawifi wawe mbali sie wanawake tunajua kuchonga pia hatareee labda kama ni walee wa kidigitale,kama wale wa analogia hapo mmefeli aisee watachongaa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom