Balozi wa Uingereza aasa: Watanzania acheni woga

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,005
Balozi wa Uingereza aasa: Watanzania acheni woga

Mwandishi Wetu Juni 11, 2008
Raia Mwema~Muungwana ni Vitendo

Kila mwaka katika wiki ya kwanza ya Juni balozi za Uingereza duniani kote huadhimisha siku ya kuzaliwa kwa Malkia Elizabeth II. Katika Tanzania sherehe hizo mwaka huu zilifanyika Jumamosi ya Juni 7 mjini Dar es Salaam. Ifuatayo ni hotuba fupi ya Balozi Philip Parham katika kuadhimisha sherehe hiyo.

KASIA na mimi tumepewa heshima na tuna furaha kuwakaribisha nyote hapa kusherehekea siku rasmi ya kuzaliwa Malkia Elizabeth (wa pili). Kama kuna mtu kati yetu hapa ambaye atakuwa na nguvu kama yeye akiwa na umri wa miaka 82, basi I’ll eat my hat - kama mumewe Prince Philip anavyosema.

Ni vigumu kwetu kuamini kwamba tayari hii ni mara ya tatu Kasia na mimi tumesherehekea siku ya kuzaliwa Malkia na ninyi nyote hapa Dar es Salaam. Mara mbili za mwisho sherehe kama hii ilikwenda sambamba na wakati ambapo timu za Uingereza zilikuwa na wasiwasi na matarajio yao ya kutwaa ubingwa katika soka ya kimataifa. Usiku wa leo hatutakuwa tukisumbuliwa na wasiwasi kama huo, tumshukuru Mungu.

Miezi 12 iliyopita imekuwa ya kuvutia: Waziri Mkuu mpya; mabadiliko katika mitazamo ya kisiasa; upinzani wa kisiasa bungeni; kutofanya vizuri katika michezo ya kimataifa - na mambo yote haya kwa nchi zote mbili; Tanzania na Uingereza, yanathibitisha moyo na ushirikiano uliopo kati ya nchi zetu kubwa hizi mbili; na tukiundeleza ushirikiano wetu kwa ajili ya usitawi, amani na usalama.

Mabadiliko ya Waziri Mkuu Tanzania yananipa fursa kusema maneno kadhaa usiku huu. Kwa wachunguzi makini kati yenu mtakumbuka kwamba wakati Mheshimiwa Mizengo Peter Pinda anachaguliwa, Parokia yake ya Kinondoni iliandaa misa maalum ya shukrani na sala kumwombea mafanikio. Na wazo kuu la padri wa Parokia hiyo lilikuwa “Usiogope” - neno linalorudiwa mara nyingi katika Agano Jipya la Biblia.

“Usiogope”: Hivyo ndivyo malaika alivyomwambia Mariam alipomjulisha kuwa atakuwa ni mama wa Yesu; na ndivyo pia malaika anavyosema pale alipowaambia Mamajusi kwamba mtoto Yesu amezaliwa; na vile vile ndivyo Yesu alivyowasalimu wafuasi wake.

“Usiogope” : Na kwa kweli usiogope - si kama eti Balozi ameamua kuendesha misa. Lakini maneno haya ya kutia moyo - "Usiogope" - ni muhimu sana kwetu sote, tuwe Wakristo, Waislamu, Wahindu, Singasinga, Wabuda, au wale wasio na dini.

“Usiogope”: Pamoja na changamoto zote, kuna nuru katika hali ya baadaye ya Tanzania. Ikiwa katika hali ya utulivu, mshikamano wa kijamii, demokrasia hai, uchumi mzuri, fursa kubwa za kiuchumi ambazo hazijatumika kikamilifu, Rais mwenye uwezo; na utashi kutoka jumuiya ya kimataifa, Tanzania ina nafasi kubwa ya kubadilika. Tanzania si nchi masikini.

Raia wake hawapaswi kuwa masikini. Matumaini ambayo nimeyaona katika macho ya watoto katika vijiji vya Lindi, Mbeya, Ruvuma na Iringa; kule Kagera, Kigoma na Morogoro; na katika macho ya watoto wa Kituo cha Dogodogo hapa Dar es Salaam - hakika matumaini hayo yasivunjwe moyo, na hili linawezekana endapo sisi sote tutatekeleza wajibu wetu.

Usiogope – na maonyo yote haya yanatuhusu sisi sote - usiogope kuzitwaa fursa ambazo zinapatikana sasa kwa nchi ya Tanzania.

Usiogope kukabiliana na watu wenye maslahi binafsi ambao wanajaribu kuzuia maendeleo kwa sababu zao za kichoyo.

Usiogope kuachia hatamu au wadhifa, au usiogope kuachia ngazi pale ambapo kazi fulani yaweza kufanywa vizuri na wengine.

Usiogope kuchunguza na kushitaki maovu endapo ushahidi na maslahi ya umma yanakuhitaji ufanye hivyo, bila kujali kuwa watuhumiwa ni watu mashuhuri kiasi gani… (Na tukumbuke: hakuna kitu kikubwa kuliko uwezo wa binadamu)

Usiogope kuendeleza na kuhamasisha ufanisi pamoja na uadilifu, na pia kuung'oa uzembe na udanganyifu. Lakini pia: Usiogope kuwaamini marafiki zako kama wanastahili uwape uaminifu huo.

Tusiogope pia kuchukua maamuzi yanayoweza kuonekana ya hatari - wakati tayari maamuzi hayo yamekwisha kuhalalishwa na viashiria vya faida yake.

Tusiogope kukiri uwepo wa vizingiti. Mara nyingi watu wanasema, "yaani kama Serikali ingefanya hivi au vile…" Ni vizuri tukajikumbusha kwamba bajeti yote ya Serikali ya Tanzania, kwa kipindi cha mwaka uliopita, ilikuwa takribani Dola bilioni 5. Kiasi hiki ni sawa kabisa na kiasi cha fedha ambacho Waingereza wanakitumia katika kununua mikanda ya DVD kwa mwaka. Hii pia ni sawa na asilimia 2.5 tu ya bajeti ya Afya ya Uingereza.

Aidha, kiasi hicho ni sawa kabisa na robo ya fedha ambayo wacheza kamari wa Uingereza wanakipoteza kwa mwaka. Pia ninasikitika kusema kwamba kiasi hiki ni sawa kabisa na makadirio ya thamani ya chakula kinachotupwa kama mabaki nchini Uingereza. Hivyo, hiki ndicho kiwango halisi cha fedha ambacho Serikali ya Tanzania inacho ili kuweza kuwapatia wananchi wake huduma ya elimu, afya, miundombinu pamoja na ulinzi kwa takribani wananchi milioni 40 waishio katika nchi hii - ambayo ni kubwa zaidi, mara nne kwa Uingereza.

Msiogope pia kubadili fikra zetu pamoja na sera zenu, endapo itajidhihirisha wazi kwamba uelekeo mpya ni sahihi.

Msiogope kuipatia sekta binafsi fursa, uhuru pamoja na kujiamini katika kuongeza nafasi za ajira, tija na ukuaji wa uchumi.

Msiogope pia kusema ukweli juu ya dola, hasa pale dola inapotishia ustawi wa heshima ya binadamu na utulivu katika ukanda huu.

Tusiogope kusheherekea mafanikio na kutoa sifa pale inapostahili - na kwa hili sifa kubwa ziiendee Tanzania kwa mchango wake mkubwa katika ukanda huu wa Afrika kwa kipindi cha miezi michache iliyopita: kwa mchango muhimu katika kuleta mapatano ya kisiasa nchini Kenya; kusaidia kutokomeza uvamizi katika visiwa vya Comoro; kusaidia mafanikio katika mchakato wa amani nchini Burundi; kukubali kuwapatia uraia wa Tanzania mamia ya maelfu ya wakimbizi; kuwezesha kufanyika kwa mazungumzo ya amani kwa ukanda wa Maziwa Makuu, pamoja na uwakilishi mzuri wa masuala ya kimaslahi ya bara la Afrika, unaofanywa na Rais Jakaya Kikwete, kama mwenyekiti wa Umoja wa Afrika.

Jambo la mwisho la kutoogopa ni: Kutoogopa kuwa na hotuba fupi na ya kijasiri. Kwa hiyo katika hili, ninawaomba kuinua glasi zenu na kuzigonganisha kwa ajili ya mafanikio, amani na afya ya Rais Jakaya Kikwete pamoja na wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
Mwingireza kamwaga sifa kweli kwa JK then anasema tusiogope ? Lazima tuogope kwa sifa zake huku tunalia pembeni , EPA, Zanzibar, Richmond ......................................................
 
Back
Top Bottom