Search results

  1. N

    Huyu mtu ananifaa kweli au niachane nae

    Hakuna cha ndoa ya siri; iwe ya Kiserikali au ya Kidini. Kabla ya ndoa kufungwa (serikalini na kidini) lazima tangazo liwekwe (Marriage ban) ubaoni kwa kipindi fulani na kanisani na misikitini lazima matangazo yafanywe mara kadhaa. Siku ya arusi, arusi lazima ifungwe mahali pa wazi na mtu yo...
  2. N

    Nini hatima ya Wakristo walio Zanzibar kwenye sherehe za Pasaka baada ya zuio la kula mchana wakati huu wa Ramadhan?

    Unamaanisha kwamba kwa kuwa uonevu umekuwa ukitokea tangu zamani, basi uachiwe uendelee tu?
  3. N

    Nimenasa sauti ya Katibu Tawala (DAS) Wilaya ya Mbogwe, Ndg. Jacob Rombo akiiba mafuta ya Serikali

    Sawa kabisa. Haina maana kupoteza muda kubishania kichwa cha habari. La muhimu ni kwamba huo ni ushahidi tosha wa kumtia hatiani mtuhumiwa. Lililopo ni kwamba vyombo husika vichukue ushahidi huo na sheria ichukue mkondo wake. Alivyofanya mtoa mada ndivyo kila raia mwema anapaswa kuwa.
  4. N

    Nimenasa sauti ya Katibu Tawala (DAS) Wilaya ya Mbogwe, Ndg. Jacob Rombo akiiba mafuta ya Serikali

    kwa kuwa wapo wengi wanaofanya uovu huo, ndiyo tukae kimya tu baada ya kugundua kosa linafanyika?
  5. N

    Vita kali kati ya Wamasai na Wachaga, 1820,s

    Najiuliza: nini hasa madhumuni ya uzi huu? Ni kuchochea uhasama kati ya Wamasai na Wachaga ili kila mmoja aseme yeye ndiye mwenye haki ya kuishi hapo? Nini hasa madhumuni ya kukumbushia historia ambayo imeisha tulizwa na haileti tatizo lo lote hivi sasa? kama lingekuwepo tatizo, ndipo tungesema...
  6. N

    Baada ya Hayati Magufuli kuombewa Chato, Mwanza nao wanaandaa maombi, binafsi naona haya yanayofanyika baada ya Chato yako kimkakati

    Hayo wanayofanya kama huyaamini, yanakuhusu nini? Pilipili ya shamba inakuwashaje? Wakatoliki tunaamini umoja wa 1) watakatifu walioko mbinguni tayari; 2) waumini ambao bado wako hapa duniani; na 3) marehemu walioko toharani wakitakaswa kutayarishwa kufika mbinguni. Hayo makundi mawili ya...
  7. N

    Ningekuwa na karama ya kulaani ningelilaani Italia (Roma) kwa kusababisha usumbufu kati ya Myahudi na Muislam

    Vita vya Warumi unavyovitaja vilitokea takriban miaka 500 kabla ya kuzaliwa Mohamedi. Vivyo hivyo na ujenzi wa msikiti wa Al Aqsa. Sasa vipi uunganishe hivyo vitu viwili na kuwalaumu Warumi?
  8. N

    Wilibrod Slaa na CHADEMA waache dharau kwa umma wa Watanzania

    Naona ni wewe peke yako unayejua kwamba Wilboard Slaa alikuwa balozi wa Tanzania huko Canada.
  9. N

    Rais Mstaafu ni Msaidizi wa Rais aliyeko madarakani ndio sababu anaweza Kutumwa kumwakilisha Rais kwenye shughuli mbalimbali!

    Rais mstaafu hawajibiki kutoa msaada wo wote. Kinachotokea ni kwamba Rais anayekuwa ofisini anaweza kumtumia huyo mstaafu kama kuna haja, na yeye akipenda. Lakini siyo kwamba ni lazima huyo mstaafu atoe huo msaada. Kwa mfano, uzito wa msiba wa kitaifa unaotokea unapimwa na hadhi ya kiongozi...
  10. N

    Je, utamkumbuka Hayati Magufuli kwa mambo gani?

    Ongeza pia kwamba kama si Magufuli, kuhamishia Dodoma makao makuu ya nchi kusingekuwepo.
  11. N

    Raia 10,000, wataalamu 140

    Kama huamini fanya hata ku-google basi. Hii siyo siri. Mashirika makuu ya habari yalitangaza na hata Serekali ya Marekani yenyewe ilitangaza.
  12. N

    Raia 10,000, wataalamu 140

    Kuhusu utaalamu na teknolojia, bada ya vita vya Yom Kippur vya mwaka 1973 kati ya Israel na Waarabu, Marekani ilitoa msaada kwa Israel na kwa Waarabu wa silaha na wataalamu wa kufundisha kutumia hizo silaha. Maelezo ya Marekani yalikuwa kwamba kama kila upande ukijua mgomvi wake amejizatiti...
  13. N

    Suala la Waziri Mkuu kununua simu kwa mkopo Vodacom ametupiga

    Hivi hawa VODA wameisha gawa dividends tangu waanze kuuza hisa? Mimi nilinunua zile za mwanzo kabisa lakini mpaka leo ni kimya tu. Napata za makampuni mengine tu; hasa TCC na TBL.
  14. N

    Dkt. Slaa: Niliwahi kusema Lowassa ni fisadi lakini mimi ni Padre, katika umauti ni lazima niiombee Roho yake iingie mbinguni

    Slaa ni Padre. Ni kwamba tu haruhusiwi kuutumia upadre wake hadharani. Baada ya kuwa Padre, unabakia hivyo hadi kufa.
  15. N

    Dkt. Slaa: Niliwahi kusema Lowassa ni fisadi lakini mimi ni Padre, katika umauti ni lazima niiombee Roho yake iingie mbinguni

    Slaa hakuasi. Alishindwa kuendelea na kazi ya Upadre kwa sababu zake binafsi; akaomba kutoendelea na kazi hiyo; akaruhusiwa; wakaagana na mwajiri (Kanisa) kwa 'kushikana mkono'. Lakini Upadri wake unabakia palepale na itakuwa hivyo mpaka kifo chake. Asichoruhusiwa ni kufanya kazi ya kipadre...
  16. N

    TANZIA Professor James Shaba afariki dunia. Alifanyia postmortem mwili wa Hayati Sokoine

    Waziri Mkuu Edward Sokoine alipofariki Aprili 1984, mwili ulilazwa Bungeni ili watu waende kutoa heshima za mwisho. Matarajio yalikuwa kwamba shughuli hiyo itafanyika kwa masaa kadhaa tu, nadhani kuanzia saa 11 jioni hadi saa 4 usiku. Baada ya hapo mwili ungepelekwa mortuary. Idadi ya watu...
  17. N

    Taarifa za Kijasusi: Hamas bingwa wa mabingwa. Hivi karibuni kutatangazwa ushindi mkubwa kwa Wapalestina

    Kama ushindi ni nchi kuchakazwa kama Gaza ilivyofanywa, basi ni heri kushindwa kuliko kusema umeshinda ukiwa hali hiyo. Hebu turudi nyuma mpaka vita vya Mwaka 1967. Baada ya upelelezi wa kijasusi wa Israel kugundua kwamba Waarabu wanapanga kuishambulia Israel, Wayahudi walianzisha vita ya...
  18. N

    Ipi ni 'sexual fantasy' yako?

    Hivi unajua utakufa lini mpaka useme unahakikisha utatimiza lengo lako kabla ya kufa? Tazama Luka 12: 16-21 (Tafsiri yangu): Baada ya mavuno mazuri sana mwaka mmoja, mpumbavu akasema: Nitabomoa ghala langu na kujenga makubwa zaidi ambamo nitahifadhi mavuno yangu ya ziada. Nitajiambia "Una nafaka...
Back
Top Bottom