Search results

  1. A

    Simu haiwezi kuunganishwa, umpigiae hana salio lakutosha

    Pole sana. Hata mimi nimeshapata jibu kama hilo na nilipouliza nikaambiwa kwamba unayempigia yuko nje ya nchi. Na kweli huyo mtu alikuwa Nairobi. Kumbe Tigo wakishagundua kwamba unatumia simu toka nje ya nchi wanakuweka "roaming" bila hata kukuuliza. Huu ni wizi na unapaswa kuchukuliwa hatua...
  2. A

    Wahaya mmelogwa na nani? mji wa Bukoba umekanda sana

    Mlalamikaji amesahau jambo moja: watu hawa hujali vijijini kwao kwanza, mjini baadaye! Kama anataka aende vijijini aone watu wanavyomwaga radhi! Hakuna mkoa nchi hii uliojengwa vijijini kama Kagera -vijiji kama miji vile!
  3. A

    Kawambwa & Lukuvi walimzunguka Pinda juu ya mapendekezo ya kamati ya kuchunguza kufeli form iv 2012

    Hapa nafikiri kuna tatizo kubwa, tena sana! Kama ukweli ndio huo basi wahusika wakiubali kubeba dhamana na hehima ya Taifa hili kwa kuonyesha msimamo tofauti na wanasiasa uchwara tulio nao. Wajumbe makini wote wa Tume watangaze kutokubaliana na kilichotangazwa na wajiuzuru nyadhfa zao! hapo...
  4. A

    Treni ya kasi Tanzania

    Ni heri umaskini wa mfukoni kuliko umaskini wa kichwani! Kama nchi hii tungekuwa maskini wa mfukoni tungekuwa na nafuu!!
  5. A

    Kauli ya Maaskofu kwenye Kikao na Rais Jakaya Kikwete kilichofanyika Ikulu 23.04.2013

    Nina hakika uwazi huu sasa ndio utakaoliokoa taifa. Wakati wa kufichaficha mambo umekwisha, nchi imeanza kuzama tayari! Tuwashukuru viongozi wetu hawa kwa kujitoa muhanga na kueleza ukweli. Ningependekeza hatua inayofuata, baada ya Rais kukutana na wale wa dini nyingine, wakutanishwe wote...
  6. A

    Msaada wakuu kwa mwenye key za Kaspesky Antivirus 2013 anisaidie

    Kwani huyo mtu atakayekupatia key yake atakuwa hajaitumia? Labda kama ana ya kompyuta tatu na hajaitumia mara zote tatu, zaidi ya hivyo haitakusaidia kwani ukiitumia tu inairegister kompyuta yako huko kwao na kwa hiyo haiwezi kuwekwa kwenye kompyuta nyingine ispokuwa hiyo tu!!
  7. A

    Tanzania hakuna Proffessor wala Chuo Kikuu ( Wote wasanii tu na Ujanja ujanja tu)...

    Tafuta habari kabla hujatangaza kutokujua kwako! Mwaka juzi Nobel Prize ilichangiwa na watu kadhaa, mmojawapo akiwa wa UDSM: na huyu ni Pro Z. Yanda wa IRA. Prof Lipumba ni Mshauri wa Uchumi wa Kimataifa. Uliyajua hayo? Huko nje unakosifia ni maprofesa wote wanafanya kazi moja?
  8. A

    Tanzania hakuna Proffessor wala Chuo Kikuu ( Wote wasanii tu na Ujanja ujanja tu)...

    Pamoja na jazba ambazo tunaweza kuwa nazo ni vizuri tukatafuta ukweli kabla ya kutoa maoni yetu. Sio kweli kwamba Tanzania hakuna Prof aliyewahi kupata Nobel Prize! Kwa taarifa yako, Nobel Prize ya mwaka juzi ilichangiwa na watu kadhaa akiwemo mmoja wa UDSM! Tukimuacha huyo, Prof Lipumba ni...
  9. A

    Kuna sheria tofauti katika kuhukumu kesi ya uchochezi

    Nafikiri mwanzisha uzi huu analo jibu ambalo hataki kuelewa au kukubali! Jibu ni kwamba mmojawapo kati ya washtakiwa hawa hana kosa lolote (achilia mbali kuwa na hatia!), na mwingine ameonekana kuwa na hatia mpaka hapo atakapojinasua kwa ushahidi. Wanaofungua mashtaka vilevile wanajua kwamba...
  10. A

    Wabunge wa CHADEMA mnakera sana

    Pamoja na kwamba kila mtu ana haki ya kutoa maoni yake kuhusu busara na nidhamu ni nini, mawazo hayo yakitanguliwa na chuki ya wazi tayari yanakuwa yamekosa mashiko! Ni dhahiri kuwa msemaji hapo juu ana walakini katika kuwahukumu wengine!
  11. A

    Lecturer part 2

    Kwa kuwa sasa umelifikisha kwenye utawala inabidi vilevile uwape na timeline. Hii ni kwa sababu wanaweza wakakuchezea kesi yako ikachukua muda mrefu na kwa hiyo ikakosa maana. Kama hujawapatia huo ushahidi (kama nguo zilizochanwa) ni vizuri ukakaa nazo kwa sababu wao hawana utaalamu wa kufanya...
  12. A

    Sijashiriki kurekodi mkanda wa video unaomwonesha ndg Lwakatare

    Huyu Bwana ni mtu mwema sana kwani ametegua kitendawili ambacho polisi wangejidai kuficha! Kumbe mambo yako wazi! Mkanda wenyewe ulionekana tangu mwanzo kwamba kuna jambo linafichwa. Itakuwaje kipande kizima anarekodiwa mtu mmoja tu, hao wengine kwa nini wanasikika lakini hawaonekani? Na huyo...
  13. A

    Hongereni walimu, mishahara juuu!

    Sio rahisi kwa srikali inayoogopa kukaa na kushauriana na walimu iwaongezee mapesa yote hayo! Kama ni kweli basi huo utakuwa ni mwanzo wa mapinduzi ya kifikra au ishara ya wakubwa kuogopa nguvu ya umma. Kama wameweza kupuuza amri ya mahakama hakuna kinachoweza kuwatisha! Lakini ngoja tusubiri...
Back
Top Bottom