Nakubaliana na mleta mada kwani hili ni suala muhimu sana. Kwa hali ilivyo sasa sioni uwezekano wa madaktari peke yao kutoa tamko kwamba wanarudi kazini. Suala hili linahusisha pande mbili Serikali na Madaktari. Tatizo ninaloliona ni serikali kuamua kufunga uwezekano wa majadiliano kwa...
Ni mchango wa hiari. Wewe kama huhitaji kuchangia nyamaza kimya. Hatuko hapa kujadili yeye amechangia nini kwa wengine. Usihukumu kwani wewe nawe utahukumiwa.
Nashauri watu wanapoanzisha mada yoyote waweke 'titles' zinazobeba ujumbe uliopo na siyo kujaribu kuvuta hisia. Tusimwumbie daktari hisia na hofu zetu. Tuache madaktari wanaomtibu ndiyo waeleze maendeleo ya mgonjwa na siyo kila mtu kurusha hewani kitu anachohisi au kuwaza. Iwapo tunaamini ukuu...
Nashauri suala hili lisipelekwe kisiasa. Tangazo litolewe kwenye vyombo vya habari kama ambavyo tayari imekwisha fanyika. Mchago upatikane katika misingi ya hiari na upendo tu. Watu wasijaribu kujinufaisha kupitia suala hili. Tuepuke agenda za siri.
Mahakama inaingiliwa pale jambo hili linatakiwa kujadiliwa bungeni ili ushauri sahihi upatikane. Kutoa maamuzi na kuyatekeleza kabla mahakama haijahukumu hakuiningilii mahakama. Hayo ni maajabu! Bunge iliunda kamati kufuatilia jambo hili, lakini bunge hilo hilo halipaswi kupokea taarifa ya...
Kuna siku Mungu atapatiliza uovu wote unaofanyika hata sirini. Mungu awanusuru hao wanaotaka kutolewa kafara ili kuuficha ukweli. Haki na kweli ya Mungu itawale katika taifa letu!
Tuwaombee madaktari wanaomhudumia ili Mungu awape hekima na maarifa katika kushiriki kazi ya Mungu wapate kuokoa maisha ya huyu jemedari. Tuongeze maombi kwa ajili ya Dr. Ulimboka, mkono wa Mungu wa uponyaji uwe juu yake. Kwa Mungu hakuna lisilowezekana! Tusikate tamaa.
Nimefurahishwa sana na mikakati ya JK kuimarisha ukaguzi wa mahesabu ya Serikali na kwa kuweka kila kitu wazi. Naamini hili litasonga mbele, na wahusika wataendelea kuifanya kazi yao kwa uadilifu na umakini. Ila bado sijaelewa kama waziri mkuu hakuijua mikakati hii ili kuweza kutoa ufafanuzi huo...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.