Hawa wanasiasa wapiga domo mkandarasi yuko na mkataba ndani ya mkataba kila kitu kimeelezwa tena kwa vifungu vya sheria mpaka ucheleweshaji na namna mkandarasi atakavyo adhibiwa (LD- Liquidated Damage) anapotokea mwanasiasa anapiga domo bila kuangalia mkataba unasema nini ni kama anatafuta...
Kila mwaka wa Fedha zaidi ya 500b zinatengwa/pitishwa kwaajili ya manunuzi ya magari iweje huyu Dc aseme wanakosa magari wanaazima kwani yote mbona ni ya umma
Huwa wanapewa malengo ya makusanyo kutoka kwa kamishina wa kodi kupitia meneja wa mikoa ya kikodi kila mwezi kwahivyo mameneja nao huwakimbiza wakuu wa vitengo hasa domestic revenue wayafikie malengo ya makusanyo waliyopewa ndo maana mameneja wa mikoa ya kikodi huwa mbogo wanapowadai...
Utaratibu upi wa kibinadamu hakuna mfanyabiashara aliye tayari kulipa kodi kwa kupenda bila kubanwa na sheria amini nakwambia pale Kkoo ni mfano tosha mfanyabiashara hakupi risiti anakuletea mtu wa kukuuzia hiyo risiti ya kutembeza mzigo kutoka Kkoo ukigoma anakwambia ni bora asiuze kwa hali...
Labda kwakuwa hayupo kwenye biashara ndo maana anayaongea hayo ila ukweli ni kuwa kufungia akauntil za bank za wafanyabiashara (Urgency notes) kupo pale pale hasa kama unadaiwa na hulipi kwa muda mrefu asidanganye umma. Wafanyabiashara siku zote hawapendi kulipa kodi huo ndio ukweli kuendelea...
Hakika hili suala la bima kwa wote linahitaji akili kubwa maana regressive tax huwa ni mzigo mzito kwa wenye kipato duni au wasio na kipato na kingine kwa ufanisi upi serikali inaweza simamia hayo makusanyo maana kama hapo awali pesa zimechotwa kwenye mfuko (NHIF) na hazilipwa mpaka leo...
Huo ufanisi wa kumudu kuendesha huo mfuko kwa ufanisi utakuwepo? Maana CAG anaeleza kwenye ripoti yake kuwa serikali imekopa pesa nyingi kwenye huu mfuko mpaka leo hii haijarejesha sasa tuendelee kuamini serikali haitarudia madudu iliyofanya huko nyuma kuchukua pesa za mfuko? Kingine kwanini...
Uko sahihi jinsi Watanzania na serikali ilicyo ni bora utaratibu ukafanyika hivyo maana huko mbeleni itakuwa majanga serikali haina ufanisi wa kuendesha shirika lofoten la biashara na likapata na likatoa huduma kwa viwango ni bora kuwahi sasahivi tumeona mwendokasi, Tazara, TTCL, shirika la...
Sio kazi wala wajibu wa waziri kusitisha/kukatisha mkataba wa mkandarasi maana upo kisheria na taratibu za kusitisha mkataba zipo ndani ya mkataba utaratibu huu hupelekea serikali kushtakiwa kutokana na kukiuka mkataba na kupelekea hasara chonde mawaziri hebu punguzeni mihemuko. Mikataba ya...
TTCL walipaswa kuwa mbele ya muda na wangekuwa mbali sana hasa kwenye hudum ya Internet kiukweli kwasasa Internet sio anasa tena bali huduma ya muhimu kama sio lazima wangejikita kuboresha huduma zao kila mtu angependa kuunganishwa nao.
Tatizo linaanza mpka wakupatie huduma hiyo lazima usote...
Inabidi wakulipe na riba kwa mujibu wa sheria ukitazama 'clauses' za mkataba lazier zitakuwa zimeeleza kuhusu hilo maana haipaswi kuzidi siku 20 toka umeomba malipo ikizidi hapa unayo haki ya kuwadai riba kwa muda waliokucheleweshea.
Navyoandika hapa naelewa uhalisia wa mambo sio kwamba nimesimuliwa hakuna cha madeni wala nini pesa hazipo huo ndo uhalisia miezi 8 imekatika wakandarasi hawajalipwa kazi zilizofanyika mwaka jana hata wanaofanya kazi kwa sasa hakuna dalili za kulipwa huo ndo ukweli tuache siasa kwenye uhalisia.
Hili ni kweli hazina kumekauka kau miradi haina pesa licha ya mafungu ya bajeti kupitishwa wakandarasi wengi wanalia njaa toka mwaka jana hakuna malipo ukifanya kazi na Serikali kwa sasa yakupasa uwe makini sana vinginenvyo kama ungaunga mwana hakika unafunga biashara. Sio Tanroads wala Tarura...
Yani hili nalo tatizo kubwa kazi wanataka zifanyike tena wanakupiga pressure ya hali ya juu na vitisho juu kuwa watampa mtu mwingine kazi kimbembe ukija kwenye malipo utawekwa pending mpka ujute kiufupi kufanya kazi na serikali kwa sasa unahitaji kujiuliza mara mbili mbili maana malipo utasubiri...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.