Ndg,
Inawezekana serikali haina pesa. Maamuzi yanayofanyika na watendaji wetu ni ya kushangaza, mfano miezi michache iliyopita posho za wabunge ziliongezwa leo hii unawaambia madaktari hamna pesa ya kuwalipa vijisenti kidogo vya kujikimu, hawawezi kukuelewa.
Ni kazi nzuri anafanya mh Mwanry, kama kweli anaamini anachokisimamia basi wote wanaohusika na matumizi mabaya ya pesa ya umma wachukuliwe hatua za kisheria. Kinyume na hapo anachokifanya yataonekana maigizo mbele ya umma wa WaTZ.
Rasilimali za nchi zinafaidisha watu wachache na nyingi kubebwa na wawekezaji chini ya utawala tulionao. Akina mama wajawazito wanajifungua kwenye hali duni kwenye zahanati zetu, wengine hupoteza maisha, mazingira duni ya kazi ktk sekta za afya, elimu, magereza, usalama wa raia. Matatizo ya waTZ...
Wananiboa Wanafiki waungao mkono hoja eti asilimia mia kwa mia. Wakati wana mambo mbalimbali ya kuchangia. Hii inaonyesha ni jinsi gani walivyo kariri hata common sense hawana.
Utachangia hoja yale unayodhani yataiboresha kwa manufaa ya Watz. Huwezi kuunga mkono hoja 100% alafu ukawa na jambo...
Kama upande mmoja wa muungano unataka kujitenga hamna haja ya kung'ang'ania. Hata ndoa, wanandoa mmojawapo akichoka inabidi mwingine akubali yaishe japo ahadi alikuwa mpaka kifo kiwatenganisha. Kwa mantiki hiyo basi hapatakuwepo na kizuizi, Wazenj kuwa na serikali yao kwa amani alikadhalika...
Rais kashindwa kuisimamia serikali na watendaji wake. Wanaoweza kudhubutu wamekuwa wakisema serikali inayumba. Maamuzi ya jeshi kuongoza nchi kwa kipindi cha mpito ni muafaka kabisa.
Huyu OCD ni kielelezo cha watawala wetu walivyolewa madaraka. Ulevi wa madaraka ni mbaya sana kuliko wa pombe maana mlevi wa pombe zikimtoka anafanyakazi inavyotakiwa, lakini mlevi wa madaraka ulevi haumtoki mpaka apoteze madaraka aliyo nayo. Iwe isiwe utawala wa namna hii una mwisho wake...
Jenga hoja yako vizuri, kwani gazeti hili linasifika kwa habari na makala motomoto juu ya mustakabali wa taifa letu. Bila kuonyesha unafiki huo utaonekana hapa JF hapakufai.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.