Mkuu huwezi kuchangia bila neno 'kugegeda'? Maana hadi kero kwenye comments zako. Hivi unajua madhara ya kurudia rudia maneno? Ni kwamba unabatizwa jina. Kuanzia sasa wewe ni Mr. Kugegeda.
Kama wakala alikuwa hapokei simu wasingeweza kukurudishia hela japo kwa wakati huo kiasi kama hicho kinakuwa kimezuiliwa kwenye akaunti ya wakala. Kumbuka wapo pia wajanja wanaotoa hela kweli na kudai hawajatoa, je wakirudishiwa si wakala atakula hasara? Next time jaribu kuwa makini maana kuna...
Kwa ufupi nenda maeneo husika na uonane na madalali utaweza kupata nyumba kwa urahisi. Angalizo kuwa makini na madalali maana wapo ambao siyo waaminifu.
Unajua hasira inaweza kukupelekea kufanya maamuzi yasiyo sahihi. Ukute ni gari la mkopo na mkopo wenyewe hujaumalizia au umehenya miaka zaidi ya kumi ukidunduliza visenti vyako halafu jamaa anakuburuza bila ya hata kusema samahani inauma niaje!
Yaani haijulikani hawa watu walikuwa na nia gani na dereva daladala. Too sad. Kama angekuwa mtu mkubwa hapo tungesema tusubiri ripoti ya tume maana kila jambo ni tume.
Nimepita hapo sasa hivi na kukuta umati mkubwa wa watu. Inasemekana watu wawili wasiojulikana wakiwa kwenye pikipiki walimfyatulia risasi dereva daladala kwa kutumia bastola na kutoweka.
Dereva daladala alishindwa kulimudu gari na baadae gari kuangukia mtaroni na dereva kupoteza maisha. Polisi...
Mtoto akizaliwa hawezi akachukua chakula mwenyewe na kuweka mdomoni. Mlezi atamlisha chakula na baada ya muda mfupi mtoto ataweza kula mwenyewe. Unaweza ukasoma history, kiswahili au geography mwenyewe ukaelewa lakini siyo Programming.
Ni bati nzuri kwa muonekano na ukiziangalia tokea mbali huwezi kuzitofautisha na vigae. Nimezipenda na ninataka kuzinunua kwa ajiri ya kuezekea nyumba yangu. Kuna rafiki yangu kaniambia siyo nzuri kwani huwa zinavuja hata upate fundi wa aina gani. Mwenye kuzifahamu vizuri naomba ushauri.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.