Huwa najiuliza kwani Arusha barabara ni moja tu ya kufanyia kazi? Ukitoka KIA mpaka kufika Sakina utakutana na kundi la askari sio chini ya watano kila baada ya kilometa moja au 2!! Unajiuliza mbona mjini kuna barabara nyingi lkn wote wamejazana barabara moja tu????
Suluhisho ni kuhakikisha msanii hatoi wimbo kabla ya kuupitisha Basata na wausikilize na kama kuna mashairi yasiyo na maadili basi msanii aambiwe akayaondoe. Maana wimbo ukishatoka huwezi kuuzuia!!
Baraza la Sanaa la Taifa kwanini mmekuwa na kigugumizi kwenye muziki usio na maadili. Siku hizi nyimbo nyingi zina matusi, hazina maadili au zinachochea mmomonyoko wa maadili lkn cha kushangaza zinapigwa kwenye vituo vya redio na Televisheni.
Watoto wetu wanaimba nyimbo za ajabu kwa kuwa...
Unaweza ku push kujiletea maendeleo kaka lkn sio kujenga barabara ya lami. Mfano watu wamejenga culverts maeneo mengi tu, lkn linapokuja suala la barabara ya kiwango cha lami, si suala la wananchi.
Pia, nakubaliana na wewe hata mbunge wa upinzani ni mtanzania, lkn siasa za kiafrika unazijua...
Mh. Samia, jimbo la Ukonga jijini Dar es Salaam kwa maoni yangu ndio jimbo lenye barabara mbovu kuliko jimbo lolote. Barabara zetu zote ni mbovu yaani ni kama tumesahaulika au tumeikosea Serikali. Barabara ya kutoka Banana kwenda Kivule hadi Msongola ni mahandaki. Kitunda mwanagati ni mahandaki...
Nazungumza na mwanangu hapa sasa hv, anasoma shule binafsi, anasema walimu hawafuati ratiba, maana unakuta somo ambalo halipo leo mwalimu wake ndio anakuja darasani na anasema usipokuwa na daftari lake unapigwa. Kwa kweli wizara ya elimu iziangalie hizi shule binafsi. Mwanangu mpaka anapinda...
Juzi nimeenda hospitali moja binafsi kumpeleka mtoto wangu akiwa na severe constipation, akahitajika afanyiwe Enema. Lkn cha ajabu nikaambiwa NHIF doesn't cover Enema, yaana kale ka chupa cha dawa Enemax hakipo kwenye bima. I had to pay 20k huku roho ikiuma. Bima gani hata dawa ndogo hivi hazipo?
Kwani huu Mwenge upo wizara gani? Hiyo wizara haina bajeti? Mwenge unajulikana na gharama zake zinajulikana, kama Serikali inaona umuhimu wake kwa nini Wizara husika isiutengee bajeti?
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.