Muswada wa sheria ya mapitio ya Katiba ulikuwa na maudhui ya kuundwa tume ya kukusanya maoni ya wananchi katika kuelekea kupata Katiba Mpya. Kwa hiyo bado fursa ipo kwa wananchi kujadili masuala mbalimbali likiwemo hili na mihimili ya dola pindi tume itakapoanza kazi ya kukusanya maoni.
Jamani hivi kwanini mnapenda kusema uongo? Kwamba Redio Mwangaza FM. ndio chanzo cha habari hii si kweli kabisa.Mimi hapa nilipo nasikiliza redio hii kuanzia saa 2.00 na hakuna kitu cha namna hiyo.Haipendezi kwa watu wazima kuwa waongo jamani. Kama kuna source nyingine,sawa,lakini sio Redio...
Mdau nakushukuru,nimekisoma hicho kipengele na kukielewa vema.Na kwangu nadhani hoja kubwa iko hapa,nanukuu"5. Kamati Kuu inaamini kuwa pamoja na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba kupitishwa, bado kuna fursa za kisiasa na kijamii katika kujenga mwafaka wa kitaifa juu ya haja, nia, mchakato na...
Mbona katika tamko hili sioni kipengere cha kuunda kamati teule ya kuonana na Mh.Rais Kikwete? Au hiyo kamati teule ya kamati kuu ya CDM ndio inatarajia kuyapeleka haya maazimio kwa JK? Na kama ndivyo,je tutarajie nini wakati moja ya maazimio ya kamati kuu linazungumizia udikteta wa CCM na...
Mdau mimi binafsi napenda nikupongeze kwa uchambuzi makini juu ya tafrani hii iliyojitokeza. Kimsingi nakubaliana na hoja zote katika makala yako.Ni hoja zinazojielekeza kwenye uhalisia wa mambo na wala sio ushabiki ndani yake.Sasa, najua sio lazima kila mtu atakuunga mkono maana ni hulka ya...
Mdau mimi binafsi napenda nikupongeze kwa uchambuzi makini juu ya tafrani hii iliyojitokeza. Kimsingi nakubaliana na hoja zote katika makala yako.Ni hoja zinazojielekeza kwenye uhalisia wa mambo na wala sio ushabiki ndani yake.Sasa, najua sio lazima kila mtu atakuunga mkono maana ni hulka ya...
Kwa utaratibu wa zoezi la kuhesabu kura, kimsingi wanachokifanya tume ya uchaguzi ni kutimiza wajibu tu kwa kuwa hawawezi kuja na matokeo tofauti na yale ambayo tayari vyama vya siasa vilivyoshiriki uchaguzi huo wanayo kupitia mawakala wao.
Mie nilitegemea mdau utakuja na orodha ya wakuu wa mikoa wapya walioteuliwa maana tetesi zilizopo ni kwamba JK anatarajia kuwatangaza wateule hao wapya jioni ya leo!
Ni kweli mdau,katika hali ya kawaida unaweza usielewe kipi ni kipi katika swali ulilouliza. Kimsingi,uanziswhaji wa maeneo mpya za kiutawala una hatua zake kabla ya kuanza rasmi. Moja ya hatua muhimu ndio hii tunayoiona hapa. Kwanza kabisa wananchi wa huwa ndio wanaotoa mapendekezo kwa mamlaka...
Kimsingi sina tatizo sana na hoja ya kurejesha mafunzo ya JKT kwa mujibu wa sheria.Ni kweli kwamba ziko faida kadhaa za kupitia kwenye jeshi hilo kama wengi walivyoweza kubainisha. Hatahivyo, si sahihi kupuuza hoja za kuwepo kwa upungufu/udhaifu mkubwa sana katika uendeshaji wa mafunzo hayo.Na...
Nimeguswa na mtizamo wako mdau kuhusu Mh. Shibuda. Sishawishiki kuamini kwamba eti Mh.huyu alitumwa na CCM kwenda CDM kwenda kuvuruga.Na hii ni kutokana na ukweli unaojengwa katika historia ya harakati za kisiasa za comrade huyu. Kwa wenye kufuatilia kwa karibu siasa za hapa nchini hasa ndani ya...
Ni vizuri tukakumbuka kwamba fedha hizi walizopewa sio ruzuku. Fedha hizi ni mikopo inayotolewa na mabenki kwa waheshimwa hawa kwa ajili ya ununuzi wa magazi kwa udhamini wa ofisi ua bunge. Kwa hiyo ni hiari kwa wabunge wa zamani na hata hawa wapya kuchukua au kutokuchukua fedha hizo kwani...
Hapana nadhani hapa umepoteza kumbukumbu. Ni kweli kwamba kuna wakati fulani wakati wa utawala wa Mzee Mwinyi,aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini. Wakati huo JK alikuwa Naibu Waziri wa Wizara hiyo. Hata hivyo, inasemekana mh. huyu baada ya kuona mambo yanenda ndivyo...
Nakushukuru Mdau kwa kuliweka wazi hilo la uhusiano wa nguvu ya umma na tawala zenye kufuata utawala wa sheria na kuzingatia misingi ya haki za binadamu, Tanzania ikiwa mojawapo. Inashangaza sana unapoona kwamba hata wasomi wazuri tu, wengine ni wahadhili wa taasisi za elimu ya juu wanashindwa...
Cha msingi hapa tuhakikishiwe kwamba mh. huyo ni kweli kabisa kwamba hakuripoti halmashauri nyingine yeyote na kwa maana hiyo basi hajawahi kushiriki kupiga kura katika chaguzi za viongozi wa halmashauri. Kinyume cha hapo basi tusubiri timwili lingine huko Arusha.
Mdau, binafsi nakupongeza kwa kuliona hilo na kuona kwamba ipo haja ya kutoa angalizo kwa kile ulichokisikia kupitia redio hiyo inayomilikiwa na taasisi ya dini ya Kiislam.
Kwangu mimi, cha msingi ninachokiona kwenye mada yako ni kuhusu uchochezi wa kidini unaofanywa na Redio hiyo na maafa...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.