Wadau, heri ya mwaka mpya 2018.
Naomba msaada tutani; - Ni nani hawa waliokuwa kwenye bodi ya TTCl mwaka 2005? Bila shaka Mkapa Benjamin alikuwa rais wakati huo. Lakini hao board members walikuwa ni akina nani hao watanzania, hasahasa huyo mwenyekiti wa hiyo bodi alikuwa ni nani? Naombea tu...
Nani hasa walikuwa ni wahusika wa hili sakata? Yaani mwenyekiti wa bodi kipindi hicho cha 05/08/2005 na hao wenzake wanne walikuwa ni akina nani? Naona walimtaja mmiliki wa hisa moja wa nje lakini ilipikuja kuwataja wabongo Omar Nundu akapotezea hiyo.
Hivi ndiyo kitu inaingia akilini,na si ile mambo ya Prof Kabudi.Unafanya mabadiliko ya sheria za madini kisha unasema hazitahusu mikataba ambayo nchi iliingia zamani na wavunaji hawa wa madini yetu,huu ni uchizi.Unataka kwenda ku'negotiate mini na wezi?
Upigaji upo kwenye vyama vyote si CCM, si Chadema kwa kutaja tu hivi viwili kwasababu ya wingi wa wafuasi.Na waaminifu wapo kwenye wapo kwenye vyama vyote tena wengi wa kutosha Magufuli kaaminiwa na watanzania, na hakuna jinsi angeweza kuwa rais wa nchi bila kupitia chama chochote kati ya...
Mkuu Lunyungu, ninasikitika sana jinsi ulivyojitoa ufahamu kwenye hii issue na kuanza kumpiga madongo Lawrence Mafuru huku ukweli wa rekodi za kichunguzi ukimuonyesha kuwa ni msafi kuliko wengine wote hao.
Sijui ni Msemwa yupi unayemuongelea hapo juu, sijui ni yule alikuwa NDC miaka ile au...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.