Acha kuandika mambo ya kipuuzi, hasa Taifa linapokuwa na shughuliki kubwa kama msiba huu wa kitaifa. Kama huna kitu cha maana cha kuandika kwa nini usikae kimya??
Uongo. Dar es salaam inaongoza kwa kuwa na watu wanaoshinda na njaa au kushindia mihogo ya kutafuna. Unachukulia hiyo nayo kama sifa ya uchumi wa kati??
Voda ni kampuni ya matapeli. Wanauza airtime kwa wateja, kisha wanachukua tena hizo air time walizouza na kuzimiliki wao. Nina hakika matumizi yangu ya maneno matapeli ni sawa kabisa: yaani kujipatia kitu usichostahili au kwa njia za uanganyifu. Wanafanya hivyo almost kwa wateja wao wote kupitia...
Chadema mnaipa nguvu nyinyi wenyewe kwa woga wenu. Kuna vyama vingi tu vya siasa, lakini kila siku mnaongelea Chadema tu, kwa nini? Kwa nini msioongelee CUF ya Lipumba instead? Acheni woga wenu. Chadema haiwezi kufa kwa kuizuia kufanya siasa. Chama kinakufaga kwa kupuuzwa na wanachama wengi...
Hamtaki tu kukiri kwamba Chadema imewashinda. Hata sasa wakati imefungwa mikono na miguu yote, bado inaendelea kuwadunda; na mnaiogopa kama nini. Nafikiri semeni ukweli: Chadema is too powerful for you. Weka huu uzi wako kisha urudishe hapa wakati kila chama kitakaporuhusiwa kufanya siasa...
KANYAMA,
Mambo mazuri huwezi kuchanganya na mabaya. Sasa tuamini lipi: CCM itashinda kwa kishindo kwa sababu imetekeleza vzr sera zake, au kwa sababu serikali imezuia vyama vingine kufanya siasa? Lipi kati ya hayo mawili wewe unaloona litaisaidia CCM kupata ushindi wa kishindo? Unapiga porojo...
Sheria si tumejiwekea wenyewe? Hata mtu ukimkamata mtu anaua red-handed, kumhukumu kifungo hapo hapo, ni lazima afikishwe mahakamani na asikilizwe kabla ya kuhukumiwa, right? Hata kazini ni hivyo hivyo. Huwezi kutoka huko ulikotoka ukamfuta mtu kazi. Hiyo itakuwa ni maisha ya banana republic...
China hawapo kwenye hiyo list? Mbona miradi yote ya ujenzi wanapewa China? Kwa hiyo ni sahihi kusema Wachina wanakuja kwetu kuchuma na si wabia wa maendeleo kama tuavyosema kila siku? Yaani tunapewa fedha toka Ulaya na Marekani, kisha Mchina ndiye anakuja kuzichukua!
Tunahangaika nini wakati sisi ni nchi tajiri? Si tukae tu kimya? Kwami tukinyimwa hizo fedha au Makonda akizuiwa Marekani Tanzania haitakuwa nchi ya viwanda??
Kwani kinachofanya nyumba zipande bei ni nini? Wewe ukikaa kule Sinza kulikosongamana kama mabanda ya mbuzi, kuna hadhi ya kulipa sh hata 30,000 kwa mwezi? You are being so unfair. Naona Dar inawalemaza sana akili. Waulize waliohama kutoka Dar na sasa wanaishi Dodoma. Watakwambia real experience.
Kila mtu anasema Dodoma shida, lakini hamsemi shida gani. Acheni kuishi kwa mazoea. Mikoa mingi iko vizuri sana kuliko Dar. Ni kutofahamu tu. Hakuna mkoa wenye standard ya chini ya maisha kwa sasa kama Dar.
Wangetakiwa wampeleke Rais mbele kidogo tu ya hiyo barabara ya kwenda Kitunda ili akaone jinsi wananchi wake wa huko wanavyoishi maisha mazuri. Barabara hiyo ina mahandaki hatari! sasa yapata miaka 4 ina hali hiyo hiyo na haijawahi kufanyiwa matengenezo. Huko wanaishi asilimia 90 ya wakazi wa...
Nafikiri tunaandika mawazo mengine ovyo ovyo. Kanisa ni kitu Holy. Litajitafakari vipi? Nafikiri ulichotakiwa kusema ni viongozi (Hasa sema Kiongozi) maana hawa ndio sisi binadamu tunaokosea na kuomba msamaha kila siku. Hakuna sababu ya mtu yeyote kutumia kosa la mtu mmoja (hata kama ni kweli)...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.