nimerudi ndugu,unalolisema halina ukweli hata kwa aslimia 0,ulomtaja hana mume mie nna mume mtu wa mbeya,ulomtaja anamtoto molato mie mtoto wangu mswahili kuanzia rangi mpaka nywele,ulomtaja mwanae ana miaka saba wangu anamiaka 14....ila yeye ndo mwanzo wa mimi kuuliza swali langu lakini...
unanihukumu mpendwa kwa kusema nna kiburi...kuhusu mchungaji kiukweli mpaka sasa nilikuwa najidanganya kuwa atabadilika leo,kesho masiku yanakata ila nnalazimika kulifasnyia kazi hilo kwa sasa,umeniacha kidogo hapo mwisho kwenye msamiati
nashukuru mpendwa wala hajaisha ladha ndo kwanza anawika...ukizingatia ujana wa mwanaume unaanza na miaka 40 sasa yeye ana mmoja zaidi kuufikia...ila nadhani akinihitaji anapaswa abadilike na acheze nafasi yake kama mzazi kwa kijana wake,na analielewa hilo
ni wake mpendwa mahali tunakoishi ukipata mtoto mwanaume anapima na kuhakikisha kabisa kuwa ni wake halafu anasign,nae alipitia yote hayo na anauhakika kwa aslimia mia moja kuwa ni wake...hakuna shaka juu ya hilo
du nashukuru kwa ushauri mpendwa,ila elimu,kazi,wapi tunapoishi siwezi kupataja kwa sababu ni mambo binafsi zaidi.hiyo ya kula ilikuwa kabla sijamtenga maana kwa sasa kuna muda mrefu sana haelewi hata tunakula wakati gani
kuhusu suala la mtoto kama wake au sio ana uhakika aslimia mia kuwa ni wake,ila sielewi ni aina gani ya mzazi au ni wale wanaume wanaodhani watoto wanachukua mapenzi yao..kwa kweli niko njia panda
nashukuru mpendwa tuko pamoja kwa hili,ila nashangazwa na baadhi ya majibu ya wachangiaji humu,kwani mwanaume kutoa pesa ya matumizi,kuwatembeleA NDUGU ZANGU NDIO MAJUKUMU YAKE YA MSINGI,naomba muelewe silalamikii hayo ila nnacholalamikia ni hii tabia ya mtu kujivua jukumu lake kama mzazi hilo...
nashukuru mpendwa maendeleo ya mtoto shule ni mazuri sana namshukuru mungu kwa hilo,ila tatizo ni pale wanapoelezwa kuelezea kjuhusu familia ndipo huwa ngumu kwake na huanza kuchora vitu vya ajabuajabu kuonyesha yanayosawiri ubongo wake kuhusu suala zima la familia,kinachonisononesha na kunipa...
nashukuru kwa kunielewa mpendwa naona wachangiaji wengine wamebaki kunilaumu tu bila kujua nna mateso kiasi gani moyoni mwangu,huwezi jua nilitamani kiasi gani kuishi maisha ya ndoa inayompendeza mungu,watoto wenye furaha na amani ya mwili mpaka akili..mategemeo yangu yameyeyuka kama barafu pua...
kwa miaka minne hatujakutana kabisa ila kabla ya hapo ilikuwa kwa mbinde sana ndo maana nikahama chumba...hamu yangu ya kukutana nae ilipotea muda mrefu sana
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.