Search results

  1. Bams

    Tanzania tuna miaka 63 ya Uhuru lakini kimaendeleo, kisiasa na kidemokrasia tuko juu kuliko Haiti iliyopata uhuru miaka 220 iliyopita. Hongera CCM

    Kweli ujinga ni sifa kama ilivyo ufupi au urefu. Fikiroa mtu analinganisha nchi ambayo eneo lake ni kama ukubwa wa mkoa mmoja wa Tanzania na nchi nzima ya Tanzania. Tanzania 945,087 sq. Km Haiti 27,560 sq. Km Tanzania population 65m Haiti population 11.45m Tz GDP per capita $1,080 Haiti...
  2. Bams

    CDF Mstaafu Mabeyo ametaka kufikisha ujumbe; je, wananchi tumeuelewa ujumbe?

    Kauli ile ya Samia kuwa eti katiba ni kijitabu tu, kwa nchi za waelewa ilitosha kabisa kwa yeye kuondolewa mara moja kwenye kiti cha Urais. Katiba uliyoapa kuilinda unaidharau na kuiita kuwa ni kijitabu!! Kama huheshimu katiba, unaongoza nchi kwa kufuata nini? Rais hajui kuwa bila katiba...
  3. Bams

    CDF Mstaafu Mabeyo ametaka kufikisha ujumbe; je, wananchi tumeuelewa ujumbe?

    Madaraka yamempofusha kiasi cha kukosa kupata kwa yale ambayo yalitaka kimtokea.
  4. Bams

    Inawezekana tuna watu wasio na uwezo katika nafasi wanazozitumikia?

    Kwanza marehemu hawezi kulaumiwa kwa kutaka kupelekwa kwao au hata angetamka chochote muda huo. Katika hali kama hiyo ya kukielekea kifo, mgonjwa anasemehewa kwa chochote anachoweza kusema.
  5. Bams

    CDF Mstaafu Mabeyo ametaka kufikisha ujumbe; je, wananchi tumeuelewa ujumbe?

    Tukio lile la yeye Samia kutaka kuporwa mamlaka ya kikatiba ilitosha kabisa kwa yeye kuona umuhimu wa kuwa na katiba mpya yenye nguvu isiyo na mianya ya kuichezea. Lakini hali imekuwa tofauti. Tumebahatika mara moja kwa sababu ya hekima ya CDF. Je, tutaendelea kubahatika ikitokea tena na tena...
  6. Bams

    CDF Mstaafu Mabeyo ametaka kufikisha ujumbe; je, wananchi tumeuelewa ujumbe?

    Ni miaka 3 imepita tangu Rais Magufuli afariki. Ni jambo la kawaida, hasa siku ya maziko au wakati wa kutangaza kifo, kutolewa taarifa za kina za mazingira ya kifo cha marehemu, na kama pengine marehemu alitoa kauli yoyote. Haikuwa hivyo kwa Hayati Magufuli. Wengi walipenda na walikuwa na...
  7. Bams

    Je, Hayati Magufuli alikabidhi nchi kwa jeshi?

    Siyo kila Rais anapougua, nchi inaachiwa kwenye uongozi wa mtu mwingine. Kasome vizuri katiba ya nchi, ndiyo utaelewa. Kama Rais ataugua zaidi ya miezi 6 kwa kiasi .cha kushindwa kutimiza wajibu wake, ndipo anapotakiwa kukasimisha madaraka yake kwa wale wanaotajwa na katiba. Rais Magufuli...
  8. Bams

    Hatimaye Dotto James aonekana hadharani

    Umeandika ujinga gani huu? Ulitakiwa uandike hao CHADEMA wamefanya kisasi gani ili watu wajue. Lakini kwa namna hii uliyoandika, unaonesha uwezo mdogo wa akili katika kujenga hoja.
  9. Bams

    CDF mstaafu Mabeyo amelikoroga, Makamu wa Rais ndiye alitakiwa kuwa mtu wa kwanza kila hatua kujua afya ya Rais

    Kwa hali aliyokuwa nayo marehemu wakati huo, ilikuwa ni wakati delicate sana. Hofu ilikiwa kwamba wabaya wake wangeweza kuitumia kummalizia. Ndiyo maana wakuu wa vyombo vya usalama wote walikuwa pale ili kuwa na uhakika kuwa hali yake mbaya ya kiafya haitumiwi na mahasimu wake. Hivyo hata...
  10. Bams

    CDF mstaafu Mabeyo amelikoroga, Makamu wa Rais ndiye alitakiwa kuwa mtu wa kwanza kila hatua kujua afya ya Rais

    Kwa hatua kama hiyo, kilichokuwa muhimu zaidi ilikuwa ni maisha yake ya baadaye, yaani maisha baada ya kifo. Ndiyo maana alitaka zaidi viongozi wa kiroho kuliko mwingine yeyote. Tunafundishwa kuwa katika ufufuo hakuna hata familia wala ndugu wa damu, wote huwa ni sawa kama alivyo mwingine yeyote.
  11. Bams

    CDF mstaafu Mabeyo amelikoroga, Makamu wa Rais ndiye alitakiwa kuwa mtu wa kwanza kila hatua kujua afya ya Rais

    Tusilaumu tu, twende kwenye uhalisia. Kuna wakati, hata kwenye familia, nani apewe taarifa kwanza juu ya hali ya mgonjwa kuzorota au kifo, hutegemea zaidi wewe mwenyewe umejiweka karibu kiasi gani na huyo mgonjwa au marehemu. Kama huwa unaenda kumwangalia mgonjwa kila mara, unapenda kujua hali...
  12. Bams

    Habari za Kifo cha Magufuli zilivyonifikia nikiwa Gerezani

    Mwanadamu hastahili kuishi au kuwa huru kwa hisani ya mwanadamu mwenzake. Kama mtu amekosea, kuna taratibu zilizowekwa katika jamii, ndizo zinazotakiwa kufuatwa, na siyo vinginevyo. Kuhakikisha watu hawaonewi, Rais Samia ni wajibu wake wala siyo hisani au huruma. Tunaposema kuwa Rais Samia...
  13. Bams

    Habari za Kifo cha Magufuli zilivyonifikia nikiwa Gerezani

    Mdude na Lisu, kuishi kwao mpaka sasa, ni kwa sababu Mungu aliamua kwaonesha wanadamu kuwa yeye akitaka mwanadamu asife, inakuwa hivyo. Waliompiga risasi Lisu, walijiaminisha kuwa kwa namna ile walivyomchakaza, alikuwa tayari amekufa. Alipofikisglhwa hospitali wakajiaminisha kuwa hata kama...
  14. Bams

    Habari za Kifo cha Magufuli zilivyonifikia nikiwa Gerezani

    Ukiishatambua kuwa pamoja na mengine yote, iwe ni madaraka, utajiri, au umaarufu wowote, bado wewe ni mwanadamu ambaye upo sawa na mwingine yeyote katika mwanzo na mwisho wako, hakika utaheshimu utu na ubinadamu wa mwenzako. Kila mwanadamu, bila ya kuangalia alizaliwa mazingira duni au ya...
  15. Bams

    Jesca Magufuli achangia Ujenzi Nyumba ya Katibu UVCCM Wilaya ya Chato. Asisitiza Kumuenzi Hayati Magufuli

    Anamaanisha Bashite aliyekokota zero kabisa, halafu akaenda kidato cha 5 kwa kutumia cheti cha Makonda.
  16. Bams

    Jesca Magufuli achangia Ujenzi Nyumba ya Katibu UVCCM Wilaya ya Chato. Asisitiza Kumuenzi Hayati Magufuli

    TANU YOUTH LEAGUE ilikuwa inawalea vijana kuwa wazalendo, lakini UVCCM ya leo inawafunza vijana kuwa majambazi ma mafisadi kupitia siasa. UVCCM ndiyo chanzo cha wasiojulikana kupitia green guard. Ukitaka kuijua UVCCM ya leo, mtazame muuaji Makonda, jambazi Sabaya, fisadi January and the like...
  17. Bams

    Kwenye Utawala wa awamu ya 5 Bashiru Ally na wateule wengine wa Rais walijipa Utukufu kuliko hata Mitume wa Mungu

    Kumbe huelewi hata tofauti kati ya mada na jukwaa!!
  18. Bams

    Hizi ni dalili kuwa CCM hawamtaki Rais Samia?

    Mambo yaliyopunguza sana kuaminika kwa Rais Samia, ni pamoja na suala la kuwapa bandari DPW na kuyapa makampuni ya huko Uarabuni hifadhi za Taifa. Jambo hilo limeleta wasiwasi mkubwa kama Rais ana dhamira ya kulinda rasilimali za nchi kwa maslahi ya sasa na ya baadaye ya Taifa. Mbarawa, Rostam...
  19. Bams

    Hayati Magufuli aliweza kuwatisha waovu, mifumo iliamka kufanya kazi

    Niliambiwa na mmoja wa watu waliobambikiwa kesi za uhujumu uchumi, wakati wa malipo yale yaliyolazimishwa na marehemu kuwa washtakiwa wote wakiri kosa, ndipo nilipoamini kuwa nchi hii hakuna wa kumwamini!! Jamaa aliambiwa kuwa ameisababishia Serikali bilioni 1. Kwenye bargain ili aachiwe...
  20. Bams

    Kwa imani ya Kikatoliki, Hayati Magufuli alibahatika kupata Kifo chema

    Mazingira yake wakati wa toba yake yalikuwa yanamwezesha kuwafikia hao aliowakosea? Hekima ya Mungu siyo ya mwanadamu. Yule jambazi aliyesulibiwa msalabani pamoja na Yesu, hakuna aliposikika akiwaomba msamaha aliokuwa amewakosea. Yeye alisema tu, "..... sisi tunapokea malipo ya matendo yetu. Ee...
Back
Top Bottom