Search results

  1. W

    Nahitaji Majogoo ya Kisasa ili Nipate Vifaranga Chotara

    Habari wakuu, Nahitaji majogoo wa kisasa ili wapande kuku wa kienyeji kupata vifaranga chotara. Kwa mwenye nao hasa maeneo ya Mwanza anijulishe tafadhali ili niweze kununua kutoka kwake.
  2. W

    Mgao wa umeme ukiendelea, Simbachawene kutoteuliwa Cabinet ya Magufuli!

    Sasa mbona hawajibishwi mkuu? Sasa kama inajulikana hivyo na hali ya umeme ni tete kiasi hiki bado tuendelee kususbiri hadi aje awajibishwe na Magufuli kweli?
  3. W

    Machemli, mbunge wa CHADEMA, ahamia ACT Wazalendo

    Mleta mada, kwenye huo mstari wa tatu neno la mwisho kwenye hiyo tweet kuna tusi kubwa mno hapo. Nadhani kuna kosa la kiuandishi kwa huyo aliyetweet. Hili ni tatizo kubwa.
  4. W

    Majibu kwa wote wanaomtuhumu Lowassa kwa Ufisadi

    Mkuu ile orodha ya mwembeyanga ilikuwa na majina zaidi 10 na wengine ndo wenye madaraka makubwa nchini hadi hivi sasa. Kwa nini Lowassa tu ndo mwenye kusemwa vibaya zaidi kuliko hao wengine?
  5. W

    Updates: Mchakato na Matokeo ya kura za maoni ya Ubunge CHADEMA nchini kote

    Hongera zake Jay wa mitulinga!!
  6. W

    Nimeupenda ustaarabu wa John Pombe Magufuli

    Hoja nyepesi sana hizo. Huwezi kumpima mtu kufaa kwenye nafasi kubwa kama ya Rais kwa kutumia vigezo hivyo unavyovisema. Kama wengi wetu tuna mawazo kama haya basi inaweza tosha kujieleza ni kwa nini nchi yetu ni masikini kiasi hiki licha ya utajiri mkubwa uliopo ndani ya milki yetu.
  7. W

    IGUNGA - Bila Mwl. Kashindye CHADEMA inajichimbia KABURI

    Haya ndo yanayosemwa na jimbo la Geita Mjini mkuu! Rogers Ruhega ambaye ndiye aliyepeperusha bendera ya Chadema mwaka 2010 na kuwapa CCM ushindani wa kutosha ameambulia nafasi ya 3 kwenye kura za maoni!! Na nimeambiwa yanayosemwa mtaani ni haya haya kwamba walioshinda wamepiga goli la mkono...
  8. W

    Mabalozi wa CCM watakiwa kuandikisha Sensa ya Wanachama

    Sasa kama hii unayoisema ndo sababu na kwa vile wewe unasema umefanya kazi huko, hebu nipe maelezo kuhusiana na huu mstari ili na mimi nielewe: ''Fanya hima ni muhimu sana kinyume cha hapo watu wako hawatapiga kura''.
  9. W

    Moses Machali ajiondoa NCCR-Mageuzi na Kujiunga ACT-Wazalendo

    Ila hii ni hatari sana kwa chama cha upinzani kuwa bize kukibomoa chama kingine cha upinzani. Ingependeza sana kama mpambano huu ungekuwa ni kati ya chama cha upinzani na chama tawala.
  10. W

    Tundu Lissu ahutubia wakazi wa Geita Mjini katika viwanja vya Nyankumbu

    Hata wewe ni walewale tu, sababu zako ni nyepesi sana!
  11. W

    Pombe Magufuli azoa wanachama 882 UKAWA

    Ni shida mkuu!! Labda wao wanajua kuhesabu zaidi kuliko wewe. Au inawezekana macho yao yanaona zaidi kuliko yako! Wanastahili kuonewa huruma tu hao na propaganda zao hizo.
  12. W

    Tundu Lissu ahutubia wakazi wa Geita Mjini katika viwanja vya Nyankumbu

    Sababu zako ni nyepesi mno mkuu!! Uraisi ni zaidi ya vitu vidogo vidogo kama hivyo!! Kwa nini usifikirie kwa mfano kupata mtu ambaye atakuja kulinda rasimali ya gesi kwa maslahi mapana ya watanzania wote? Magufuli amesema nini wakati wanapitisha kwa dharula hiyo sheria ya gesi hivi karibuni...
  13. W

    Irene Uwoya naye ajitupa kwenye siasa, Achukua fomu ya ubunge viti maalum Tabora

    Tatizo kuna wabunge wameifanya kazi ya ubunge ionekane ni rahisi sana na ndo maana naona kila mtu sasa anataka kuelekea huko! Sasa kama mimi natakiwa kusema ''ndiyoooo'' au ''hapanaaa" kwa kitu ambacho pengine hata sikijui undani wake kwa vile kimeletwa kwa hati ya dharula pale bungeni shida iko...
  14. W

    Nisikilizeni CHADEMA: Tatizo ni UKAWA, Hili ndilo chaguo langu la rais wa 5

    Mkuu makala yako ni ndefu lakini nimeisoma yote. Unachokisema ndo ukweli wenyewe. Umeeleweka.
  15. W

    Elections 2015 Lowassa: Tusipopata mabadiliko CCM Wananchi watatafuta nje ya CCM

    Hivi hii sheria mpya ya makosa ya mtandao haijaanza kufanya kazi kweli?
  16. W

    Joshua Nassari apata ajali ya chopa

    Hizi sasa nadhani labda ni chuki zako mkuu tu na hakuna kigezo kingine unachokitumia. Pointi yangu ni kwamba hata kama akiacha kutumia chopa na akapanda gari, bado nalo linaweza kupata ajali vie vile!! Naamini tutakuwa tumeelewana hapo.
  17. W

    Joshua Nassari apata ajali ya chopa

    Mkuu hiyo ni ajali tu kama zilivyo ajali zingine!! Hata angezungukia jimbo lake kwa gari bado angeweza kupata ajali vile vile ambayo labda hata ingemletea madhara makubwa kuliko hata hayo aliyoyapata kwenye hiyo ajali ya chopa.
  18. W

    Tanzania: Petroleum Act, 2015 (Muswada wa Mafuta na Gesi) - Uchambuzi

    Sasa mkuu watu wakiwa wameshasaini mikataba ya miaka 99 kwa kutumia sheria hiyo kama itakuwa ni mbovu itatusaidia kweli kama taifa? Hata kama itakuja kupitiwa upya? Inawezekana tukawa tunarudi kule kule kwenye asilimia 3 ya dhahabu!!
  19. W

    Uandikisha wa BVR Igoma Mashariki (Kanda maalumu) ni mizengwe tupu

    Mkuu ukumbuke kuna kipaumbile kinatolewa kwa wazee, walemavu, wamama wenye watoto na wajawazito!!
  20. W

    Profesa Lipumba kuunguruma Muhambwe leo

    Huko aliko sidhani kama atafanya shughuli za wananchi kwa kutumia hiyo elimu yake aliyonayo na ambayo wewe imekufanya umwite kijana msomi!! Kuna maprofesa tayari wako huko lakini wanayoyatetea na kuyapitisha kwenye vikao vya bunge yanamshangaza kila mtu.
Back
Top Bottom