Kupinga kwa hoja zenye mantiki ni sawa. Kuwafundisha vijana kukubali kila kitu ni upumpavu.
Kutukana (viongozi au yeyote siyo sawa na ni kosa la jinai).
Tunatakiwa kufundisha watu wetu wakubaliane na mambo ya faida kwao, jamii na taifa kwa ujumla, kupinga yale yote yaliyo kinyume chake. Huo...
Kinachotakiwa ni mabadiliko ya mfumo wa utawala kwa faida ya wengi.
Iwe CCM au upinzani, itategemea nani atawahi. Mama Samia kaja na 4R, Makonda kajaribu ktatua kero kwa uwazi, Nchimbi na Mongela kutatua kero kimya kimya huku upinzani ukitoa hoja za kutatua matatizo na changamoto kwa njia zao...
Tatizo la vyeti siyo dogo kama ilivyoaminiwa kwenye serikali ya Magufuli. Lina uhusiano wa moja kwa moja na kura feki, serikali feki, mahakama feki, watu feki (wasiojulikana),.....
Huwezi kufukia shimo kwa kuchimba jingine halafu ukajisifu umeondoa tatizo.
Hizi ni fikra mbaya kwa mustakabali wa jamii na taifa kwa ujumla.
Wazalendo wapo na pia tunatakiwa tuwajenge wengine kifikra (wenzetu, watoto wetu na vizazi vijavyo).
Kwa hiyo, unachotakiwa ni kutaja au kushawishi hatua dhidi ya wezi na mafisadi kuambatanisha na vitendo vyao.
Katika idadi ya...
Usafiri bora huenda sambamba na mipango miji bora yenye miundombinu inayoendana na idadi ya watu.
Ni asilimia ndogo ya majiji na miji inayopangwa (iwe rasmi au siyo rasmi), na hiyo ni changamoto kubwa ambayo haitapata suluhu kwa urahisi.
Majiji yana njia mbili hadi nne za kuingilia bila...
Ni muhimu chama kurudi kwenye mstari na utaratibu wa asili wa maadili, uungwana utu na heshima kwa wote. Tabia za unyama na kujitoa ufahamu ili kupata teuzi ni upumbavu usiokubalika na sio sawa kwa mustakabali mwema wa jamii, chamachama, serikali na taifa.
CCM lazima iwe mfano wa kuigwa kwa...
Kazi ya kutatua kero na kufanya shughuli zilizopangwa kwa maendeleo ya wananchi ni ya serikali.
Chama kinaenezwa kwa kufundisha itikadi na sera ili wananchi wengi wavutiwe wajiunge.
Kama serikali haitekelezi sera na itikadi, itawajibishwa kwa vikao vya ndani na matokeo ya uwajibishwaji huo...
Aweso anapiga kazi vizuri.
Hata hivyo, kwa ujumla wake, wanasiasa ni walaji (consumers) ambao hula kodi za wananchi (kwa sababu siyo wazalishaji, yaani producers kwenye jamii au taifa).
Ili tupate maendeleo endelevu, kodi zetu zinatakiwa zielekezwe kwa wazalishaji (wakulima, wafugaji, watoa...
Mzalendo wetu maua yake yapo sana, Ila kwenye magari sikuona makali yake, hata mkurugenzi wa Geita ilionekana sawa tu.
Huu waweza kuwa mfupa uliomshinda fisi.
Mvua bado zinahitajika. Matendo ya binadamu kama kuingilia mtiririko wa asili wa maji (ujenzi wa mabwawa), kuishi sehemu hatarishi (kama mabondeni) na kutojenga miundombinu imara (barabara, reli, majengo,....) ndiyo chanzo cha matatizo.
Kwanza kabisa tumshukuru Mungu kwa kutupa mvua nzuri...
Serikali ya Tanzania na taifa kwa ujumla halina dini rasmi, Ila wananchi wana Imani zao.
Kwa hiyo, RC Makonda ana haki ya msingi kabisa ya kuamini na kuabudu.
Je tukio la maombi ni la kiserikali au kiofisi?
Hayo siyo mambo yake binafsi na Kadinali Pengo au kanisa?
Kuingilia shughuli zake za...
Kila raia, awe kiongozi au asiye na cheo ana wajibu wa kulinda jamii na nchi kwa ujumla.
Hakuna sababu ya kuitia hofu jamii kwa kutoa taarifa kama hizi hadharani, wasambazaji na wauzaji ni maadui wa ustawi wetu, hasa kwa vizazi vijavyo, wanatakiwa washughulikiwe na kumalizwa kimya kimya.
Kama...
Kuongeza, spika na bunge lake waweza kumuondoa Rais madarakani.
Hata hivyo, katika fikra za wabunge kuomba badala ya kuitaka serikali kufanya au kutimiza wajibu wake kwa wananchi, changamoto ni kubwa.
Kiongozi apatikane kwa utaratibu wa kugombea zaidi kuliko kuteuliwa.
Kama ikibidi kuteua, wawe watu wazima wenye uzoefu wa maisha katika nyanja mbalimbali badala ya sarakasi za siku hizi za kutafuta uteuzi.
Tafsiri ya greatness of a leader ni ka Afrika ni yule anayesumbua wananchi wenye uwezo kiuchumi warudi chini, hata kama nchi itakuwa masikini zaidi.
Fikra za kimasikini (kijamaa na kijima) hutukuza sana viongozi wanaozuia juhudi za mtu mmoja mmoja kuzalisha na badala yake kuendeleza kugawana...
Sijasema na siwezi kuwaza kuwa waachwe hivyo.
Jitihada zinafanyika na mabadiliko kutoka hali duni kwenda bora (maendeleleo) yapo. Changamoto ni kasi ndogo kutokana na tamaduni.
Jamii au nchi huendelea kwa kasi kutokana na tamaduni (fikra na vitendo) za wananchi wakazi wa eneo hilo.
Wananchi ndiyo TISS namba moja.
Hawa wafanyakazi wa TISS ni waajiriwa tu, hivyo kuvunja TISS ni wananchi kujielewa kwa kuwa active zaidi katika ulinzi wa nchi na uundaji wa serikali.
Ni muhimu sana kwa wananchi kujua kuwa wao wana haki ya kuwa TISS namba moja, vinginevyo kizazi chao cha baadaye...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.