Azori Gwanda yuko wapi? Aanze kwa kuhakikisha ukweli kuhusu 'kupotea' kwake unawekwa wazi. Familia yake wajue kama yuko hai au la, na warudishiwe mtu wao!
Anaitwa Haambiliki! Anajua amekosea, yuko uchi na kuchutama hataki! Kwani hajui kama amekosea? Anajua lakini kwa kauli yake, 'Mimi ni Jiwe'.
Sent using Jamii Forums mobile app
Jamani msilolijua nyamazeni. Mama Mahiga mwanawe ni mgonjwa sana, kitu kilichopelekea mama kuitwa aende kumuuguza. Alipofika Nairobi kuna karantini ya siku 14! Bado hajamaliza hata hiyo karantini mumewe anafariki ghafla, mwanawe yuko taabani. Ombeni yasiwakute. Huyu mama anapitia kipindi kigumu...
Kwa hiyo tuamini ya kuwa waliokufa mpaka sasa bado ni 16? Mnatufanya wajinga kiasi hicho? Katika siku chache binafsi nimepoteza watu watatu wa karibu. Mmoja kazikwa na Serikali jana, mwingine anazikwa na Serikali leo. Wa tatu kafariki leo asubuhi kwa changamoto ya upumuaji, hatujajua maziko yake...
Pole sana. Ndipo tulipofikishwa. Mhudumie mgonjwa wako sehemu nyingine kama ulivyoamua kumpeleka private. Mkirudi nyumbani kaeni ndani. Hakuna msaada kutoka kwa viongozi, jilinde mwenyewe na uwapendao!
Sent using Jamii Forums mobile app
Mama yangu kazaliwa na kakulia Kariakoo Mtaa wa Muhonda. Sasa hivi ndio tumemhamisha anakaa Magomeni Mapipa. Ana miaka 80. Kijijini nimpeleke wapi? Siyo kila mtu anayeishi mjini au anayeishi Dar ni mtu wa kuja. Wenyeji walikuwepo na wapo. Wageni rudisheni wazee wenu vijijini wenyeji tuacheni...
Pole sana. Ungewahi kumpeleka kwa daktari wa wanyama huenda wangegundua tatizo lake. Sasa hao watoto wake wasiliana na daktari wa wanyama haraka iwezekanavyo akupe ushauri wa uhakika.
Jaribu namba zifuatazo
0715 573747, 0712 660406, 0657 531212, 0767 989656. Hizo namba nilikuwa nazitumia kama miaka mitatu iliyopita, inawezekana zimebadilika. Ushauri mzuri zaidi jaribu kucheck kwenye Google huenda wakawa na latest information na contact details za uhakika zaidi. Wanaitwa Quiz...
Kuna agencies zinaweza kukusaidia. Sikumbuki jina vizuri lakini nafikiri Quizup (?) walikuwa na ofisi yao Kinondoni. Sisi walitusaidia sana wakatupatia mtu wa kumtunza baba yetu (RIP) alipokuwa mgonjwa wa kitandani na kuhitaji huduma kama hiyo. Mama yetu ni mzee asingeweza kumhudumia baba, na...
Kwetu sisi mama ni mtu muhimu sana kwa mtoto. Mama hasingiziwi, tofauti na baba (naomba msinirushie madongo). Siku hizi kuna DNA Test ya kuthibitisha vinasaba vya baba, lakini zamani kulikuwa hakuna namna ya kuthibitisha kuwa huyo anayetajwa kuwa baba wa mwana ni baba kweli au kasingiziwa. Kwa...
Yaani kesho mbali sana. Hiyo siyo dalili nzuri. Mtoto anapata kitu kinachoitwa fetal distress. Ikitokea hali hiyo madaktari wanakazana kumwokoa mtoto kwa maji ya uchungu au hata Ceasarian Section (Upasuaji). Nayajua, sikutanii, yalishatukuta. Kesho mbali sana mtoto asipocheza anaanza kukosa...
No, no, no. Imetosha, amewahudumia Wazee waliomlea na kumsomeaha. Hana deni kwa hao ndugu wa mama yake ambao hawakutaka hata kujiongeza wakati Wazee walipokuwa hai. Wapambane na hali zao na yeye akazane kujijenga mwenyewe na familia yake!
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.