Sasa nimejua Kwa nini Klopp alikuwa anatuyeyusha kusajili DM. Huyu dogo James MacOnell anaonekana kuwa na miguu SG8 kabisa.
Anajua kuingia uvunguni, anajua kuchungulia pa kupeleka mpira. Klopp anaondoka kaacha watu pale dimba la kati kama watano hivi.
Nenda baba kawasalimie Hispania!
Nenda...
Jinsi CJ17 alivyokuwa anazunguka pale uwanjani, alimpa kazi nyepesi sana Mc10. Hakika dogo amekuwa mtamu kama mcharo. Sijui kiwango cha maumivu aliyopata ni makubwa kiasi gani; yasije yakawa makubwa yakamrudisha nyuma tena.
Kuna dogo mmoja anatumia mguu wa kushoto. Nafikiri mechi kadhaa alizopewa nafasi. Naam! Ni Billy Koumatio Ana mwili mkubwa hivi, ni black. Yuko wapi? Profile yake inasemaje?
Mosdef hapa umekuwa mkali kidogo ingawa naelewa sababu ya kuwa mkali hivi..
Hata hivyo usivunjike moyo kutushirikisha experience yako ndani ya Anfield. Ni muda binafsi nimekuwa nikifuatilia makala zako hapa ambazo si za kishabiki.
Unajua hata jana kulikuwa na maelekezo. Sidhani kama Jarell alicheza faulo pale. Labda mnaojua mpira mnisaidie.
Mimi nimeona mguu wa Jarell ukiingia kati ya miguu ya mshambulizi wa Palace mara baada ya mpira kuchezwa.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.