Serikali yetu pendwa chonde chonde tupia jicho kwa barabara hii ya Wazo-Madale. Tuliambiwa iko kwenye budget ya 2016/2017 sasa mwaka umeisha. Kweli wakazi wa huku tunapata shida ya usafiri maana hata daladala wanaogopa kuleta magari yao. Bajeti ya mwaka ujao msitusahau.
Nimelipia kuunganishiwa (three phase-Dar es Salaam) umeme toka tarehe 18/4/ 2017 mpaka leo sioni dalili yoyote. Siku 30 za kusubiri zinatoa mwanya kwa mtu kupita mlango mwingine. Badilikeni, punguza hizo siku.
Kama mteja haitaji nguzo siku saba zinatosha kumpa umeme.
Kuamua kutumia cheti cha mtu mwingine ili atoboe kimaisha anaonyesha ni mpambanaji, sio mtu wakubweteka. Inawezekana mazingira yake ya kusoma hayakuwa mazuri kumwezesha kufaulu. Je hivyo vyuo vingine alifeli? Tatizo liko kwenye vita aliyoianzisha. Mwenyezi Mungu msaidie katika kazi hii.
Jamani tatizo la vyoo na bafu kwa hapa Dar es Salaam ni janga kubwa sana. Wenye nyumba wengi ni waroho wa pesa hata hawathamini maisha na afya za wapangaji wao. Unakuta mtu anapokea kodi ya laki moja kwa mwezi lakini kutenga kidogo ukatengeza choo kikawa na hadhi ya kutumiwa na binadamu unaona...
Inakera sana unaponunua kitu ukiomba risiti unaambiwa bado tunafuatilia EFD TRA. Nyie TRA kwani inachukua miaka mingapi kumpatia mtu hiyo machine. Mapato bado yanavuja sana wafanyabiashara wengi hawana hizo machine, wapeni bwana tutengeneze Tanzania.
Nauza Kuku kienyeji wenye uzito kati ya kilo 1.5 -2. kuna jogoo wachache na tetea wako 100. Bei ni sh. 15000 kwa kila mmoja. Tetea wameanza kutaga. Tuko Dar e salaam. Piga namba 0766302961 kwa maelezo zaidi.
Sio Airtel tu peke yao ambao ni wezi, hata VODACOM ni wezi tena wa mchana kweupe. Mtu unaunganishwa na mambo yao ya promotion za Jay bila kujua na unakatwa 300 kila meseji; unaweka hela kwenye simu usiponunua kifurushi baada ya dakika chache hela hakuna eti unakatwa za connection ya internet uwe...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.