Jambo la Msingi ni kumuombea heri marehemu, lakini hizi ngonjera za uaminifu, sijui usafi, upendo nk nk ni yeye tu ndiye aliujua ukweli wake.
Urais ni haki ya Mtanzania yeyote mwenye sifa na hakuwa na hakimiliki ya nafasi hiyo, hivyo kukosa kwake ni sawa na wale wengine walioukosa.
Moja ya habari kubwa kila yanapotangazwa matokeo ya mitihani ya kitaifa huwa udanganyifu unaofanywa na watahiniwa, hii ni kwa darasa la nne na Saba, kwa elimu ya msingi, kidato cha pili, nne na sita kwa elimu ya sekondari na hata kwenye vyuo vya taaluma mbali mbali.
Ni takribani siku kumi...
Nilivyoelewa article, wameonyesha chanzo kingine cha uzalishaji umeme safi ambacho ni rahisi lakini kitazalisha umeme mwingi zaidi kuliko vyanzo vyote vilivyopo
Moja ya ugonjwa wa nchi hii ni kutochangamkia fursa zilizopo kwa wakati muafaka, ajabu hatua huchukuliwa wakati tumepitwa na mabadiliko ya teknolojia.
Tulizembea kwenye uzalishaji umeme kwa kutumia mkaa wa mawe, ikaja oil and gas, na sasa upepo, hapa ni nchi kavu na baharini kote fursa zipo...
Nchi ya ajabu sana hii, badala ya kuitumia treni hiyo kama pilot project inayowapa majibu ya kuwepo mahitaji makubwa kwa huo usafiri jijini, wao wapo kupiga siasa.
Heri hizo njia za mwendokasi kutumika kama miundombinu ya usafiri wa treni kuliko hayo mabasi.
Mkuu,
Hiyo inawezekana kabbisa, anamaliza 1995, the 1996 anajiunga kwa diploma au cheti then diploma, vyovyote vile inawekana, the baada ya masomo ya chuo anafanya kazi hazina kama afisa, hivyo inawezekana masters akafanya 2000-2002. Hapo kumbuka kuna majukumu ya familia na mambo kama hayo...
Kashililika naye tatizo tu, kwani aliyetoa hizi taarifa za kukatishwa safari kwa huyo Mbunge ni vyombo vya habari au ofisi yake mwenyewe iliyosambaza mawasiliano yao na Mbowe!!!!
Ukitisha kura ya maoni leo hii, zaidi ya asilimia 70 ya Watanganyika watahitaji serikali tatu au kuvunjilia mbali muungano na hardly 50pc ya Wazanzibari watahitaji serikali tatu au kuvunja muungano, inayobakia itahitaji serikali mbili. Huu ni mtazamo wa mwanazuoni mmoja nikiwa katika mazungumzo...
Katika sera iliyotolewa Okt mwaka jana, suala la kuanzishwa huo Mfuko lipo kwenye sekta hiyo ya gesi na mafuta. Pamoja na huo mfuko pia inazungumzia kuanzishwa kwa Kampuni ya taifa ya uchimbaji gesi ambayo itakuwa kadiri muda unavyoenda, ni utaratibu uliotumiwa na Norway walipoanza uchimbaji...
Kesi za kashfa ni zaidi ya hapo, mdai atatakiwa kuthibitisha alivyochafuliwa na thamani yake katika jamii, na mdaiwa naye atatakiwa kuthibitisha ni jinsi gani jamaa asivyo na hiyo thamani anayodai kuwa nayo. Hapa ndipo kimbembe kilipo, kwani mdaiwa anakuwa na uwanja mpana zaidi, na ili...
Mbowe anazuga tu, hawezi peleka pua yake mahakamani kwani anafahamu atakavyoumbuliwa. Ugumu wa kesi za kashfa unatakiwa kuthibitisha usafi wake, na unaowashitaki wanathibitisjha uchafu wako!!!
Hii mbinu tu ya kufifisha mjadala wa usanii wanaoufanya, kuwaaminisha Watanzania kwamba wao ni wasafi...
Mtoi,
Nimesoma na kurudia mara mbili, bado siuoni uthibitisho wa kutengezewa hizo kashfa za ugaidi, ninachokiona hapa ni hisia zenu tu.
Unapokuja na allegations nzito kama hizo uthibitisho ni muhimu sana, lakini narration pekee haishawishi.
Pili, leo mnawanyoshea vidole vidole waandishi wa...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.