Baba, hayo madini yapo Tz pekee, wilaya ya Simanjiro pekee, hapo Mirerani tu. Kwa hiyo wacha ukuta ujengwe kwani sh . ngapi bana? Tumeibiwa mno, tumepuuzwa mno, wacha wajenge labda tutaokoa hii rasilimali yetu adimu. Jenga, jenga, jenga........ Bravo raisi wangu kwa uamuzi wa busara.
Kuna hili lingine linaitwa 'BASHA MUHANDIS' likiwa na maana ya Chief Engineer nalo lina mzizi kutoka lugha ya kiarabu, lakini hapa kwetu naona haliwezi kuwa na mshiko kwani lina ukakasi kidogo.
Shida ipo hapo mkuu wangu, huwa napata wasiwasi kuwa idadi ya watz wenye upeo wa fikra sahihi ni ndogo. Angalia muda unaopotea kwa watu hawa kwenda kusikiliza akadabladabla za hawa wanaojiita majina makubwa , upako, nabii, mlima wa moto n.k wangeutumia hata kulima tuta la mchicha wangeokoa...
Ubora wa mbegu unategemea sehemu shamba lilipo, hivyo ni vyema kuwasiliana na watalamu wa kilimo au maofisa ugani wa eneo lako ili wakushauri ipasavyo.
Jamani tuiache serikari ifanye kazi, waziri Mkuu si kichuguu kilichoota Dodoma eti kila wakati yupo huko tu, watanzania wengine pia wanahitaji huduma yake. Eti wawekezaji wangemfuata dodoma! kwa hiyo na hilo gari wangelazimika kulisafirisha kwa ajili ya mheshimiwa kujionea na kukagua kama...
Watu humu ndani wachache wanaokubali kukosolewa, tulishasema humu neno Amiri ndiyo UKUU wenyewe kwa hiyo si sahihi kusema 'amiri jeshi mkuu' bali inatosha tu kusema AMIRI JESHI.
Umemaliza, ingawa ni ukweli mchungu sana. Nikiwaambia hivyo watu huwa wanabaki midomo wazi, lakini si chochote bali ukweli. (Angalia 'Siku sita za uumbaji').
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.