Soonest? Labda baada ya kujihakikishia kuwa wewe na yeye manapenda kwa dhati na hamna nia ya kuchezeana na kufanya uhuni. Pia ni vyema mkaziangalia afya zenu mapema kabla humjajikuta mmeingia kwenye mahusiano ya kimapenzi yenye wimbi la majuto ya milele.
Hakuna ufahari wala sifa yoyote ya...
Pole kwa hizo changamoto Mjukuu wangu.
Binafsi, naona njia ya kuishi na mtu mgomvi ni kumuelewa na kuikubalia hali na tabia aliyonayo. Unahitaji pia kuwa mvumilivu na kuongeza ukaribu wako na yeye kujua chanzo au asili ya yeye kuwa mgomvi. Isije kuwa kauli zake na matendo yake kwa kiasi...
Mjukuu, sijui level ya upendo wako kwake ikoje, lakini kama unampenda kwa dhati, ni vyema kukaa naye na kuongea naye kujua ukweli wa hili jambo na kama ni kweli kujua nini hasa kilimsibu mpaka akaamua kuongeza makalio.
Kipeperushi ulichokiona juu ya meza yake si ushahidi wa kutosha kuamini...
Kaka pole sana kwa presha iliyokupata Ila kwa dunia ya leo ilivyo, hatupimi afya ya mtu kwa kumuangalia au kumuuliza, kama unahitaji mahusiano yenye amani na afya, suala la KUPIMA si la kubeza, unaweza kuishia shimo la hewa!
Nimepitia uzi wako haraka haraka nikajikuta najiuuliza maswali ya kipuuzi kama ifuatayo ...
Una uhakika wenye ndoa ndiyo wenye mapenzi ya uhakika? Haufahamu kuwa kuna wengine wameolewa tu kwa sababu ya umri kufika? Au wengine kwa sababu ya kutaka watoto? Au wengine kwa kutaka mali? Au wengine...
Nafikiri huenda malezi ya wazazi kwa kuacha kazi za ndani, upishi na majukumu mengine ya kazi za familia kufanywa na wasichana wa kazi. Wapo wengine wamekuwa bize mno na kazi za kujitafutia kipato na suala la kupika kwako ni kama kupoteza muda. Kuna baadhi ambao wamezaliwa wavivu na wazembe. Pia...
Sasa huyo si ameshakuwa mke wa mtu? Kama ni msaada unaweza kutoa kama kwa rafiki wa kawaida lakini siyo yeye kukufanya wewe ndo nyumba ndogo yake au ATM machine yake. Siku ukikamatwa ndo utajua ubaya wa kula vya watu!
Nakushauri, tafuta mwingine wa kwako, acha kupoteza muda na vya watu au...
Dogo, si ungemuuliza tu huyu mpenzi wako kuwa amejipangaje kwa sasa kuhakikisha kuwa akiwa mbali na wewe huko masomoni mapenzi yenu yatadumu na hayatatokea kama yalivyomkuta mwenzio aliyekutangulia?
Ila kwa maelezo yako, na kama kweli sababu aliyotoa huyo mpenzi wako ni halisi, basi ni kwamba...
Nimefikiria kipuuzi tu, nikapata sababu lukuki kama ifuatavyo
Hajui kutofautisha nafasi ya mpenzi na marafiki wa kawaida au
Inawezekana hajawaambia hao rafiki zake kuwa ana mchumba/mpenzi ambaye ni wewe na hayuko tayari kufanya hivyo sasa au
Ana mwingine ambaye anatambulika na hao rafiki zake...
Kiongozi, kichwa cha habari na maelezo ya ndani vinanitatiza! Unataka kumuacha kwa sababu hakuombi hela au unataka kumuacha kwa sababu ya UDUKUZI wake?
By the way, nafikiria jinsi ulivyomkaribisha huyo binti, naona kama something is missing kwenye huo uzi kuufanya uaminike.
Hapo juu mi nashauri ni bora wakaacha kabisa ....
Maana mapenzi huwa sijui ni kitu gani, hayana siri, iko siku tu wapenzi watajisahau na mambo kuvuja. Madhara yake nafikiri kila mtu anayafahamu; kufumaniwa kupigwa, talaka, ugomvi, kuambukizana magonjwa nk
Pole ndugu, tunakutakia kila la kheri katika zoezi hili. Nafahamu uchungu na adha ya kukaa bila ajira. Pitia pia Zoom Tanzania, BrighterMonday na mitandao mingine ya ajira pamoja na kuwasiliana na makampuni yanayowatafutia watu ajira, huenda kwa kudra zake Mungu akabahatika.
Hili suala ni gumu kidogo kulielezea ...
Wapo wanapata mizuka ya ki-ukweli na pia wapo wanaojifanyisha! Cha msingi mshauri mpenzio apunguze kelele kama wewe haupendezwi nazo!
Duuuu, hiyo sentensi juu imenishanga kidogo, watu 7? Labda inawezekana siyo michepuko kwa maana ya michepuko huenda ni meseji za utani wa ndani zinazosababishwa na kuzoeana na watu kupitiliza.
Huwa nashauri kila siku, ni vyema wapenzi na wanandoa kuwa na mipaka ya utani na mawasiliano na watu...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.