Madhara ya kutumia pombe ni makubwa kuliko inayoitwa faida.Wanywaji wengi wa pombe husahau kuhudumia familia zao,hujiingiza kwenye ufsika,wanakuwa na maendeleo duni,wanazeeka kabla ya wakati,wanapoteza heshima katika jamii,ni watumwa wa pombe wanawaza pombe usiku na mchana n.k.
Uamuzi wa kuzima local channels kwenye ving'amuzi vya DSTV,AZAM TV na ZUKU mmetukomoa sisi wananchi.Mngeachia tu,asiyetaka kulipia ajiunge na STARTIMES.Tangu mfunge hivyo ving'amuzi siangalii TBC wala siji kuwa mpenzi wa TBC
Tunataka uchaguzi huru.Msipindue maamuzi ya wananchi.Yaliyotokea Korogwe na kwingineko dhidi ya vyama shindani ni udhihirisho kwamba tuna safari ndefu ya kukomaa kidemokrasia.Haki ya wananchi inapokwa na kuacha uchungu ambao hatimaye siku ya siku utazaa maafa makubwa.Serikali iliyoko madarakani...
Kama mfumo huo utatekelezwa wanaenda kuua biashara ya makampuni ya simu na vile vile uchumi wa nchi utashuka.Mtu mmoja kuwa na line nyingi kunaongeza manunuzi na hatimaye kodi huongezeka.
Tatizo kubwa ambalo lilifanywa na bado linafanywa ni kuingia kwenye chaguzi kwa wapinzani wakidhani wanaweza kushinda chaguzi bila katiba mpya.Ni ndoto !!!.Ukombozi wa kweli kwa watanzania utatokana na kuwa na katiba mpya na siyo viraka vya katiba.Shituka mapema vinginevyo mtalia sana na mwisho...
Chonde chonde vyama vya upinzani unganeni pamoja kudai katiba mpya vinginevyo katika chaguzi zijazo mtakwama.Mkichelewa kudai katiba mpya ccm itaendelea .....
Askofu Kakobe ametoa hoja na kinachotakiwa hoja zake zijibiwe siyo kwa jaziba au matusi.Mtu mwenye busara hakurupuki kudandia hoja bali hutafakari kwanza.
Laiti kama Mtumishi wa Mungu Antony Lusekelo angekuwa anakiri makosa na kuomba msamaha angejiokoa yeye na kondoo anaowachunga,lakini kwa vile anakataa ni suala la muda tu ataumbuka.Mungu hapendi kuona kazi yake inaharibiwa na jina lake kutukanwa.
Shule nyingi zinatoa adhabu za kikatili.Sina hakika kama mwalimu wa sekondari ya Canaan iliyoko Mlowo,Mbozi kama anafahamu suluba zinazoendeshwa na walimu wake.Wahusika fuatilia shuke hiyo
Serikali ya JPM imeanza vizuri,lakini katika suala la kuzuia bunge kurushwa live serikali haijaona mbali,itaanza kuchukiwa.Tuko kwenye ulimwengu wa utandawazi.Kuminya uhuru wa habari hakutaisaidia serikali kinyume chake utaiharibu.Tumeanza kumkumbuka JK
Kusuasua kwa rais John Magufuli kutaja baraza la mawaziri kunatokana na utata wa uchaguzi Zanzibar.Je,anaweza kuunda baraza la mawaziri bila Zanzibar?.Hapa ndipo penye utata.
samwel Sita alikuwa kipenzi cha Watanzania,lakini alipoongoza bunge maalum la katiba na kukubali maoni ya wananchi kuchakachuliwa ndipo wananchi walipomwona hafai.Kwa aliyoyafanya wakati wa bunge maalum la katiba hafai kushika nafasi hiyo nyeti ya uspika wa bunge la jamhuri ya muungano
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.