Wakuu joining the army is serious business i hope you know that part of the application is the signing of your death bond, you can die in training or loose some vital part.
Good luckUANDIKISHWAJI
Askari
Mtu yeyote ataandikishwa kujiunga na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa sifa zifuatazo: -
· Awe raia wa Tanzania
· Awe na Elimu ya kidato cha nne na kuendelea na awe amefaulu..
· Awe hajaoa/hajaolewa
· Awe na umri kuanzia miaka 18 hadi 25
· Awe na tabia na mwenendo mzuri
· Awe na akili timamu na afya nzuri
Masharti ya Utumishi
· Askari atapewa nambari ya utumishi baada ya kufaulu mafunzo ya awali.
· Atalitumikia Jeshi kwa kipindi cha mwanzo cha miaka sita, baada ya hapo atafanya kazi kwa mkataba wa miaka miwili miwili kwa kibali cha Mkuu wa Majeshi.
Maafisa
· Bodi ya Uteuzi wa Maafisa (Officers Selection Board)
huwafanyia usaili askari wenye elimu ya kidato cha sita na kuendelea toka Vikosini na Shule za askari wapya (Recruitment Schools).
· Watakaofaulu masailiano hayo hupewa hadhi ya Afisa Mwanafunzi (Officer Cadet), na hupelekwa Chuoni (Tanzania Military Academy) kwa mafunzo ya uafisa kwa muda wa mwaka mmoja.
source: tpdf (dot) go (dot) tz

Reply With Quote


:
Chaguo ni lako.
Follow Us Here