JamiiSMS
  Show/Hide This

  Topic: ajira hizi hapa . angalia secretaiate ya ajira tar 26/6/2012 usiogope omba tu

  Report Post
  Results 1 to 6 of 6
  1. galagaja mtoto's Avatar
   Member Array
   Join Date : 24th May 2012
   Posts : 84
   Rep Power : 499
   Likes Received
   18
   Likes Given
   26

   Default ajira hizi hapa . angalia secretaiate ya ajira tar 26/6/2012 usiogope omba tu

   JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
   OFISI YA RAIS
   SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA
   UMMA

   Kumb. Na EA.7/96/01/B/183 29 Juni, 2012
   1   TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI

   Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma anakaribisha maombi ya
   Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi za kazi 569 mbalimbali kwa Waajiri
   (Taasisi za Umma) kama ifuatavyo:
   Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Wizara ya Maji, Wizara ya
   Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Katibu Tawala Mkoa wa Arusha, Iringa, Kigoma,
   Mwanza (Geita), Mara, Morogoro, Rukwa, Ruvuma, Tanga, Halmashauri ya Jiji la
   Mwanza, Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga, Lindi, Halmashauri ya Wilaya ya
   Chato, Chamwino, Chunya, Kahama, Kishapu, Kiteto, Kongwa, Kyela, Magu, Maswa,
   Mbozi, Meatu, Monduli, Mbinga, Mbulu, Mpanda, Msalala, Mpwapwa, Rufiji, Rungwe,
   Simanjiro, Shinyanga, Songea, Tandahimba, Ukerewe na Halmashauri ya Mji Njombe.

   Aidha, tangazo hili linapatikana kwenye tovuti zifuatazo: PUBLIC SERVICE RECRUITMENT SECRETARIAT - PSRS,
   Public Service Management na PMORALG - Home -

   NB: MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.
   i.Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania wasiozidi umri wa miaka 45.
   ii.Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
   iii.WAOMBAJI KAZI KWA NAFASI ZA AFISA MTENDAJI WA KATA DARAJA LA II,
   AFISA MTENDAJI WA KATA DARAJA LA III, AFISA MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA
   LA II, AFISA MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III NA AFISA MTENDAJI MTAA
   DARAJA LA III AMBAO WALIOMBA NAFASI KAMA HIZO KATIKA TANGAZO LA
   TAREHE 25 MEI 2012 HAWAPASWI TENA KUOMBA NAFASI HIZI
   iv.Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia
   katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za
   kazi kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.

   v.Nafasi ya kazi inayoombwa iandikwe katika kichwa cha habari cha barua na juu
   ya bahasha, kutozingatiwa hili kutasababisha maombi ya kazi kuwa batili.
   vi.Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye
   anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees)
   watatu wa kuaminika.
   vii.Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya kidato
   cha nne na kidato cha sita kwawale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu
   mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Viambatanisho hivyo vibanwe
   sawa sawa kuondoa uwezekano wa kudondoka/kupotea.
   - Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
   - Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
   - Computer Certificate
   - Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
   - Picha moja “Passport size” ya hivi karibuni iandikwe jina kwa nyuma.
   viii.“Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za
   kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS)
   HAVITAKUBALIWA.
   ix.Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa
   kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
   x.Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika
   utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo
   katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.
   xi.Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi zitapelekea wahusika watachukuliwa
   hatua za kisheria.
   xii.WAAJIRI WOTE WALIOPO NJE YA DAR ES SALAAM WANAOMBWA
   KUSAMBAZA MATANGAZO HAYA KWENYE MBAO ZA MATANGAZO NA
   MAENEO MENGINE.
   xiii.Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 14 Julai, 2012
   xiv.Aidha, uwasilishaji wa barua kwa mkono katika ofisi za Sekretarieti ya ajira
   HAURUHUSIWI.
   xv.Maombi yanaweza kuandikwa kwa Lugha ya Kiswahili au Kiingereza na yatumwe

   kupitia posta kwa anuani ifuatayo.

   Katibu, AU Secretary,
   Sekretariati ya Ajira katika Public Service Recruitment
   Utumishi wa Umma, Secretariat,
   SLP.63100, P.O.Box 63100
   Dar es Salaam. Dar es Salaam
   2


   Nafasi hizo (569) za kazi mbalimbali katika Utumishi wa Umma mbalimbali ni kama
   ifuatavyo:
   1.0 MHAIDROJIOLOJIA DARAJA LA II (HYDROGEOLOGISTS GRADE II ) –
   NAFASI 16
   Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Katibu Tawala Mkoa wa Geita
   1.1 MAJUKUMU YA KAZI
   · Kukusanya Takwimu, kutafiti pamoja na kutayarisha Taarifa za Kihadrolojia
   zenye maelezo fasaha ya kitaalaamu
   · Kujenga (installation ) na kukarabati vifaa vya utafiti wa maji chini ya Ardhi na
   kukarabati vituo vya kuratibu rasilimali za maji chini ya ardhi
   · Kusimamia uchimbaji wa visima vya maji na kuhakiki uwezo wa kisima kutoa
   maji. (Pumping Test)
   · Kukusanya sampuli za maji na udongo kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa
   kimaabara.
   · Kutathimini (monitoring )rasilimali za maji chini ya ardhi kwenye sehemu za
   kidakio cha maji ( sub catchment)

   1.2 SIFA ZA MWOMBAJI
   · Kuajiriwa wenye Shahada ya Jiolojia au jiofizikia na haidrolojia kutoka vyuo vikuu
   vinavyotambuliwa na Serikali.
   · Wawe na ujuzi wa kutumia Kompyuta.

   1.3 MSHAHARA
   Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS E.

   2.0 MHANDISI DARAJA LA II - MAJI (WATER ENGINEER GRADE II) – NAFASI 3
   Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Tawala Mkoa wa Tanga, Geita, Halmashauri ya Wilaya
   ya Shinyanga

   2.1 MAJUKUMU YA KAZI
   · Atafanya kazi chini ya uangalizi wa Mhandisi aliyesajiliwa (Professional engineer)
   na bodi ya usajili ya Wahandisi ili kupata uzoefu unaotakiwa.
   · Kufanya ukaguzi wa Miradi ya Maji
   · Kufuatilia utekezaji wa Sheria, Kanuni za Maji
   · Kutayarisha bajeti ya mwaka ya Maji
   · Kusimamia na kuratibu kazi za Maji zinazotolewa na makandarasi

   2.2 SIFA ZA MWOMBAJI
   · Kuajiriwa mwenye Shahada ya Uhandisi wa Rasilimali za Maji kutoka vyuo vikuu
   vinavyotambuliwa na Serikali. Wawe na ujuzi wa kutumia kompyuta.

   2.3 MSHAHARA
   Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS E kwa mwezi.
   3


   3.0 MHIFADHI WANYAMAPORI II – NAFASI 13 (IMERUDIWA)
   Nafasi hizi ni kwa ajili ya Wizara ya Maliasili na Utalii
   3.1 MAJUKUMU YA KAZI
   · Kufanya doria ndani na nje ya maeneo ya hifadhi au mbuga za wanyama
   · Kusimamia utekelezaji wa utaratibu wa uwindaji na utalii
   · Kulinda binadamu na mali zake dhidi ya wanyama hatari.
   · Kukusanya na kulinda nyara za Serikali
   · Kufanya usafi na ulinzi
   · Kubeba na kutunza vifaa vya doria
   · Kudhibiti uingiaji na utokaji wa watu na mali kwenye hifadhi
   · Kutunza vielelezo vya ushahidi vya nyara
   · Kudhibiti wanyamapori waharibifu
   · Kukagua vibali na leseni za matumizi ya wanyamapori.
   · Kudhibiti mioto mikali kwenye mapori.

   3.2 SIFA ZA MWOMBAJI
   · Kidato cha IV au Kidato cha VI
   · Wenye Stashahada/Astashahada ya Uhifadhi wa Wanyamapori kutoka Chuo cha
   Usimamizi wa Wanyamapori Mweka au Chuo kingine kinachotambuliwa na
   Serikali.
   · Waliopitia mafunzo ya nidhamu na ukakamavu yanayotolewa na vyuo vya
   wanyamapori watapewa kipaumbele. Wale watakaopata nafasi lakini hawana
   mafunzo hayo, watapewa mafunzo husika kama sehemu ya mafunzo ya
   “Induction”.

   3.3 MSHAHARA
   Kwa kuzingatia viwango vya Serikali ngazi ya Mshahara TGS.B na C kwa mwezi.

   4.0 MKUFUNZI MSAIDIZI DARAJA LA I (ASSISTANT TUTOR GRADE I) – NAFASI
   35
   Nafasi hizi ni kwa ajili ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
   4.1 MAJUKUMU YA KAZI
   · Kufundisha masomo ya fani mbalimbali zinazofundishwa katika vyuo
   · Kuandika mtiririko na mpangilio wa masomo
   · Kusimamia masomo ya vitendo
   · Kuwapima wanachuo wakati wa mazoezi na kwenye mitihani

   4.2 SIFA ZA MWOMBAJI
   · Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha Nne/Sita waliofuzu mafunzo ya Stashahada
   kutoka Chuo Cha Maendeleo ya Jamii (Rungemba au Buhare) au Chuo kingine
   kinavyotambuliwa na Seikali AU
   4


   · Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha Nne/Sita waliofuzu mafunzo ya Stashahada
   kutoka Chuo Cha Ufundi kinachotambuliwa na Seikali katika fani zifuatazo:
   i. Uashi (Masonry) - Nafasi 5
   ii. Useremala (Carpentry) - Nafasi 6
   iii. Uunganishaji Vyuma (Welding) - Nafasi 4
   iv. Ushonaji (Sewing)– Nafasi 5
   v. Ufundi Magari (Motor Vehicle Mechanics) – Nafasi 5
   vi. Umeme (Electrical) – Nafasi 5
   vii. Kompyuta (Computer) – Nafasi 5

   4.3 MSHAHARA
   Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS B. kwa mwezi.

   5.0 AFISA MTENDAJI WA KATA DARAJA LA II (WARD EXECUTIVE OFFICER
   GRADE II) – NAFASI 55
   Nafasi hizi ni kwa ajili ya Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto, Maswa, Mbulu, Meatu,
   Rungwe na Shinyanga
   5.1 MAJUKUMU YA KAZI
   · Atakuwa Mtendaji Mkuu wa Kata na kiungo cha Uongozi kwa Idara zote katika
   kata na atashughulikia masuala yote ya kata
   · Atakuwa Mhamasishaji mkuu wa Umma katika mikakati mbalimbal.i ya uzalishaji,
   mali, kuondoa njaa na Umasikini.
   · Atakuwa ni Katibu wa kamati ya maendeleo ya kata.
   · Ataratibu na kusimamia upangaji wa shughuli za maendeleo ya kata, vijiji na
   Mtaa.
   · Atatafsiri sera na kusimamia utekelezaji wa sheria ndogondogo katika Kata
   yake.Atamsaidia Mkurugenzi Kuratibu na kusimamia shughuli za Uchaguzi katika
   Kata.
   · Kumsaidia na kumwakilisha Mkurugenzi katika kusimamia maendeleo ya eneo
   lake.
   · Kusimamia utendaji kazi wa wataalamu na watendaji wengine katikangazi ya
   Kata.
   · Kuratibu na kuandaa taarifa za utekelezaji na kuziwasilisha kwa mkurugenzi na
   nakala kwa Katibu Tarafa.
   · Atakuwa mwenyekiti katika vikao vinavyowahusisha wataalamu na watendaji wa
   vjiji, na NGO’S katika kata yake.
   · Atakuwa Msimamizi na mratibu wa takwimu zote zinazokusanywa katika vijiji,
   vitongoji, na kata yake.

   5.2 SIFA ZA MWOMBAJI
   · Kuajiriwa wenye Shahada ya Sanaa yenye mwelekeo wa Sayansi ya Jamii
   (Social Sciences) Utawala, (Public Administration and Local Gorvernment),
   5


   Sheria au Sifa nyingine inayolingana na hizo kutoka Chuo chochote
   kinachotambuliwa na Serikali.

   5.3 MSHAHARA
   Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS D. kwa mwezi.

   6.0 AFISA MTENDAJI WA KATA DARAJA LA III (WARD EXECUTIVE OFFICER
   GRADE III) – NAFASI 68
   Nafasi hizi ni kwa ajili ya Halmshauri ya Wilaya ya Chunya, Kongwa, Kyela, Mbozi,
   Msalala, Mvomero, Shinyanga na Kishapu
   6.1 MAJUKUMU YA KAZI
   · Atakuwa Mtendaji Mkuu wa Kata na kiungo cha Uongozi kwa Idara zote katika
   kata na atashughulikia masuala yote ya kata
   · Atakuwa Mhamasishaji mkuu wa Umma katika mikakati mbalimbali ya uzalishaji,
   mali, kuondoa njaa na Umasikini.
   · Atakuwa ni Katibu wa kamati ya maendeleo ya kata.
   · Ataratibu na kusimamia upangaji wa shughuli za maendeleo ya kata, vijiji na
   vitongoji.
   · Atatafsiri sera na kusimamia utekelezaji wa sheria ndogondogo katika Kata
   yake.Atamsaidia Mkurugenzi Kuratibuna kusimamia shughuli za Uchaguzi katika
   Kata.
   · Kumsaidia na kumwakilisha Mkurugenzi katika kusimamia maendeleo ya eneo
   lake.
   · Kusimamia utendaji kazi wa wataalamu na watendaji wengine katika ngazi ya
   Kata.
   · Kuratibu na kuandaa taarifa za utekelezaji na kuziwasilisha kwa mkurugenzi na
   nakala kwa Katibu Tarafa.
   · Atakuwa mwenyekiti katika vikao vinavyowahusisha wataalamu na watendaji wa
   vjiji, na NGO’S katika kata yake.
   · Atakuwa Msimamizi na mratibu wa takwimu zote zinazokusanywa katika vijiji,
   vitongoji, na kata yake.

   6.2 SIFA ZA MWOMBAJI
   · Kuajiriwa waliohitimu kidato cha nne au sita na kuhudhuria mafunzo ya
   Stashahada yenye mwelekeo wa Sayansi ya Jamii (Social Sciences) Utawala,
   (Public Administration and Local Gorvernment), Stashahada ya Sheria au Sifa
   nyingine inayolingana na hizo kutoka Chuo chochote kinachotambuliwa na
   Serikali.

   6.3 MSHAHARA
   Kwa kuzingatia viwango vya Serikali ngazi ya Mshahara TGS C kwa mwezi.

   6


   7.0 AFISA MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA II (VILLAGE EXECUTIVE OFFICER
   GRADE II) – NAFASI 25
   Nafasi hizi ni kwa ajili ya Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa, Maswa na Rombo.
   7.1 MAJUKUMU YA KAZI
   · Atakuwa Mtendaji na Mshauri Mkuu wa Serikali ya Kijiji na Kamati zake katika
   Mipango ya Maendeleo ya kijamii na Utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo.
   · Atakuwa Afisa Mhasibu wa Serikali ya Kijiji na atasimamia mapato na matumizi
   ya Serikali ya kijiji
   · Atakuwa Mlinzi wa Amani na Msimamizi wa Utawala Bora katika Kijiji.
   · Ataratibu na kusimamia upangaji wa utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo ya
   kijiji
   · Atakuwa Katibu wa Kamati ya Halmashauri ya Kijiji.
   · Atatafsiri Sera, ataratibu na kusimamia utekelezaji wa Sheria ndogondogo za
   Halmashauri ya Kijiji.
   · Ataratibu na kuandaa taarifa ya utekelezaji wa kazi katika eneo lake na
   kuziwasilisha kwenye Halmashauri ya Kijiji na baadae kwenye kata .
   · Ataongoza vikao vya maendeleo ya Kijiji vitavyowahusisha wananchi na
   wataalamu waliopo kwenye eneo lake.
   · Atahamasisha wananchi katika kampeni za kuondoa njaa, umasikini, na
   kuongeza uzalishaji mali.
   · Atasimamia matumizi bora ya Nguvu kazi.
   · Atakuwa Kiongozi wa Wakuu wa Vitengo vya Kitaalamu Katika Kijiji.
   · Atasimamia ukusanyaji wa kumbukumbu za walipa kodi, wataalamu mbalimbali
   na NGO waliopo katika kijiji.

   7.2 SIFA ZA MWOMBAJI
   · Kuajiriwa wenye elimu ya kidato cha IV na VI waliohitimu Stashahada ya
   kawaida katika fani yoyote yenye mwelekeo wa Sayansi ya Jamii (Social
   Sciences) Utawala, (Public Administration and Local Gorvernment), Stashahada
   ya Sheria au Sifa nyingine inayolingana na hizo kutoka Chuo chochote
   kinachotambuliwa na Serikali.

   7.3 MSHAHARA
   Kwa kuzingatia viwango vya Serikali ngazi ya Mshahara TGS C kwa mwezi.

   8.0 AFISA MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III (VILLAGE EXECUTIVE OFFICER
   GRADE III) – NAFASI 181
   Nafasi hizi ni kwa ajili ya Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Kyela, Magu, Mbozi,
   Mbulu, Msalala, Meatu, Mvomero na Rungwe
   8.1 MAJUKUMU YA KAZI
   · Atakuwa Mtendaji na Mshauri Mkuu wa Serikali ya Kijiji na Kamati zake katika
   Mipango ya Maendeleo ya kijamii na Utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo.
   7


   · Atakuwa Afisa Mhasibu wa Serikali ya Kijiji na atasimamia mapato na matumizi
   ya Serikali ya kijiji
   · Atakuwa Mlinzi wa Amani na Msimamizi wa Utawala Bora katika Kijiji.
   · Ataratibu na kusimamia upangaji wa utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo ya
   kijiji
   · Atakuwa Katibu wa Kamati ya Halmashauri ya Kijiji.
   · Atatafsiri Sera, ataratibu na kusimamia utekelezaji wa Sheria ndogondogo za
   Halmashauri ya Kijiji.
   · Ataratibu na kuandaa taarifa ya utekelezaji wa kazi katika eneo lake na
   kuziwasilisha kwenye Halmashauri ya Kijiji na baadae kwenye kata.
   · Ataongoza vikao vya maendeleo ya Kijiji vitavyowahusisha wananchi na
   wataalamu waliopo kwenye eneo lake.
   · Atahamasisha wananchi katika kampeni za kuondoa njaa, umasikini, na
   kuongeza uzalishaji mali.
   · Atasimamia matumizi bora ya Nguvu kazi.
   · Atakuwa Kiongozi wa Wakuu wa Vitengo vya Kitaalamu Katika Kijiji.
   · Atasimamia ukusanyaji wa kumbukumbu za walipa kodi, wataalamu mbalimbali
   na NGO waliopo katika kijiji.

   8.2 SIFA ZA MWOMBAJI
   Kuajiriwa wenye Elimu ya Kidato cha Nne au cha sita waliohitimu Astashahada
   (Certificate) katika Fani yoyote yenye mwelekeo wa Sayansi ya Jamii (Social Sciences)
   Utawala, (Public Administration and Local Gorvernment), Astashahada ya Sheria au
   Sifa nyingine inayolingana na hizo kutoka Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
   8.3 MSHAHARA
   Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS B kwa mwezi.

   9.0 AFISA MTENDAJI MTAA DARAJA LA III (MTAA EXECUTIVE OFFICER
   GRADE III) – NAFASI 8
   Nafasi hizi ni kwa ajili ya Halmashauri ya Wilaya ya Kahama na Shinyanga.
   9.1 MAJUKUMU YA KAZI
   · Atakuwa Mtendaji na Mshauri Mkuu wa Serikali ya Mtaa na Kamati zake katika
   Mipango ya Maendeleo ya kijamii na Utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo.
   · Atakuwa Afisa Mhasibu wa Serikali ya Mtaa na atasimamia mapato na matumizi
   ya Serikali ya Mtaa
   · Atakuwa Mlinzi wa Amani na Msimamizi wa Utawala Bora katika Mtaa
   · Ataratibu na kusimamia upangaji wa utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo ya
   Mtaa
   · Atakuwa Katibu wa Kamati ya Halmashauri ya Mtaa.
   · Atatafsiri Sera, ataratibu na kusimamia utekelezaji wa Sheria ndogondogo za
   Halmashauri ya Mtaa
   8


   · Ataratibu na kuandaa taarifa ya utekelezaji wa kazi katika eneo lake na
   kuziwasilisha kwenye Halimashauri ya Mtaa na baadae kwenye Kata.
   · Ataongoza vikao vya maendeleo ya Mtaa vitavyowahusisha wananchi na
   wataalamu waliopo kwenye eneo lake.
   · Atahamasisha wananchi katika kampeni za kuondoa njaa, umasikini, na
   kuongeza uzalishaji mali.
   · Atasimamia matumizi bora ya Nguvu kazi.
   · Atakuwa Kiongozi wa Wakuu wa Vitengo vya Kitaalamu Katika Mtaa.
   · Atasimamia ukusanyaji wa kumbukumbu za walipa kodi, wataalamu mbalimbali
   na NGO waliopo katika Mtaa.

   9.2 SIFA ZA MWOMBAJI
   · Kuajiriwa wenye Elimu ya Kidato cha Nne au cha sita waliohitimu Astashahada
   (Diploma) katika Fani yoyote yenye mwelekeo wa Sayansi ya Jamii (Social
   Sciences) Utawala, (Public Administration and Local Gorvernment), Atashahada
   ya Sheria au Sifa nyingine inayolingana na hizo kutoka Chuo chochote
   kinachotambuliwa na Serikali.

   9.3 MSHAHARA
   Kwa kuzingatia viwango vya Serikali ngazi ya Mshahara TGS B kwa mwezi.

   10.0 SEKTA YA MIFUGO
   10.1 DAKTARI WA MIFUGO DARAJA LA II (VETERINARY OFFICER GRADE II ) –
   NAFASI 4
   Nafasi hizi ni kwa ajili ya Halmashauri ya Wilaya ya Chato
   10.1.1 MAJUKUMU YA KAZI
   · Kutoa huduma za Afya ya Mifugo
   · Kufanya Uchunguzi wa Magonjwa ya Mifugo katika eneo au sehemu alipo.
   · Kutayarisha na kusimamia mipango ya kuzuia kuthibiti, na kutokomeza
   magonjwa ya mifugo katika eneo lake.

   10.1.2 SIFA ZA MWOMBAJI
   · Kuajiriwa wenye Shahada ya kwanza ya Tiba ya Mifugo kutoka Chuo Kikuu cha
   Sokoine cha Kilimo au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali Nambao
   wamesajiriwa na bodi ya Madaktari wa Mifugo nchini.

   10.1.3 MSHAHARA
   Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS F. kwa mwezi

   MADARAKA


   · Anaweza kupewa majukumu ya/ Madaraka ya kuwa DSMS AU DVO
   9


   10.2 AFISA MIFUGO MSAIDIZI DARAJA LA II (LIVESTOCK FIELD OFFICER
   GRADE II) – NAFASI 14
   Nafasi hizi ni kwa ajili ya Halmashauri ya Manispaa ya Lindi na Halmashauri ya Wilaya
   ya Chato
   10.2.1 MAJUKUMU YA KAZI
   · Atafanya uchunguzi wa magonjwa ya mifugo kwa wafugaji wa eneo lake.
   · Kwa kushirikiana na wakaguzi wa Afya, atakagua nyama na machinjio mara kwa
   mara.
   · Atakusanya takwimu za nyama na mazao yatokanayo na mifugo kama ngozi na
   kuandika ripoti
   · Atatibu magojwa ya mifugo chini ya usimamizi wa Daktari wa Mifugo na kushauri
   wafugaji jinsi ya kukinga mifugo dhidi ya magonjwa
   · Atatembelea wafugaji mara kwa mara na kuwapa ushauri fasaha wa kitaalamu
   katika eneo la kazi
   · Atakusanya takwimu zote za maendeleo ya mifugo katika eneo lake.
   · Atashauri na kusimamia ujenzi wa majosho, machinjio, vibanio, na miundo
   mbinu inayohusiana na ufugaji bora.
   · Atasimamia uchanganyaji wa dawa ya josho.
   · Atahusika na uhamilishaji (Artificial Insermination) na uzalishaji (Breeding) wa
   mifugo kwa ujumla
   · Atashauri wafugaji kuhusu mbinu bora za kuzalisha maziwa na utunzaji wa
   ndama.
   · Atafanya kazi zingine za fani yake kama atakavyopangiwa na mkuu wake wa
   kazi.

   10.2.2 SIFA ZA MWOMBAJI
   · Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha sita waliofuzu mafunzo ya Stashahada ya
   mifugo kutoka chuo cha kilimo na mifugo (MATI AU LITI) au chuo kingine
   chochote kinachotambuliwa na Serikali
   10.2.3 MSHAHARA
   Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C kwa mwezi

   11.0 SEKTA YA KILIMO
   11.1 AFISA KILIMO DARAJA LA II (GRADE II ) – NAFASI 2
   Nafasi hizi ni kwa ajili ya Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga
   11.1.1 MAJUKUMU YA KAZI
   · Kudhibiti visumbufu vya mazao na mimea.
   · Kukusanya takwimu za bei za mazao kila wiki na kila mwezi.
   · Kukusanya takwimu za upatikanaji wa mazao katika masoko kila wiki/kila mwezi.
   · Kuendesha mafunzo ya wataalam wa kilimo.
   · Kufanya ukaguzi wa ubora na matumizi ya pembejeo na zana.
   · Ufuatiliaji wa mwenendo wa soko la mazao ya biashara.
   10


   · Kuendesha mafunzo juu ya hifadhi bora ya udongo na maji.
   · Kutoa habari juu ya teknolojia mpya kwa wadau.
   · Kuandaa/kuandika taarifa za utekelezaji kwa sekta ndogo ya mazao.
   · Kusimamia/kuendeleza taaluma ya uzalishaji mboga, matunda, maua na mazao
   mengine.
   · Kusimamia/kuendeleza uzalishaji wa mbegu bora.
   · Kuandaa, kutayarisha kufunga na kusambaza mbegu bora.
   · Kufanya majaribio ya magonjwa kwenye mbegu.
   · Kufanya ukaguzi wa mbegu mpya kwa kushirikiana na watafiti wa mbegu kabla
   ya kupitishwa.
   · Kuendesha mafunzo ya kuzalisha mboga, matunda, maua na viungo.
   · Kuhamasisha uzalishaji wa mazao ya bustani.
   · Kufanya utafiti mdogo mdogo wa mazao yanayofaa kulimwa katika sehemu ya
   kilimo cha umwagiliaji.
   · Kufanya utafiti wa udongo.
   · Kuhamasisha uanzishaji wa vikundi vya wakulima/wamwagiliaji.
   · Kuzalisha mbegu za msingi baada ya kuzalishwa na watafiti.
   · Kuendesha/kusimamia vishamba vya majaribio vya mbegu na uchunguzi
   maabara ili kuondoa utata juu ya mbegu.

   11.1.2 SIFA ZA MWOMBAJI
   · Kuajiriwa wenye Shahada ya kilimo au Shahada ya Sayansi waliojiimarisha
   katika mchepuo wa kilimo kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine au vyuo
   vingine vinavyotambuliwa na Serikali.

   11.1.3 MSHAHARA
   Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D kwa mwezi.

   11.2 AFISA KILIMO MSAIDIZI DARAJA LA II (GRADE II ) – NAFASI 3
   Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Halmashauri ya
   Wilaya ya Tunduru na Halmashauri ya Mji Njombe
   11.2.1 MAJUKUMU YA KAZI
   · Kushirikiana na watafiti kuendesha vishamba vya majaribio.
   · Kukusanya/kuhifadhi takwimu za majaribio.
   · Kuwafundisha wakulima mbinu za kilimo bora.
   · Kuwafikishia wakulima matokeo ya utafiti.
   · Kuwafundisha wakulima mbinu bora za kilimo, matumizi ya mbolea na madawa,
   pembejeo za kilimo.
   · Kukusanya na kutunza takwimu za mazao na bei kwa wiki, mwezi, robo na
   mwaka ngazi ya halmashauri.
   · Kukusanya takwimu za mvua.
   · Kushiriki katika savei za kilimo.
   11


   · Kushirikiana na vikundi vya wakulima kuhusu matatizo na teknolojia sahihi za
   kutumia.
   · Kupanga mipango ya uzalishaji.
   · Kupima uotaji wa mbegu na kusimamia taratibu za ukaguzi.
   · Kutathmini na kusavei maeneo ya vyanzo vya maji kwa ajiili ya kuhifadhi.
   · Kutunza miti mizazi.
   · Kuwatambua wasambazaji wa pembejeo.
   · Kutoa mafunzo ya lishe kwa wakulima.
   · Kufanya vipimo vya ubora, unyevunyevu na uotaji wa mbegu.
   · Kusimamia taratibu za ukaguzi.
   · Kudhibiti visumbufu vya mazao na mimea.
   · Kusimamia shughuli za kila siku za majaribio ya kilimo.
   · Kuwaelimisha wakulima juu ya matumizi bora ya udongo na maji.
   · Kutoa ushauri wa kilimo mseto.
   · Kuandaa sheria ndogo za hifadhi ya mazingira.
   · Kutoa taaluma ya uzalishaji wa mboga, matunda, maua na viungo

   Anaweza kuwa Bwana Shamba wa Kata/Kijiji.

   11.2.2 SIFA ZA MWOMBAJI
   · Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha Sita (VI) wenye stashahada ya kilimo kutoka
   vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.

   11.2.3 MSHAHARA
   Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C kwa mwezi.

   12.0 SEKTA YA AFYA
   12.1 DAKTARI DARAJA LA II (GRADE II ) – NAFASI 4
   Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Tawala Mkoa wa Arusha, Morogoro na Halmashauri ya
   Wilaya ya Chato
   12.1.1 MAJUKUMU YA KAZI
   · Kufanya kazi zote za matibabu hospitalini zinazohusiana na magonjwa
   mbalimbali yakiwemo magonjwa ya watoto, magonjwa ya kina mama na upasuaji
   wa dharura
   · Kutoa na kusimamia elimu ya afya pamoja na kuboresha afya ya jamii katika
   Wilaya na Mikoa au eneo lake la kazi
   · Kuchunguza, kufatilia na kuzuia milipuko ya magonjwa
   · Kutunza takwimu na kuzitumia kama inavyoelekezwa katika misingi ya MTUHA
   · Kupanga na kutathmini huduma za afya katika eneo lake la kazi
   · Kufundisha wanafunzi na watumishi waliopo kwenye eneo lake la kazi
   · Kusimamia na kuelekeza wafanyakazi walio chini yake
   · Kufundisha wanafunzi katika vyuo vya afya vilivyopo eneo lake la kazi
   12


   · Kubuni na kuendesha utafiti na kusambaza matokeo
   · Kubuni na kutayarisha mikakati ya kuinua ubora wa huduma ya fani yake
   · Kushiriki, kuhakiki na kuboresha huduma za afya (medical audit and quality
   improvement)
   · Kutoa huduma za outreach katika Wilaya/Mkoa wake
   · Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na
   elimu, uzoefu na ujuzi wake

   12.1.2 SIFA ZA MWOMBAJI
   · Kuajiriwa wenye Shahada ya Udaktari kutoka Vyuo Vikuu/ Vyuo
   vinavyotambuliwa na Serikali waliomaliza mafunzo ya kazi “Interniship” ya muda
   usiopungua miezi kumi na miwili na kupata usajili kutoka Baraza la Madaktari
   Tanganyika (Medical Council of Tanganyika)

   12.1.3 MSHAHARA
   Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGHS E. kwa mwezi.

   12.2 DAKTARI MSAIDIZI ( GRADE II ) – NAFASI 4
   Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Tawala Mkoa wa Arusha, Halmashauri ya Wilaya ya
   Chato na Rungwe
   12.2.1 MAJUKUMU YA KAZI
   · Kutambua matatizo ya wagonjwa na kutoa huduma za tiba, kinga na huduma
   kwa kina mama na watoto
   · Kufanya upasuaji wa dharura na wa kawaida
   · Kupanga, kutekeleza na kutathmini huduma za afya sehemu zao za kazi
   · Kupanga utekelezaji wa mipango ya kukabili majanga na dharura mbalimbali
   · Kufanya utafiti katika maeneo mbalimbali ya afya ili kuboresha utoaji huduma
   · Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na
   elimu, uzoefu na ujuzi wake

   12.2.2 SIFA ZA MWOMBAJI
   · Kuajiriwa wenye Stashahada ya juu ya Tiba ya miaka isiyopungua miaka miwili
   (2) kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali walio na leseni ya kufaaynya kazi
   kutoka Baraza la Madaktari Tanganyika (Medical Council of Tanganyika) pamoja
   na uzoefu wa kazi kwa muda usiopungua miaka mitatu

   12.2.3 MSHAHARA
   Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGHS C kwa mwezi.

   12.3 AFISA AFYA MAZINGIRA DARAJA LA II (ENVIRONMENT OFFICER GRADE
   II) – NAFASI 1
   Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa
   12.3.1 MAJUKUMU YA KAZI
   13


   · Kutoa ushauri na kusimamia njia bora za usambazaji wa maji safi na salama na
   utupaji wa taka
   · Kuelimisha jamiii juu ya mbinu za kujikinga na milipuko ya magonjwa
   · Kukusanya na kuchambua takwimu za Afya ya Mazingira
   · Kusimamia utekelezaji wa Sheria zinazohusu Afya ya Mazingira
   · Kuandaa taarifa za utekelezaji na kuziwasilisha katika mamlaka husika
   · Kuandaa na kufuatilia mikakati ya kuboresha na kusimamia usalalma wa afya
   kazini
   · Kuhakiki afya bandarini na mipakani
   · Kuratibu na kuhakiki kaguzi za vyakula, maji, kemikali, viwanda, sehemu za kazi
   na maeneo ya jamii
   · Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na
   elimu, uzoefu na ujuzi wake

   12.3.2 SIFA ZA MWOMBAJI
   · Kuajiriwa wenye Shahada ya Sayansi za Afya ya Mazingira na mafunzo kazini na
   kusajiliwa na Bodi ya Wataalam wa Afya Mazingira

   12.3.3 MSHAHARA
   Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGHS C kwa mwezi.

   12.4 AFISA AFYA MAZINGIRA MSAIDIZI (GRADE II ) – NAFASI 2
   Nafasi hizi ni kwa ajili ya Halmashauri ya Wilaya ya Babati na Rufiji
   12.4.1 MAJUKUMU YA KAZI
   · Kudhibiti na kuzuia milipuko ya wagonjwa
   · Kupambana na kuzuia wadudu na wanyama wanaoeneza magonjwa
   · Kusimamia uzikaji wa maiti zisizotambuliwa na zile zinazotokana na magonjwa
   ya kuambukiza
   · Kuandaa taarifa mbalimbali za Afya ya Mazingira katika ngazi ya kata na
   kuziwasilisha katika mamlaka husika
   · Kukusanya na kuchambua takwimu za Afya ya Mazingira katika kata na kutoa
   mrejesho ili kuchukua hatua zinazostahili
   · Kutoa elimu ya afya ya mazingira kwa jamii
   · Kukagua mazingira katika sehemu vinapotengenezwa vyakula ili kuhakikisha
   usalama na afya ya jamii
   · Kusimamia sheria za afya ya mazingira katika ngazi ya Kata pamoja na kusaidia
   jamii katika kutengeneza sheria ndogondogo
   · Kuhamasisha jamii katika kuboresha vyanzo vya maji na Usafi wa Mazingira
   · Kuhamasisha jamii kuhusu utekelezajiwa Huduma za Afya ya msingi katika ngazi
   ya Kata
   · Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na
   elimu, uzoefu na ujuzi wake
   14


   12.4.2 SIFA ZA MWOMBAJI
   · Kuajiriwa wenye Stashahada ya Sayansi ya Afya ya Mazingira ya miaka mitatu
   kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali na awe amesajiliwa na Bodi ya
   Wataalam wa Afya Mazingira

   10.1.1 MSHAHARA
   Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGHS B kwa mwezi.

   12.5 AFISA MUUGUZI DARAJA LA II (NURSING OFFICER GRADE II) – NAFASI 6
   Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Tawala Mkoa wa Morogoro, Halmashauri ya Wilaya ya
   Mbinga na Halmashauri ya Mji Njombe
   12.5.1 MAJUKUMU YA KAZI
   · Kufanya kazi za kiuguzi za kuhudumia wateja katika jamii, hospitalini na sehemu
   zote zinapotolewa huduma za afya
   · Kukusanya takwimu muhimu za afya
   · Kuwaelekeza na kusimamia wauguzi walio chini yake
   · Kutoa huduma kwa wagonjwa majumbani
   · Kutoa ushauri nasaha
   · Kutayarisha mpango wa kazi kwa ajili ya huduma za uuguzi
   · Kutoa huduma za kinga na uzazi
   · Kuelimisha wagonjwa na jamii
   · Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na
   elimu, uzoefu na ujuzi wake

   12.5.2 SIFA ZA MWOMBAJI
   · Kuajiriwa wenye Shahada ya Uuguzi kutoka Chuo Kikuu kinachotambuliwa na
   Serikali, waliohitimu mafunzo ya vitendo kazini (Internship) ya mwaka mmoja,
   waliosajiliwa na Baraza la Wauguzi na Wakunga Tanzania

   12.5.3 MSHAHARA
   Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGHS C kwa mwezi.

   12.6 AFISA MUUGUZI MSAIDIZI DARAJA LA II (ASSISTANT NURSING OFFICER
   GRADE II ) – NAFASI 12
   Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Tawala Mkoa wa Mara, Rukwa, Kigoma, Halmashauri
   ya Jiji la Mwanza, Halmashauri ya Wilaya ya Babati, Mbozi, Mtwara na Monduli
   12.6.1 MAJUKUMU YA KAZI
   · Kutoa huduma za uuguzi
   · Kukusanya takwimu muhimu za afya
   · Kuwaelekeza kazi wauuguzi walio chini yake
   · Kuwaelimisha wagonjwa na jamii kuhusu matatizo yao ya kiafya
   · Kutoa huduma za kinga na uzazi
   15


   · Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na
   elimu, uzoefu na ujuzi wake

   12.6.2 SIFA ZA MWOMBAJI
   · Kuajiriwa wenye Stashahada (Diploma) ya Uuguzi ya muda usiopungua miaka
   miwili kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali, waliohitimu mafunzo ya vitendo
   kazini (Internship) ya mwaka mmoja, waliosajiliwa na Baraza la Wauguzi na
   Wakunga Tanzania

   10.1.2 MSHAHARA
   Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGHS B kwa mwezi.

   12.7 MUUGUZI DARAJA LA II (NURSE GRADE II ) – NAFASI 18
   Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Tawala Mkoa wa Arusha, Iringa, Mara, Rukwa, Kigoma
   Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro, Mtwara, Rufiji, Rungwe na Tandahimba
   12.7.1 MAJUKUMU YA KAZI
   · Kufanya kazi za kiuguzi za kuhudumia wateja katika jamii, hospitali na sehemu
   zote zinapotolewa huduma za afya
   · Kusimamia na kuratibu kazi zote za wahudumu wa afya katika sehemu yake ya
   kazi
   · Kukusanya takwimu na kutayarisha taarifa za utendaji wake wa kazi
   · Kutoa huduma kwa wagonjwa majumbani
   · Kutoa ushauri nasaha
   · Kutoa huduma za kinga na uzazi wa mpango
   · Kutoa huduma za uzazi na afya ya mototo
   · Kuwaelimisha wagonjwa na jamii kuhusu matatizo yao ya kiafya
   · Kufuatilia utunzaji wa vitendea kazi katika maeneo yake ya kazi
   · Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na
   elimu, uzoefu na ujuzi wake

   12.7.2 SIFA ZA MWOMBAJI
   · Kuajiriwa wenye cheti cha Uuguzi cha miaka miwili kutoka katika Chuo
   kinachotambuliwa na Serikali na kuandikishwa (Enrolled) na Baraza la Wauguzi
   na Wakunga Tanzania

   12.7.3 MSHAHARA
   Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGHS A kwa mwezi.

   12.8 TABIBU DARAJA LA II (GRADE II ) – NAFASI 17
   Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma, Halmashauri ya Wilaya ya
   Babati, Chato, Rufiji, Mbinga, Rungwe, Tunduru, Tandahimba na Halmashauri ya Mji
   Njombe


   16


   12.8.1 MAJUKUMU YA KAZI
   · Kufanya kazi zote zinazofanywa na Tabibu Msaidizi
   · Kutambua na kutibu magonjwa ya kawaida
   · Kusimamia utendaji wa watumishi walio chini yake na kufanya upasuaji mdogo
   · Kushauri na kuhamasisha wananchi kuchangia huduma za Afya za Mfuko wa
   Afya ya Jamii
   · Kuweka kumbukumbu za vifaa na zana za kutolea huduma
   · Kuweka kumbukumbu, kuandaa na kutoa taarifa za utekelezaji
   · Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na
   elimu, uzoefu na ujuzi wake

   12.8.2 SIFA ZA MWOMBAJI
   · Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne/sita wenye Stashahada ya Tabibu ya
   muda usiopungua miaka mitatu kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali

   12.8.3 MSHAHARA
   Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGHS B kwa mwezi.

   12.9 TABIBU MSAIDIZI DARAJA LA II (ASSISTANT GRADE II) – NAFASI 5
   Nafasi hizi ni kwa ajili ya Halmashauri ya Wilaya ya Babati, Chato, Mtwara, Rufiji na
   Tunduru
   12.9.1 MAJUKUMU YA KAZI
   · Kutoa huduma za Kinga na Tiba
   · Kutambua na kutibu magonjwa
   · Kutoa huduma ya Afya ya Msingi (Primary Health Care)
   · Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na
   elimu, uzoefu na ujuzi wake

   12.9.2 SIFA ZA MWOMBAJI
   · Kuajiriwa wenye Cheti cha Mtihani wa Taifa wa kidato cha nne (IV) ambao
   wamehitimu Mafunzo ya Miaka Miwili ya Tabibu Wasaidizi (Clinical Assistants
   Certificate)

   12.9.3 MSHAHARA
   Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGHS A kwa mwezi.

   12.10 FIZIOTHERAPIA DARAJA LA II (PHYSIOTHERAPIST GRADE II ) – NAFASI 1
   Nafasi hii ni kwa ajili ya Katibu Tawala Mkoa wa Arusha
   12.10.1 MAJUKUMU YA KAZI
   · Kutoa tiba kwa kuzoeza viungo/kwa vitendo
   · Kukusanya na kutunza takwimu na taarifa za mgonjwa
   · Kutunza vifaa vya kutolea tiba
   · Kutoa elimu ya Afya kwa jamii kuhusu kutambua dalili na kuzuia ulemavu
   17


   · Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na
   elimu, uzoefu na ujuzi wake

   12.10.2 SIFA ZA MWOMBAJI
   · Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne/sita wenye Stashahada ya miaka mitatu
   katika fani ya Fiziotherapia kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali

   12.10.3 MSHAHARA
   Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGHS B kwa mwezi.

   12.11 MTEKNOJOJIA DARAJA LA II - MAABARA (TECHNOLOGIST GRADE II) –
   NAFASI 11
   Nafasi hizi ni kwa ajili ya Halmashauri ya Wilaya ya Babati, Mbinga, Monduli, Mpanda,
   Rufiji na Simanjiro
   12.11.1 MAJUKUMU YA KAZI
   · Kupima sampuli zinazoletwa maabara
   · Kuhifadhi sampuli zinazotakiwa kufanyiwa uchunguzi au kupelekwa Maabara za
   ngazi za juu
   · Kufanya kazi za ukaguzi wa maabara ambazo zimepatikana wakati wa
   uchunguzi
   · Kufundisha watumishi walio chini yake
   · Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na
   elimu, uzoefu na ujuzi wake

   12.11.2 SIFA ZA MWOMBAJI
   · Kuajiriwa wenye Stashahada ya katika fani ya Uteknolojia ya muda wa miaka
   mitatu katika fani ya Maabara kutoka chuo kinachotambuliwa na Seriakli na
   ambao wamesajiliwa na Mabaraza pale inapohusika

   12.11.3 MSHAHARA
   Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGHS B kwa mwezi.

   12.12 MTEKNOJOJIA DARAJA LA II – DAWA (TECHNOLOGIST GRADE II) NAFASI
   1
   Nafasi hii ni kwa ajili ya Halmashauri ya Jiji la Mwanza,
   12.12.1 MAJUKUMU YA KAZI
   · Kuainisha, kuandaa na kuagiza mahitaji ya dawa na vfaa tiba katika eneo lake la
   kazi
   · Kugawa dawa na vifaa tiba kwa wagonjwa na watumishi
   · Kuhifadhi dawa na vifaa tiba
   · Kuelimisha jamii kuhusu matumizi sahihi ya dawa
   · Kukagua dawa, vifaa tiba kemikali, vitendanishi na vipodozi katika eneo lake la
   kazi
   18


   · Kutoa taarifa juu ya madhara yatokanayo na matumizi ya dawa na vifaa tiba
   · Kuratibu kazi za kamati ya dawa na vifaa tiba
   · Kufanya uchuguzi wa ubora wa dawa, vifaa tiba kemikali, vitendanishi na
   vipodozi
   · Kufanya kaguzi mbalimbali katika sehemu zinazohifadhiwa dawa
   · Kusimamia utendaji wa kazi watumishi walio chini yake
   · Kutunza kumbukumbu za dawa na vifaa tiba
   · Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na
   elimu, uzoefu na ujuzi wake

   12.12.2 SIFA ZA MWOMBAJI
   · Kuajiriwa wenye Stashahada ya katika fani ya Uteknolojia ya muda wa miaka
   mitatu katika fani ya Madawa kutoka chuo kinachotambuliwa na Seriakli na
   ambao wamesajiliwa na Mabaraza pale inapohusika

   12.12.3 MSHAHARA
   Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGHS B kwa mwezi.

   12.13 MTEKNOJOJIA MSAIDIZI – MAABARA (ASSISTSNT TECHNOLOGIST -
   LABORATORY) – NAFASI 2
   Nafasi hizi ni kwa ajili ya Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe
   12.13.1 MAJUKUMU YA KAZI
   · Kuandaa vitendanishi (reagents) vya kufanyia vipimo vya Maabara
   · Kufanya kazi za awali sampuli zinazoletwa maabara
   · Kukusanya damu kutoka kwa wagonjwa na watu wanaojitolea
   · Kurekodi matokeo ya vipimo kwenye regista
   · Kutayarisha vifaa vya kazi
   · Kuhifadhi kwa mujibu wa taratibu sampuli zote zinazohitaji kuhifadhiwa baada ya
   uchunguzi
   · Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na
   elimu, uzoefu na ujuzi wake

   12.13.2 SIFA ZA MWOMBAJI
   · Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne wenye cheti cha miaka miwili katika fani ya
   Maabara kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali na ambao wamesajiliwa na
   Mabaraza pale inapohusika

   12.13.3 MSHAHARA
   Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGHS A kwa mwezi.

   12.14 MHUDUMU WA AFYA (MEDICAL ATTENDANT) – NAFASI 26
   Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma, Ruvuma, Halmashauri ya
   Manispaa ya Sumbawanga, Halmashauri ya Wilaya ya Babati, Mbozi, Mpanda,
   19


   Monduli, Rufiji, Rungwe, Simanjiro, Tandahimba, Mbinga na Halmashauri ya Mji
   Njombe
   12.14.1 MAJUKUMU YA KAZI
   · Kufanya kazi atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na elimu,
   uzoefu na ujuzi wake

   12.14.2 SIFA ZA MWOMBAJI
   · Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne waliopata mafunzo ya mwaka mmoja
   katika fani ya afya

   12.14.3 MSHAHARA
   Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGHOS A kwa mwezi.

   13.0 MKAGUZI WA HESABU WA NDANI DARAJA LA II (INTERNAL AUDITOR
   GRADE II) – NAFASI 15
   Nafasi hizi ni kwa ajili ya Waajiri Mbalimbali katika Utumishi wa Umma
   13.1 MAJUKUMU YA KAZI
   · Kufanya ukaguzi wa hesabu katika idara
   · Kusahihisha na kuidhinisha ripoti za ukaguzi
   · Kusahihisha na kuidhinisha hoja za ukaguzi wa ndani (Internal Audit Queries)

   13.2 SIFA ZA MWOMBAJI
   · Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha sita wenye cheti cha kati cha Uhasibu
   (Intermidiate Stage) kinachotolewa na NBAA au sifa zinazolingana na hizo. Au
   · Kuajiriwa wenye Shahada ya Biashara/ Sanaa yenye uelekeo wa Uhasibu au
   Stashahada ya juu ya Uhasibu (Advanced Diploma in Accounting) kutoka vyuo
   au Taasisi yoyote inayotambuliwa na Serikali.

   13.3 MSHAHARA
   Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D kwa mwezi.

   14.0 MHASIBU DARAJA LA II (ACCOUNTANT GRADE II) – NAFASI 15
   Nafasi hizi ni kwa ajili ya Waajiri Mbalimbali katika Utumishi wa Umma

   14.1 MAJUKUMU YA KAZI
   · Kuidhinisha hati za malipo.
   · Kuandika taarifa ya mapato na matumizi ya mwezi.
   · Kusimamia Wahasibu Wasaidizi katika kazi zao za kila siku.
   · Kusimamia shughuli za uhasibu kwenye Kitengo cha Idara.
   · Kuandika taarifa ya maduhuli.
   20


   14.2 SIFA ZA MWOMBAJI
   Kuajiriwa wenye ‘mojawapo’ ya sifa zilizotajwa hapa chini:-
   · ‘Intermediate certificate’ inayotolewa na NBAA.
   · Shahada ya Biashara/Sanaa yenye mwelekeo wa Uhasibu au Stashahada ya juu
   ya Uhasibu kutoka Chuo Kikuu/Taasisi yoyote inayotambuliwa na Serikali.
   · Stashahada ya Juu ya Uhasibu Serikalini (Advanced Diploma in Government
   Accounting)

   14.3 MSHAHARA
   Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D kwa mwezi.

   21


  2. Asa'rile's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 29th June 2012
   Posts : 419
   Rep Power : 561
   Likes Received
   100
   Likes Given
   57

   Default Re: ajira hizi hapa . angalia secretaiate ya ajira tar 26/6/2012 usiogope omba tu

   God bless u, wewe mzalendo unayewajali watanzania wenzako

  3. Zux de's Avatar
   Senior Member Array
   Join Date : 29th April 2012
   Posts : 227
   Rep Power : 532
   Likes Received
   15
   Likes Given
   8

   Default Re: ajira hizi hapa . angalia secretaiate ya ajira tar 26/6/2012 usiogope omba tu

   Mungu atutangulie katika hili.

  4. ndomyana's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 24th January 2012
   Posts : 4,671
   Rep Power : 1435
   Likes Received
   642
   Likes Given
   23

   Default Re: ajira hizi hapa . angalia secretaiate ya ajira tar 26/6/2012 usiogope omba tu

   Daa, ngoja niendelee kubahatisha

  5. Kilahunja's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 19th December 2011
   Posts : 1,468
   Rep Power : 3469035
   Likes Received
   258
   Likes Given
   18

   Default Re: ajira hizi hapa . angalia secretaiate ya ajira tar 26/6/2012 usiogope omba tu

   Dah, watu wa diploma wanafaid kushnda wenye shahada..mana kaz zao za kumwaga.


  6. mtwa mkulu's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 11th September 2013
   Posts : 1,640
   Rep Power : 330628
   Likes Received
   342
   Likes Given
   22

   Default Re: ajira hizi hapa . angalia secretaiate ya ajira tar 26/6/2012 usiogope omba tu

   Hawajatoa tena mwaka huu?


  Posting Permissions

  • You may not post new threads
  • You may not post replies
  • You may not post attachments
  • You may not edit your posts
  •  

  Who are WE?

  JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

  You are always welcome! Read more...

  Where are we?

  We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

  For anything related to this site please Contact us.

  Contact us now...

  DISCLAIMER

  JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

  Read more...

  Forum Rules

  JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

  You MUST read them and comply accordingly. Read more...

  Privacy Policy

  We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

  Read our Privacy Policy. Proceed here...