JamiiSMS
  Show/Hide This

  Topic: Nafasi za kazi Wizara ya Kilimo na Chakula

  Report Post
  Results 1 to 14 of 14
  1. mwankuga's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 30th August 2010
   Posts : 285
   Rep Power : 623
   Likes Received
   50
   Likes Given
   59

   Default Nafasi za kazi Wizara ya Kilimo na Chakula

   JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
   WIZARA YA KILIMO CHAKULA NA USHIRIKA
   [IMG]file:///C:/DOCUME~1/XPPRESP3/LOCALS~1/Temp/msohtmlclip1/01/clip_image002.jpg[/IMG]
   TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI

   Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika anawatangazia Watanzania wote wenye sifa zilizoanishwa hapa chini watume barua za maombi ya kazi zifuatazo.

   1. Afisa Utafiti Kilimo Daraja la II (Agricultural Research Officer II) Nafasi 70

   (a) Sifa za waombaji Wawe wamehitimu Shahada ya Kilimo (Bsc Agriculture General), Uchumi Kilimo, Uhandisi Kilimo, Food Science and Technology, Biotechnology Laboratory Sciences, Agronomy,Bsc Environmental Science na Horticulture kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.

   (b) Majukumu

   Kusaidia kukusanya na kuandika ripoti za utafiti chini ya maelekezo ya Afisa Utafiti Kilimo Mwandamizi.
   Kukusanya, kurekodi na kuchanganua takwimu za kazi za Utafiti zinazoendelea.
   Kusaidia katika kuendesha semina na kuwaelekeza wakulima jinsi ya kutumia teknolojia mpya kwa kuzingatia hali ya uchumi na mazingira yake. Kutoa ripoti ya maendeleo ya Utafiti na mapendekezo ya Utafiti katika Mikutano ya kanda.
   Kufanya shughuli za Utafiti chini ya maelekezo na uangalizi wa Afisa Utafiti Kilimo Mwandamizi.
   Pamoja na kazi nyingine za Utafiti kama atakavyopangiwa na kiongozi wake wa kazi.

   (c) Mshahara
   Mishahara ya Watumishi wa Serikali ngazi ya TGRS A.

   2. Mhandisi Kilimo Daraja la II (Agro Engineer II). Nafasi 88

   Waombaji watakaochaguliwa watapangiwa kazi Wizara ya Kilimo chakula na Ushirika na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

   (a)
   Sifa za waombaji

   Wawe wamehitimu Shahada ya Uhandisi yenye mwelekeo mkubwa katika fani ya Kilimo, Umwagiliaji,Ujenzi,Ufundi na Mazingira kutoka Chuo Kikuu kinachotambuliwa na Serikali

   (b) Majukumu
   Kuandaa program za mafunzo kwa wakulima kutumia zana za Kilimo
   Kushirika katika kufundisha wakulima na matumizi bora ya zana.
   Kushiriki katika ujenzi wa miradi ya Umwagiliaji
   Kushiriki kutengeneza michoro/ramani za umwagiliaji.
   Kukusanya takwimu za miradi ya umwagiliaji
   Kufuatilia program za mafunzo ya wanyamakazi mafundi wa matrekta wa wakulima jinsi ya matumizi ya wanyama kazi na matrekta
   Kushiriki kuratibu na kutoa huduma za umwagiliaji pamoja na matumizi ya maji. Pamoja na kazi zingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi.
   Kupitia mapendekezo ya miradi mbalimbali ya ufundi yanayowasilishwa Wizarani.
   Kusimamia mikataba ya ujenzi/ukarabati wa miundombinu ya umwagiliaji.
   Kushirikiana na mafundi sanifu kuwafundisha wakulima uendeshaji wa skimu za umwagiliaji

   (c)
   Mshahara
   Mishahara ya Watumishi wa Serikali ngazi ya TGS E.

   3. Afisa Kilimo Daraja la II (Agro – Officers II) Nafasi 378
   Waombaji watakaochaguliwa watapangiwa kazi Wizara ya Kilimo chakula na Ushirika na Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).
   (a) Sifa za waombaji
   Wawe wamehitimu Shahada ya Sayansi Kilimo (Bsc.Agriculture General,Bsc.Horticulture,Bsc.A gronomy,Bsc.Environmental Sciences) na Mazingira kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine au vyuo vingine vinavyotambuliwa na Serikali.

   (b) Majukumu
   Kudhibiti visumbufu vya mazao na mimea Kukusanya takwimu za bei za mazao kila wiki na kila mwezi
   Kukusanya takwimu za upatikanaji wa mazao katika masoko kila wiki/mwezi
   Kuendesha mafunzo ya wataalamu wa Kilimo
   Kufanya ukaguzi wa ubora na matumizi ya pembejeo na zana.
   Ufuatiliaji wa mwenendo wa soko la mazao ya biashara
   Kuendesha mafunzo juu ya hifadhi bora ya udongo na maji
   Kutoa habari juu ya teknolojia mpya kwa wadau
   Kuandaa/ kuandika taarifa za utekelezaji kwa sekta ndogo ya mazao.
   Kusimamia/kuendeleza taaluma ya uzalishaji mboga, matunda, maua na mazao mengine.
   Kusimamia/kuendeleza uzalishaji wa mbegu bora
   Kuandaa, kutayarisha, kufunga na kusambaza mbegu bora
   Kufanya ukaguzi wa mbegu mpya kwa kushirikiana na Watafiti wa mbegu kabla kupitishwa
   Kuendesha mafunzo ya kuzalisha mbegu matunda, maua na viungo
   Kuhamasisha uzalishaji wa mazao ya bustani
   Kufanya utafiti mdogo mdogo wa mazao yanayofaa kulimwa katika sehemu ya Kilimo cha Umwagiliaji.
   Kufanya utafiti wa udongo
   Kuhamasisha uanzishaji wa vikundi vya wakulima/ wamwagiliaji
   Kuzalisha mbegu za msingi baada ya kuzalishwa na watafiti
   Kuendesha/kusimamia vishamba vya majaribio vya mbegu na uchunguzi maabara ili kuondoa utata juu ya mbegu.

   (c) Mshahara Mishahara ya Watumishi wa Serikali ngazi ya TGS D.

   4.
   Mkufunzi Kilimo Daraja la II (Agricultural Tutor II) Nafasi 38
   Waombaji watakaochaguliwa watapangiwa kazi ya kufundisha katika vyuo vilivyo chini ya Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika na Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi.

   (a) Sifa za waombaji Wawe wamehitimu Shahada ya kwanza yenye mwelekeo wa Kilimo (Bsc.Agriculture General,Bsc.Agricultural Engineer,Bsc. Agronomy, Bsc.Irrigation Engineer) kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo- Sokoine au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.

   (b) Majukumu
   Kufundisha kozi za stashahada na astashahada za kilimo nadharia na vitendo
   Kuandaa mtiririko na mpangilio wa masomo (Lesson Sequences and Plans)
   Kusoma na kuelewa vema mihutasari ya mafunzo na kuitafsiri kwenye masomo
   Kuandaa na kufundisha kozi za wakulima
   Kuandaa na kupanga somo la vitendo na kusimamia wanachuo wakati wa kujifunza
   Kupima maendeleo ya wanachuo kwenye mitihani kwa kipindi chote kinachohusika na kutunza alama zao.
   Kupima maendeleo ya wanachuo kwa kushirikiana na Maafisa Kilimo wa Wilaya/Viwandani wakati wa mafunzo kwa vitendo (Field Practicals).
   Kutekeleza shughuli nyingine za kikazi kadri atakavyopangiwa na Mkuu wake wa kazi.

   (c) Mshahara
   Mishahara ya Watumishi wa Serikali ngazi ya TGS D. Waombaji wote katika barua zao ni lazima waonyeshe sehemu ambayo wangependa kupangiwa kwa nafasi zile zinazohusisha zaidi ya wizara moja. Hata hivyo uamuzi wa mwisho juu ya vituo ni wa mwajiri/ Mamlaka za ajira ambako nafasi zinapatikana. \

   MAMBO YA KUZINGATIA Barua za maombi ziambatane na Curriculum Vitae (CV), picha ndogo mbili ukubwa wa pasipoti, cheti cha kuzaliwa, vivuli vya vyeti vya kuhitimu elimu ya sekondari na Shahada husika . Waombaji wawe na umri usiozidi miaka 45. Wahitimu walioajiriwa Serikalini hawaruhusiwi kuomba nafasi hizi kwasababu tayari wana ajira Wahitimu waliotuma maombi yao kabla ya tangazo hili wanashauriwa kutuma maombi upya. Barua zote za maombi ziwasilishwe katika muda wa siku 14 kuanzia tarehe ya kwanza ya kuonekana tangazo hili. Tangazo hili linapatikana pia kwenye tovuti ya Wizara, Tanzania -- Ministry Of Agriculture, Food and Cooperatives- Home Page Barua za Maombi zitumwe kwa:

   Katibu Mkuu,

   Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika,
   S.L.P. 9192,
   DAR ES SALAAM.
   Last edited by mwankuga; 6th January 2012 at 20:11.
   engmtolera likes this.
   "THE REVOLUTION IS NOT AN APPLE THAT FALLS WHEN IT IS RIPE,YOU HAVETO MAKE IT FALL" (CHE GUEVARA)

  2. Mwanyasi's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 16th November 2010
   Location : Karibu na wewe
   Posts : 3,626
   Rep Power : 157068437
   Likes Received
   1919
   Likes Given
   2206

   Default Re: Nafasi za kazi Wizara ya Kilimo na Chakula

   Saaafi, hii kilimo pili mmh! Thanks for the info....!
   "Twimatule,,,,, ngaaani"

  3. engmtolera's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 21st October 2010
   Posts : 5,000
   Rep Power : 5581
   Likes Received
   1256
   Likes Given
   1169

   Default Re: Nafasi za kazi Wizara ya Kilimo na Chakula

   safi sana,haya agro engineers from sua kitu hichoooooooo,
   "You Can Not Jail Him First And Hear Him Later"

  4. nsangaman's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 30th June 2011
   Location : Serengeti
   Posts : 276
   Rep Power : 578
   Likes Received
   39
   Likes Given
   10

   Default Re: Nafasi za kazi Wizara ya Kilimo na Chakula

   Hongera wizara ya misosi
   Hapo kuna intavyuu kweli,au ukiandika barua unasubiria kuitwa kunako kazi.

  5. mikatabafeki's Avatar
   Banned Array
   Join Date : 29th December 2010
   Posts : 10,068
   Rep Power : 0
   Likes Received
   2372
   Likes Given
   1745

   Default Re: Nafasi za kazi Wizara ya Kilimo na Chakula

   ahsabnte kwa taarifa za kilimo TATU.


  6. Perry's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 24th February 2011
   Posts : 9,191
   Rep Power : 2520
   Likes Received
   693
   Likes Given
   26

   Default Re: Nafasi za kazi Wizara ya Kilimo na Chakula

   Haya sasa wasuaso,uwanja wenu huo.

  7. Ndibalema's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 26th April 2008
   Location : Mbagala
   Posts : 10,766
   Rep Power : 291617782
   Likes Received
   4175
   Likes Given
   3881

   Default Re: Nafasi za kazi Wizara ya Kilimo na Chakula

   Mwenye kujua hayo madaraja ya mshahara tafadhali atufafanulie.
   "Makalio ya sufuria hayaogopi moto"

  8. Kalunguine's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 27th July 2010
   Location : ARUSHA -TANZANIA
   Posts : 2,525
   Rep Power : 1076
   Likes Received
   112
   Likes Given
   471

   Default Re: Nafasi za kazi Wizara ya Kilimo na Chakula

   Mmmh jamani,ndo umeziona leo kazi za Mwezi Novemba na deadline imeshapita!!
   EMT likes this.

  9. Kilahunja's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 19th December 2011
   Posts : 1,454
   Rep Power : 3469024
   Likes Received
   256
   Likes Given
   18

   Default Re: Nafasi za kazi Wizara ya Kilimo na Chakula

   Na gazet la leo mwananch limetoa majina walochaguliwa na maeneo ya kazi.
   EMT likes this.

  10. EMT's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 13th January 2010
   Location : Tandahimba
   Posts : 14,201
   Rep Power : 429499868
   Likes Received
   13874
   Likes Given
   8595

   Default Re: Nafasi za kazi Wizara ya Kilimo na Chakula

   Quote By Lizy II View Post
   Mmmh jamani,ndo umeziona leo kazi za Mwezi Novemba na deadline imeshapita!!
   Kakopi na kupaste tuu bila kusoma. Huu ni mfano mzuri kwa wale sema kuwa viongozi huwa wana-represent who we are.
   "Poverty makes people do reckless things, but [the rich] do worse to protect their [interests]" - Immortal Technique.


  11. ndyoko's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 2nd November 2010
   Posts : 4,683
   Rep Power : 1864
   Likes Received
   1308
   Likes Given
   1977

   Default Re: Nafasi za kazi Wizara ya Kilimo na Chakula

   Quote By Ndibalema View Post
   Mwenye kujua hayo madaraja ya mshahara tafadhali atufafanulie.
   Ukiondoa hao agricultural engineers, maofisa wote waliotaja salary scale yao ni TGS D mshahra unaanzia na 470,000/= ambapo ukikatwa hayo makato lukuki, unatoka na net salary ya around 360,00 hivi. Kazi kwako sasa
   If you can not get what you love, then love what you have

  12. soledad's Avatar
   Member Array
   Join Date : 17th September 2011
   Location : dodoma
   Posts : 73
   Rep Power : 526
   Likes Received
   21
   Likes Given
   1098

   Default Re: Nafasi za kazi Wizara ya Kilimo na Chakula

   Na gazet la leo mwananch limetoa majina walochaguliwa na maeneo ya kazi.

   gazeti la mwananchi lina majina lakini sio ya hizo zilizotangazwa novemba, majina hayo no ya maafisa klilimo wasaidizi daraja la iii

  13. soledad's Avatar
   Member Array
   Join Date : 17th September 2011
   Location : dodoma
   Posts : 73
   Rep Power : 526
   Likes Received
   21
   Likes Given
   1098

   Default Re: Nafasi za kazi Wizara ya Kilimo na Chakula

   ]Na gazet la leo mwananch limetoa majina walochaguliwa na maeneo ya kazi

   majina ya ktk mwananchi sio ya hizo kazi za novemba ni ya maafisa kilimo wasaidizi daraja iii

  14. ntamaholo's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 30th August 2011
   Location : Mwilavya
   Posts : 6,236
   Rep Power : 2067
   Likes Received
   1473
   Likes Given
   504

   Default Re: Nafasi za kazi Wizara ya Kilimo na Chakula

   heko mkuu kutu up date
   UTUMISHI WA HAKI, NI SULUHISHO LA MAOVU YOTE


  Posting Permissions

  • You may not post new threads
  • You may not post replies
  • You may not post attachments
  • You may not edit your posts
  •  

  Who are WE?

  JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

  You are always welcome! Read more...

  Where are we?

  We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

  For anything related to this site please Contact us.

  Contact us now...

  DISCLAIMER

  JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

  Read more...

  Forum Rules

  JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

  You MUST read them and comply accordingly. Read more...

  Privacy Policy

  We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

  Read our Privacy Policy. Proceed here...