Jamani wadau naomba kwa yeyote ayejua nafasi za kazi zinatoka lini kwenye hizo sehemu nilizozitaja aniambie.Najua kuna watu wengi wa kila namna hapa jukwaani.Nataka kumpeleka mdogo wangu kwenye kozi yoyote inayofuata toka sehemu hizo.
Asanteni sana
Jamani wadau naomba kwa yeyote ayejua nafasi za kazi zinatoka lini kwenye hizo sehemu nilizozitaja aniambie.Najua kuna watu wengi wa kila namna hapa jukwaani.Nataka kumpeleka mdogo wangu kwenye kozi yoyote inayofuata toka sehemu hizo.
Asanteni sana
We MKURYA ?
Ana elimu gani huyo mdogo wako? Watatangaza magazetini hasa kwa wale Proffessional ndio wata aply directly makao makuu na hawa wengine lazima wapitie JKT ndio aqualify kwenda Jwtz
Muda mfupi uliopita nilikuwa naongea na Commisiner wa Polisi kuhusu ajira ndani ya jeshi la Polisi amesema kwa sasa kule CCP kuna recruit kozi inaendelea ambapo inategemewa kuisha 2012 mwezi wa 2 au 3 baada ya hapo ndipo wataajiri wengine,hvyo tegemea labda kwa kipindi hicho.Hata hivyo ametoa angalizo kuwa Jeshi la Polisi linasitasita kuajiri wasomi wengi maana wanaleta usumbufu kwa viongozi wa ngazi za juu za jeshi hilo kwa kuhoji kila jambo kinyume kabisa na maadili ya jeshi ambapo askari anatakiwa kuitikia NDIYO AFANDE hata kama anaonewa/kudhurumiwa haki yake.
wakati anazubaa zubaa mpeleke veta akatafute cheti kingine inamaana sana kama atakuwa na kitu cha ziada
Mpelekeni ualimu huyo
Hakika wanaokula mali ya mayatima kwa dhuluma, bila shaka wanakula moto matumboni mwao na wataungua katika huo moto.
The Holy Quran 4:10
jaman jaman!huyo mdogo wako amekosa nini mpk unataka aende majeshini?najua WaTanzania wengi dhana ya kupeleka ndugu au watoto wao kigezo nikuwa wamfeli shuleni,au wamepata division 4 za mwsho so jeshini ni last option,mdogo wako ana elimu gan?majeshini bila elimu ya kueleweka unataka mdogo wako akawe mtumwa na manamba wa kutupwa,atakuwa ni mtu wa kukataa tamaa kama tunavyoona wanajeshi askari wetu hapa Tz na kuishia ktk gongo,hakikisha awe na elimu kwanza angalau digrii ndio umpeleke,kutwa wenzetu hao wanasema maslahi duni,japokuwa hawasemi direct lkn hawana kitu na serikali imewatupa kimapato,angalia ni nn sbb ya wewe kutaka kumpeleka huko...iwish ningeonana face to face nikwambia uozo mwingne mwng ulipo majeshini hasa ktk vyuo vyao vya mafunzo.....Yaan acha tuu!
Nimeona mchangiaji mmoja hapo juu amesema ampeleke ualimu. Hivi ualimu ni kazi ya walio feli? Nauliza tu maGT.
Jamani mimi ni mhitimu wa mafunzo ya kilimo na mifugo je naweza nikapata nafasi ya kujiunga na jwtz kutokana na hiyo proffesional niliyo nayo?
Nafasi za jeshi huwa zinatoka muda gani?
Follow Us Here