JamiiForums |The Home of Great Thinkers - Conversation Between Mtanzania and Uwiano Maalum

Go Back   JamiiForums |The Home of Great Thinkers > Mtanzania


Conversation Between Mtanzania and Uwiano Maalum
Showing Visitor Messages 1 to 2 of 2
  1. Uwiano Maalum
    7th April 2009 01:06 AM
    Uwiano Maalum
    Nimeona visitor message yako kwangu kuhusu Kiongozi mstaafu aneugulia kule kwa Zuma.

    Kwanza, nafurahi kuona kuna watu wanaelewa kwamba sio vizuri viongozi wakiwa wanakimbilia kutibiwa nje wakiwaacha wananchi wanakufa kwa kukosa dawa za magonjwa yanayotibika kama Malaria.

    Lakini Mtanzania, sikuelewi unaposema unafahamiana na ndugu za yule Mzee kwa hiyo usingependa kuwaongezea masikitiko ndio maana umeficha mawazo yako huku. Jamaa wanajua wewe ndio "Mtanzania"?

    Kama hawajui ila tu unawaonea huruma basi huna uchungu wa kweli na mali za umma zinavyotumika kuhudumia wachache. Wengine pia tuna jamaa na marafiki uongozini huko wanakamua na tunawasema nyuma ya hizi pseudo names zetu. Sasa kama tunatumia majina bandia na bado tunaogopa hapo sasa hatuna uzalendo.

    Viongozi wanapojipatia luxury ya matibabu nje ambayo wananchi hawapati huo sio utu.
  2. Mtanzania
    6th April 2009 10:55 PM
    Mtanzania
    Mkuu Uwiano Maalum,

    Kwenye hili la matibabu nje nakuunga mkono kwa asilimia 100. Inabidi hawa wazee hata waone aibu kukimbilia nje kutibiwa. Hizo pesa inatakiwa zitusaidie kutengeneza hospitali zetu. Afadhali hata tutengeneze muhimbili na wao kuwawekea maeneo ya maana pale ili muda mwingine hata maskini wengine wafaidike na hizo huduma kuliko kumwaga pesa nyingi nje kutajirisha wageni.

    Hili suala linanipa shida sana na huko nyuma nimelielezea kwa kirefu hapa JF. Kwenye hili siwezi ku comment kule kwasababu namfahamu huyo Dr. na nisingependa kuendeleza majonzi kwenye mambo yao ya familia. Watanzania tuelemike, tuheshimu kutengeneza huduma zetu nyumbani kuanzia shule, afya mpaka barabara badala ya kushabikia vya wageni.
    Jioni njema.

Tuma Ukurasa huu kwa rafiki yako!


All times are GMT +3. The time now is 11:06 AM.

Powered by JamiiForums.com
Copyrights reserved to JamiiForums.com