Mleta mada asante sana kwa kuwekea msisitizo vipengele hivyo vinavyoangusha wengi.
Kilimo ni shughuri ya kiuchumi kama biashara nyingine. Kwa anaetaka kufanya kwa tija lazima kujifunza mbinu za ujasilia mali nyingi iwezekanavyo. Mbinu hizo zitamsaidia kujua nini cha kulima, wapi soko, iwapo...
Laki saba inatosha kwa eka moja tu. Usiwaze eka mbili hasa kama watarajia kupanda kitaalamu labda kama ni wa kurusharusha mbegu unaishia kuvuna gunia saba kwa eka
Wakuu majira kama haya mwaka jana nilinyanyasika kuuza nyanya debe kwa buku....mwaka huu majira haya mm roho ya ppaka niliyestahimili kurudia kulima nyanya majira haya haya hatarishi nakamua bei ya 15,000 debe!! Wadau hivi kumetokea nn!! nchini? Hali hii itafuatwa na mafuriko ya nyanya Sept -...
Kuna mambo mengine mengi ya kuzingatia unaponunua pump.
Aina ya umwagiaji
Wamwagiliaji mjini Morogoro humwagia kwa kuifuata mimea na kutembea na mpira shamba zima kila mmea ukimwagiwa maji peke yake. Kwa umwagiaji wa aina hii wakulima hutumia pump ndogo za inchi 2. Saizi ya pump hizi ni nzuri...
Kuhusu hizo picha za Google earth, si sahihi kutumia picha hizo kama uthibitisho wa hali ya uoto uliopo muda huu. Google earth huwa updated baada ya muda mrefu kupita kwaio yawezekana zikawa picha za zamani na zisiwasilishe hali ilivyo leo.
Asante wakuu kwa juhudi za kunitafuta. Nashukuru na nafarijika sana ninapodhihirishiwa kuwa michango yangu JF inasaidia jamii. Mimi nipo sana jukwaani, nimekuwa mzito kuchangia jukwaani kutokana na kujichimbia sana kwenye dili langu la huko maporini kuchoma mkaa maana maeneo yetu hayo ya...
Mkuu Soya beans sio maharage ni zao tofauti kabisa ingawa liko jamii moja sawa na maharage, mbaazi na kunde. Soya beans ni maarufu kwa kusheheni protein kuliko mazao mengine jamii ya mikunde. Kwenye kutengeneza vyakula vya kuku source rahisi ya protein huwa ni dagaa. Wataalamu siku hizi badala...
Sijawahi kufanya huo utafiti maana huwa nanunua starter mash mfuko mmoja tu kuwalisha kuku mia moja kwa mwezi wa kwanza na kisha hununua growers mash mifuko miwili na huwalisha hao kuku mia kwa mwezi mwingine, baada ya hapo kuku huwa wakubwa huwaachia wakapekue na pia huwatengenezea cha ziada...
Asante sana kwa maneno yako yanayotia moyo. Kuna wachangiaji walinilalamikia niachane na kuchoma mkaa kutokana na athari zake kwenye mazingira. Kwakuwa nilishajua utamu wa biashara ya mkaa niliamua kutengeneza mkaa kwa kutumia mabua ya mpunga na mabua ya mahindi, kama hujui ingia You Tube Kuna...
Unachonga sifa za madikteta kufit agenda yako ya kumchafua mkombozi wa wanyonge, mtatoka mapovu sana mimi ninachojua unawakilisha majizi, mafisadi na wanufaikaji wa mfumo unaoenda kufumuliwa. Na mtatumbuliwa tu hata mseme vipi! Maandishi yako yanaonesha unafanya hapa mahali pa kujifunzia kujenga...
Mlioko mashambani limeni sana zao la mikunde aina ya soya (soya beans) haya yanaondoa kabisa haja ya kutumia dagaa kwenye utengenezaji wa chakula cha kuku, kinachotakiwa ni kununua amino acid aina mbili ambazo zinakosekana kwenye soya bean lakini zinapatikana kwenye maduka ya kilimo. Ukilima...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.