1. Mkuu Kevo,
- Ahsante sana kwa ujumbe mzito sana na nimefarijika mimi na familia yangu, yaani mke na watoto wangu wawili, ninakuombea kwa Mungu pia akupe mwaka mpya na Kritsmas njema.
2. Mkulu Bubu,
- Heshima mbele sana na ninashukuru sana kwa ujumbe huu wa heri, ninaomba kurudisha kwako na familia yako, kwamba Mungu awape mwaka mpya wenye mafanikio na Kritsmas njema sana,
3. Mkuu Lusajo,
- Wewe ni the future
JF, ninakutakia yote mema ya kuanzia mwaka mpya na Kritsmas pia, ninashukuru kwa ujumbe wako na ninakutakia mafanikio mema,
4. Mkuu Steve D,
- Heshima ikurudie na shukrani kwa ujumbe wako, mimi na familia yangu tuko sawa na sasa hivi tunajitayarisha kwenda kanisani kutoa heshima angalau kidogo kwa Muumba ninaomba ufikishe salaam zangu na familia yangu kwa familia yako.
5. Wakulu Congo na Nelson,
- Heshima pia kwenu wote, sio kwamba nimewa-ignore hapana ila unajua shughuli za maisha, lakini ninaomba kuwatakia Kritsmas njema na mwaka mpya ulio na neeema.