Bubu Ataka Kusema na wakuu wengineo ambao huwa mnapitia ukurasa
huu (ambao wasiojisajili hudhani ndo wanaona mawasiliano yote ya JF) nawashukuru kwa salaam zenu za Sikukuu hizi. Aidha nawashukuru sana kwa ushirikiano mliotupa kwa mwaka 2008 na kuwa nasi katika dhahma za hapa na pale na kuonesha ushirikiano wa karibu katika nyanja mbalimbali.
Furaha yangu daima ni kujua kila mwana JF yu mzima na anaendelea vema na harakati zake za maisha na anafanikiwa katika kila afanyalo.
Mwenyezi Mungu mwingi wa Rehema akupe faraja wewe na familia yako pamoja na wote wanaokutegemea (taifa ndani yake) ili kila utakalolifanya kwa mwaka 2009 liwe na baraka zake Mwenyezi Mungu na likusaidie wewe kufikia malengo uliyojiwekea pamoja na jamii inayokuzunguka.
Invisible