Matangazo madogomadogoMatangazo ya misiba, mikutano n.k yawekwe hapa.
ONYO: Usiweke links za aina yoyote! Uongozi wa JF hautahusika kwa namna yoyote kwa mawasiliano ya mauzo yaliyowekwa na wanachama bila kutushirikisha.
Mwandishi wa Habari wa siku nyingi Mike Sikawa (55) amefariki Dunia,Nyumbani kwake Njiro - Arusha siku ya Jumatatu (17.11.2008).Marehemu Sikawa amefarikiki baada ya kusumbuliwa na Ugonjwa wa Kisukari kwa muda mrefu.
Katika uhai wake amewahi kufanya kazi Katika kampuni ya magazeti ya serikali (TSN),Pia amewahi kuwa Mtangazaji wa BBC Idhaa ya Kiswahili huko Johannesburg - Afrika kusini.Marehemu ameacha mke na watoto wawili.(wanaishi South Afrika).Mazishi ya marehemu yatakuwa kwao Arumeru Arusha...Mwenyezi Mungu amlaze mahali Pema Peponi!!
__________________ Its not enough to do good if you can do better.
hata katika magazeti sijaona watu hawatilii mkazo lakini poleni wahusika wa msiba huu , sijui jk akitoka huko alipo ataenda katika msiba ngoja tuone
Sasa hapa JK wa watu anahusika nini na wewe Shy!! jamani mwacheni mtoto wa mwenzenu na yeye kazaliwa kama wewe. mumpumzishe basi. sio kila kitu kumpaka matope. huyu ni rais wa nchi mpe heshima yake. huo msiba unahusika nini!!!! looo ungepewa wewe kuwa rais wa nchi ungeweza? acha hizo. mengine mumpumzishe baba wa watu %#@*&%$#*&%$#@
Mara nyingi hawa ndugu zetu wakati fulani wanapoandika habari huwa hawafanyi research hata kidogo. Ndio maana JF will always be first. Sina hakika kama kweli huyu mheshimiwa ameacha mjane Amerika ya Kusini
Samahani kwa kuchepuka.
Mkuu Bongolander, ukisoma vema sehemu uliyohighlight utabaini kuwa kuna kiunganisha NA. Hiki kinatenganisha kati ya mjane NA watoto. Hivyo katika fasihi, kiambishi kinachofuata baada ya kiungabnishi hicho kinaweza kumaanisha kinahusisha nomino iliyotajwa baada ya kiunganishi. Kwa maana hiyo, katika habari ulioikosoa. kuna uwezekano kuwa walioko Amerika ya kusini ni watoto, ambayo ni nomino iliyotajwa baada ya kiunganisha.
Asante
Jamii ijuayo uwiano thabiti kati ya dharau, ubinafsi, chuki na ustaarab dhidi ya jamii nyingine na baina ya watu wake ni jamii yenye maendeleo. Isiyojua ni dumazi. SD1-09.
Fikra ni nyenzo endelezi au potofu. Changamoto tuliyonayo ni kuchanganua na kutenganisha kati ya fikra endelevu na fikra potofu, kwani mwisho wa fikra ni matendo pale fikra hazibakii kuwa fikra. SD6-07Rev.2-09.