JamiiSMS
  Show/Hide This

  Topic: Angalia njia mpya ya Wachina kutafuta wachumba!

  Report Post
  Results 1 to 12 of 12
  1. #1
   ldleo's Avatar
   Member Array
   Join Date : 9th January 2010
   Posts : 13
   Rep Power : 610
   Likes Received
   0
   Likes Given
   0

   Default Angalia njia mpya ya Wachina kutafuta wachumba!

   Muda mfupi uliopita, "supamaketi maalum ya mapenzi" ilizinduliwa katika mtaa wenye maduka mengi mjini Beijing,. Supamaketi hiyo haiuzi matunda wala vyakula na matumizi ya kila siku, kinachouzwa ni mapenzi tu. Katika supamaketi hiyo, watu wasio na wachumba wanaweza kuchagua watu wanaoona wanawafaa.

   Tarehe 9 Novemba "Supamaketi ya mapenzi ya ninakutafuta" iliyoko katika uwanja wa Xihuan mjini Beijing ilizinduliwa. Baada ya kuzinduliwa tu, kazi yake ilifanyika katika hali motomoto. Kila siku watu wengi wasio na wachumba wanakwenda kwenye supamaketi hiyo kuwatafuta na kuwachagua watu wanaowapenda. Katika supamaketi hiyo, data za watu wasio na wachumba zinawekwa katika rafu kwa kufuata utaratibu wa jinsia, umri na mapato, kwa hiyo watu wote wasio na wachumba wanaokwenda kwenye supamaketi hiyo, wanaweza kuchagua watu wanaoona wanawafaa kwa mujibu wa data hizo, kama wakiona watu fulani wanawafaa, basi wanaweza kuwasiliana na watu hao kwa kupitia wafanyakazi wa supamaketi hiyo baada ya kuthibitisha vitambulisho vyao. Mhusika wa supamaketi hiyo Bibi Zhang Ying alifahamisha kuwa, wazo la kuanzisha supamaketi hiyo lilitokana na uzoefu na raslimali zao za kuendesha tovuti ya kutafuta mchumba. Bibi Zhang alisema,
   "Tovuti ya kutafuta mchumba inayoitwa 'ninakutafuta' imeendeshwa kwa miaka mitatu, kwa kupitia uendeshaji wa tovuti hiyo, na kuwasiliana na watu wasio na wachumba, tumegundua kuwa watu hao wanataka kuwa na njia ya moja kwa moja, pia wanataka kupata data husika zinazoaminika zaidi. Kwa hiyo tulifikiri kuzindua supamaketi hiyo. Watu wasio na wachumba wakija wanaweza kuona data hizo zinazoaminika. Wanalokuta ni jukwaa kubwa zaidi kuliko tovuti."
   Katika "supamaketi ya mapenzi", data zote zinathibitishwa, na kila data ina picha ya mtu mhusika asiye na mchumba, kwa hiyo inawapa watu wasio na wachumba urahisi wa kuchagua, na wakiridhika wanaweza kuwasiliana nao mara moja. Supamaketi hiyo inafunguliwa kila siku, na haipumziki hata wakati wa wikiendi na sikukuu, hivyo watu wasio na wachumba wakiwa na wakati, wanaweza kutembelea supamaketi hiyo, huenda watakutana na watu wanaweza kuwapenda. Katika mchakato huo, washauri kuhusu mambo ya ndoa kwenye supamaketi hiyo wanafanya kazi muhimu. Bibi Zhang Ying alisema,
   "Kazi za washauri kuhusu mambo ya ndoa ni kufahamu matakwa ya watu wasio na wachumba, na kuwasaidia kujua matakwa hayo halisi, kazi hii ni muhimu sana, kwa sababu watu wengi wasio na wachumba hawajui matakwa yao halisi, au matakwa yao hayaendani na hali zao."
   Washauri kuhusu mambo ya ndoa wanapaswa kuthibitisha kwanza data husika za watu wasio na wachumba walioandikishwa kwenye supamaketi hiyo, halafu wanaweza kutoa huduma nzuri na mapendekezo kwa watu wasio na wachumba, ili kuwasaidia wakutane na watu wanaowafaa zaidi. Bibi Gao Shan ni mshauri kuhusu mambo ya ndoa, alisema hivi sasa vijana huwa wanakutana na matatizo mengi wakati wa kuchagua watu wanaowapenda, na "supamaketi ya mapenzi" inataka kuwapa watu wasio na wachumba fursa nyingi zaidi na kuwasaidia kuondoa matatizo. Alisema,
   "Watu huona kuwa kutafuta marafiki kupitia mtandao wa internet si jambo halisi, na wanahitaji muda kuwafahamu marafiki hawa kwa undani, labda mpaka mwisho wanakuwa hawajui wanachofahamu kama ni kweli au la, kwa hiyo mchakato huo umesababisha matatizo kadhaa wakati wa kutafuta marafiki. Baadhi ya watu wanawaomba jamaa au marafiki zao wawasaidie kuwatambulisha kwa kujuana na kujulisha mtu fulani, lakini huenda jamaa na marafiki zao hawajui kwa uhalisi ni nini. Hivyo tunawasaidia kuondoa matatizo hayo mawili makubwa, kwanza data zote katika supamaketi yetu zinaaminika, tumekutana na watu hao, na picha zao pia ni za maishani, kwani uaminifu ni jambo la kwanza na la msingi, pili kwa kuwa hapa ni supamaketi, hivyo watu wanaweza kuwachagua wenyewe, wanaochagua ni wanaowapenda."

   Hivi sasa katika "supamaketi ya mapenzi", kuna watu zaidi ya 500 wanaoweza kuchaguliwa. Ni rahisi kushiriki kwenye supamaketi hiyo, unapaswa kutoa habari yako halisi ya kimsingi, na kutoa Yuan 20 kutengeneza data, halafu data zako zinaweza kuwekwa kwenye rafu. Unaweza kutembelea supamaketi hiyo bila malipo, na kama unaona kuna mtu fulani uliyevutiwa naye, unaweza kumwuliza na kusaidiwa na washauri kuhusu mambo ya ndoa kwenye supamaketi hiyo, na kuna wanaopenda kukusaidia. Kwa upande mmoja, pia unapaswa kutoa Yuan 20 kutengeneza data zako, baada ya kuthibitisha wanaweza kutoa data hizo kwa mtu unayependa kukutana naye; kwa upande mwingine, kama mtu huyo anakubali kukutana nawe, watawasaidia kuwapa njia ya kuwasiliana, au kuwasaida kuchagua muda na sehemu ya kukutana. Supamaketi ikiwasaidia watu wawili kukutana, itatoza Yuan 100. Fedha hizo sio nyingi na data zinaaminika, kwa hiyo supamaketi hiyo inawavutia "wateja" wengi.
   Msichana Zhou Xianyu kutoka Hangzhou amefanya kazi hapa Beijing kwa zaidi ya miaka 10, kwa kuwa hakuwasiliana na watu wengi, hivyo bado hana mchumba. Baada ya kuiona "supamaketi ya mapenzi", alitembelea na kutaka kutafuta mtu anayempenda. Alisema,
   "Kwa kuwa sikuwasiliana na watu wengi, hivyo fursa ya kukutana na mtu ninayeona ananifaa anayefaa sio nyingi, kwa hiyo bado sijakutana na anayefaa. Naona haya kwenda sehemu za kutafuta wachumba. Lakini wazazi wangu wana wasiwasi. Nimetembelea "supamaketi" hiyo kutazama kama kuna mtu anayenifaa. Naona hapa ni salama."
   Mjini Beijing kuna vijana wasio na wachumba kama msichana Zhou. Habari zilizotolewa na shirika la habari la China zinasema, hivi sasa mjini Beijing wasichana zaidi ya laki 5 bado hawana wachumba, na wavulana wasio na wachumba hata ni mara 1.5 kuliko wasichana, na idadi hiyo inaongezeka siku hadi siku. Basi "supamaketi ya mapenzi" inatoa fursa kubwa kwa watu hao, lakini vipi njia hiyo inakubaliwa na watu bado inahitaji muda. Bibi Zhang Ying alisema, "Matumaini yetu ni kuwasaidia wale wanaotaka kutafuta mchumba na kufunga ndoa. Tuna matumaini kuwa siku moja watu wakitaja supamaketi yetu, wanaweza kuisifu na kusema kuwa, data zinazotolewa hapa ni za kuaminika, na watu wasio na wachumba wanaweza kwenda kwenye supamaketi hiyo kutafuta wachumba, naona hayo yametimiza lengo letu la kuanzisha tovuti hiyo."
   (Makala hii inatoka http://swahili.cri.cn/)


  2. drphone's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 29th September 2009
   Posts : 3,553
   Rep Power : 1332
   Likes Received
   129
   Likes Given
   17

   Default Re: Angalia njia mpya ya Wachina kutafuta wachumba!

   mh dunia inakwisha sasa ikija bongo itapata wateja sana
   THE BEST IS YET TO COME.

   THE GREATEST EXPERIENCE IS TO MEET YOURSELF AND FALL IN LOVE WITH YOURSELF.

  3. #3
   ldleo's Avatar
   Member Array
   Join Date : 9th January 2010
   Posts : 13
   Rep Power : 610
   Likes Received
   0
   Likes Given
   0

   Default Re: Angalia njia mpya ya Wachina kutafuta wachumba!

   Quote By drphone View Post
   mh dunia inakwisha sasa ikija bongo itapata wateja sana
   Is it amazing that wachina wengi wanaochapa kazi, hawana wakati wa kutafuta wachumba au kudate, hivyo imekuwa njia mkato, lakini labda siyo nzuri.

  4. Akili Kichwani's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 7th January 2010
   Location : In da Skull
   Posts : 1,500
   Rep Power : 908
   Likes Received
   164
   Likes Given
   84

   Default Re: Angalia njia mpya ya Wachina kutafuta wachumba!

   swaaafi sana, sasa mambo ya kuliana bia na mishikaki kwisha, unaenda market unachukua mzigo, mchezo umeisha! da soko huria limetukomboa, tulikuwa tunahangaika kutongoza weeeeeeeeeeeee tunaliwa pesa na demu anayeyuka!!!!

   jamani wadau tuungane tupate wawekezaji haraka watuwekee haya maduka bongo immediately.

   itabidi nipitie china nikiwa njiani kurudi home niangalie uwezekano wa kuibuka na mchina,

   tehe tehehehe...................

  5. Darwin's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 14th May 2008
   Posts : 909
   Rep Power : 875
   Likes Received
   43
   Likes Given
   6

   Default Re: Angalia njia mpya ya Wachina kutafuta wachumba!

   Iko Warrant kwamba unayemnunua!!! oops unayempata kama utadumu naye? na ni siku ngapi unaweza kupewa unayemtaka nakumjaribu kwamba anafaa!!? Kama hafai unarudishiwa pesa zako?
   St. Shaughn 5 : 31 "If I bear witness of myself, my witness is not true" Jesus says about himself


  6. SHUPAZA's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 4th August 2009
   Posts : 533
   Rep Power : 736
   Likes Received
   13
   Likes Given
   1

   Default Re: Angalia njia mpya ya Wachina kutafuta wachumba!

   Dah! hii kali sasa mpaka watu wameanza kuuzwa utu wa mtu sasa umekuwa hauna samani mh!

  7. FirstLady1's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 29th July 2009
   Location : Mama Mwenye Nyumba
   Posts : 16,103
   Rep Power : 85937919
   Likes Received
   4348
   Likes Given
   7806

   Default Re: Angalia njia mpya ya Wachina kutafuta wachumba!

   hii habari imenifanya nitabasamu tu kisha kubaki na mshangao
   No one is in charge of your happiness except you...
   God time is the best..
   Tupo wangapi?

  8. Kimbweka's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 16th July 2009
   Posts : 8,577
   Rep Power : 7511
   Likes Received
   1574
   Likes Given
   137

   Default Re: Angalia njia mpya ya Wachina kutafuta wachumba!

   Mbona wabongo wanafanya indirectly pale mlimani city
   "Life comes once only: No retake/replay/rewind/once-more. One should enjoy it, be happy & keep happy others too."

  9. #9
   ldleo's Avatar
   Member Array
   Join Date : 9th January 2010
   Posts : 13
   Rep Power : 610
   Likes Received
   0
   Likes Given
   0

   Default Re: Angalia njia mpya ya Wachina kutafuta wachumba!

   Quote By FirstLady1 View Post
   hii habari imenifanya nitabasamu tu kisha kubaki na mshangao
   Kuishi kwingi ni kuona mengi, lakini sipendi utamaduni huo wa fastfood!Mapenzi siyo mchezo.

  10. Henge's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 14th May 2009
   Posts : 6,669
   Rep Power : 2122
   Likes Received
   1287
   Likes Given
   2421

   Default Re: Angalia njia mpya ya Wachina kutafuta wachumba!

   Quote By SHUPAZA View Post
   Dah! hii kali sasa mpaka watu wameanza kuuzwa utu wa mtu sasa umekuwa hauna samani mh!

   hii nzuri saana wakuuu inawapa mwanya hata wanawake kufanya choice nzuri na Inakupa Uhuru wakuchagua umpendaye hureeeee chainese ila kutuletea bandia ndo noma

  11. Sajenti's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 24th April 2008
   Posts : 3,680
   Rep Power : 1502
   Likes Received
   350
   Likes Given
   95

   Default Re: Angalia njia mpya ya Wachina kutafuta wachumba!

   Quote By Akili Kichwani View Post
   swaaafi sana, sasa mambo ya kuliana bia na mishikaki kwisha, unaenda market unachukua mzigo, mchezo umeisha! da soko huria limetukomboa, tulikuwa tunahangaika kutongoza weeeeeeeeeeeee tunaliwa pesa na demu anayeyuka!!!!

   jamani wadau tuungane tupate wawekezaji haraka watuwekee haya maduka bongo immediately.

   itabidi nipitie china nikiwa njiani kurudi home niangalie uwezekano wa kuibuka na mchina,

   tehe tehehehe...................
   .. I like this...Kweli ndugu yangu maana vi-date na mizinga na uhakika wa mzigo huna...
   To get something you never had, you need to do something you never did

  12. #12
   bht's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 14th May 2009
   Posts : 10,164
   Rep Power : 85904272
   Likes Received
   1571
   Likes Given
   1348

   Default Re: Angalia njia mpya ya Wachina kutafuta wachumba!

   Quote By Akili Kichwani View Post
   swaaafi sana, sasa mambo ya kuliana bia na mishikaki kwisha, unaenda market unachukua mzigo, mchezo umeisha! da soko huria limetukomboa, tulikuwa tunahangaika kutongoza weeeeeeeeeeeee tunaliwa pesa na demu anayeyuka!!!!

   jamani wadau tuungane tupate wawekezaji haraka watuwekee haya maduka bongo immediately.

   itabidi nipitie china nikiwa njiani kurudi home niangalie uwezekano wa kuibuka na mchina,

   tehe tehehehe...................
   kule HEz ni wengi Kuliko Shez, sasa we AK si ni he? hautapata!!!
   You dont have to win every Argument, Agree to Disagree


  Similar Topics

  1. Utoh na njia mpya kumsafisha Jairo
   By Lokissa in forum Habari na Hoja mchanganyiko
   Replies: 21
   Last Post: 24th August 2011, 13:31
  2. Njia za kujadiliana mishahara na mwajili mpya wakati wa interview
   By Kimla in forum Nafasi za Kazi na Tenda
   Replies: 18
   Last Post: 28th April 2011, 14:08
  3. Serikali kutafuta njia mbadala kushindwa kwa shule za kata
   By Rutashubanyuma in forum Jukwaa la Elimu (Education Forum)
   Replies: 2
   Last Post: 2nd February 2011, 20:59
  4. Uwekezaji wa wachina waiweka Zambia njia panda...............
   By Rutashubanyuma in forum International Forum
   Replies: 4
   Last Post: 29th December 2010, 15:43
  5. Angalia aina hii mpya ya nyadhifa
   By KiuyaJibu in forum Jokes/Utani + Udaku/Gossips
   Replies: 0
   Last Post: 12th May 2009, 17:20

  Posting Permissions

  • You may not post new threads
  • You may not post replies
  • You may not post attachments
  • You may not edit your posts
  •  

  Who are WE?

  JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

  You are always welcome! Read more...

  Where are we?

  We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

  For anything related to this site please Contact us.

  Contact us now...

  DISCLAIMER

  JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

  Read more...

  Forum Rules

  JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

  You MUST read them and comply accordingly. Read more...

  Privacy Policy

  We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

  Read our Privacy Policy. Proceed here...