Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Suala la kuwa na imani tofauti linapotatiza taasisi ya ndoa...!

    Report Post
    Page 7 of 7 FirstFirst ... 567
    Results 121 to 138 of 138
    1. #1
      Mtambuzi's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 29th October 2008
      Location : Dar Es Salaam
      Posts : 6,182
      Rep Power : 27035
      Likes Received
      8457
      Likes Given
      17777

      Default Suala la kuwa na imani tofauti linapotatiza taasisi ya ndoa...!



      Kujadili dini ni mojawapo ya mijadala inayokwepwa na baadhi ya wanajamii ili kuepusha shari na kudumisha amani. Lakini linapokuja swala mahusiano hususan pale watu wawili wenye imani tofauti za kidini wanapotaka kuoana, unaweza kuzuka mjadala mzito miongoni mwa ndugu na jamaa wa wapenzi hao na wakati mwingine hata marafiki hutokea kupinga muunganiko huo.

      Ninao mfano unaonihusu. Mdogo wangu anayenifuatia kuzaliwa alipata mchumba (mume) mwenye imani tofauti na imani yetu, jambo hilo lilizusha mtafaruku katika familia yetu kila mmoja akisema lake. Ilitokea tu mimi na baadhi ya ndugu zangu akiwemo baba tuliafiki ule muunganiko wao na ndoa ikafungwa na sasa ndoa yao ni imara na imetimiza miaka tisa mwaka huu wakiwa na watoto watatu.

      Ukweli ni kwamba jambo hili limekuwa likileta mtafaruku katika baadhi ya familia na wakati mwingine familia hujikuta ikisambaratika hasa pale ambapo familia moja inashindwa kukubali utashi wa mtoto wao kuolewa au kuoa mtu mwenye imani tofauti na mara nyingi hii hutokea katika familia zenye msimamo mkali wa kidini. Kama inavyofahamika mapenzi ni kitu cha ajabu sana. Pale ambapo penzi linapochipua hufunika imani zetu kiasi cha kujikuta wakati mwingine tunazisaliti imani hizo ambazo hata hivyo baadhi yetu hazikuwa utashi wetu bali tu tumejikuta tukiwa humo kwa sababu ni imani ambazo tumezaliwa na kukuta wazazi wetu wakiwa ni wafuasi wa imani hizo.



      Huu ni mtihani mgumu sana kwetu na mara nyingi waathirika wa mtihani huu wengi wao ni wanawake na watoto ukilinganisha na wanaume. Wakati mwingine huwa najiuliza inakuwaje mtu anampata mpenzi anayempeda sana na mwenye sifa azitakazo lakini anashindwa kufunga naye ndoa kwa sababu ya kuwa na imani tofauti? Lakini pia wapo ambao wanalazimika kufunga ndoa na wapenzi wao sio kwa sababu wamependana, bali ni kwa sababu tu imani zao zinafanana…………!

      Kuna wanawake wengi sana wa kiasi cha kutosha wanalazimika kuishi katika ndoa ngumu kwa sababu ya imani zao, kilichowavuta kuingia katika muunganiko huo ni imani zao lakini sio upendo. Lazima tukubali kwamba mapenzi ni kitu kingine na imani ni kitu kingine. Kuingia katika ndoa kwa kigezo cha imani kunakuwa na changamoto zake ambazo mara nyingi hazina matokeao mazuri.

      Naamini hata humu JF wapo ambao wamewahi kukabiliana na mtihani huu au wako katika hati hati ya kukabiliana na mtihani huu. Hebu tupeane uzoefu juu ya jambo hili linalowatatiza wengi.

      Swali: Iwapo wewe ni single, Je uko tayari kufunga ndoa na mtu mwenye imani tofauti na imani yako? Je umejiandaaje kukabiliana na changamoto za wazazi, ndugu, marafiki na jamii kwa ujumla watakapopinga muunganiko wenu ?

      Nisingependa mjadala huu uwe ni wa kidini.

      Nadhani mmenielewa.........

      Invisible, bobsega, Pdidy and 1 others like this.


    2. #121
      Eiyer's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 17th April 2011
      Posts : 8,961
      Rep Power : 6904
      Likes Received
      2747
      Likes Given
      36

      Default Re: Ndoa na tofauti ya dini.....

      Well tuzungumzie dini inalitazamaje hili.Ukristo hauna mipaka,ninaposema hauna mipaka nina maana kuwa huhesabiwi kuwa mwenye kosa kuoana na mwenye dini tofauti,badala yake unaonekana ni mwenye imani iliyokomaa.Tatizo hapa sio dini zote ila baadhi ya dini.Tatizo linakuja kwa sababu dini hizo zinawatazama wale wenye dini nyingine kama less human,ukioana na mtu wa imani tofauti unakua umeikosea dini.Tatizo ni dini sio watu!
      Mtambuzi likes this.

    3. #122
      Horseshoe Arch's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th August 2009
      Location : Block A
      Posts : 1,316
      Rep Power : 770
      Likes Received
      171
      Likes Given
      39

      Default Re: Ndoa na tofauti ya dini.....

      Miaka yangu niliyoishi duniani nimepita na kuona wengi,wenye hulka,tabia na mienendo tofauti tofauti...nimejiingiza kwenye mahusiano mara mbili tatu achilia mbali 'hit & run' na mabinti wa dini niliyoiasili kwa wazazi wangu of which nachelea kuiita 'dini yangu'. Thereinafter nimekutana na binti mkamilifu na enye vikorombwezo anuai vinavyonipa mshawasha miaka nenda rudi (aliyeasili dini tofauti na niliyoasili mimi toka kwa wazazi wake)...tumejiiba vya kutosha na baadae tukaamua kukaa chini na kuhoji nafsi zetu..sitaoa dini yake,vivyo hivyo nae hataolewa na dini yangu! Tutaoana wenyewe...dini itaendelea kujihifadhi kwenye vitabu vitakatifu na mapenzi yetu yatarindima mioyoni mwetu daima!
      Mtambuzi likes this.
      We are what we think. With our thoughts we make the world.

    4. #123
      Kimbweka's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 16th July 2009
      Posts : 7,923
      Rep Power : 7252
      Likes Received
      1302
      Likes Given
      109

      Default Re: Ndoa na tofauti ya dini.....

      Quote By Straddler View Post
      Amen..!! Mheshimiwa Kimbweka!!! Afadhali ya leo umetupa darasa muhimu. Lakini kule kwenye jukwaa al-maarufu??
      Hahahahaha kule nin kwa kujivinjari bhana...teh tehte tehe
      "Life comes once only: No retake/replay/rewind/once-more. One should enjoy it, be happy & keep happy others too."

    5. #124
      kisukari's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 16th July 2010
      Posts : 2,629
      Rep Power : 3888
      Likes Received
      1415
      Likes Given
      661

      Default Re: Ndoa na tofauti ya dini.....

      sister wangu na mume wake,dini tofauti.na wapo zaidi ya miaka 20 katika ndoa yao.wamezaa watoto 3,watoto wamefata dini ya baba yao.nina rafiki yangu mwengine,mama yao na baba yao ni dini tofauti.na wapo pamoja zaidi ya miaka 25,na wana wajukuu.siku za sikukuu,iddi na x.mas husheherekea.kwa ninaowafahamu mimi naona maisha yako poa,inategemea wenyewe na makubaliano yenu
      Mtambuzi and SnowBall like this.

    6. #125
      Highlander's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th February 2012
      Posts : 1,781
      Rep Power : 727
      Likes Received
      553
      Likes Given
      632

      Default Re: Ndoa na tofauti ya dini.....

      Ndoa ya dini mbili tofauti inawezekana kabisa kudumu penye nia ya kuidumisha. Lakini mafanikio yake yanategemea sana hao wawili wanajua nini kuhusu dini. Yaani kujua Dini ni nini hasa. Mama mmoja Mkristo wa Madhehebu ya Lutheran nadhani, mfanyakazi mstaafu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anaitwa Mama Kundya (sijui Lydia jina lake la kwanza vile?) aliolewa na Mtanzania mwenzake Muumini wa dini ya Kiislamu (Kama anaitwa Ramadhani Kundya vile?), na ndoa hii ilikuwa ndoa ya amani kabisa. Hili la AMANI nina uhakika nalo. Dini ni utaratibu unaokubalika na jamii kumtafuta, kumjua, na kujenga uhusiano na Muumba, au kitu fulani kinachoaminika kuwa na nguvu na mamlaka kuu juu ya binadamu. Jamii mbalimbali zinakubaliana namna ya kufanya hili, na hiki ndicho kinazaa dini. Ukijua hili sasa unakuwa unajua kuwa dini karibu zote duniani zina lengo linalofanana, ambalo ni kumcha Mungu; tunatofautiana tu namna na kutekeleza hili. Kwa bahati nzuri dini nyingi zimeweka misingi ya haki za binadamu kama haki ya kuishi na haki nyingine zinazoainishwa katika umoja wa mataifa, kuwa sehemu ya imani kuwa ndicho Mungu anachokitaka kifanywe na binadamu wote. Kwa maana hii, dini zote zinaunganishwa na ari ya kumcha Mungu na wajibu wa kulinda haki za binadamu, Hivyo, mtoto wa kiume anapomtamani binti, au binti kumtamani kijana wa kiume kutoka imani tofauti, na ikatokea wote wawili nyota zao za mapenzi zimekubaliana, sasa panakuwapo vitu vitatu vinavyokubaliana, japo wanatoka katika dini tofauti: ari ya kumcha Mungu, wajibu wa kulinda haki za binadamu, na hamu ya kuwa pamoja. Hawa wawili wakiwa na uwezo mkubwa wa kufikiri, yaani kule kufikiri kunakoondoa ushabiki kama ule wa watu wenye upeo mdogo wa kufikiri, wanaweza kuishi kwa pamoja -hata kwa kuruhusu kila mmoja wao kumcha Mungu kwa namna anayoenda, na watatoa uhuru kwa watoto wao kuchagua namna watayopenda. Mama Kundya aliweza. Najua Pia kuwa mkuu wa kitengo cha biashara cha UDEC katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam aitwaye Mariam Nchimbi ni muumini wa Dini ya Kiislam ambaye anaishi na Mume wake Mwanajeshi Eng. Nchimbi ambaye ni Mkristo wa Madhehebu ya Kikatoliki nadhani, na ndoa yao ni ndoa ya amani kabisa. Watu wenye uelewa mkubwa, wasomi, wanajua dini zina lengo moja, ila majina ya hizi dini na taratibu zake vinabadilikabadilika kutokana na mila na desturi za binadamu wanaounda hizo dini kutofautiana tofautiana kidogo. Lakini ukweli ni kwamba dini zina lengo moja. Migogolo mingi ya kidini inatokana na ujinga wa wafuasi. Kwa mifano hii miwili, nataka kusema inawezekana kabisa wapenzi wa dini mbili tofauti kuishi katika ndoa yenye amani kabisa.


    7. #126
      SnowBall's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 13th September 2011
      Location : Amsterdam, Nertherlands
      Posts : 2,628
      Rep Power : 24029
      Likes Received
      2400
      Likes Given
      3298

      Default Re: Ndoa na tofauti ya dini.....

      Quote By kisukari View Post
      sister wangu na mume wake,dini tofauti.na wapo zaidi ya miaka 20 katika ndoa yao.wamezaa watoto 3,watoto wamefata dini ya baba yao.nina rafiki yangu mwengine,mama yao na baba yao ni dini tofauti.na wapo pamoja zaidi ya miaka 25,na wana wajukuu.siku za sikukuu,iddi na x.mas husheherekea.kwa ninaowafahamu mimi naona maisha yako poa,inategemea wenyewe na makubaliano yenu
      Naunga mkono hoja mia kwa mia..
      Mtambuzi likes this.
      ..''I wasted time, and now those time waste me''...Shakespear

    8. #127
      natu's Avatar
      Member Array
      Join Date : 4th October 2011
      Posts : 23
      Rep Power : 394
      Likes Received
      5
      Likes Given
      78

      Default Re: Usijidanganye! DINI TOFAUTI ZINA MAAFA YAKE KWENYE NDOA

      Quote By MwanaFalsafa1 View Post
      Mkuu baba yako angekua mdini angeoa Mkristo? Au una maanisha ni mshika dini? Maneno mengine angalia mkuu ukikosea kidogo tu unaleta tafsiri nyingine.
      nafikiri babake ni mdini ndio mana akaoa mkristo kwa sababu ninavyojua waislamu wanaruhusiwa kuoa wanawake wa vitabu

    9. #128
      Nakshi's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 30th June 2012
      Location : any where in this world i am in available
      Posts : 242
      Rep Power : 399
      Likes Received
      95
      Likes Given
      84

      Default Re: Suala la kuwa na imani tofauti linapotatiza taasisi ya ndoa...!

      kwani wote tunamuabudu nani? ni MUNGU, muislam ana muabudu mungu na mkristo vilevile na wote tunaomba na kusali juu yake yeye mungu me naona haina shida muislam kumoa/kuolewa mkristo na mkristo kumuoa/kuolewa muislam.
      Pdidy and Mtambuzi like this.

    10. #129
      decruca's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 18th June 2012
      Posts : 166
      Rep Power : 386
      Likes Received
      34
      Likes Given
      14

      Default Re: Suala la kuwa na imani tofauti linapotatiza taasisi ya ndoa...!

      kwa ambao bado hawajaingia kwenye ndoa nashauri wazingatie sana dini zao, hii itasaidia binti kutokubali hata urafiki na kijana asiye dini yake as well as kijana hatatafuta girlfriend asiye dini yake, maana hapo ndio mwanzo wa mahusiano yanayopelekea uchumba hadi ndoa. Mimi mwenyewe jpili hii ya juzi nimekatazwa kwenda na watoto wangu wa kuwazaa mwenyewe kanisani kisa sio dhehebu la baba yao iliniuma ila sikuwa na jinsi. Baba yao anadai waende kwenye dhehebu lake. hapo ni wote wakiristo sasa ingekuwa mkristo na muislam sijui ndio ingekuje kabisa.

    11. #130
      Jangakuu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th April 2012
      Posts : 369
      Rep Power : 434
      Likes Received
      139
      Likes Given
      257

      Default Re: Suala la kuwa na imani tofauti linapotatiza taasisi ya ndoa...!

      Swala Dini kwenye ndoa ni suala muhimu sana, katokana mambo yafuatayo

      1. Kuwalea watoto katika mstari na kuwahimiza kumpenda Mungu.

      Watoto wanaplekwa Msikini wana ambiwa "Mkristo ni kafili," na wengine wanaplekwa kanisani wana ambiwa "Yesu ni njia ya kweli na uzima" Wote wakirudi nyumbani ,Wana wauliza wazazi wao upi ni ukweli? kulingana na mafundisho kila mtu aliyoyapata.Wazazi wanabaki kuangliana . Hii inaleta picha mbaya kwa watoto.
      2.Kuepuka migogoro ya ndoa hasa pale Mzee yupo kwenye Mfungo wa Ramadhani na mama yupo kwenye Mambo ya Kiinjili (kanisani)
      3.Mafundisho ya Dini ni tofauti kila fundisho la dini moja,linakashifu dini nyingine.

      Mfano. Waislam wanasema Wakristo ni makafili, na mafundisho ya kiislamu yanasema Muhislamu safi hawezi kushare vitu na Kafili hasa .Tendo la ndoa na some times Chakula.NB. Baadhi ya mafundisho ya Dini fulani yanakataza kula baadhi ya vyakula e.g kitimoto.
      Na Baadhi ya Dini inasemekana kwamba Wanafuga Majini, Ibada za kikristo zinafukuza Majini.
      kwa Mtaji huo nyumba Haiwezi kusettle.

      Muhimu: Watu watakaa kwenye ndoa wakiwa na dini tofauti if and only if.Watahamua wote kuweka Dini zao pembeni na kuamua kujiunga na Dini nyingine ya Upagani(fiftyfifty uisilamu na aukristo) lakini huwezi ukuwa Mkristo Deep au Muhislamu Deep, ukiishi kwenye ndoa kama hiyo.

      Kwa hiyo natoa ushauri, ndoa iwe za watu wenye imani moja!! unless kila mtu aache misingi ya Dini yake. waamue kuwa Wapagani.

      Regards,

      jangakuu
      Pdidy likes this.

    12. #131
      Pdidy's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd November 2007
      Posts : 12,328
      Rep Power : 3455
      Likes Received
      1336
      Likes Given
      864

      Default Re: Suala la kuwa na imani tofauti linapotatiza taasisi ya ndoa...!

      Quote By mtambuzi View Post


      kujadili dini ni mojawapo ya mijadala inayokwepwa na baadhi ya wanajamii ili kuepusha shari na kudumisha amani. Lakini linapokuja swala mahusiano hususan pale watu wawili wenye imani tofauti za kidini wanapotaka kuoana, unaweza kuzuka mjadala mzito miongoni mwa ndugu na jamaa wa wapenzi hao na wakati mwingine hata marafiki hutokea kupinga muunganiko huo.

      ninao mfano unaonihusu. Mdogo wangu anayenifuatia kuzaliwa alipata mchumba (mume) mwenye imani tofauti na imani yetu, jambo hilo lilizusha mtafaruku katika familia yetu kila mmoja akisema lake. Ilitokea tu mimi na baadhi ya ndugu zangu akiwemo baba tuliafiki ule muunganiko wao na ndoa ikafungwa na sasa ndoa yao ni imara na imetimiza miaka tisa mwaka huu wakiwa na watoto watatu.

      ukweli ni kwamba jambo hili limekuwa likileta mtafaruku katika baadhi ya familia na wakati mwingine familia hujikuta ikisambaratika hasa pale ambapo familia moja inashindwa kukubali utashi wa mtoto wao kuolewa au kuoa mtu mwenye imani tofauti na mara nyingi hii hutokea katika familia zenye msimamo mkali wa kidini. Kama inavyofahamika mapenzi ni kitu cha ajabu sana. Pale ambapo penzi linapochipua hufunika imani zetu kiasi cha kujikuta wakati mwingine tunazisaliti imani hizo ambazo hata hivyo baadhi yetu hazikuwa utashi wetu bali tu tumejikuta tukiwa humo kwa sababu ni imani ambazo tumezaliwa na kukuta wazazi wetu wakiwa ni wafuasi wa imani hizo.



      huu ni mtihani mgumu sana kwetu na mara nyingi waathirika wa mtihani huu wengi wao ni wanawake na watoto ukilinganisha na wanaume. Wakati mwingine huwa najiuliza inakuwaje mtu anampata mpenzi anayempeda sana na mwenye sifa azitakazo lakini anashindwa kufunga naye ndoa kwa sababu ya kuwa na imani tofauti? Lakini pia wapo ambao wanalazimika kufunga ndoa na wapenzi wao sio kwa sababu wamependana, bali ni kwa sababu tu imani zao zinafanana…………!

      Kuna wanawake wengi sana wa kiasi cha kutosha wanalazimika kuishi katika ndoa ngumu kwa sababu ya imani zao, kilichowavuta kuingia katika muunganiko huo ni imani zao lakini sio upendo. Lazima tukubali kwamba mapenzi ni kitu kingine na imani ni kitu kingine. Kuingia katika ndoa kwa kigezo cha imani kunakuwa na changamoto zake ambazo mara nyingi hazina matokeao mazuri.

      naamini hata humu jf wapo ambao wamewahi kukabiliana na mtihani huu au wako katika hati hati ya kukabiliana na mtihani huu. Hebu tupeane uzoefu juu ya jambo hili linalowatatiza wengi.

      swali: iwapo wewe ni single, je uko tayari kufunga ndoa na mtu mwenye imani tofauti na imani yako? Je umejiandaaje kukabiliana na changamoto za wazazi, ndugu, marafiki na jamii kwa ujumla watakapopinga muunganiko wenu ?

      nisingependa mjadala huu uwe ni wa kidini.

      nadhani mmenielewa.........

      mkuu ukisoma baibo neno la mungu ni taa ya miguu yangu
      sasa basi nimekuwa na maombi ya ufahamu kw akila mwana jf si kwasababu tumelogwa bali
      tumegafilika...ukilijua neno yoh 17:17 nalo neno litakuweka huru

      sasa basi ukisoma baibo iko wazi kuhusu imani na naamini akuna atakaekimbilia tena kuhusu hili

    13. #132
      Pdidy's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd November 2007
      Posts : 12,328
      Rep Power : 3455
      Likes Received
      1336
      Likes Given
      864

      Default Re: Suala la kuwa na imani tofauti linapotatiza taasisi ya ndoa...!

      Quote By nakshi View Post
      kwani wote tunamuabudu nani? Ni mungu, muislam ana muabudu mungu na mkristo vilevile na wote tunaomba na kusali juu yake yeye mungu me naona haina shida muislam kumoa/kuolewa mkristo na mkristo kumuoa/kuolewa muislam.
      tema mate chini na mungu akuongoze
      kama wanavyosema msiba unauma usikukute sikia kwa wenzio sasa ikikuta hili ndio
      utajua umuhimu wa hii mada
      wito
      kama ujaolewa na unafikiria kuolew ana dini nyingine aijalishi nyumba nog ya katikati basi
      airisha kuolewa sio lazima uolewe kwenye mateso

    14. #133
      neggirl's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 30th July 2009
      Posts : 2,212
      Rep Power : 945
      Likes Received
      883
      Likes Given
      1284

      Default

      This topic is very complicated aisee, nafikir unaweza kupata jibu sahihi pale utakapobananishwa na haya mawili kwa pamoja lol(mapenzi ya dhati na Imani unayoimani)

    15. #134
      Catherine's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 30th June 2012
      Location : Dar
      Posts : 1,241
      Rep Power : 599
      Likes Received
      739
      Likes Given
      208

      Default

      Quote By kisukari View Post
      sister wangu na mume wake,dini tofauti.na wapo zaidi ya miaka 20 katika ndoa yao.wamezaa watoto 3,watoto wamefata dini ya baba yao.nina rafiki yangu mwengine,mama yao na baba yao ni dini tofauti.na wapo pamoja zaidi ya miaka 25,na wana wajukuu.siku za sikukuu,iddi na x.mas husheherekea.kwa ninaowafahamu mimi naona maisha yako poa,inategemea wenyewe na makubaliano yenu
      nimeona wanandoa wengi wenye dini tofauti wamedumu muda mrefu kwenye ndoa. Naamini ukiweza kuheshimu imani ya mwenzio hata yeye mwenyewe utamuheshimu na maisha yatakuwa ya furaha sana.
      Mtambuzi likes this.

    16. #135
      Mwanamayu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th May 2010
      Location : Manzese
      Posts : 3,049
      Rep Power : 1072
      Likes Received
      240
      Likes Given
      112

      Default Re: Suala la kuwa na imani tofauti linapotatiza taasisi ya ndoa...!

      Imani tofauti ni issue kubwa sana na very sensitive. Cha msingi ni kupata mwenza mwenye imani sawa!

    17. #136
      Jwagu's Avatar
      Member Array
      Join Date : 19th July 2007
      Location : Dodoma
      Posts : 58
      Rep Power : 620
      Likes Received
      8
      Likes Given
      3

      Default Re: Suala la kuwa na imani tofauti linapotatiza taasisi ya ndoa...!

      Mie mrutery, mchumba RC, yeye tunapendana sana, ila wakati huo hataki kwenda kinyume na matakwa ya wazazi wake. tumejaliwa mtoto, ila ndoa imekwama kwa sababu ya msimamo huo wa matakwa ya wazazi. najua nawa confuse kwa kusema tunapendana ila dini zinatutenganisha, kuna mengine ya ndani yanayoashiria hayo ila kwa kusimulia uta conclude kuwa hakuna upendo hapo!
      Mtambuzi likes this.

    18. #137
      mafia boy's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 7th January 2013
      Posts : 133
      Rep Power : 350
      Likes Received
      13
      Likes Given
      66

      Default Re: Suala la kuwa na imani tofauti linapotatiza taasisi ya ndoa...!

      mmmmh bwana watu waowane kwa imani zao maana endapo watoana kwa imani tofauti hao wote watakua wanamkosea mwenyezi mungu kama watakua wanamuamini kwa mfano waislam hawaruhusiwi kumuoa mtu asieamiini uislam,so endapo itatokea kuoa itakua kaoa tu si kwamba ndoa yake inatambulika na mwenyezi mungu,atakua anahesabiwa kama anaishi tu na mtu kama wanavyoishi watu wengine,ila si kindoa inayotakiwa na yeye,na itakua hujawatendea haki watoto katika mambo ya mirath na kadhalika,pia huifanyi dini yako kuenda mbele kwakua utakua haujafuata maamlisho na makatazo ya imani yako

    19. #138
      Vicent daudi's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 9th December 2012
      Posts : 116
      Rep Power : 351
      Likes Received
      17
      Likes Given
      1

      Default Re: Suala la kuwa na imani tofauti linapotatiza taasisi ya ndoa...!

      Kazi kweli mm pia. Nilipata shida sana pale nilipotaka kuoa muislamu wazazi waligoMa eti mpaka mm nibadili din nilikataa coz wao wanataka nimfuate binti na binti alikuwa tayari kubadili din basi tulichukuana hivyo na baadae church kama kawaida mpaka walipomtenga baadae wazazi wakakubali japo nduguze wamegoma baadae sana shemeji yangu aliyenitukana akaja bongo kutoka mbwinde eti kutafuta life bila hiyana nikamtafutia chumba akakaa na Kazi nikamtafutia akamwagiza mkewe wakaish wote baadae akaniambia anataka kubadili dini nikamwambia poa mpaka sasa ni mfuasi wa kristo aliporudi kwao mbwinde walishangaa na kudai Kuwa nimemlazimisha alidai hapana n maamuzi yake bila kushawishiwa na mtu

    Page 7 of 7 FirstFirst ... 567

    Similar Topics

    1. Hivi computer zina bit depth tofauti ?
      By Tectoner in forum Tech, Gadgets & Science Forum
      Replies: 1
      Last Post: 7th December 2011, 19:01
    2. Nasikia zina tofauti anaejua msaada pliz!!
      By kazuramimba in forum Jukwaa la Elimu (Education Forum)
      Replies: 9
      Last Post: 8th November 2011, 00:02
    3. Wakwe wanamnyima raha kwenye ndoa yake, ushauri please
      By marianne in forum Mahusiano, mapenzi, urafiki
      Replies: 9
      Last Post: 20th March 2011, 23:06
    4. Re: Hivi dini ya Kiislam na Kikristu zina tofauti?
      By Gama in forum Habari na Hoja mchanganyiko
      Replies: 0
      Last Post: 26th November 2010, 07:33

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...