Mahusiano, mapenzi, urafikiTubadilishane mawazo kuhusu mahusiano, mapenzi, urafiki, n.k na kushauriana. TAFADHALI: Hii si sehemu ya kuweka picha chafu ama kutumia lugha kali sana. Zitafutwa!
Kule uswahilini mara nyingi ndiko kunakosikika hili neno,naomba kuuliza, jambo lenyewe ni kubemenda mtoto. Sijawahi kuona mtoto aliyebemendwa. Hivi ni kweli kitu hicho kipo? na kinasababishwa na nini hasa? Kwa anayejua tafadhali mwaga hapa.
George_Porjie you are wrong, The farmer you half correct:
Kubemeda mtoto ni matokeo ya Mama na Baba wenye kichanga kufanya zinaa (kutembea nje ya ndoa yao) wakati kichanga kile bado kinanyonyeshwa. Hii dhana kwa tafsiri ya kisasa maana yake ni "malnutrition".
Endapo Mama ataendekeza ebeneke wakati anayonyesha most likely lishe kwa mtoto itapungua sana and equally endapo Baba ataendekeza "nyumba ndogo" kipindi hicho Mama atakuwa stressed na hataweza kumpatia mtoto lishe ya kufaa (esp kama anamnyonyesha unakuta hata maziwa hayatoki ifaavyo).
Kubemenda = Kwashakoo
Weekend Njema
Very correct and insightful. Ni maneno yenye tafsida. Kwa wengine hupitishwa kizazi na kizazi bila kujua maana. One has to think outside the box sometimes
__________________ "Absence of evidence is not evidence of absence" - No win-win situation
kubemenda mtoto ni ile hali ya kufanya mapenzi na mama mjamzito aliyekaribu kujifungua say miezi 7.5 hadi 9, na kutoa mbegu za kiume ambazo huweza kumwathiri mtoto tumboni
mara nyingi mtoto aliyebemendwa anakua na mabaka mwilini meusi hivi, mara nyingi tumboni, kwenye mbavu au sehemu za mikono(watoto nilio wahi kuwaona)
Mtoto akiwa tumboni anakuwa yuko ndani ya kifuko, mbegu zinaingia ingiaje tena na kumwathiri?! Uliyoyasema kuhusu mtoto kuwa na mabaka mabaka, sidhani kama sababu ndiyo hiyo, sidhani. In fact uliyoyasema mimi naona ni aina mojawapo ya mwendelezo wa imani zilizokuwa unfounded zenye lengo la kunyanyapaa baadhi ya watu (wenye mabakamabaka). Kwani naamini kuna jambo lingine kabisa tofauti na hiyo sababu uliyotoa inayosababisha hayo mabakamabaka.
__________________
Jamii ijuayo uwiano thabiti kati ya dharau, ubinafsi, chuki na ustaarab dhidi ya jamii nyingine na baina ya watu wake ni jamii yenye maendeleo. Isiyojua ni dumazi. SD1-09.
Fikra ni nyenzo endelezi au potofu. Changamoto tuliyonayo ni kuchanganua na kutenganisha kati ya fikra endelevu na fikra potofu, kwani mwisho wa fikra ni matendo pale fikra hazibakii kuwa fikra. SD6-07Rev.2-09.
Jf, the home of great thinker? Hii inatia shaka kwa majibu hapo juu. Waliogusia malnutrition na malezi hafifu wako right, walioongelea ngono , hizo ni misconception. Nimefanya thesis kwa hii kitu. Mwanzo wa neno ni pwani, ni inatokana na malezi hafifu ya kimlo kwa mtoto baada ya kuingiliwa na mapenzi mapya au stress kwa mlezi wa mtoto.
Haina tofauti na maana ya kwashiorkor, ambayo mwanzo wake ni ghana, ikiwa na maana ya mtoto aliyetelekezwa baada ya mama kupata mtoto mwingine kabla ya aliyefuatishwa kukua, au kuweza kutokuwa tegemezi. Ingieni google wakubwa.
IELEWEKE KUWA KUFANYA MAPENZI NA MAMA MJAMZITO, HAKUNA UHUSIANO NA MTOTO ATAKAYE ZALIWA KAMA YAI LILISHATIWA KIINI CHA KIUME. MADHARA PEKEE NI KAMA MAMA ANACERVICAL INCOPETENCE[SHINGO YA KIZAZI ILIYOLEGEA] . JF HII IWE MADA MAALUMU TUWATOE WATU MITONGOTONGO.
Jf, the home of great thinker? Hii inatia shaka kwa majibu hapo juu. Waliogusia malnutrition na malezi hafifu wako right, walioongelea ngono , hizo ni misconception. Nimefanya thesis kwa hii kitu. Mwanzo wa neno ni pwani, ni inatokana na malezi hafifu ya kimlo kwa mtoto baada ya kuingiliwa na mapenzi mapya au stress kwa mlezi wa mtoto.
Haina tofauti na maana ya kwashiorkor, ambayo mwanzo wake ni ghana, ikiwa na maana ya mtoto aliyetelekezwa baada ya mama kupata mtoto mwingine kabla ya aliyefuatishwa kukua, au kuweza kutokuwa tegemezi. Ingieni google wakubwa.
IELEWEKE KUWA KUFANYA MAPENZI NA MAMA MJAMZITO, HAKUNA UHUSIANO NA MTOTO ATAKAYE ZALIWA KAMA YAI LILISHATIWA KIINI CHA KIUME. MADHARA PEKEE NI KAMA MAMA ANACERVICAL INCOPETENCE[SHINGO YA KIZAZI ILIYOLEGEA] . JF HII IWE MADA MAALUMU TUWATOE WATU MITONGOTONGO.
asante mkuu kwa mchango wako,ngono na ukuaji wa mtoto anayepata lishe ya nguvu uhusiano uko wapi hapo.
Mkuu leta nyingine,ili tukiunganisha na wenzetu tunapata jibu safi.
Kubemendwa sio malnutrition. Wala havina uhusiano. Mtoto anaweza akawa anapata chakula vizuri kabisa na bado akabemendwa. Kwangu mimi na ambavyo nafahamu ni ile hali ya mama kufanya mapenzi na kumnyonyesha mtoto baada ya muda usio mrefu. Inakuwaje. Mama anayenyonyesha anapofanya mapenzi (katika hali ya kawaida, yaani staili ya kifo cha mende) kutakuwa na msuguano kati ya mwili wake (na hasa sehemu za matiti) na ule wa mwanaume. Msuguano huo utasababisha joto la maziwa ndani ya matiti kuongezeka (kwa lugha nyingine maziwa hayo yanakatika, yanakuwa hayako katika hali ya kawaida ya utulivu). Sasa kabla maziwa hayo ndani ya matiti hayajakaa sawa, mtoto akanyonyeshwa, lazima ataharisha, tena ataharisha maziwamaziwa. Kitendo cha kuharisha maziwamaziwa hivi ndio kinaitwa kubememdwa. Kwa hiyo inawezekana kabisa baba na mama ndani ya ndoa wakambemenda mtoto.
sahihi kabisa congo, ningependa kuongezea
mama ambaye ananyonyesha akishamaliza kufanya mapenzi anatakiwa ayakamue yale maziwa machafu (maziwa yanayokatika) mpaka maziwa masafi yaanze kutoka, alafu aoge(au ajikoshe sehemu za matiti na kifuani) kabla ya kumnyonyesha mwanawe.
mama akiweza kufanya hivi hambemendi mtoto hata siku moja na kama hawezi kufanya hivi ni bora amwenyeshe mtoto wake maziwa ya chupa
__________________ You can not keep 40m people quite forever....
one year one month one day they will wake up..........
Last edited by Semilong; 4th July 2009 at 04:33 PM..
sijui maana halisi ya mnachokiengelea,lakini bado napata wakati mgumu kuelewa hizo 'imani' za wengi.maana naona maelezo mengi hayaelezei ukweli.
mmh ngoja tusubiri tuone wengine watasemaje huenda ukweli ukaja baadaye.
Jamani mimi ni mgumu kuamini mambo mengine. Ukweli hapa inabidi kutenganisha athari za kiafya na zile za kiimani potofu. Kwa mfano sitetei mzazi kutoka nje, lakini hii haimanishi kumuathiri mtoto, ila kama hiyo itapunguza matunzom kwa mtoto ndiyo inaathiri.
Mtu anaweza asitoke nje ya ndoa na asimtunze mtoto. Japo ukweli ni kwamba kutoka nje ya ndoa mara nyingi(sio mara zote) huathiri ku-care familia.