Anakataa kuzaa, eti mpaka baada ya kumaliza Masters!
Mahusiano, mapenzi, urafikiTubadilishane mawazo kuhusu mahusiano, mapenzi, urafiki, n.k na kushauriana. TAFADHALI: Hii si sehemu ya kuweka picha chafu ama kutumia lugha kali sana. Zitafutwa!
Jamaa’ngu mmoja ana mchumba’ke ila sasa ni kama hawaelewani kwenye suala la kuzaa…..jamaa sasa ana 30yrs old anataka mtoto na msichana ndio kwanza yuko college…..na shori kakomaa anasema yeye atazaa mpaka ahitimu masters ambayo kama kuipata ni baada ya miaka minne 4….
…mna mshaurije huyu jamaa na mchumba’ke…...
nakubaliana nawe kwa mengine lakini hili sio. Miaka sio issue saana. Yaani mtu ana 35 akioa wa 25 imepitwa na wakati? Mkiwa wate 30s utaona jinsi atakavyokuwa anazeeka faster kabla yako then unaanza za huku na kule.
Ungesema reasonable age difference.
Mkuu age ndiyo is not a matter. Ila ninacho sema mimi unaangalia on a person to person basis. Mkuu hapa hauoni jamaa kaona anachelewa but the girl yeye anaona bado muda anao na anataka kusoma? Kama anaona anachelewa atatute binti ambae kamaliza mambo yote ya shule na pia kama yupo tayari kumsubiria amsubirie. SIkumaanisha mkuu kuwa mkipishana miaka kumi msioane ila ni obvious hapa kuwa jamaa anaona muda kwake umeenda na binti kwake anaona time is on her side.
__________________ "Ask not what your country can do for you, ask what you can do for your country"-JFK.
Jamaa yako inaonesha anakuwa mgumu sana kusoma alama za nyakati..Kwa kifupi huyo shori hamzimii msela kiivo na ndio maana jamaa anapomletea mambo ya kuzaa sijui kutotoa..anamchek kidaini huku moyoni akijisemea ' huyu vipi!!? '
Mi nawajua sana mademu mazee, akiwa hakuzimii na wala haoni future na wewe ataleta gunia la visingizio..Kwa kifupi shori ameegesha tu kwa mshikaji kujikinga mvua na mvua ikiisha anatambaa..
100% nakuunga mkono,miguu,kichwa na kiwiliwili,huyo demu ameshamuona jamaa mzigo wa kinyesi haubebeki.Jamaa ajue kuwa hiyo master ndio utenganisho wao,aaamini aasiaaamini ukweli ndio huo.
kwani jamani...inaruhusiwa kuzaa na mchumba wako au mke wako??....nadhani jamaa anapanick upuuzi tuu...wewe huwezi kuzaa na mchumba...anatakiwa azae na mkewe...hapo naona shorty yupo smart...ila kama ungeniambia short hataki kuolewa na kuwa mke kabla hajachukuwa masterz then ningesema mshkaji atafute demu mwingine aoe kisha azae naye
kingine ambacho najaribu kujiuliza...kwani mwanaume ukiwa na 30yrs ndio mwisho wa kuzaa?...au anataka kutuambia kuwa right time ya mwanaume kuzaa ni 30yrs?....
nachokiona hapa ni kuwa dada yetu amakuwa smart kuliko mshkaji ambaye hata mie naona anataka kumzalisha dada yetu bila ndoa kisha aoe mtu mwingine then dada yetu awe na mtoto asiye na malezi ya pande mbili......PATAMU HAPO.
USHAURI.....kijana kama unampenda binti...toa mahari, funga ndoa...then watoto na mipango mingine itakuwa ndani ya ndoa yenu...mkitaka kuzaa watoto 1, 2, 10, 20 etc na mkitaka kuzaa kabla ya masters, au hata baada ya kuwa mawaziri....yooote ni maamuzi yenu wanandoa.....usipende shortcut za mambo serious na maisha ya wenzako,....NI MTAZAMO TU
Naomba nenda uchagani ukaone wapenzi wengi wanazaa wakiwa wachumba na kufunga ndoa wakiwa na wajukuu japo maadili ya dini hayaruhusu,tembea uone.
Pengine binti anahofia kutokuolewa akizaa kabla ya ndoa. Mwambie rafiki yako amwoe huyo binti kwanza na atakubali tu kuzaa akiwa kwenye ndoa kuliko kuzaa akiwa kwenye uchumba.
mkuu ni mipangilio ya jamaa akifikisha umri fulani aachane na kuzaa.....imagine unazaa una 40 huyo mtoto atakuita baba au babu? pia kumbuka life expactancy ya mtanzania ni miaka 37 kama sijakosea....
Mkuu kulingana na UN life expectancy kwa male ni 51 na female ni 54 (kwa TZ) so hapo ni too much exaggeration,
Quote:
suala lilikuwa ndoa+mtoto.....
kama ni hivyo na bado binti akakataa, basi hakuna kitu apo, jamaa atambae tu
__________________ "" Nalisema nitayakiri maasi yangu kwa Bwana, naye atanisamehe upotovu wa dhambi zangu"
Mimi nimemshauri wakati akimsubiria bibie amalize masters yake na yeye anahitaji mtoto basi atafute wa kumzalia na wakubaliane na bibie......maana naona jamaa ananyanyaswa...
Sina uhakika kama nimesoma vizuri.....si ni wachumba?watazaaje sasa!Wasubiri wafunge ndoa ndo wazae.Si ndo taratibu au?
Sorry kama siendi na wakati !
Kama huyo dada amekataa kuzaa inamaana chances are high kuwa amekataa vyote
Huyu binti anatengeneza mazingira ya kumkatisha tamaa jamaa na huyu binti tayari katika kichwa chake anayo plan yake na anajua wazi jamaa hawezi vumilia kwa 4yrs na sasa jamaa ana 30 lazima atakata tamaa ni bora amweke wazi na jamaa awe na msimamo.
__________________ Ukiuza utumbo usiogope nzi. Chuda Raha
Siku atakapoambiwa nasafiri kikazi kwenda mkoa wiki mbili na yeye akae na mtoto wa miezi mitatu atafanyaje? Huyo demu yuko sahihi ila jamaa yetu ndo kimeo. Ndoa za kupulizia zilikuwa zamani, mwambie jamaa awe makini,atavurugwa na huyo demu bure.
kwani jamani...inaruhusiwa kuzaa na mchumba wako au mke wako??....nadhani jamaa anapanick upuuzi tuu...wewe huwezi kuzaa na mchumba...anatakiwa azae na mkewe...hapo naona shorty yupo smart...ila kama ungeniambia short hataki kuolewa na kuwa mke kabla hajachukuwa masterz then ningesema mshkaji atafute demu mwingine aoe kisha azae naye
mkuu hukunisoma.....nilisema jamaa anataka ndoa+kuzaa....upo? kitu ambaco yeye anataka ni wafunge ndoa then wazae sasa kwa 4yrs muhanga anaona kama ni mateso kisa masters......
kingine ambacho najaribu kujiuliza...kwani mwanaume ukiwa na 30yrs ndio mwisho wa kuzaa?...au anataka kutuambia kuwa right time ya mwanaume kuzaa ni 30yrs?....
mkuu nani ana mpango wa kuitwa babu na watoto wake? miaka hii maisha mafupi......