Anakataa kuzaa, eti mpaka baada ya kumaliza Masters!
Mahusiano, mapenzi, urafikiTubadilishane mawazo kuhusu mahusiano, mapenzi, urafiki, n.k na kushauriana. TAFADHALI: Hii si sehemu ya kuweka picha chafu ama kutumia lugha kali sana. Zitafutwa!
Jamaa’ngu mmoja ana mchumba’ke ila sasa ni kama hawaelewani kwenye suala la kuzaa…..jamaa sasa ana 30yrs old anataka mtoto na msichana ndio kwanza yuko college…..na shori kakomaa anasema yeye atazaa mpaka ahitimu masters ambayo kama kuipata ni baada ya miaka minne 4….
…mna mshaurije huyu jamaa na mchumba’ke…...
Yo Yo mi naona huyu binti hampendi jamaa ako hii ni zuga tu unajua kama shori hakupendi atakutafutia visababu vidogo vidogo ili ushindwe mwambie jamaa apige chini tu mashori wapo kibao.
__________________ Ukiuza utumbo usiogope nzi. Chuda Raha
Yo yo acha kuwa na mtazamo finyu! suala la huyo dada kusoma ni suala la mtu binafsi na future yake (ni maisha ya mtu hapa unazungumzia) na kati ya vitu ambavyo mimi binafsi sipendi kuingiliwa ni pamoja na maisha yangu binafsi, to me my first priority is me & myself! siwezi kuruhusu eti mchumba alazimishe kuharibu mipangilio yangu eti kisa mtoto, wakati majority hata si waaminifu, wewe utakatisha mambo yako kisa mimba na mtoto, yeye huku akiwa kakutia mimba still anaendelea na mambo yake kwani habebi tumbo wala hanyonyeshi, yeye anapata PhD, wewe ndio unaanza kurudi kwenye masters, then kesho aseme hukusoma kama yeye, mara akuletee watoto wa nje. Mie ningemuona hy dada namwambie akomae na msimamo wake, huyo mume akiona anchelewa mbona visichana vya x-std 7 ambavyo havina wazo laolote la kuendelea hata na kozi ya ushonaji viko kibao tu mtaani, atafute kamoja aoe ili azae hata 10 akitaka! halafu mke wa ndoa usijali ana mvuto gani ukitaka mivuta tafuta machangu hao alwayz wana mvuto! mambo ya kuangalia sura na shepu hata kama mke mwenyewe mzigo yamepitwa na wakati kaka! get up
He he he..
Ahh nyie mnaongeaga tu..Hivi wewe umeona wapi watu wanaaihirisha ndoa kwa miaka 4? Miaka 4 ni mingi sana aisee na kama ni katoto katakuwa kanaenda nursery school tena kanaweza hata kujua kusoma na kuandika...! hi hi hi
Jamaa kutaka mtoto inamaanisha jamaa ndo amefika Kigoma mwisho wa reli, anataka kuanzisha ka-familia na yeye aitwe baba..na mamsapu pembeni ..ila mdada ndio hivyo..stimu hazipo..anachelea kusema ukweli. Suala la kusema mdada ajitangulize maono yake ndio dalili ya kutompenda msela..hakuna kingine..kama unampenda..shori anayemzimia mtu hawezi kurusha hilo suala kwa miaka 4..huo utakuwa ujuha flani ivi..
__________________ Avatar's Msg: Hiyo ni trailer ya wapenda kula vya watu. Ha ha ha..
kwani jamani...inaruhusiwa kuzaa na mchumba wako au mke wako??....nadhani jamaa anapanick upuuzi tuu...wewe huwezi kuzaa na mchumba...anatakiwa azae na mkewe...hapo naona shorty yupo smart...ila kama ungeniambia short hataki kuolewa na kuwa mke kabla hajachukuwa masterz then ningesema mshkaji atafute demu mwingine aoe kisha azae naye
kingine ambacho najaribu kujiuliza...kwani mwanaume ukiwa na 30yrs ndio mwisho wa kuzaa?...au anataka kutuambia kuwa right time ya mwanaume kuzaa ni 30yrs?....
nachokiona hapa ni kuwa dada yetu amakuwa smart kuliko mshkaji ambaye hata mie naona anataka kumzalisha dada yetu bila ndoa kisha aoe mtu mwingine then dada yetu awe na mtoto asiye na malezi ya pande mbili......PATAMU HAPO.
USHAURI.....kijana kama unampenda binti...toa mahari, funga ndoa...then watoto na mipango mingine itakuwa ndani ya ndoa yenu...mkitaka kuzaa watoto 1, 2, 10, 20 etc na mkitaka kuzaa kabla ya masters, au hata baada ya kuwa mawaziri....yooote ni maamuzi yenu wanandoa.....usipende shortcut za mambo serious na maisha ya wenzako,....NI MTAZAMO TU
__________________ if we die the next generation will fight them too..and the one after them untill the victory is on our side
kwani jamani...inaruhusiwa kuzaa na mchumba wako au mke wako??....nadhani jamaa anapanick upuuzi tuu...wewe huwezi kuzaa na mchumba...anatakiwa azae na mkewe...hapo naona shorty yupo smart...ila kama ungeniambia short hataki kuolewa na kuwa mke kabla hajachukuwa masterz then ningesema mshkaji atafute demu mwingine aoe kisha azae naye
kingine ambacho najaribu kujiuliza...kwani mwanaume ukiwa na 30yrs ndio mwisho wa kuzaa?...au anataka kutuambia kuwa right time ya mwanaume kuzaa ni 30yrs?....
nachokiona hapa ni kuwa dada yetu amakuwa smart kuliko mshkaji ambaye hata mie naona anataka kumzalisha dada yetu bila ndoa kisha aoe mtu mwingine then dada yetu awe na mtoto asiye na malezi ya pande mbili......PATAMU HAPO.
USHAURI.....kijana kama unampenda binti...toa mahari, funga ndoa...then watoto na mipango mingine itakuwa ndani ya ndoa yenu...mkitaka kuzaa watoto 1, 2, 10, 20 etc na mkitaka kuzaa kabla ya masters, au hata baada ya kuwa mawaziri....yooote ni maamuzi yenu wanandoa.....usipende shortcut za mambo serious na maisha ya wenzako,....NI MTAZAMO TU
Kama huyo dada amekataa kuzaa inamaana chances are high kuwa amekataa vyote
__________________ Avatar's Msg: Hiyo ni trailer ya wapenda kula vya watu. Ha ha ha..
Kama hawawezi kuelewana kwa suala dogo kama hilo, je wakiingia kwenye ndoa itakuwaje
By the way wanatakaje mtoto na huku hawajaoana?
Anaweza kuzaa,naona huyu ndugu anaehitaji mtoto amekaa akafikiria musktaka bali wa maisha yake akaona siku zina songea na umri wa kuishi nao unapungua,so naona ameona asiondoke kwenye hii dunia pasipo kuacha mtoto.
Na mshauri jamaa atafute mwanamke ambae atakuwa ni mke wake then ndio wazaae nae.Unajua kuna madhara mengi sana kuzaa mtoto nje ya ndoa mwishowe mtoto hanakosa malezi ya pande zote mbili.
__________________ Mtu aliye dhalimu ni chukizo kwa wenye haki,na mnyofu wa mwenendo ni chukizo kwa waovu.
Wangapi wanazaa wakiwa college jamani na wanaendelea na kitabu kama kawa? Huyu binti anatafuta njia ya kumkataa jamaa ndo maana kampa miaka 4 akivumilia hiyo atawepewa tena 6 hehehehe
__________________ Ukiuza utumbo usiogope nzi. Chuda Raha
Mambo ya kuoana watu mumepishana miaka 10 sijui yamesha pitwa na wakati. Tell your bro to wait or move on.
nakubaliana nawe kwa mengine lakini hili sio. Miaka sio issue saana. Yaani mtu ana 35 akioa wa 25 imepitwa na wakati? Mkiwa wate 30s utaona jinsi atakavyokuwa anazeeka faster kabla yako then unaanza za huku na kule.
Wangapi wanazaa wakiwa college jamani na wanaendelea na kitabu kama kawa? Huyu binti anatafuta njia ya kumkataa jamaa ndo maana kampa miaka 4 akivumilia hiyo atawepewa tena 6 hehehehe
na huyo bwana nae asiwe king'ang'anizi lazima usomi wake umsaidie pia kusoma alama za nyakati, kama binti ni myeyushaji atamjua tu si lazima apige ramli, na kama nia ni kusoma tu ila wanapendana atamvumilia tu, kwani upendo wa kweli huvumilia!