habari za leo wana jamii..??? dah sijuwi hata nianzie wapi..! ila ukishangaa ya Musa utashangaa ya firauni! kama unavojuwa ilikuwa tarehe 18-8-2012 ilikuwa namvisha pete mtarajiwa, alifika hapa zenji tarehe 16 usiku tulipanga siku iliyo fuata yani tarehe 17 twende kupima afya zetu. hatujawahi kunfanya tedo la ndoa hata cku 1 sikupenda kufanya mapenzi kwahofu maana ukiwa na hofu huwezi faidi mahaba.tulifika hosbital ya JWTZ ipo bububu hapa zenji. vipomo nikama hivi H I V poa uzazi ana mimba ya miezi 3
na wiki mbili. sikuamin kabisa nikamuuliza alikuwa hajuwi?? hakusema lolote! na aliondoka bila kumuaga mtu yoyote, mpoka hivi leo yani mda huu hapokei sim yangu, nimempigia sim dada ake kasema amefika leo Dar. jamani nifanye nini..?? naomba ushauri wenu.....
Katoe sadaka ya shukrani, ulikuwa ushikishwe mzigo huo.
ushauri wangu nakushauri uachane nae maadamu sio baba watoto mtarajiwa wa kiumbe kilichoko tumboni,tafuta mwanamke mwingine,mbona wanawake wako wengi tu?hapo kitu alichotaka kufanya ni kukubambikizia hiyo mimba kuwa ni ya kwako na alikuwa anataka kukupa mzigo wewe ukastukia dili hivyo amua kuvua gamba ndugu yangu.hata endapo utamsamehe ukaamua kumwoa hakika hataweza kuwa mwaminifu katika ndoa yako bali itakuwa ndoa ya malumbano kila uchwao.mpaka anafikia hatua ya kubeba mimba ni kwamba anakidumu wake anayempenda hebu jiulize kwanza kaka tuko wangapi?tulizana maisha mafupi.
Sasa kakaangu uamuzi wako wa kupima kwanza umekusaidia sana kuepuka kulea mwana asiye wako! Mshukuru sana Mungu aliyekuongoza kwenye jambo hili. Furahi na shangilia na huyo dada mpishe apite mbali. Tafuta mwingine.
Sasa kakaangu uamuzi wako wa kupima kwanza umekusaidia sana kuepuka kulea mwana asiye wako! Mshukuru sana Mungu aliyekuongoza kwenye jambo hili. Furahi na shangilia na huyo dada mpishe apite mbali. Tafuta mwingine.
Dah, nimekuonea huruma sana kaka yangu, ukizingatia nilikuwa nakufatilia tangu ulipotoa tangazo la kutafuta mchumba hapa JF, ulipompata ukatujulisha kwa furaha zote nasi tukafurahi pamoja nawe, ukatutaarifu na kutukaribisha kwenye sherehe ya kumvalisha pete huyo laaziz wako...Dah..
Kumbe mwisho wa siku ndio umepata bonge la surprise hivyooo!! Ila mi naomba tuu nikupe onyo my brother, usikurupuke kumpata mpenzi leo halafu baada ya miez mitatu tuu useme unaoa.. Dunia ya sasa yataka kuchunguzana ndugu hata kwa miezi sita walau.. Natumaini utakuwa umejifunza..! Pole saaana bro!
Follow Us Here