JamiiSMS
  Show/Hide This

  Topic: Sifa za Mwanamume wa kweli (A real man) tena wa Kiafrika

  Report Post
  Page 1 of 27 123 11 ... LastLast
  Results 1 to 20 of 522
  1. Dark City's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 18th October 2008
   Location : Roaming
   Posts : 15,764
   Rep Power : 272909914
   Likes Received
   11012
   Likes Given
   17657

   Default Sifa za Mwanamume wa kweli (A real man) tena wa Kiafrika

   Ndugu wadau, baada ya kuona na kushiriki mijadala mingi, nimeonelea nitoe mchango wangu ili ndugu, dada, binti na wajukuu zetu waweze kuelewa tunavyomfahamu mwanamume wa kweli (A real man) tena wa Kiafrika.
   1. Siku zote hujitahidi kwa kila njia kuonesha kuwa yeye ni mwanamume na siyo mvulana mkubwa (big boy) au mwanamke asiye kuwa na maziwa huku akiwa ndani ya suruali.
   2. Hufanya maamuzi pale pale inapotakiwa na husimama kidete kuhakikisha maamuzi yake muhimu (yale ya busara) yanatekelezwa tena kwa gharama yoyote. Mwanamume wa kweli hatoi kauli tata na kauli zake huwa ni aina fulani ya maelekezi (orders) ya jinsi ya kudeal na issues zote muhimu ndani nyumba!
   3. Huwa halii lii ovyo hata kama kafiwa. Hujitahidi kutowaambukiza weliomzunguka emotional break down. Kwa hiyo, inapobidi kulia, huficha sura yake. Mwanamume wa kweli hawezi kuangua kilio mbele za watu hata kama kafiwa na Mungu wake!!
   4. Hatelekezi familia hata siku moja bali uhakikisha ustawi wa familia yake unakuwa kipaumbele chake cha kwanza. Watoto watapata matunzo mazuri (bila ubaguzi) kwa kadri ya uwezo wa familia na mke wake atapewa kipaumbele cha kwanza katika matumizi ya rasrimali za familia (family resources)
   5. Hufanya kila njia mke wake awe na furaha na amani kwa kumpa haki zake zote za ndoa bila mzaha (she needs a full dose).
   6. Inapotokea akachepuka mara moja moja, hutengeneza mikakati ya kuhakikisha kuwa tahadhari kubwa imefanyika ili kumlinda mke wake na familia kwa ujumla…Ushauri wa The Boss hutumika katika mambo haya. CLICK HERE
   7. Husimama kwenye mstari ili kusimamia mambo ya msingi (principles) katika uendeshaji wa familia yake kama kiongozi imara. Na pale anapokosea, hutumia mbinu za kiutu uzima kuweka mambo sawa. Kamwe hatakubali shinikizo la mke wake katika kutatua matatizo ya kifamilia ndani ya nyumba yake!
   8. Mwanamume wa kweli hafanyi mambo ya mzaha mzaha na kuomba omba misamaha isiyo na kichwa wala miguu! Hata hivyo, anaweza kuomba msamaha kwa mke wake katika mambo ambayo hayagusi misingi na uwepo wa ndoa. Ila kamwe, hatakiwi kukiri kutoka nje ndoa. Hata pale anapokamatwa ugoni (labda akutwe bolt imefungwa na nut), atatumia mbinu zozote ikiwa ni pamoja na msaada wa wanaume wenzake (wakati mwingine hata wanawake) kutunza imani ya mke kwake. Hata siku moja, hatakiwi kumweleza mke wake (kwa kinywa chake) eti katembea nje ya ndoa.
   9. Siku zote atakuwa mwanamume na baba na hatafanya michezo ya kucheka cheka kipuuzi ama mbele ya watu au wanafamilia…Lazima kila kinywa kikiri kuwa kweli huyu ni baba ndani ya nyumba!!
   10. Hakimbii matatizo hata yakiwa makubwa kiasi gani…Atayakabili kwa mbinu zozote zile ili kulinda heshima ya uanaume na ubaba wake….Ndiyo maana, watoto wadogo wanaamini kuwa baba hashindwi na jambo lolote. Kuwaonesha watoto na hata mke kuwa baba ana vitu asivyoviweza ni kuwaharibu kisaikolojia!
   11. Ataonesha siku zote kwamba hasemi uongo. Hata pale atakaposema uongo mtakatifu (mfano, kumficha kitu mke wake ili kutomvunja moyo au kuharibu imani yake kwake), atalinda maneno yake kwa gharama zozote!!
   12. Atapigania himaya yake kwa nguvu na gharama zozote zile….Hawezi kukubali kudhalilishwa mbele ya mke na watoto wake! Bora afe kuliko kuona hayo yakifanyika machoni pake!


   Nawatakia week njema,

   Babu DC!!

   Updates   Quote By snowhite View Post
   1. mwanaume wa kiafrika anapenda apokewe anaporudi nyumbani nakumbuka iliuwa lazima tumpokee baba akirudi home
   2. mwanaume wa kifrika anataka kuandaliwa chakula kilichopikwa na mkewe tena chakula chenyewe sio tambi na sausage mbili.lazima iwe wali/ugali na samaki kwa mfano mboga za majani zilizoungwa karanga na maharage ya nazi hivo ndo vyakula nilikuwa naona babangu anapikiwa nyumbani kwetu
   3. mwanaume wa kiafrika akiingia ndani wote kimyyyaaaa,babangu alikuwa ana kiti chake sebuleni hicho hakalii mtu hata asiwepo home mwezi,alikuwa ana vyombo vyake vya chakula havitumiwi na mtu hivyo
   4. mwanaume wa kaifrika ni problem solver,tulikuwa tunaogopa sana umeme ukikatika halafu baba hayupo nyumbani
   5. mwanaume wa kiafrika alikuwa na mwendo ambao ukiuona tu unajua yes huyu babake mtu,nakumbuka tulikuwa tukiongozana kwenda kanisani sisi mbele,then mama halafu baba nyuma
   6. mwanaume wa kiafrika kabla ya kulala anazunguka nyumba yake yote kuangalia usalama na kuwa wa mwisho kufunga milango,
   7. mwanaume wa kiafrika haonekani katika kila tukio mtaani mengi anamuachia mkewe
   8. mwanaume wa kiafrika anatunza familia na kuilinda   LOL!

   Quote By gfsonwin View Post
   babu DC nimesoma michango ya watu wote kimsingi nimekubali sasa leo kwa mara ya kwanza nimekutana na vile vitu nivipendavyo na ambavyo navifurahia katika maisha. naomba niongee kitu hapa.
   1. Mwanaume halis wa kiafrika huwa haogopi kuface tatizo hata siku moja.
   2. Mwanaume halisi wa kaifrika siku zote ana msimamo hata ama msimamo wake hauko sawa huwa anabaki nao na anaurekebisha mwenyewe kipole pole.
   3. Mwanaume halisi wa kiafrika kauli yake ni moja tu kama ndiyo ni ndiyo na kama siyo ni syo na hana ndiyo siyo.
   4. Mwanaume halisi wa kiafrika huwa akichinja mbuzi nyumbani kwake huakikisha analisha mwenyewe watu wa familia yake. yaani mama anapika nyama isha anitenga mezani baba anakata kata anawapa wanawe. uchagani ndo ilivyo.
   5. Mwanaume halisi wa kiafrika huwa haingii chumbani kwa binti zake na wala haingii jikoni kuangalia kinachoendelea.
   6. Mwanaume halisi wa kaifrika huona faharisana juu ya mtoto wake anaye mtii na anayefaulu sana ila kwa anyefeli lol! huangusshiwa msalaba huo mama.
   Last edited by Dark City; 17th August 2012 at 22:15.
   "WE ALWAYS DON'T CHANGE UNTIL THE COST OF STAYING THE SAME EXCEEDS THE COST OF CHANGE.... 31 OKTOBA 2010 AND 25 OCTOBER 2015 WILL REMAIN MY LANDMARKS"

   Retired Maj Gen DC (1947)...[email protected]


  2. Kongosho's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 21st March 2011
   Location : Location loading...
   Posts : 36,166
   Rep Power : 138795851
   Likes Received
   23335
   Likes Given
   23325

   Default Re: Sifa za Mwanamume wa kweli (A real man) tena wa Kiafrika

   haswaaaa, na wakati wa sikukuu haleti maua bali jogoo na mchele.

   Idd hiyo, wee nanii, nataka hivyo.

  3. Kongosho's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 21st March 2011
   Location : Location loading...
   Posts : 36,166
   Rep Power : 138795851
   Likes Received
   23335
   Likes Given
   23325

   Default Re: Sifa za Mwanamume wa kweli (A real man) tena wa Kiafrika

   yaani babu DC hapo namba 9, mie hoi.

   Sio baba anacheka cheka hadi vifungo vya shati vinafunguka mbele ya hausi gelo lol

  4. Ndahani's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 3rd June 2008
   Location : Somewhere
   Posts : 11,248
   Rep Power : 4467
   Likes Received
   3567
   Likes Given
   6900

   Default Re: Sifa za Mwanamume wa kweli (A real man) tena wa Kiafrika

   Dark City,
   Kuna wanaume siku hizi wanatelekeza watoto kwa hoja za kuacha mbachao kwa msala upitao. Ijumaa itakuwa njema umetukumbusha.
   We are all inventors, each sailing out on a voyage of discovery, guided each by a private chart, of which there is no duplicate. The world is all gates, all opportunities.
   Ralph Waldo Emerson

  5. mwaJ's Avatar
   JF Tanzanite Member Array
   Join Date : 27th September 2007
   Location : Nowhere
   Posts : 4,086
   Rep Power : 14867
   Likes Received
   2925
   Likes Given
   2116

   Default Re: Sifa za Mwanamume wa kweli (A real man) tena wa Kiafrika

   Quote By Kongosho View Post
   haswaaaa, na wakati wa sikukuu haleti maua bali jogoo na mchele.

   Idd hiyo, wee nanii, nataka hivyo.
   Haswaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa aaaaaaaaaaa!
   “Anyone who has never made a mistake has never tried anything new” -
   Albert Einstein


  6. Dark City's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 18th October 2008
   Location : Roaming
   Posts : 15,764
   Rep Power : 272909914
   Likes Received
   11012
   Likes Given
   17657

   Default Re: Sifa za Mwanamume wa kweli (A real man) tena wa Kiafrika

   Quote By Kongosho View Post
   yaani babu DC hapo namba 9, mie hoi.

   Sio baba anacheka cheka hadi vifungo vya shati vinafunguka mbele ya hausi gelo lol

   Ahsante sana Kongosho......mbona sasa uzi wangu hujautendea haki.....au hicho ki-button kimefutwa??


   Sidhani kama kuna mtu (hata wanawake) anayemhusudisha baba anayecheka cheka kama taahira!!

   Umesahau lile tangazo la Kanumba la StarTimes lilivyokera watu??

   Babu DC!!
   "WE ALWAYS DON'T CHANGE UNTIL THE COST OF STAYING THE SAME EXCEEDS THE COST OF CHANGE.... 31 OKTOBA 2010 AND 25 OCTOBER 2015 WILL REMAIN MY LANDMARKS"

   Retired Maj Gen DC (1947)...[email protected]

  7. Dark City's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 18th October 2008
   Location : Roaming
   Posts : 15,764
   Rep Power : 272909914
   Likes Received
   11012
   Likes Given
   17657

   Default Re: Sifa za Mwanamume wa kweli (A real man) tena wa Kiafrika

   Quote By Kongosho View Post
   haswaaaa, na wakati wa sikukuu haleti maua bali jogoo na mchele.

   Idd hiyo, wee nanii, nataka hivyo.
   Kwenye hili, misimamo ya wanaume wa kweli inajulikana,

   Hebu muulize @akukumbushe anavyopokelewaga matenga ya kuku, tena mitetea kiimba nyimbo za kuaga kwao!!

   Raha sana kumpekekea mama watoto zawadi za kweli ambazo siyo hizo zenu za kisanii!!

   Babu DC!!
   "WE ALWAYS DON'T CHANGE UNTIL THE COST OF STAYING THE SAME EXCEEDS THE COST OF CHANGE.... 31 OKTOBA 2010 AND 25 OCTOBER 2015 WILL REMAIN MY LANDMARKS"

   Retired Maj Gen DC (1947)...[email protected]

  8. Bishanga's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 29th June 2008
   Location : SIRIUS
   Posts : 15,349
   Rep Power : 3799452
   Likes Received
   9866
   Likes Given
   8644

   Default Re: Sifa za Mwanamume wa kweli (A real man) tena wa Kiafrika

   Salute mkuu disii!
   Nakuunga mkono kwa asilimia kubwa isipokuwa hapo namba 3. Mkuu kufiwa kunauma ni balaa,mwaka jana nilifiwa na baba yangu,we acha tu,msiba hauna ushujaa. Kambarage na ubabe wake 1984 unakumbuka alivyomlilia Sokoine?
   Tuanze roll call ya wachangiaji ( interesting to know watasemaje):
   gfsonwin, Kaunga, Mamndenyi, cacico BADILI TABIA, Yummy FirstLady1, Zion Daughter and the gang.

  9. Bishanga's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 29th June 2008
   Location : SIRIUS
   Posts : 15,349
   Rep Power : 3799452
   Likes Received
   9866
   Likes Given
   8644

   Default

   Quote By Kongosho View Post
   yaani babu DC hapo namba 9, mie hoi.

   Sio baba anacheka cheka hadi vifungo vya shati vinafunguka mbele ya hausi gelo lol
   @ kongosho,una mme weye?

  10. Ndahani's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 3rd June 2008
   Location : Somewhere
   Posts : 11,248
   Rep Power : 4467
   Likes Received
   3567
   Likes Given
   6900

   Default Re: Sifa za Mwanamume wa kweli (A real man) tena wa Kiafrika

   Quote By Kongosho View Post
   yaani babu DC hapo namba 9, mie hoi.

   Sio baba anacheka cheka hadi vifungo vya shati vinafunguka mbele ya hausi gelo lol
   Teh teh teh...wengine wamejaliwa kucheka cheka..watafanyaje sasa? Nyumba zao wanajenga kwa mizaha mizaha na siku zinaenda. Nyumba zinakuwa za kiswahili kama nyumba nyingine
   We are all inventors, each sailing out on a voyage of discovery, guided each by a private chart, of which there is no duplicate. The world is all gates, all opportunities.
   Ralph Waldo Emerson

  11. Ndahani's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 3rd June 2008
   Location : Somewhere
   Posts : 11,248
   Rep Power : 4467
   Likes Received
   3567
   Likes Given
   6900

   Default Re: Sifa za Mwanamume wa kweli (A real man) tena wa Kiafrika

   Quote By Bishanga View Post
   Salute mkuu disii!
   Nakuunga mkono kwa asilimia kubwa isipokuwa hapo namba 3. Mkuu kufiwa kunauma ni balaa,mwaka jana nilifiwa na baba yangu,we acha tu,msiba hauna ushujaa. Kambarage na ubabe wake 1984 unakumbuka alivyomlilia Sokoine?
   Tuanze roll call ya wachangiaji ( interesting to know watasemaje):
   gfsonwin,@ kaunga,@ mamndenyi,@ cacico,@ badili tabia, @ yummy,@ firstlady ziondaughter and the gang.
   Bishanga, unalia ila sio kupiga kungwi maana utaleta tafrani kijijini.
   We are all inventors, each sailing out on a voyage of discovery, guided each by a private chart, of which there is no duplicate. The world is all gates, all opportunities.
   Ralph Waldo Emerson

  12. snowhite's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 2nd August 2012
   Location : nyumbani
   Posts : 12,683
   Rep Power : 383638555
   Likes Received
   12704
   Likes Given
   10273

   Default Re: Sifa za Mwanamume wa kweli (A real man) tena wa Kiafrika

   nani atupe ya mwanamke wa kiafrika?

  13. Neiwa's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 17th February 2012
   Location : My Profile
   Posts : 725
   Rep Power : 7085
   Likes Received
   565
   Likes Given
   703

   Default Re: Sifa za Mwanamume wa kweli (A real man) tena wa Kiafrika

   Mkuu DC, Ukipata mwanaume anayejitambua kuwa yeye ni mwanaume, sio tu kwa kutamka bali kwa kutambua nafasi yake katika jamii kama kaka, baba, mtoto, mume na Kiongozi; AMINI nakuambia mengine yoote hufuata with flow. Sababu mwanaume anayejitambua (kwa vitendo na si maneno); atathamini yale yote ya msingi katika maisha na katika jamii. Iwe ni mwanamke, iwe kazi or iwe majukumu na wajibu wake. Akitambua hilo na kufanyia kazi huo utambuzi basi mengine yaliyo ya msingi na mema na yakumpandisha/kuonesha kuwa yeye ni mwanaume wa kweli yatafuata yenyewe...
   "Sometimes its Ok not to be Ok"

  14. Kongosho's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 21st March 2011
   Location : Location loading...
   Posts : 36,166
   Rep Power : 138795851
   Likes Received
   23335
   Likes Given
   23325

   Default

   nina kidumu na kimtetea, kiko so african hadi raha.

   Quote By Bishanga View Post
   @ kongosho,una mme weye?

  15. Kongosho's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 21st March 2011
   Location : Location loading...
   Posts : 36,166
   Rep Power : 138795851
   Likes Received
   23335
   Likes Given
   23325

   Default Re: Sifa za Mwanamume wa kweli (A real man) tena wa Kiafrika

   Bishanga, kulia si hoja but kiukweli baba bora akalilie chumbani.
   Akilia hadharani familia yote inataharuki hata kama ni msibani.

   Sijui kwa wengine, but nikiona baba yangu analia?! Nitachanganyikiwa sana kwa kweli.

  16. SnowBall's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 13th September 2011
   Location : Amsterdam, Nertherlands
   Posts : 3,066
   Rep Power : 226845
   Likes Received
   2811
   Likes Given
   4007

   Default Re: Sifa za Mwanamume wa kweli (A real man) tena wa Kiafrika

   Dark City Nimeipenda hii ''Lazima kila kinywa kikiri kuwa kweli huyu ni baba ndani ya nyumba!!
   ..''I wasted time, and now those time waste me''...Shakespear

  17. Mgaya D.W's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 20th January 2012
   Posts : 729
   Rep Power : 646
   Likes Received
   254
   Likes Given
   673

   Default Re: Sifa za Mwanamume wa kweli (A real man) tena wa Kiafrika

   heko babu dc,naamini pia wewe ni moja ya wanaume wa kweli wa kiafrika.good analysis!....like!

  18. The Boss's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 18th August 2009
   Location : DARESALAAM
   Posts : 30,576
   Rep Power : 429503172
   Likes Received
   30843
   Likes Given
   29184

   Default Re: Sifa za Mwanamume wa kweli (A real man) tena wa Kiafrika

   Asante asante mkuu
   nitarudi....
   Whenever you find yourself on the side of the majority, it is time to pause and reflect.

  19. BADILI TABIA's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 13th June 2011
   Location : DUNIANI
   Posts : 25,163
   Rep Power : 397048790
   Likes Received
   12733
   Likes Given
   12091

   Default Re: Sifa za Mwanamume wa kweli (A real man) tena wa Kiafrika

   siku si nyingi hii itasambaa kwenye facebook na group zake.....

   ila namba 6 - ndo maanamaradhi hayaishi, mume moto mke moto....

   namba 7 - hivi wanaume wakikiri makosa yao wanachubukaga ngozi eeeh? maana tabia hiyo mnayo sana...

   ba namba 9 - hiyo nyumba itakua balaa, baba akirudi watoto wanajifungia chumbani, muda wa baba ku-bond na watoto upo kweli?

   namba 8 - i reserve my comments..loh!!!!!!
   "whoever wins the war gets to write the history"

  20. James Jahazi's Avatar
   Junior Member Array
   Join Date : 24th February 2012
   Location : Dar
   Posts : 7
   Rep Power : 497
   Likes Received
   2
   Likes Given
   0

   Default Re: Sifa za Mwanamume wa kweli (A real man) tena wa Kiafrika

   sawa kabisa hakuna ubishi, nimeipenda gold digger wote piga chini.


  Page 1 of 27 123 11 ... LastLast

  Posting Permissions

  • You may not post new threads
  • You may not post replies
  • You may not post attachments
  • You may not edit your posts
  •  

  Who are WE?

  JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

  You are always welcome! Read more...

  Where are we?

  We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

  For anything related to this site please Contact us.

  Contact us now...

  DISCLAIMER

  JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

  Read more...

  Forum Rules

  JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

  You MUST read them and comply accordingly. Read more...

  Privacy Policy

  We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

  Read our Privacy Policy. Proceed here...