Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Kwa nini wanaume wengi siku hizi hawapendi kuoa…………?

    Report Post
    Page 1 of 3 123 LastLast
    Results 1 to 20 of 44
    1. #1
      Mtambuzi's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 29th October 2008
      Location : Dar Es Salaam
      Posts : 6,089
      Rep Power : 27012
      Likes Received
      8205
      Likes Given
      17307

      Default Kwa nini wanaume wengi siku hizi hawapendi kuoa…………?


      Kumekuwa na maswali yasiyo na majibu miongoni mwa jamii kwamba imekuaje vijana wa kiume wamekuwa ni waongo sana hasa linapokuja swala la kuoa? Kwa kadiri siku zinavyozidi kwenda ndivyo ambavyo idadi ya wanaume wanaoogopa kuoa inazidi kuongezeka. Utakuta wapenzi wanaambiana kwamba wanapendana na kuahidiana kuwa wataoana, lakini kitakachotokea baada ya hapo ni mwanaume kuanza kupiga chenga kwa visingizio lukuki.

      Kwa nini hali hiyo hutokea?

      Ukweli ni kwamba hakuna jibu la moja kwa moja juu ya tatizo hilo, lakini yapo mambo ambayo yanaweza kutupa angalau tafakuri. Nitajaribu kudadavua baadhi ya sababu zinazowafanya wanaume siku hizi kukwepa kuingia katika taasisi ya ndoa:

      1 Ukosefu wa mtu wa kumchukulia kama mfano: Hapa nawazungumzia wale watoto wa kiume waliolelewa malezi ya upande mmoja yaani walilelewa na mama peke yao. Sina maana ya kudharau au kutweza malezi ya mama, la hasha, lakini ni vyema mkafahamu kwamba kuwa na baba asiye na malezi mazuri si sawa na kutokuwa na baba. Na ndio maana nikasema ukosefu wa mtu wa kumchukulia kama mfano. Achilia mbali aina ya malezi atakayoyapata kwa familia yawe mazuri au mabaya lakini lazima kutakuwa na tabia za kiume zitakazoakisi malezi ya mtoto wa kiume katika familia husika. Watoto waliolelewa na mama peke yao kuna kitu huwa wanakosa, kwani wanakuwa hawana mtu wa kumchukulia kama mfano kwa upande wa jinsia ya kiume na hapo ndipo hujikuta wakijifunza wenyewe namna ya kuongea na kutenda kama wanaume kwa sababu katika makuzi yao hawakupata fursa ya kuwa karibu na baba zao. Kwa kuwa siku hizi kuna kundi kubwa la kina mama ambao wamejikuta wakiachiwa mzigo wa malezi ya watoto, baada ya aidha kuachwa na waume zao au kuzalishwa na kutelekezwa (Single mothers), na hapo ndipo tunaposhuhudia mtoto wa kiume anapokua kwa umri na kimo huku akiwa hana mtu wa kumuangalia kama mfano wa mume anavyotakiwa kuwa katika familia zaidi ya kujifunza mambo hayo kupitia katika TV, senema au miziki. Wanaume waliopitia malezi ya aina hii huchelewa sana kuoa kwani huyaangalia maisha ya ndoa kwa namna ya kujaribu na ndipo hapo wengi huishia kuishi kinyumba na wanawake kwa ajili ya kutaka kujifunza namna ya maisha ya ndoa yanavyotakiwa kuwa na ndio sababu huchukua muda mrefu kufanya maamuzi. Na mara nyingi huishia kubadilisha wanawake kutokana na kutokuwa na uhakika wa kile wanachokitafuta.

      2 Mgogoro wa kiuchumi: Kuna kundi kubwa la vijana siku hizi hawana ajira au hawana uhakika na kipato. Ukweli ni kwamba hakuna mwanaume atakayependa kujiingiza kwenye ndoa wakati hana kazi au hana uhakika na kipato chake. Na hiyo ni kutokana na wanawake wengi siku hizi kuonekana kujali zaidi wanaume wenye uhakika na kipato. Hii misemo ya wanawake ya kebehi dhidi ya wanaume wasio na ajira au kipato, kama vile “mwanaume suruale” ina mchango mkubwa sana katika kuwafanya wanaume kukwepa kuoa iwapo hawana ajira au hawana uhakika na kipato chao.

      3 Wanawake wengi kuwa na kiwango cha elimu ya juu: Siku hizi wanawake wengi wameibuka katika kutafuta elimu ya juu kwa juhudi kubwa. Idadi ya wanawake wanaojiunga na vyuo vikuu ni wengi tofauti na ilivyokuwa zamani. Na hiyo ni kutokana na wazazi wengi kubadili mtazamo wao juu ya mtoto wa kike. Zamani mtoto wa kike alichukuliwa kama kitega uchumi. Kwa maeneo ya vijijini na katika familia masikini, watoto wa kike walikuwa wanatazamwa kama, ‘biashara ya kesho’ ambapo watauzwa kwa njia ya mahari. Kwa hiyo thamani yao ilikuwa ni kuolewa, ni ile ya kibidhaa na sio kibinadamu. Lakini tofauti na zamani siku hizi hata kule vijijini kumekuwa na mwamko mkubwa sana wa kumsomesha mtoto wa kike hadi elimu ya juu. Kutokana na mwamko huo wanawake wengi wamejikuta wakiona elimu kama kimbilio pekee la kuepukana na mfumo dume. Mwanamke gani atakubali kunyanyaswa na mwanaume akiwa na elimu yake na labda pia akiwa na kazi yake yenye mshahara na marupurupu ya kutosha, naamini watakuwa ni wachache sana ambao hawajiamini au waliathiriwa na malezi. Kwa upande wa wanaume nao, wamejikuta wakiwaogopa wanawake hawa wenye elimu ya juu kwa hofu ya kuzidiwa kipato na labda kukosa sauti kama mwanaume na hiyo inatokana na ego tu.

      4 Wanaume huwaona wanawake kama tishio wanapokuwa na mafanikio makubwa kifedha: Inaweza kutokea mwanaume anaweza kuwa na uhusiano na mwanamke ambaye labda tu nisema ni mbangaizaji. Wakati huo anaweza kuahidi kufunga ndoa na mwanamke huyo, lakini iwapo itatokea mwanamke huyo akapata mafanikio kibiashara na kuinuka kifedha. Kama mwanamke asipokuwa makini anaweza kusababisha mwanaume huyo akaingia mitini. Sababu kubwa hapo inaweza kuwa ni hofu ya kuogopa kuongozwa na mwanamke. Kumbuka kwamba mfumo dume bado umetawala vichwani mwa wanaume wengi kutokana na malezi. Mwanaume asiyejiamini ni vigumu sana kwake kuoa mwanamke aliyemzidi kipato. Kwa sababu akifanyiwa jambo dogo tu, inakuwa kama ametoneshwa. Atahisi kutaka kutawaliwa na mwanamke huyo. Jambo ambalo wanawake wanatakiwa kulifahamu ni kwamba kila mwanaume anataka kutambuliwa na kuheshimiwa kama shujaa kabla ya kumfuata msichana. Iwapo utakuwa umesimama iwe ni kifedha au kielimu pale unapotafuta kupata mwenza, inabidi ujishushe sana la sivyo utadoda.

      5 Wanaume wengi siku hizi wana hofu ya majukumu, hasa ya kulea watoto: Kutokana na malezi yao au kile wanachokijua kuhusu watoto, baadhi ya vijana huamini kwamba, kulea watoto ni jambo gumu sana. Lakini wengine wanaamini kwamba, hata mke anapaswa kulelewa kama ilivyo kwa mtoto. Hivyo wanaamua kutafuta kwanza uwezo ambao haupatikani kiurahisi. Kuna wengine, ambao wamefundishwa au kuelekezwa na mila na desturi zao kwamba, kabla hawajaoa, ni lazima wawe na nyumba kwanza, tena kwao. Kwa hiyo, hawa hadi waje wapate uwezo wa fedha wanakuwa wameshachelewa.

      6 Kuna baadhi ya wanaume, maisha bila ya ndoa wanayaona kuwa ndiyo bora kuliko yale ya ndoa: Kuna baadhi ya wanawake hujirahisisha sana kwa wanaume. Siku hizi ni jambo la kawaida sana kukuta mwanaume anaishi na mwanamke bila ndoa, wenyewe wanaita Trial Marriage. Na hapo ndipo unapokuta wanaume hawaoni tena umuhimu wa kuoa. Sasa kama mwanamke anaweza tu kuishi na mwanaume bila ya ndoa na mwanaume huyo akapata huduma zote kutoka kwa mwanamke huyo, unadhani ni kitu gani kitamvuta kufunga ndoa. Jambo lingine ni ile dhana kwamba maana ya ndoa ni tendo la ndoa. Siku hizi wanaume wengi wamejikuta wakiwa hawahitaji tena kuoa kwa sababu tendo hilo linapatikana kiurahisi tofauti na zamani. Siku hizi inawezekana kabisa kumtongoza binti leo na kupata tendo siku hiyo hiyo….. Na hapa siwazungumzii makahaba. Nawazungumzia mabinti zetu ambao wengine ukiwaona ni watu wa kuheshimiwa ukiwaangalia kwa nje lakini kwa ndani hawana lolote, vijana wa siku hizi wenyewe huwaita maharage ya Mbeya.

      Kuna sababu nyingi zinazotajwa kusababisha wanaume siku hizi kujivuta sana katika kufanya maamuzi ya kutafuta mwenza. Lakini hizo chache nilizozitaja zina mchango mkubwa.
      Last edited by Mtambuzi; 9th August 2012 at 09:35.

    2. Study Abroad

    3. #2
      Masanilo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd October 2007
      Location : Swat valley, Keta Keta
      Posts : 19,051
      Rep Power : 5465
      Likes Received
      3480
      Likes Given
      1898

      Default Re: Kwa nini wanaume wengi siku hizi hawapendi kuoa…………?

      Sababu wanawake hawapendi olewa! Siku nyingine Andika ulipoikopi hii habari usiwe mwizi wa maarifa ya wengine Plagiarism
      andate and Dr. Wansegamila like this.

    4. #3
      snowhite's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd August 2012
      Location : nyumbani
      Posts : 7,649
      Rep Power : 19921
      Likes Received
      7678
      Likes Given
      7175

      Default Re: Kwa nini wanaume wengi siku hizi hawapendi kuoa…………?

      mh!nadeclare interest hapa!ngoja nipite
      Mtambuzi likes this.
      IT TAKES A MAN TO CONSTRUCT A HOUSE BUT IT NEEDS A WOMAN TO MAKE A HOME!

    5. #4
      Mtambuzi's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 29th October 2008
      Location : Dar Es Salaam
      Posts : 6,089
      Rep Power : 27012
      Likes Received
      8205
      Likes Given
      17307

      Default Re: Kwa nini wanaume wengi siku hizi hawapendi kuoa…………?

      Quote By Miganiko
      Sababu wanawake hawapendi olewa! Siku nyingine Andika ulipoikopi hii habari usiwe mwizi wa maarifa ya wengine Plagiarism
      Kama wewe unaijua link nilipokopi basi weka hapa.......................

    6. #5
      MKATA KIU's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st November 2010
      Posts : 1,376
      Rep Power : 767
      Likes Received
      906
      Likes Given
      27

      Default Re: Kwa nini wanaume wengi siku hizi hawapendi kuoa…………?

      Bachelors life is so sweet, everyday kwenye mihangaiko, chakula bar, account inakuwa inasoma as hakuna expenditure nyingi so rahis kusave na kufika dream destinations, dates and flitring na watu tofaut kwa wingi,

      Sio kwamba tunachelewe but tunaienjoy bachelors life kidogo ukirud geto unalala bila kelele wala maswali ya mtu yeyote,sometimes uko abroad sometimes uko bongo, sometimes uko town sometimes uko bush kote huko unasaka opportunity bila stress... Sometimes dala dala sometimes upo kwenye mkoko yaan your own decisions.

      Swala la Kuoa ni baadae sana hadi tufike 30 tumeshaweka vitega uchumi vya kutosha maana hospital zenyewe siku hizi hadi india hata watoto wakiumwa as nchi imechakachuliwa hii, kuoa bila kujiandaa utadata
      sakapal and ze encyclopedia like this.

    7. Miaka 50

    8. #6
      markj's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th July 2012
      Posts : 1,006
      Rep Power : 547
      Likes Received
      164
      Likes Given
      143

      Default Re: Kwa nini wanaume wengi siku hizi hawapendi kuoa…………?

      Wao wenyewe hawapendi kuolewa! Wanapenda kubadilisha mahandsome tu! Sasa wakiolewa watabadilishaje ma hb! Si ndo mwanzo wa kugombana! WE UONI HATA PICHA ZA THREAD HII NI MA HB TU! WEKA ZA KWENDA ATM UONE? watoto wakike skuizi wanapenda kuzaa na ma hb wa kuchanganya! akipata watoto wa 2 wa kibongo 1 na africast 1! na akiwa na kazi yake ya bank teller basi haitaji kuolewa nimwendo wakuuza surana watoto, na kuchakachuana na ma hb mbalimbali! ndoa kwa ujumla zilisha kisha, za skuizi ni kuongezea watu gharama tu!
      Amsterdam likes this.
      MZUNGU AKIJICHUBUA HUJUE MOYONI ANA UAFRICA!.by stamina

    9. #7
      BADILI TABIA's Avatar
      JF Bronze Member Array
      Join Date : 13th June 2011
      Location : DUNIANI
      Posts : 14,552
      Rep Power : 5612
      Likes Received
      6210
      Likes Given
      2281

      Default Re: Kwa nini wanaume wengi siku hizi hawapendi kuoa…………?

      Mtambuzi habari ako baba.....

      Next topic wafundishe wanaume 'kujiamini'
      Mtambuzi and sakapal like this.

    10. #8
      King Kong III's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 15th October 2010
      Location : Enaboishu-Umenyeni
      Posts : 11,884
      Rep Power : 5054
      Likes Received
      3197
      Likes Given
      2619

      Default Re: Kwa nini wanaume wengi siku hizi hawapendi kuoa…………?

      Namba 2
      BAGAH likes this.

    11. #9
      jeneneke's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th July 2012
      Posts : 708
      Rep Power : 487
      Likes Received
      292
      Likes Given
      264

      Default Re: Kwa nini wanaume wengi siku hizi hawapendi kuoa…………?

      Mh me leo naangalia picha natumaini ile ya pili ni mtu na mama yake.Ya pili kutpka mwisho imenivutia sana
      sakapal likes this.

    12. #10
      Asabaya's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th February 2012
      Posts : 619
      Rep Power : 489
      Likes Received
      127
      Likes Given
      21

      Default Re: Kwa nini wanaume wengi siku hizi hawapendi kuoa…………?

      kweli kabisa unko.

    13. #11
      Timtim's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 9th February 2008
      Posts : 399
      Rep Power : 655
      Likes Received
      44
      Likes Given
      22

      Default Re: Kwa nini wanaume wengi siku hizi hawapendi kuoa…………?

      Sababu ni kuogopa majukumu, uoga wa maisha na uhuni uliokithiri.
      Mtambuzi likes this.

    14. #12
      salito's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th December 2011
      Location : Dar es salaam
      Posts : 971
      Rep Power : 567
      Likes Received
      215
      Likes Given
      138

      Default Re: Kwa nini wanaume wengi siku hizi hawapendi kuoa…………?

      Mkuu hiyo namba moja inategemea na jinsia,kwa mtoto wa kiume akilelewa na baba pekee ndio linakuwa tatizo maan haoni umuhimu na kazi ya mama nyumbani,hivyo hivyo na wa kike akilelewa na mama,lakini wa kiume akilelewa na mama,anakuwa na mapenzi na wanawake sababu ya mapenzi aliyopewa na mama,na ataamini bila mwanamke mambo hayaendi,hivyo hivyo na kwa mwanamke,huu ni mtazamo wangu tu,unasemaje brother?
      andate likes this.

    15. #13
      LEARNED BROTHER's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 7th March 2012
      Posts : 101
      Rep Power : 383
      Likes Received
      21
      Likes Given
      6

      Default Re: Kwa nini wanaume wengi siku hizi hawapendi kuoa…………?

      My priority kwa sasa ni kupata mtoto na sio mke. Suala la kuoa kwakweli hata siliwazii kabisa.

    16. #14
      andate's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 9th June 2011
      Posts : 1,155
      Rep Power : 633
      Likes Received
      399
      Likes Given
      2137

      Default Re: Kwa nini wanaume wengi siku hizi hawapendi kuoa…………?

      Quote By salito
      Mkuu hiyo namba moja inategemea na jinsia,kwa mtoto wa kiume akilelewa na baba pekee ndio linakuwa tatizo maan haoni umuhimu na kazi ya mama nyumbani,hivyo hivyo na wa kike akilelewa na mama,lakini wa kiume akilelewa na mama,anakuwa na mapenzi na wanawake sababu ya mapenzi aliyopewa na mama,na ataamini bila mwanamke mambo hayaendi,hivyo hivyo na kwa mwanamke,huu ni mtazamo wangu tu,unasemaje brother?
      You are genius. Mleta mada ame-copy bila ku-digest.
      Nini unachoweza kujifunza kwa mababa wengi wa kiafrika? Anaondoka asubuhi kwenda kazini, akitoka kazini anapitia bar, akifika nyumbani amelewa fujo mtindo mmoja. Mtoto hata hupewi mwanya wa kujua baba ana-deals gani mjini ukajifunza.
      Hiyo namba moja inahitaji review, iko more wrong than right. Ni mababa wachache sana wa kiafrika unaweza ukajifunza kutoka kwao. At least baba wa kichaga atakufundisha kusimamia miradi yake hao wengine sifahamu.
      salito likes this.

    17. #15
      Elli's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 17th March 2008
      Location : Kijito-Upele
      Posts : 8,513
      Rep Power : 0
      Likes Received
      2102
      Likes Given
      1839

      Default Re: Kwa nini wanaume wengi siku hizi hawapendi kuoa…………?

      hapanihusu hapa mie nilioa muda tu umeshapita sasa

    18. #16
      Kimbori's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st February 2012
      Posts : 1,182
      Rep Power : 601
      Likes Received
      158
      Likes Given
      11

      Default Re: Kwa nini wanaume wengi siku hizi hawapendi kuoa…………?

      Vijana wengi hawaoni faida ya ndoa. Kama ni huduma za ngono zipo kila wakati (asubuhi, mchana, jioni na usiku). Pia, wazazi wameshindwa kuwashinikiza vijana wao wa kiume waoe. Vijana wengi huoa baada ya shinikizo kutoka katika familia (dada, kaka, mama n.k), marafiki na jamaa.
      Hata mimi sijui kama nitaoa kirahisi rahisi, japo mimi si mzinzi.
      salito likes this.
      "If you live without discipline, you will die without dignity"

    19. #17
      nyumba kubwa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 8th October 2010
      Posts : 4,047
      Rep Power : 2305
      Likes Received
      2874
      Likes Given
      3969

      Default Re: Kwa nini wanaume wengi siku hizi hawapendi kuoa…………?

      Mtambuzi unatisha. Hili la single mother mi nina ushaidi. Mume wangu kwao wako sita wote watoto wa kiume...walilelewa na mama tu; na aliwalea vizuri kwa kuwa alikuwa na uwezo tu.

      Lakini ni mume wangu tu (last born) ndio ameoa. Kaka zake wanazaa zaa tu na wanawake tofauti hawataki commitment. Sikuwa najua ni kwa nini, now I know.
      Mtambuzi likes this.

    20. #18
      nyumba kubwa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 8th October 2010
      Posts : 4,047
      Rep Power : 2305
      Likes Received
      2874
      Likes Given
      3969

      Default Re: Kwa nini wanaume wengi siku hizi hawapendi kuoa…………?

      Kuna wengi tu walotoka kwenye familia za wazazi walevi lakini wao wakataka kuoa ili ku prove kuwa inawezekana kuwa responsible. Unakuta wanajitahidi kuwa opposite ya wazazi wao. Utasikia mimi nilikuwa navaa viatu mpaka vinachanika...sitaki kabisa mtoto wangu ajisikie mnyonge shuleni.

      Mimi mama yangu alikuwa analia kila siku sababu ya tabia ya baba...sitakaa nimtese mke wangu.

      Kwa hiyo kuna learning through other people's mistakes.


      Quote By andate
      You are genius. Mleta mada ame-copy bila ku-digest.
      Nini unachoweza kujifunza kwa mababa wengi wa kiafrika? Anaondoka asubuhi kwenda kazini, akitoka kazini anapitia bar, akifika nyumbani amelewa fujo mtindo mmoja. Mtoto hata hupewi mwanya wa kujua baba ana-deals gani mjini ukajifunza.
      Hiyo namba moja inahitaji review, iko more wrong than right. Ni mababa wachache sana wa kiafrika unaweza ukajifunza kutoka kwao. At least baba wa kichaga atakufundisha kusimamia miradi yake hao wengine sifahamu.
      MANAKE MKARI and salito like this.

    21. #19
      jeneneke's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th July 2012
      Posts : 708
      Rep Power : 487
      Likes Received
      292
      Likes Given
      264

      Default Re: Kwa nini wanaume wengi siku hizi hawapendi kuoa…………?

      At least baba wa kichaga atakufundisha kusimamia miradi yake .Nimependa san hii ndo mana natafuta mume wa kichaga.

    22. #20
      Sabry001's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th June 2011
      Location : everywhere
      Posts : 967
      Rep Power : 608
      Likes Received
      287
      Likes Given
      199

      Default

      Quote By jeneneke
      At least baba wa kichaga atakufundisha kusimamia miradi yake .Nimependa san hii ndo mana natafuta mume wa kichaga.
      nikupe mdogo wangu?

    23. FemaTV & Radio
    Page 1 of 3 123 LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...