Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Mahusiano yanapovunjika, wanawake ndio huumia zaidi...!

    Report Post
    Page 1 of 7 123 ... LastLast
    Results 1 to 20 of 126
    1. #1
      Mtambuzi's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 29th October 2008
      Location : Dar Es Salaam
      Posts : 6,094
      Rep Power : 27014
      Likes Received
      8231
      Likes Given
      17325

      Default Mahusiano yanapovunjika, wanawake ndio huumia zaidi...!

      Kwa kuangalia idadi ya watu wanaoathirika kufuatia kuvunjika kwa uhusiano kati ya mwanamke na mwanaume mtu atagundua kwamba wanawake ndiyo ambao hupatwa na athari kubwa zaidi. Kwa mfano ukichukua watu ishirini, wanawake kumi ambao wameachwa na wapenzi wao na wanaume kumi ambao nao wameachwa pia na wapenzi wao, utagundua kwamba, wakati ni wanaume watatu tu kati ya hao kumi ndio watakaosumbuliwa sana na na hali hiyo, kwa wanawake idadi itakuwa ni saba kati ya hao kumi.

      Watu wengi wanaweza kukimbilia kwenye kusema hali hiyo inatokana na utegemezi wa wanawake kwa wanaume. Hii ikiwa na maana kwamba, wanaathirika zaidi kwa sababu, kwa kuachwa ina maana pia kwamba hawataweza tena kupata mahitaji ambayo walikuwa wanapewa na wanaume hao. Dhana kama hii inaweza kuwa na ukweli fulani, lakini hali halisi inakataa. Kuna wanawake ambao wana uwezo mkubwa nap pengine ndiyo wanaowalisha na kuwavisha wanaume, lakini wanapoachwa na wanaume hao huathirika sana.

      Wanawake wa aina hii inadaiwa kwamba huathirika zaidi kuliko wale walio tegemezi. Kuathirika huku kwa ziada huhusishwa kwa kiasi kikubwa na ukweli kwamba wanaume ni watu wa kutoa ili kupalilia penzi, lakini hapa badala ya kutoa wanapewa na bado wanaondoka. Hili huwatanza wanawake wa aina hii. Lakini sababu ambayo huenda wengi wetu tulikuwa hatuijui kuhusiana na suala hili la wanawake kuathirika zaidi baada ya kuvunjika kwa penzi au kuachwa ni ‘ndoto.’ Kimaumbile wanawake huota zaidi ndoto za mchana au hufikiria zaidi kuhusu maisha yao ya kimapenzi yatakavyokuwa ukilinganisha na wanaume. Siyo kufikiria tu, bali hufikiria kwa njia inayoonyesha kuwa maisha hayo yatakuwa kama peponi.

      Wanawake, wakiwa bado wasichana (baada ya kuvunja ungo) huanza kufikiria na kupiga picha jinsi busu lao la kwanza litakavyokuwa, mtu ambaye watabusiana awali. Hufikiria pia kuhusu wapenzi wao wa awali watakavyokuwana jinsi itakavyokuwa watakaposhiriki nao tendo kwa mara ya kwanza na huwa wanapiga picha ya jinsi siku yao ya harusi itakavyokuwa na watu watakaowaona. Katika kupiga picha huko huwa wanafikiria namna ambavyo mambo hayo yote yatakavyoenda vizuri bila doa, huwa wanajiona wakiwa wamefanikiwa katika hatua zote na hatimaye kuishi kwa raha mustarehe milele na watakaokuwa wapenzi wao. Kwa upande wa wanaume hakuna ndoto za aina hii na hata kama zipo ni kwa wachache sana, wakati kwa wanawake ni kama sehemu ya makuzi kwao.

      Kwa hali hiyo, ukiacha mazingira wanamokulia wanawake, kwa sehemu kubwa hukua wakiwa na hizo ndoto zao, ambazo kwao siyo ndoto bali ukweli. Wanapokuja kwenye ukweli wa uhusiano hugundua kwamba busu la awali siyo kama walivyotegemea liwe, mpenzi wa awali siyo kama walivyomtegemea awe na wala maisha ya ndoa siyo matamu kama walivyokuwa wameota. Kwa kuwa hawakujiandaa wala kutegemea mazingira magumu ya uhusiano, hawakuwa wakiota kuhusu ugumu wa uhusiano bali wororo, wanapokutana na masuala ya kuvunja moyo kama kuachwa hubabaika sana. Kwa kuwa akilini mwao walikuwa na picha ya mafanikio katka uhusiano, kushindwa kwa uhusiano, huwafanya wajione kwamba, wao ndiyo wakosaji, wameshindwa kulinda uhusiano ambao katika ndoto zao waliamini kwamba ni mzuri na usio na doa

      Ukiangalia kwa makini katika uhusiano, wanawake ndio wanaojitahidi sana kulinda uhusiano usivunjike, wao ndiyo wavumilivu zaidi, ndiyo ambao hujitahidi kuyarudisha mambo yaende sawa pale yanapokwenda kombo hata kama kufanya hivyo kunawagharimu. Yote hii ni juhudi yao ya kutaka kuishi kwa kadiri ndoto zao za kabla zilivyowaonyesha, kwamba uhusiano kati ya mwanamke na mwanaume ni mtamu, mororo na usio na chembe ya doa…………………

      Kesho nakuja na mada, kwa nini wanaume wengi hawapendi kuoa siku hizi.......................... .!
      Last edited by Mtambuzi; 9th August 2012 at 08:36.

    2. Miaka 50

    3. #2
      andybird314's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 23rd January 2012
      Location : Tanzania
      Posts : 2,675
      Rep Power : 967
      Likes Received
      552
      Likes Given
      283

      Default re: Mahusiano yanapovunjika, wanawake ndio huumia zaidi...!

      Nice ulichosema ni kweli hata mimi nakubaliana na hilo
      Mtambuzi likes this.
      Kweli kuishi Tanzania kuona mengi

    4. #3
      asigwa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st September 2011
      Location : TANDHANIYA
      Posts : 4,389
      Rep Power : 1265
      Likes Received
      1209
      Likes Given
      1253

      Default re: Mahusiano yanapovunjika, wanawake ndio huumia zaidi...!

      mkuu umenena vema sana...kuhusu day dreaming ni kweli kisaikolojia mwanamke huwa na daydreaming nyingi sana zinozohusu mahusianao ya kimapenzi na mara zote mapenzi yanapoenda kombo kwao huwa ni hatari sanatofauti na wanaume ndio maana kuna msemo "MAPENZI YA MWANAMKE YAKO MOYONI ILA YA WANAUME YAKO KICHWANI"...

      Nachojua siri kubwa ya kusolve ishu ya kuachwa ni kuendelea na day dreaming wakati uhusiano ni mbovu. Hii kwa wataalamu wa metaphysics & law of attraction huwa na effect kubwa sana kuchange hali ya mambo
      Mtambuzi likes this.
      !!..BAR ikiwa na wahudumu wa KIUME TUPU sikai dakika nyingi..!!

    5. #4
      BADILI TABIA's Avatar
      JF Bronze Member Array
      Join Date : 13th June 2011
      Location : DUNIANI
      Posts : 14,585
      Rep Power : 5620
      Likes Received
      6213
      Likes Given
      2288

      Default re: Mahusiano yanapovunjika, wanawake ndio huumia zaidi...!

      nausubiri mjadala wako wa kesho...

      ila kwa uzoefu wangu mie sikuumia kihivyo....labda kwa vile nilikua mtu wa kuacha na si kuachwa..... ingawa kipindi cha mpito huwa kinaumiza kidogo.............

      acha waje wlioumizwa watupe experience, kwa nini binadamu mlokutana wote na meno 32 akuumize moyo?
      Mtambuzi and ummu kulthum like this.
      "Behind every great fortune there is a crime."
      - Honore de Balzac (1799-1850)

    6. #5
      jeneneke's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th July 2012
      Posts : 714
      Rep Power : 489
      Likes Received
      297
      Likes Given
      269

      Default re: Mahusiano yanapovunjika, wanawake ndio huumia zaidi...!

      Hili ndo jibu nilitaka kutoa.
      "MAPENZI YA MWANAMKE YAKO MOYONI ILA YA WANAUME YAKO KICHWANI"...

      Halafu Mtambuzi hao maharusi hapo juu nawafahamu huyo kaka ni mmalawi anafanya mahali fulani naenda kumwambia umetoa picha yake bila idhini yake akudai fidia..

    7. RukaaJuu Final

    8. #6
      Little Angel's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st August 2011
      Posts : 587
      Rep Power : 509
      Likes Received
      193
      Likes Given
      141

      Default re: Mahusiano yanapovunjika, wanawake ndio huumia zaidi...!

      Quote By BADILI TABIA
      nausubiri mjadala wako wa kesho...

      ila kwa uzoefu wangu mie sikuumia kihivyo....labda kwa vile nilikua mtu wa kuacha na si kuachwa..... ingawa kipindi cha mpito huwa kinaumiza kidogo.............

      acha waje wlioumizwa watupe experience, kwa nini binadamu mlokutana wote na meno 32 akuumize moyo?
      BT, mmi nakumbuka niliacha ilihali bado napenda but sikuwa na jinsi. oh no by that time i thout it was end of my life. aah baadae nikazoea tu. sasa nimekua mwalimu na ambassador. looh maisha haya ni shule

    9. #7
      Kiranga's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th January 2009
      Posts : 14,169
      Rep Power : 41579
      Likes Received
      6067
      Likes Given
      1058

      Default re: Mahusiano yanapovunjika, wanawake ndio huumia zaidi...!

      Wanawake gani? Maana wanawake wote si sawa.
      Allow others to say their say, but always say your piece, it's only right.

    10. #8
      King Kong III's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 15th October 2010
      Location : Enaboishu-Umenyeni
      Posts : 11,927
      Rep Power : 5063
      Likes Received
      3201
      Likes Given
      2661

      Default re: Mahusiano yanapovunjika, wanawake ndio huumia zaidi...!

      Nakukubali wewe ni Jembe aka Mnyama!! Unyama unyamani Unyago Unyagoni.
      Mtambuzi likes this.

    11. #9
      BADILI TABIA's Avatar
      JF Bronze Member Array
      Join Date : 13th June 2011
      Location : DUNIANI
      Posts : 14,585
      Rep Power : 5620
      Likes Received
      6213
      Likes Given
      2288

      Default re: Mahusiano yanapovunjika, wanawake ndio huumia zaidi...!

      unaona eeeh,
      ukishasoma alama za nyakati, au kama mtu hasomeki, kila siku unaambulia maumivu, heri uumie muda mfupi kumuacha kuliko kuumia muda mrefu kwa kuuguza donda sugu.....

      naamini mapenzi ni kutake risk, na kwenye mapenzi maumivu hayakosekani... loh

      Quote By Little Angel
      BT, mmi nakumbuka niliacha ilihali bado napenda but sikuwa na jinsi. oh no by that time i thout it was end of my life. aah baadae nikazoea tu. sasa nimekua mwalimu na ambassador. looh maisha haya ni shule
      "Behind every great fortune there is a crime."
      - Honore de Balzac (1799-1850)

    12. #10
      NyotaMalaika's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 6th August 2012
      Posts : 103
      Rep Power : 362
      Likes Received
      42
      Likes Given
      14

      Default re: Mahusiano yanapovunjika, wanawake ndio huumia zaidi...!

      Hapo haswa kwenye daydreaming...
      Mtambuzi likes this.

    13. #11
      mito's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th June 2011
      Posts : 1,047
      Rep Power : 610
      Likes Received
      442
      Likes Given
      1349

      Default re: Mahusiano yanapovunjika, wanawake ndio huumia zaidi...!

      Pamoja na ukweli kwamba wanawake wanapenda kwa moyo wakati wanaume wanapenda kwa akili kama alivyosema asigwa na jeneneke, pia kuumia zaidi kwa mwanamke kunatokana na ukweli kwamba wao kupata replacement (mwenza mwingine) ni ishu zaidi kuliko kwa mwanaume
      Mtambuzi likes this.
      Haki ya mtu haipotei, inacheleweshwa tu!

    14. #12
      jouneGwalu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th April 2011
      Location : Studio
      Posts : 2,341
      Rep Power : 969
      Likes Received
      1314
      Likes Given
      1755

      Default re: Mahusiano yanapovunjika, wanawake ndio huumia zaidi...!

      Nitakuwa na mengi kesho....

      Kwa hili la leo kwaa uzoefu nimeshuhudia wote tunaumia tu, inategemea na mahusiano yenyewe na mtu uliyapa uzito gani na jinsi ulivyopagawa na mwenzio na jinsi mnavyoachana....

      Kila sheria ina "exceptions" zake!
      Invisible, BAK, Mtambuzi and 2 others like this.

    15. #13
      Kongosho's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st March 2011
      Location : Location loading...
      Posts : 25,223
      Rep Power : 13077
      Likes Received
      14125
      Likes Given
      14996

      Default re: Mahusiano yanapovunjika, wanawake ndio huumia zaidi...!

      maumivu ya utegemezi wa 'material needs' ni afadhali kuliko maumivu ya utegemezi wa kihisia.

      Mie sikubaliani na hii hoja moja kwa moja.
      Kwani Whitney Houstoni alikuwa anamtegemea Bobby Brown kwa lipi?
      Nadhani alikuwa tegemezi kihisia kuliko ki-material.

    16. #14
      Mtambuzi's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 29th October 2008
      Location : Dar Es Salaam
      Posts : 6,094
      Rep Power : 27014
      Likes Received
      8231
      Likes Given
      17325

      Default re: Mahusiano yanapovunjika, wanawake ndio huumia zaidi...!

      Quote By jouneGwalu
      Nitakuwa na mengi kesho....

      Kwa hili la leo kwaa uzoefu nimeshuhudia wote tunaumia tu, inategemea na mahusiano yenyewe na mtu uliyapa uzito gani na jinsi ulivyopagawa na mwenzio na jinsi mnavyoachana....

      Kila sheria ina "exceptions" zake!
      Kwa kuangalia idadi ya watu wanaoathirika kufuatia kuvunjika kwa uhusiano kati ya mwanamke na mwanaume mtu atagundua kwamba wanawake ndiyo ambao hupatwa na athari kubwa zaidi. Kwa mfano ukichukua watu ishirini, wanawake kumi ambao wameachwa na wapenzi wao na wanaume kumi ambao nao wameachwa pia na wapenzi wao, utagundua kwamba, wakati ni wanaume watatu tu kati ya hao kumi ndio watakaosumbuliwa sana na na hali hiyo, kwa wanawake idadi itakuwa ni saba kati ya hao kumi.
      Mkuu naamini kipengele hicho hapo juu kinahusika sana kujibu kauli yako.......................... .

    17. #15
      Ngongoseke's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st January 2012
      Posts : 1,084
      Rep Power : 589
      Likes Received
      255
      Likes Given
      237

      Default

      Quote By jeneneke
      Hili ndo jibu nilitaka kutoa.
      "MAPENZI YA MWANAMKE YAKO MOYONI ILA YA WANAUME YAKO KICHWANI"...

      Halafu Mtambuzi hao maharusi hapo juu nawafahamu huyo kaka ni mmalawi anafanya mahali fulani naenda kumwambia umetoa picha yake bila idhini yake akudai fidia..
      Unajuaje kama katoa bila idhini yao?huenda yeye pia anawafaham
      Mtambuzi likes this.

    18. #16
      Scofied's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th June 2012
      Location : A-City
      Posts : 1,278
      Rep Power : 606
      Likes Received
      332
      Likes Given
      58

      Default re: Mahusiano yanapovunjika, wanawake ndio huumia zaidi...!

      well said mkuu Mtambuzi , wanaume tunatakiwa tuwe wa kweli ili tusiwaumize
      Mtambuzi likes this.

    19. #17
      Kimbori's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st February 2012
      Posts : 1,188
      Rep Power : 603
      Likes Received
      161
      Likes Given
      11

      Default re: Mahusiano yanapovunjika, wanawake ndio huumia zaidi...!

      "Women treat friendship like glass and it break, men treat friendship like football but do not get crack"
      "If you live without discipline, you will die without dignity"

    20. #18
      King'asti's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th November 2009
      Location : The Jungle
      Posts : 17,216
      Rep Power : 28909
      Likes Received
      11693
      Likes Given
      4819

      Default re: Mahusiano yanapovunjika, wanawake ndio huumia zaidi...!

      I totally disagree mzazi.
      Wanawake wanaweza ku-move on haraka sana kwa sababu ni wepesi ku-seek support kutoka kwa wanawake na wanaume pia (emotionally)
      Wanawake wanaotegemea wenzi wao ndo wanaishia nahisi. Ngoja nimalizie sikukuu, keshooo tutajadiliana hili. Navuna ufuta

    21. #19
      Kiranga's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th January 2009
      Posts : 14,169
      Rep Power : 41579
      Likes Received
      6067
      Likes Given
      1058

      Default re: Mahusiano yanapovunjika, wanawake ndio huumia zaidi...!

      Quote By King'asti
      I totally disagree mzazi.
      Wanawake wanaweza ku-move on haraka sana kwa sababu ni wepesi ku-seek support kutoka kwa wanawake na wanaume pia (emotionally)
      Wanawake wanaotegemea wenzi wao ndo wanaishia nahisi. Ngoja nimalizie sikukuu, keshooo tutajadiliana hili. Navuna ufuta
      Tatizo mtoa mada kawalundika "Wanawake" wote kama akili yao moja vile.

      Ndio maana nikauliza wanawake wanaozungumzwa hapa ni wanawake wepi?

      Sijapata jibu.
      Allow others to say their say, but always say your piece, it's only right.

    22. #20
      Mtambuzi's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 29th October 2008
      Location : Dar Es Salaam
      Posts : 6,094
      Rep Power : 27014
      Likes Received
      8231
      Likes Given
      17325

      Default re: Mahusiano yanapovunjika, wanawake ndio huumia zaidi...!

      Quote By jeneneke
      Halafu Mtambuzi hao maharusi hapo juu nawafahamu huyo kaka ni mmalawi anafanya mahali fulani naenda kumwambia umetoa picha yake bila idhini yake akudai fidia..
      Hizi picha naziweka kwa makubaliano na wahusika na wengine wapo humu humu JF

    Page 1 of 7 123 ... LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...