mmh! mimi sijui ninzie wapi ila ngoja nianze kwa maswali haya ka hawa bachelor's kama wewe
platozoom na
Eiyer.
Nawaona
Mtambuzi na
mito pia
Mwali wakiongelea migogoro miye n sawa na wamepatia kabisa. Lakini hapa tumeulizwa maswali haya:-
1. Kwa nini watu wanaoa/kwa nini tuoe
2. Changamoto za kuzingatia kwenye ndoa
3. Sababu zipi za zitakufanya uvunje ndoa
majibu kwa mtazamo wangu;
1) Binafsi naomba niwaambie sababu kubwa ya kwanini watu wanaoa ni ili kupata wenza maisha yao. Ujue kwamba bibadam huwez kuwa kama kisiwa upo muda ambao unahitaj mweza ambaye atakuwa ni sehem yako ya maisha ambaye utakuwa tayari kushare nae amani, furaha na upendo wako ambaye utakuwa huru kujieleza kwake na ambaye pia atakuwa huru kukusikiliza, kukusaidia na hata kukushauri. Unategemea mtu huyu awepo wakati wa raha na tabu ambaye wewe utajitoa kwake kwa halia na mamali na yeye ajitoe kwako kwa hali na mali. hapa silaha kubwa ni uaminifu
2)changamoto za kuzingatia kwenye ndoa kwangu mimi ni nyingi sana, kwani ikumbukwe kwamba sisi sote tu bnadamu na tunamapungufu hivyo basi mapungufu yote ama udhaifu wa aina yeyote ambao tunao basi ni changamoto kwa wenzi wetu.. Hapa silaha kubwa ni uvumilivu.
3) sababu kubwa za kukufanya uvunje ndoa binafsi mimi kama mimi sijaiona lakin kwa kua hapa dunian tunatofautiana basi hizi zaweza kuvary mfano
mito kasema cheating,
Mwali kasema kipato na matumuzi yake , mwingine atasema kudharauliwa na kunyanyaswa, mwingine atasema ulevi nk. Kwahiyo ni swala la mtu binafsi. silaha ya hapa ni upendo na msamaha.
Ngoja ni kwambie
platozoom, mimi huwa nina kanuni yangu ya 50% and that is our motto in ma house hata mgeni akija unaweza ukakutana na hili neno "nusu nusu" utashangaa sana ila liko established kwamba katika chochote kile ili upate furaha nacho lazima ucontribute by 50% na pia katika kosa lolote lazima wewe umecontrribute by 50% so to me before hujanza kumlaumu na kutupia lawama mwenzi just look at yourself and assess your nusu umeitimiza kweli?
kumbuka hata leo nikikukaribisha nyumbani kwangu ili ufurahie ugeni wako kwangu u have to play your 50% honestly and be reassured kwamba you will enjoy. sasa hapo na mimi nikiplay zile nusu yangu lazima utapata furaha tu na hutoboreka . sasa huo ni mdfano tu wa maisha ya kawaida waweza pia kuurelate kwenye maisha ya ndoa.
All in all lazima Mungu akutangulie ili akuwekee silaha zote hizo kwa wepesi na si vinginevyo.
Hope hii BEGY PARTY nimeifanya vyema ma kungwi wenzangu watanisaidia tena zaid. Jumapili njema maswali yenu yawekeni nitayajibu nikitoka kanisani saa tano.
Follow Us Here