Yupo huyu mdada kweli anapendeza sanaaaaaa
Yupo huyu kijana kweli anampenda huyu mdada lol..
Penzi lao laelekea kuwaka na halina kizima moto lakini,
Upo mushkeli katika dimbwi la mahaba yao tarajiwa..
Mdada anapokunjia ndita ampendaye atarajie nini?
Sijui ana deko lipi huyu mdada badala ya kicheko
Kila amwonapo njemba wake huanza kukuda ndita!
Jambo aulizwapo huanza kujibu mazogo bila lengo
Kijana ameghafilika hajui anapendwa au anavumiliwa tu
Mdada anapokunjia ndita ampendaye atarajie nini?
Swahiba wa mdada wadai naye kashikwa pabaya
Ila hizo ni hadaa zake aonekane kama hajapenda sana
Khofu yake akionekana kafa pengine asije kufa kikwelikweli
Hana imani na kijana kama naye anampenda kiuthabiti
Mdada anapokunjia ndita ampendaye atarajie nini?
Njemba sasa imetosheka na udhia sasa yawasha mataa
Mdada kaghafirika hajui la kufanya kwani ndita siyo utu
Kibuti chanukia nami kuwasuluhisha nimeghairi kabisa
Waswahili husema wagombanapo ndugu chukua kapu ukavune
Mdada anapokunjia ndita ampendaye atarajie nini?

Reply With Quote





Follow Us Here