Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Soma inakuhusu uliye kwenye ndoa

    Report Post
    Page 1 of 2 12 LastLast
    Results 1 to 20 of 24
    1. #1
      bemg's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th April 2010
      Posts : 1,614
      Rep Power : 783
      Likes Received
      218
      Likes Given
      350

      Post Soma inakuhusu uliye kwenye ndoa

      Inahuzunisha lakini kuna fundisho kuu kwetu sote.

      “Nilipofika nyumbani usiku ule, mke wangu aliponitayarishia chakula, nilimshika mkono na kumwambia, Kuna kitu nataka nikwambie. Mke wangu alikaa chini na kula chakula kimya akiwa tayari kunisikiliza. Tena nikagundua macho yake yalionyesha anaumizwa na kitu moyoni. Nilishindwa hata namna ya kuanza kufumbua kinywa changu. Lakini ilibidi nimwambie ili ajue nilikuwa nikifikiri nini juu yake.

      Nataka kukupa talaka. Nilianza kusema kwa utulivu. Alionekana kutokereka na maneno yangu badala yake aliniuliza kwa sauti ya upole ‘kwa nini?’ Sikumjibu swali lake. Kutojibu kulimfanya akasirike. Akatupa kijiko na akanikaripia, ‘wewe si mwanamume!’ Usiku ule, hakukuwa na maongezi kati yetu. Alikuwa akilia kwa kwikwi. Nilifahamu kwamba alitaka kujua ni nini kimetokea kwenye ndoa yetu. Lakini kwa hakika nisingeweza kumpa jibu wala sababu ya kuridhisha; alionekana si mali kitu kwangu penzi langu lilikwishahamia kwa Jane. Sikumpenda tena mke wangu mawazo yote yalikuwa kwa Jane. Kwa kweli nilimdharau mke wangu, nilimtusi vibaya kwa ajili ya Jane!

      Huku moyo wangu nikijua wazi kwamba nafanya kosa, niliandika talaka ambayo ilionyesha kwamba yeye (mke wangu) angepata nyumba yetu, gari na atakuwa na hisa 30% ya kampuni yetu. Aliangalia talaka ile na kuichana vipande vipande.

      Mke ambaye tumeishi nami kwa miaka 10 alionekana mgeni machoni mwangu. Nilimuonea huruma kwa muda, rasilimali na nguvu alizopoteza lakini sikuweza kurudi nyuma kwa sababu Jane aliuteka moyo wangu kisawasawa. Hatimaye mke wangu alilia kwa uchungu na sauti mbele yangu, jambo ambalo kwa hakika nilitarajia. Kwangu mimi kilio chake kilinipa nafuu na kuongeza kiburi kwamba mimi ni mshindi.

      Wazo la kuachana na mke wangu limenisumbua kwa miaka mitano na sasa limeendelea kuimarika na kuwa jambo la hakika zaidi.

      Siku iliyofuata nilikuja nyumbani kwa kuchelewa sana nikakuta mke wangu akiandika jambo mezani. Sikutamani hata kula chakula alichonipikia nilikwenda moja kwa moja chumbani na usingizi ulinichukua mara moja kwa sababu nilikuwa nimechoka baada ya kula raha za kufa mtu na Jane.

      Usiku nilishtuka usingizini mke wangu alikuwa bado akiandika. Sikujali kabisa nikajifunika vyema shuka na kulala tena. Asubuhi yake alinikabidhi masharti ya talaka yake: hakutaka kitu chochote kutoka kwangu lakini alihitaji apate angalau mwezi mmoja wa kujiandaa kabla hajaachika. Akaomba kwamba katika kipindi hicho cha mwezi mmoja sote mimi na yeye tujitahidi kuishi maisha ya upendo au kawaida kwa kadiri itakavyowezekana. Sababu yake ilikuwa ndogo lakini muhimu: mwanetu wa kiume alikuwa akikaribia kufanya mtihani katika mwezi uliofuata kwa hiyo hakupenda mtoto aathirike kisaikolojia kwa sababu ya kuachana kwetu. Hili halikuwa tatizo kwangu, nilikubali mpango wake. Lakini alikuwa na sharti la ziada, aliniomba nikumbuke jinsi nilivyombeba siku za fungate yetu hasa siku ya harusi yetu. Akaniomba na kunisihi kwamba katika kipindi hicho cha mwezi mmoja niwe nambeba kutoka kitandani kwetu mpaka mlango wa kutokea kila asubuhi. Nilidhani anakaribia kuwa kichaa. Ili kufanya siku zetu za mwisho zisiwe na migogoro nilikubaliana na masharti yake ya ajabu.

      Kama kawaida kesho yake nilimsimulia Jane kuhusu masharti ya kuachana na mke wangu, kwani kila tulichokuwa tukiongea na mke wangu hata kutoelewana kidogo lazima nikamweleze malkia wangu. Jane alicheka sanaaaa, aliona ni ujinga mtupu. ‘Hata akitumia ujanja wa namna gani talaka ni lazima’, alisema Jane tena kwa dharau kubwa mno. Mimi na mke wangu hatukuwahi kugusana kwa miaka miwili tangu Jane apate kutambua nampenda na kumthamini kuliko mke wangu. Alitumia kila njia hata madawa akawa anapulizia kitandani nikifika kwakwe nakuta kitanda kimerembwa kwa mapambo mbalimbali na nyumba kunikia marashi kumbe ni madawa, Nikijilaza pale naona kama nimefika mbinguni na nikirudi nyumbani ugomvi, hasira na chuki zinaanzia nje ya geiti hadi kufika ndani ni ngumi na mateke tuu yanatawala.

      Mke wangu alikuwa mzuri kuliko Jane, mwaminifu, mwenye upendo na uvumilivu mkubwa. Nilianza kutimiza masharti ya kuachana na mke wangu kwa mbeba; kwa mara ya kwanza sote tulinuniana. Mwanetu alifurahi sana na kupiga makofi nyuma yetu, ‘aah baba kambeba mama mikononi mwake’. Maneno yake yalinichoma moyoni moja kwa moja. Kutoka chumbani kwetu hadi sebuleni, halafu tena mpaka mlangoni, ni zaidi ya mita kumi nimembeba mke wangu. Alifumba macho na kusema kwa sauti laini na ya upole; usimwambie mwanetu juu ya talaka. Nilikubali kwa kichwa, ingawa nilijisikia vibaya. Nilimuweka chini nje ya nyumba.

      Alienda kituoni kusubiri basi la kazini kwake nami nikaendesha gari kwenda kumchukua Jane nimpeleke ofisini kwake. Siku ya pili, zoezi lilikuwa rahisi kwetu sote. Aliegemea kifuani pangu. Nilisikia harufu nzuri ya uturi aliofukiza kwenye blauzi yake. Nikagundua kwamba sijamuangalia kwa makini mke wangu kwa kipindi kirefu sana. Nikagundua hakuwa binti tena. Kulikuwa na mikunjo usoni na nywele zake zilianza kuwa nyeupe! Ndoa yetu imekula urembo wake. Kwa dakika moja nikafikiri kwa nini namfanyia hivi? Nae analia na Mungu kila wakati?

      Siku ya nne nilipombeba hisia za mapenzi kati yetu zilirejea. Huyu ni mwanamke aliyejitoa kuishi nami, kanizalia kijana na tumeishi kwa miaka kumi sasa.

      Siku ya tano na ya sita ilikuwa wazi kwamba mapenzi yetu yalikuwa yakimea upya. Nilijitahidi kutomwambia Jane kuhusu jambo hili. Kadiri mwezi ulivyokaribia kwisha niliona raha kumbeba mke wangu na zoezi likawa rahisi zaidi. Pengine kufanya kazi hii kila siku kuliniimarisha zaidi, na akili yangu ikaanza kufunguka.

      Alikuwa akichagua nini cha kuvaa asubuhi. Alichagua mavazi kadhaa hakupata linalomfaa. Kisha akaguna, ‘nguo zangu zote zimekuwa kubwa’. Nikagundua kwamba mke wangu amepungua sana, nadhani ndiyo maana niliweza kumbeba kirahisi. Ghafla jambo likanichoma moyoni... mke wangu ana uchungu mwingi na maumivu makuu moyoni mwake. Bila kujitambua nikamgusa kichwa chake. Mara mtoto wetu akatokeza na kusema ‘baba ni wakati wa kumbeba mama muende kazini’. Kwake kumuona baba akimbeba mama likawa ni jambo la furaha sana. Mke wangu alimuonyesha ishara mwanetu asogee karibu na akamkumbatia kwa upendo mkuu. Niligeuza uso wangu nisije nikabadili mawazo katika dakika ya mwisho. Kisha nikambeba mikononi mwangu kutoka chumbani, sebuleni halafu mpaka mlangoni. Mkono wake laini ulikuwa umeizunguka shingo yangu kwa upendo wa ajabu. Nilimkumbatia mwili wake; ilikuwa ni mithili ya siku ya ndoa yetu. Lakini wepesi wake ulinitia mashaka na kunikosesha amani sana.

      Siku ya mwisho nilipombeba nilipata shida hata kupiga hatua moja. Mtoto wetu alishakwenda shuleni. Nilimshika kwa karibu na kumwambia sikubaini kwamba maisha yetu yalikosa upendo. Nikaenda zangu ofisini bila kumpitia Jane…. Nikashuka garini hata bila kufunga mlango, Maana nilihisi nikichelewa tu ninaweza kubadili nilichoamua.... nikapanda ngazi. Jane sikumfuata nyumbani kwake nimpeleke kazini ila nilimwona asubuhi na mapema, akifungua mlango nikamwambia, ‘Samahani, Jane, sihitaji tena kumtaliki mke wangu’. Akaniangalia kwa kustaajabu, halafu akagusa kichwa changu. Akaniuliza ‘Unaumwa?’ Nikaondoa mkono wake kichwani kwangu. ‘Samahani, Jane, nimesema sitaki kumtaliki mke wangu. Nadhani ndoa yangu haikuwa na furaha kwa sababu sikuthamini undani wa maisha yetu, mimi na mke wangu, si kwamba hatupendani ila wewe ndio umekuwa sumu ya ndoa yangu. Nimetambua hilo tangu nilipombeba siku ya ndoa yetu nilitakiwa kumbeba siku zote za maisha yetu, nampenda mke wangu sitamuacha mpaka kifo kitakapotutenganisha.’

      Ikawa kama Jane alizinduka usingizini. Akanizaba kibao cha nguvu, akajiegemeza mlangoni na kuanza kulia. Nikashuka ngazi na kuondoka zangu. Nikaingia kwenye duka la maua nikaagiza maua mengi mazuri kwa ajili ya mke wangu. Muuzaji akaniuliza aandike nini kwenye kadi? Nikatabasamu na kuandika “Nitakubeba kila asubuhi mke wangu mpaka kifo kitakapotutenganisha”. Jioni ile nilifika nyumbani na maua mikononi mwangu, tabasamu kubwa usoni nikakimbia mpaka chumbani, nikapokelewa na maiti ya mke wangu kitandani.

      Kumbe mke wangu alikuwa akisumbuliwa na saratani kwa miezi kadhaa nami nilishindwa kubaini kwa sababu nilihamishia akili yangu kwa Jane nikamsahau mke wangu mpendwa pamoja na mwanetu. Alijua kwamba angekufa karibuni na alitaka asiniingize katika chuki na mwanetu kama ningelazimisha talaka mapema.

      Angalau machoni mwa mwanangu, ndugu, jamaa na marafiki naonekana ni mume mwema….

      Jamani vitu vidogo vidogo vizuri ni vya msingi sana katika mahusiano yetu... Siyo majumba au magari au fedha zilizoko kwenye benki. Hivi vitakupa tu mazingira ya kufurahi lakini vyenyewe siyo furaha wala faraja ya moyo wako. Kwa hiyo jitahidi kuwa na muda mzuri na mazingira ya kuwa na mwenzi wako, kuwa rafiki wa mwenzi wako. Fanya vitu mlivyofanya wakati wa uchumba na wa ndoa yenu ambavyo vitawaweka karibu siku zote. Muwe na ndoa yenye furaha. Mara nyingi watu hushindwa katika ndoa kwa kutotambua ni kwa kiasi gani walikuwa karibu wakati wa kujenga uhusiano wao. Yakikufika yaliyonipata utajuta na kutubu sana lakini muda utakuwa umeisha. Maji yakimwagika kuyazoa ni kitendawili!

      Mungu awabariki nyote mliosoma na kujifunza hapa.

      Ni jambo zuri na la kupendeza sana ndugu kuishi pamoja kwa umoja

    2. Miaka 50

    3. #2
      BHULULU's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th June 2012
      Posts : 3,021
      Rep Power : 8382
      Likes Received
      838
      Likes Given
      697

      Default Re: Soma inakuhusu uliye kwenye ndoa

      Ahsante mkuu ujumbe, kazi imebaki kwetu
      bemg likes this.

    4. #3
      happiness win's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 30th August 2011
      Posts : 1,187
      Rep Power : 628
      Likes Received
      442
      Likes Given
      141

      Default Re: Soma inakuhusu uliye kwenye ndoa

      Natamani kila mwenye ndoa na anayetarajia kuipata asome stori yote hiyo maana kuna mengi ya kujifunza hapo. Tatizo ni kwamba shetani mvuruga ndoa atawapa uvivu watu wasisome ili wasijifunze na wazidi kuharibu maisha yao ya ndoa.
      bemg likes this.

    5. #4
      Nivea's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 21st May 2012
      Posts : 5,680
      Rep Power : 0
      Likes Received
      3141
      Likes Given
      4053

      Default Re: Soma inakuhusu uliye kwenye ndoa

      Too late hapa jf
      bemg and Dr. Wansegamila like this.

    6. #5
      cedrickngowi's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 9th June 2012
      Location : Arusha
      Posts : 119
      Rep Power : 373
      Likes Received
      18
      Likes Given
      23

      Default Re: Soma inakuhusu uliye kwenye ndoa

      Ooooh man!so sad.We never know what we have till we lost them.

    7. RukaaJuu Final

    8. #6
      Nsuri's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd October 2011
      Posts : 591
      Rep Power : 504
      Likes Received
      194
      Likes Given
      135

      Default Re: Soma inakuhusu uliye kwenye ndoa

      Ina ujumbe mzuri sana, tatizo binadamu tunasahau mapema na kuishi hapa duniani kama tutaishi milele!!
      bemg likes this.
      " To be happy, we must not be too concerned with others"

    9. #7
      Maliasili's Avatar
      Member Array
      Join Date : 21st October 2010
      Location : Jyvaskyla, Finland
      Posts : 32
      Rep Power : 442
      Likes Received
      13
      Likes Given
      14

      Default Re: Soma inakuhusu uliye kwenye ndoa

      Daaaaaaahhh!
      bemg likes this.
      ‘...Tumefika hapa tulipo kwa sababu ya udhaifu wa Rais Jakaya Kikwete,....., na tumefika hapa tulipo kwa sababu ya upuuzi wa CCM​..'

    10. #8
      Catherine's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 30th June 2012
      Location : Dar
      Posts : 1,241
      Rep Power : 595
      Likes Received
      739
      Likes Given
      208

      Default Re: Soma inakuhusu uliye kwenye ndoa

      Dah! Umeniharibia siku yangu jamani.
      bemg likes this.

    11. HP1
      #9
      HP1's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th February 2012
      Posts : 1,375
      Rep Power : 643
      Likes Received
      262
      Likes Given
      16

      Default Re: Soma inakuhusu uliye kwenye ndoa

      Hadithi nzuri, iweke katika magazeti ya Shigongo, au Mpe Ally Yakuti atengeneze film script
      bemg likes this.
      Use what you get to get what you want

    12. #10
      DALA's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 24th August 2009
      Posts : 149
      Rep Power : 525
      Likes Received
      27
      Likes Given
      22

      Default Re: Soma inakuhusu uliye kwenye ndoa

      Its me in black and white! Thankx for the timely message!
      bemg likes this.

    13. #11
      Risa's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 10th February 2012
      Posts : 158
      Rep Power : 398
      Likes Received
      27
      Likes Given
      92

      Default Re: Soma inakuhusu uliye kwenye ndoa

      Yaani mpaka mchozi umenitoka. Pole sana jamani.
      bemg likes this.

    14. #12
      The Infamous's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th May 2009
      Posts : 653
      Rep Power : 641
      Likes Received
      80
      Likes Given
      112

      Default Re: Soma inakuhusu uliye kwenye ndoa

      duh, ntaiandikia wimbo hii...
      bemg likes this.

    15. #13
      Ruttashobolwa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd February 2012
      Posts : 13,484
      Rep Power : 19785
      Likes Received
      4302
      Likes Given
      1248

      Default Re: Soma inakuhusu uliye kwenye ndoa

      Imerudi tena
      bemg likes this.

    16. #14
      Ruttashobolwa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd February 2012
      Posts : 13,484
      Rep Power : 19785
      Likes Received
      4302
      Likes Given
      1248

      Default

      Quote By Risa
      Yaani mpaka mchozi umenitoka. Pole sana jamani.
      wowowowowow nyamaza mtoto Rissa hoooooooooo
      bemg likes this.

    17. #15
      Risa's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 10th February 2012
      Posts : 158
      Rep Power : 398
      Likes Received
      27
      Likes Given
      92

      Default Re: Soma inakuhusu uliye kwenye ndoa

      Quote By ruttashobolwa
      wowowowowow nyamaza mtoto Rissa hoooooooooo
      haya nimenyamaza Rutta, afadhali umeniumuliza jamani.
      bemg likes this.

    18. #16
      Ruttashobolwa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd February 2012
      Posts : 13,484
      Rep Power : 19785
      Likes Received
      4302
      Likes Given
      1248

      Default

      Quote By Risa
      haya nimenyamaza Rutta, afadhali umeniumuliza jamani.
      unajua ukilia sana siku nyingine ikija ya kusikitisha kama hii unaweza kucheka!
      bemg likes this.

    19. #17
      charminglady's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 16th April 2012
      Posts : 8,863
      Rep Power : 17532
      Likes Received
      4889
      Likes Given
      5322

      Default

      Quote By ruttashobolwa
      Imerudi tena
      umeona eeh,mara nyingne itaandikwa kichina. mie mara ya kwanza kuisoma hii story ilikuwa imeandikwa kwa kiingereza. na tangu hapo nshaisoma km mara tano hapa jf!
      bemg likes this.

    20. #18
      goodmother's Avatar
      Member Array
      Join Date : 21st July 2012
      Posts : 22
      Rep Power : 348
      Likes Received
      13
      Likes Given
      3

      Post

      Quote By bemg
      Inahuzunisha lakini kuna fundisho kuu kwetu sote.

      “Nilipofika nyumbani usiku ule, mke wangu aliponitayarishia chakula, nilimshika mkono na kumwambia, Kuna kitu nataka nikwambie. Mke wangu alikaa chini na kula chakula kimya akiwa tayari kunisikiliza. Tena nikagundua macho yake yalionyesha anaumizwa na kitu moyoni. Nilishindwa hata namna ya kuanza kufumbua kinywa changu. Lakini ilibidi nimwambie ili ajue nilikuwa nikifikiri nini juu yake.

      Nataka kukupa talaka. Nilianza kusema kwa utulivu. Alionekana kutokereka na maneno yangu badala yake aliniuliza kwa sauti ya upole ‘kwa nini?’ Sikumjibu swali lake. Kutojibu kulimfanya akasirike. Akatupa kijiko na akanikaripia, ‘wewe si mwanamume!’ Usiku ule, hakukuwa na maongezi kati yetu. Alikuwa akilia kwa kwikwi. Nilifahamu kwamba alitaka kujua ni nini kimetokea kwenye ndoa yetu. Lakini kwa hakika nisingeweza kumpa jibu wala sababu ya kuridhisha; alionekana si mali kitu kwangu penzi langu lilikwishahamia kwa Jane. Sikumpenda tena mke wangu mawazo yote yalikuwa kwa Jane. Kwa kweli nilimdharau mke wangu, nilimtusi vibaya kwa ajili ya Jane!

      Huku moyo wangu nikijua wazi kwamba nafanya kosa, niliandika talaka ambayo ilionyesha kwamba yeye (mke wangu) angepata nyumba yetu, gari na atakuwa na hisa 30% ya kampuni yetu. Aliangalia talaka ile na kuichana vipande vipande.

      Mke ambaye tumeishi nami kwa miaka 10 alionekana mgeni machoni mwangu. Nilimuonea huruma kwa muda, rasilimali na nguvu alizopoteza lakini sikuweza kurudi nyuma kwa sababu Jane aliuteka moyo wangu kisawasawa. Hatimaye mke wangu alilia kwa uchungu na sauti mbele yangu, jambo ambalo kwa hakika nilitarajia. Kwangu mimi kilio chake kilinipa nafuu na kuongeza kiburi kwamba mimi ni mshindi.

      Wazo la kuachana na mke wangu limenisumbua kwa miaka mitano na sasa limeendelea kuimarika na kuwa jambo la hakika zaidi.

      Siku iliyofuata nilikuja nyumbani kwa kuchelewa sana nikakuta mke wangu akiandika jambo mezani. Sikutamani hata kula chakula alichonipikia nilikwenda moja kwa moja chumbani na usingizi ulinichukua mara moja kwa sababu nilikuwa nimechoka baada ya kula raha za kufa mtu na Jane.

      Usiku nilishtuka usingizini mke wangu alikuwa bado akiandika. Sikujali kabisa nikajifunika vyema shuka na kulala tena. Asubuhi yake alinikabidhi masharti ya talaka yake: hakutaka kitu chochote kutoka kwangu lakini alihitaji apate angalau mwezi mmoja wa kujiandaa kabla hajaachika. Akaomba kwamba katika kipindi hicho cha mwezi mmoja sote mimi na yeye tujitahidi kuishi maisha ya upendo au kawaida kwa kadiri itakavyowezekana. Sababu yake ilikuwa ndogo lakini muhimu: mwanetu wa kiume alikuwa akikaribia kufanya mtihani katika mwezi uliofuata kwa hiyo hakupenda mtoto aathirike kisaikolojia kwa sababu ya kuachana kwetu. Hili halikuwa tatizo kwangu, nilikubali mpango wake. Lakini alikuwa na sharti la ziada, aliniomba nikumbuke jinsi nilivyombeba siku za fungate yetu hasa siku ya harusi yetu. Akaniomba na kunisihi kwamba katika kipindi hicho cha mwezi mmoja niwe nambeba kutoka kitandani kwetu mpaka mlango wa kutokea kila asubuhi. Nilidhani anakaribia kuwa kichaa. Ili kufanya siku zetu za mwisho zisiwe na migogoro nilikubaliana na masharti yake ya ajabu.

      Kama kawaida kesho yake nilimsimulia Jane kuhusu masharti ya kuachana na mke wangu, kwani kila tulichokuwa tukiongea na mke wangu hata kutoelewana kidogo lazima nikamweleze malkia wangu. Jane alicheka sanaaaa, aliona ni ujinga mtupu. ‘Hata akitumia ujanja wa namna gani talaka ni lazima’, alisema Jane tena kwa dharau kubwa mno. Mimi na mke wangu hatukuwahi kugusana kwa miaka miwili tangu Jane apate kutambua nampenda na kumthamini kuliko mke wangu. Alitumia kila njia hata madawa akawa anapulizia kitandani nikifika kwakwe nakuta kitanda kimerembwa kwa mapambo mbalimbali na nyumba kunikia marashi kumbe ni madawa, Nikijilaza pale naona kama nimefika mbinguni na nikirudi nyumbani ugomvi, hasira na chuki zinaanzia nje ya geiti hadi kufika ndani ni ngumi na mateke tuu yanatawala.

      Mke wangu alikuwa mzuri kuliko Jane, mwaminifu, mwenye upendo na uvumilivu mkubwa. Nilianza kutimiza masharti ya kuachana na mke wangu kwa mbeba; kwa mara ya kwanza sote tulinuniana. Mwanetu alifurahi sana na kupiga makofi nyuma yetu, ‘aah baba kambeba mama mikononi mwake’. Maneno yake yalinichoma moyoni moja kwa moja. Kutoka chumbani kwetu hadi sebuleni, halafu tena mpaka mlangoni, ni zaidi ya mita kumi nimembeba mke wangu. Alifumba macho na kusema kwa sauti laini na ya upole; usimwambie mwanetu juu ya talaka. Nilikubali kwa kichwa, ingawa nilijisikia vibaya. Nilimuweka chini nje ya nyumba.

      Alienda kituoni kusubiri basi la kazini kwake nami nikaendesha gari kwenda kumchukua Jane nimpeleke ofisini kwake. Siku ya pili, zoezi lilikuwa rahisi kwetu sote. Aliegemea kifuani pangu. Nilisikia harufu nzuri ya uturi aliofukiza kwenye blauzi yake. Nikagundua kwamba sijamuangalia kwa makini mke wangu kwa kipindi kirefu sana. Nikagundua hakuwa binti tena. Kulikuwa na mikunjo usoni na nywele zake zilianza kuwa nyeupe! Ndoa yetu imekula urembo wake. Kwa dakika moja nikafikiri kwa nini namfanyia hivi? Nae analia na Mungu kila wakati?

      Siku ya nne nilipombeba hisia za mapenzi kati yetu zilirejea. Huyu ni mwanamke aliyejitoa kuishi nami, kanizalia kijana na tumeishi kwa miaka kumi sasa.

      Siku ya tano na ya sita ilikuwa wazi kwamba mapenzi yetu yalikuwa yakimea upya. Nilijitahidi kutomwambia Jane kuhusu jambo hili. Kadiri mwezi ulivyokaribia kwisha niliona raha kumbeba mke wangu na zoezi likawa rahisi zaidi. Pengine kufanya kazi hii kila siku kuliniimarisha zaidi, na akili yangu ikaanza kufunguka.

      Alikuwa akichagua nini cha kuvaa asubuhi. Alichagua mavazi kadhaa hakupata linalomfaa. Kisha akaguna, ‘nguo zangu zote zimekuwa kubwa’. Nikagundua kwamba mke wangu amepungua sana, nadhani ndiyo maana niliweza kumbeba kirahisi. Ghafla jambo likanichoma moyoni... mke wangu ana uchungu mwingi na maumivu makuu moyoni mwake. Bila kujitambua nikamgusa kichwa chake. Mara mtoto wetu akatokeza na kusema ‘baba ni wakati wa kumbeba mama muende kazini’. Kwake kumuona baba akimbeba mama likawa ni jambo la furaha sana. Mke wangu alimuonyesha ishara mwanetu asogee karibu na akamkumbatia kwa upendo mkuu. Niligeuza uso wangu nisije nikabadili mawazo katika dakika ya mwisho. Kisha nikambeba mikononi mwangu kutoka chumbani, sebuleni halafu mpaka mlangoni. Mkono wake laini ulikuwa umeizunguka shingo yangu kwa upendo wa ajabu. Nilimkumbatia mwili wake; ilikuwa ni mithili ya siku ya ndoa yetu. Lakini wepesi wake ulinitia mashaka na kunikosesha amani sana.

      Siku ya mwisho nilipombeba nilipata shida hata kupiga hatua moja. Mtoto wetu alishakwenda shuleni. Nilimshika kwa karibu na kumwambia sikubaini kwamba maisha yetu yalikosa upendo. Nikaenda zangu ofisini bila kumpitia Jane…. Nikashuka garini hata bila kufunga mlango, Maana nilihisi nikichelewa tu ninaweza kubadili nilichoamua.... nikapanda ngazi. Jane sikumfuata nyumbani kwake nimpeleke kazini ila nilimwona asubuhi na mapema, akifungua mlango nikamwambia, ‘Samahani, Jane, sihitaji tena kumtaliki mke wangu’. Akaniangalia kwa kustaajabu, halafu akagusa kichwa changu. Akaniuliza ‘Unaumwa?’ Nikaondoa mkono wake kichwani kwangu. ‘Samahani, Jane, nimesema sitaki kumtaliki mke wangu. Nadhani ndoa yangu haikuwa na furaha kwa sababu sikuthamini undani wa maisha yetu, mimi na mke wangu, si kwamba hatupendani ila wewe ndio umekuwa sumu ya ndoa yangu. Nimetambua hilo tangu nilipombeba siku ya ndoa yetu nilitakiwa kumbeba siku zote za maisha yetu, nampenda mke wangu sitamuacha mpaka kifo kitakapotutenganisha.’

      Ikawa kama Jane alizinduka usingizini. Akanizaba kibao cha nguvu, akajiegemeza mlangoni na kuanza kulia. Nikashuka ngazi na kuondoka zangu. Nikaingia kwenye duka la maua nikaagiza maua mengi mazuri kwa ajili ya mke wangu. Muuzaji akaniuliza aandike nini kwenye kadi? Nikatabasamu na kuandika “Nitakubeba kila asubuhi mke wangu mpaka kifo kitakapotutenganisha”. Jioni ile nilifika nyumbani na maua mikononi mwangu, tabasamu kubwa usoni nikakimbia mpaka chumbani, nikapokelewa na maiti ya mke wangu kitandani.

      Kumbe mke wangu alikuwa akisumbuliwa na saratani kwa miezi kadhaa nami nilishindwa kubaini kwa sababu nilihamishia akili yangu kwa Jane nikamsahau mke wangu mpendwa pamoja na mwanetu. Alijua kwamba angekufa karibuni na alitaka asiniingize katika chuki na mwanetu kama ningelazimisha talaka mapema.

      Angalau machoni mwa mwanangu, ndugu, jamaa na marafiki naonekana ni mume mwema….

      Jamani vitu vidogo vidogo vizuri ni vya msingi sana katika mahusiano yetu... Siyo majumba au magari au fedha zilizoko kwenye benki. Hivi vitakupa tu mazingira ya kufurahi lakini vyenyewe siyo furaha wala faraja ya moyo wako. Kwa hiyo jitahidi kuwa na muda mzuri na mazingira ya kuwa na mwenzi wako, kuwa rafiki wa mwenzi wako. Fanya vitu mlivyofanya wakati wa uchumba na wa ndoa yenu ambavyo vitawaweka karibu siku zote. Muwe na ndoa yenye furaha. Mara nyingi watu hushindwa katika ndoa kwa kutotambua ni kwa kiasi gani walikuwa karibu wakati wa kujenga uhusiano wao. Yakikufika yaliyonipata utajuta na kutubu sana lakini muda utakuwa umeisha. Maji yakimwagika kuyazoa ni kitendawili!

      Mungu awabariki nyote mliosoma na kujifunza hapa.
      ki ukweli machozi yamenitoka. funzo zuri kweli.
      bemg likes this.

    21. #19
      Kaunga's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th November 2010
      Location : Wild wild west
      Posts : 8,438
      Rep Power : 13324
      Likes Received
      7667
      Likes Given
      6911

      Default

      Quote By charminglady
      umeona eeh,mara nyingne itaandikwa kichina. mie mara ya kwanza kuisoma hii story ilikuwa imeandikwa kwa kiingereza. na tangu hapo nshaisoma km mara tano hapa jf!
      Lkn kila unapoisoma inauma eeh!

    22. #20
      bemg's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th April 2010
      Posts : 1,614
      Rep Power : 783
      Likes Received
      218
      Likes Given
      350

      Default Re: Soma inakuhusu uliye kwenye ndoa

      Quote By cedrickngowi
      Ooooh man!so sad.We never know what we have till we lost them.
      man you should know its powerful to make your marriage strong with full happiness
      Ni jambo zuri na la kupendeza sana ndugu kuishi pamoja kwa umoja

    Page 1 of 2 12 LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...