Katika kile kinachoonekana kupunguza kasi ya CDM na kiongozi wake machachari Dr Wilbroad Slaa Mbunge wa viti Maalum wa chama hicho Rose Kamili amekwenda mahakamani kumshtaki Katibu mkuu wake Dr Wilbroad Slaa kwa kile anachopinga uhusiano wa Dr Slaa na mke wake mtarajiwa Josephine Mushumbusi.
Katika hati ya mashtaka aliyo nayo Rose analalamikia kutelekezwa yeye na watoto wake wawili baada ya Josephine kuingilia ndoa yao.Anaiomba mahakama itamke uhusiano wa Dr Slaa na Josephine ni batili.
Kuna tetesi zimezagaa Rose Kamili amenunuliwa ili kuvuruga mijakati ya CDM kuiandama serikali ya CCM
Source:Tanzania Daima
Updates from Mwananchi...Majibu ya Dr Slaa
Dk Slaa: Nimeyazoea
Alipotakiwa kuzungumzia kesi hiyo nje ya Mahakama, Dk Slaa alisema: “Hayo mambo nimeyazoea na kimsingi hayanipi shida yoyote.”
Alipoulizwa endapo anajipanga vipi kulipa fidia hiyo alijibu: “Kesi ni kesi hivyo siyo kila kinachoombwa kwenye kesi lazima kilipwe.”
Hata hivyo, Dk Slaa alisema asingependa kuzungumzia suala hilo kwa undani kwa kuwa liko kwa mawakili wake lakini akasema amebaini kuwa hizo ni hila na michezo michafu ya kisiasa.
“Kwanza siyo pingamizi moja tu, kuna pingamizi mbili mahakamani lakini kwa ufupi ifahamike kuwa hizo ni hila.”

Reply With Quote


Follow Us Here