Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Nilipovunja ungo!

    Report Post
    Page 1 of 2 12 LastLast
    Results 1 to 20 of 27
    1. #1
      vukani's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 30th December 2009
      Location : Dar and Arusha
      Posts : 241
      Rep Power : 1417
      Likes Received
      132
      Likes Given
      178

      Default Nilipovunja ungo!

      Ilikuwa ni mwaka 1998 na ninaukumbuka vizuri sana huo mwaka, kwani ndio mwaka niliovunja ungo, ni kipindi hicho ambapo nilianza kushangaa maumbile yangu jinsi yalivyobadilika na nilikuwa nahisi kuwa na mamlaka makubwa sana, sikutaka kuchuliwa kama mtoto tena ingawa nikuwa bado ni mtoto, kwa umbo na umri.
      Nilikuwa nagombana na mama pamoja na dada zangu mara kwa mara pale nyumbani na sikusikia la mtu. Nilikuwa ni mbishi na mkorofi kwa kila mtu pale nyumbani, lakini mama yangu alikuwa ainichukulia kwa tahadhari sana, daima alizoea kusema kuwa hayo ni mapito tu. Kipindi hicho sikumuelewa juu ya kauli ile, lakini sasa nimemuelewa, tena vizuri sana.

      Siku moja wakati naenda shule nilikutana na kijana mmoja mzuri na mtanashati hivi na kama bahati nzuri wote tulikuwa tunaelekea kituoni, kupanda basi, nilijikuta nikivutiwa na yeye na nilitamani sana kumsemesha lakini nilikuwa nawaonea aibu sana wanaume nikabaki nikimuangalia kwa jicho la kumuiba. Tulipofika kituoni nilijikuta kila saa nikimtazama, na kila akigeukia upande niliposimama na kugongana macho na mimi nilikuwa naangalia pembeni kwa aibu.

      Nilitamani sana kumsemesha lakini sikuweza kufanya hivyo kutokana na aibu na pia nilikuwa nawaogopa wanaume. Nakumbuka wakati nilipokuwa mdogo, nilikuwa namsikia mama yangu akizungumza na dada zangu na kuwaeleza juu ya athari za kujenga mahusiano na wanaume katika umri mdogo, sikuwa nayasikiliza yale mazumgumzo kwa kuwa nilijua hayanihusu, jambo lingine ni juu ya tabia yangu sikuwa nawapenda sana wanaume na nilikuwa sina kawaida ya kuwazoea wavulana hata wale niliokuwa nikisoma nao.

      Lakini tangu nimuone huyu kaka kwa jicho la kwanza, nilijikuta nikivutiwa naye ingawa sikujua kuwa navutiwa naye ili iweje, ila nilitamani sana kuwa naye karibu. Nikiwa katika lindi la mawazo huku nikiwa katika dunia ya peke yangu basi lilifika na yule kijana alipanda na kuondoka na kuniacha pale kituoni nikiwa nimeshikwa na butwaa huku nikijilaumu kwa kutomsemesha wala kumuuliza jina lake.

      Sikuchukua muda nami nikapata basi na kupanda na kuelekea shuleni. Nilipofika shuleni ile sura ya yule kijana ilikuwa ikinijia mara kwa mara, na siku hiyo masomo hayakupanda kabisa mpaka mwalimu wangu mmoja akaniuliza kama nilikuwa naumwa, nikikataa kwa kumjibu kuwa siumwi, lakini nadhani aliona kuwa sikuwa katika hali ya kawaida siku hiyo. Niliporudi jioni nilikutana na kaka mmoja jirani yetu, ambaye nilikuwa nasoma na mdogo wake shule moja lakini madarasa tofauti, alinisimaisha na kuniuliza kama nimemuacha wapi mdogo wake, nilimjibu kwa kifupi kuwa nilimuacha kituoni, mara ghafla yule kijana akaja pale tulipo na kunisalimia kwa kunishika mkono, nilijikuta nikitetemeka na mapigo ya moyo wangu yakienda mbio, nilimjibu huku nikiangalia pembeni kwa aibu sikutaka kukutanisha macho na yeye, nadhani hata yeye alihisi jambo kwani aliniachia mkono wangu.

      Yule kijana tunayeishi naye jirani alinitambulisha kwa yule kijana kuwa ni mjomba wake na yuko pale kwa muda akisubiri kujiunga na masomo ya kidato cha tano, ambapo alikuwa amepangiwa kwenda kusoma Tabora Boys. Kuanzia siku hiyo nilikuwa siishi kwenda kwa akina yule binti tuliyekuwa tunasoma naye lengo lilikuwa ni kutaka kumuona huyu kijana, ingawa sikuweza kuzungumza naye kutokana na kuwa muda mwingi alikuwa bize sana akijisomea.

      Siku moja kama kawaida yangu nilikwenda pale nyumbani kwa rafiki yangu lengo langu kama kwaida lilikuwa ni kataka kumuona yule kijana na siku hiyo nilipania sana nizungumze naye, na kweli siku ile ilikuwa ni kama bahati kwangu nilimkuta yuko peke yake pale nyumbani na mtumishi wao wa pale nyumbani. Alianzisha mazungumzo na swali lake la kwanza alitaka kujua kuwa kama nimeokoka, nilimjibu kuwa sijaokoka, nilimrudishia swali lile kwa kumuuliza kama na yeye ameokoka. Jibu lake lilipenya moyoni mwangu kama mkuki moyoni. Alinijibu kwa upole kuwa ameokoka tangu akiwa darasa la tano, kutokana na kumtegemea yesu na ndio maana amekuwa akifaulu tangu darasa la saba mpaka sasa anatarajia kujiunga na kidato cha tano.

      Jibu lake halikunifurahisha hata kidogo, lakini sikujua sababu ni nini?
      Alitumia fursa ile kunishawishi niokoke na kumkubali yesu kuwa mwokozo wangu, nilimkatalia katukatu kuwa sikuwa tayari kuokoka, alinipa mifano mingi katika biblia, lakini hakuna hata moja lililoniingia katika mazungumzo yake bali nilikuwa najisikia furaha kwa jinsi alivyokuwa akizungumza kwa upole kama ananibembeleza, mawimbi ya sauti yake yalikuwa yakipenya katika masikio yangu kama vile aina fulani ya muziki mororo.

      Nilikuwa natamani aendelee kuongea tena na tena. Lakini mara ghafla wenyeji walirudi na sikuwa na budi kuaga na kuondoka. Nilianza kuzoeana na yule kijana lakini mazungumzo yake ya kunishawisi niokoke sikuyapenda, hata hivyo ilibidi nikubali kuambatana naye kanisani anaposali ilimradi niwe naye karibu, kule nyumbani nilikuwa naaga kuwa nakwenda kwa rafiki yangu kujisomea.

      Pale kanisani alinitambulisha kama mgeni wake ambaye amekubali kumpokea yesu kristo, nilishangiliwa sana na kupongezwa kwa uamuzi wangu ule, ingawa dhamira yangu ya kuwepo mahali pale haikuwa ni kwa ajili ya wokovu kama ilivyosemwa bali ilikuwa ni mapenzi niliyokuwa nayo kwa huyu kijana. Nilianza kujenga wivu, kila nikimuona anaongea na msichana mwingine pale kanisani kwao, roho ilikuwa inaniuma sana.

      Siku moja wakati tunatoka kanisani alikuwa akinisindikiza kurudi nyumbani, mara tukakutana na kaka yangu mkubwa akaniuliza natoka wapi na yule niliyefuatana naye ni nani, nilimjibu kwa kiburi na jeuri kuwa haimuhusu, basi kaka alimfokea sana yule kijana kuwa anataka kuniharibia maisha na kumtishia kuwa atampiga. Yule kijana kwa uungwana aliondoka zake bila kusema chochote na kurudi kwao. Niliumia sana na niliporudi nyumbani nilijifungia chumbani kwangu na kulia sana.

      Mama alikuja chumbani kwangu na kuniuliza sababu ya kulia, nilimueleza kila kitu, mama hakusema kitu aliondoka zake, lakini kaka alikuja huku nyuma na kunifokea sana.
      Kesho yake nilisikia alikwenda pale alipofikia yule kijana na kumfokea sana yule kijana na kutoa onyo kuwa akimkuta na mimi atamfunga aozee jela. Ukweli ni kwamba kaka yangu huyu mkubwa alikuwa ni mkorofi sana, na alikuwa haelewani hata na dada zangu kwa kuwaingilia katika mambo yao wakati walipokuwa wanasoma.

      Nilipopata taarifa juu ya yule kijana kufuatwa na kufokewa na kaka, iliniuma sana na niliamua kuchukuwa uamuzi hatari wa kutaka kujiua kwa kuhisi kudhalilishwa pale mtaani, nilikunywa idadi kubwa ya vidonge ambavyo hata sikujua kama vilikuwa ni vidonge gani na kujifungia chumbani kwangu, baadae nilianza kujiskia vibaya na hivyo nikaanza kuugulia, dada yangu alinisikia na alipoingia chumbani kwangu na kunikuta katka hali ile, nilimsikia akimuita mama kwa sauti kubwa “mama mwanao anakufa” nilipoteza fahamu na niliposituka nilijikuta nikiwa hospitalini nikiwa nimetundikiwa Dripu.

      Siku iliyofuata niliruhusiwa na kurudi nyumbani, mama yangu alichukuwa nafasi ile ya kuwepo kwangu nyumbani kwa mapumziko ya kuumwa kunipa darasa juu ya mabadiliko ya kimwili baada ya kuvunja ungo na hisia za kimapenzi, mama alikuwa wazi kwangu kwa kunieleza kila kitu juu ya mapenzi ya utotoni na athari zake na jinsi ya kuepuka vishawishi na namna ya kukabiliana na changamoto za usichana, na kikubwa zaidi aliniasa sana juu ya kuwaepuka wavulana wakware.

      Naomba nikiri kuwa kwa swala langu yule kijana hakuwa na makosa na kamwe hakuwahi kunitamkia jambo lolole linalohusu na mapenzi wala kuonesha dalili za kunitamani licha ya kujipendekeza sana kwake, bali mimi ndiye niliyekuwa na kiherehere.

      Baadae nilipata taarifa kuwa yule kijana aliamua kurudi kwao ili kuepusha shari. Ilinichukuwa takribani mwaka mzima yule kijana kufutika katika mawazo yangu kabisa, kwani pamoja na semina ya mama lakini nilikuwa najikuta tu natamani nikutane naye barabarani, jambo ambalo halikutokea na wala halitakuja kutokea.

      Miaka miwili baadae nilipata habari ya kusikitisha, na ambayo iliniacha na majonzi hadi leo, yule kijana alifariki kwa ajali wakati akirudi nyumbani kwao baada ya kumaliza mitihani ya kidato cha sita. Ingawa nilishamsahau kutokana na kujitambua lakini habari za kifo cha yule kijana kilinisitua sana na kunikumbusha machungu ya siku ile niliyotaka kujimaliza kwa ajili yake. Najua ilikuwa ni utoto, lakini kwangu mimi lile lilikuwa ni darasa tosha.
      Labda niwaulize wana JF, hivi ni wazazi wangapi ambao wako wazi kwa mabinti zao kwa kuwaeleza ukweli juu ya mabadiliko ya miili yao pindi wanapovunja ungo?
      Je ni wazazi wangapi ambao wako tayari kuwakabili mabinti zao na kuwaambia ukweli huu bila kuogopa mila na desturi ambazo nyingi zimepitwa na wakati?

      Jamani umri wa kuvunja ungo una misukosuko na vitimbi vingi……….


      Ngekewa, Laigwanan76 and Kongosho like this.
      "What I need from you is LOVE"

    2. Miaka 50

    3. #2
      HEART's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th November 2011
      Location : kijitonyama
      Posts : 1,202
      Rep Power : 2732
      Likes Received
      462
      Likes Given
      128

      Default Re: Nilipovunja ungo!

      daah...si mchezo..
      The Boss likes this.

    4. #3
      kichwat's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th March 2010
      Posts : 1,043
      Rep Power : 691
      Likes Received
      215
      Likes Given
      24

      Default Re: Nilipovunja ungo!

      superb presentation.
      Tatizo letu kubwa ni utamaduni wa Kiafrika, hauna demokrasia ndani ya familia, ni kisultani zaidi. Na nafasi ya mwanamke ni duni. Lakini tumo kwa transition.

    5. #4
      The Boss's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 18th August 2009
      Location : DARESALAAM
      Posts : 18,144
      Rep Power : 21611
      Likes Received
      13481
      Likes Given
      17780

      Default Re: Nilipovunja ungo!

      aiseee
      sijui wangapi waliniwaza mwaka mzima enzi hizo za foolish age ?lol
      charminglady likes this.
      Watch your thoughts,They become words, Watch your words, They become deeds, Watch your deeds, They become habits, Watch your habits, They become character, Watch your character, It becomes your destiny!

    6. #5
      dfreym's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th October 2010
      Posts : 279
      Rep Power : 593
      Likes Received
      49
      Likes Given
      164

      Default Re: Nilipovunja ungo!

      dah........ barua ndefu kama hiiiii........ ngoja nitarudi kuisoma, hebu niangalie kwanza habari za upepo
      If money doesn’t grow on trees then why banks have branches?

    7. FemaTV & Radio

    8. #6
      telitaibi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd May 2012
      Posts : 459
      Rep Power : 446
      Likes Received
      83
      Likes Given
      79

      Default Re: Nilipovunja ungo!

      naona umejiachia kweli nitasoma wakati mwingine imenipa uvivu kitabu chote nipe jina la kitabu hiki

    9. #7
      Amour Nyaluc's Avatar
      Junior Member Array
      Join Date : 28th June 2012
      Posts : 2
      Rep Power : 0
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Default Re: Nilipovunja ungo!

      dah stor iko poa sana!
      foolish age ni kipindi che vitimbi vingi sana...

    10. #8
      King'asti's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th November 2009
      Location : The Jungle
      Posts : 17,130
      Rep Power : 28891
      Likes Received
      11625
      Likes Given
      4793

      Default

      Lol! Hivi uki-google huwezi pata jibu ama server imelemewa?

      Mnakumbuka love calculator? Unaandika majina yenu, unakata common sylabi, afu namba unaenda kusoma jibu. Unakuta yoote majibu ni positive ila hata hatukustukia! Kha!
      Quote By The Boss
      aiseee
      sijui wangapi waliniwaza mwaka mzima enzi hizo za foolish age ?lol
      The Boss and Kongosho like this.

    11. #9
      Ngekewa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 8th July 2008
      Posts : 4,483
      Rep Power : 1450
      Likes Received
      388
      Likes Given
      181

      Default Re: Nilipovunja ungo!

      Quote By kichwat
      superb presentation.
      Tatizo letu kubwa ni utamaduni wa Kiafrika, hauna demokrasia ndani ya familia, ni kisultani zaidi. Na nafasi ya mwanamke ni duni. Lakini tumo kwa transition.
      Hivyo unahisi pana kosa hapo? Unafikiri hata hao wazungu kwanini wameweka umri fulani wa kuruhusu mahusiano ya kimwili? Unasema tuko kwenye Transition kuelekea wapi ambapo bado hatujafika? Hii hadithi si kitu chengine bali ni majuto ya huyo alieitowa kwa kuona jinsi jamii ilivyoondoka kule kuzuri ilikokuwa.

    12. #10
      Ngekewa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 8th July 2008
      Posts : 4,483
      Rep Power : 1450
      Likes Received
      388
      Likes Given
      181

      Default Re: Nilipovunja ungo!

      Quote By The Boss
      aiseee
      sijui wangapi waliniwaza mwaka mzima enzi hizo za foolish age ?lol
      Hukuwepo wewe wakati ule wa raha, unaouita foolish age.

    13. #11
      BADILI TABIA's Avatar
      JF Bronze Member Array
      Join Date : 13th June 2011
      Location : DUNIANI
      Posts : 14,555
      Rep Power : 5614
      Likes Received
      6211
      Likes Given
      2281

      Default Re: Nilipovunja ungo!

      duh. . . . . . . . !

    14. #12
      watu8's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 19th February 2010
      Location : Juu ya Tukutuku
      Posts : 15,042
      Rep Power : 31281
      Likes Received
      7453
      Likes Given
      7465

      Default Re: Nilipovunja ungo!

      wadada wengi huwa na mshawasha sana hasa kuanzia darasa la 5 hadi la 7...
      nakumbuka kipindi twasoma watoto wa kiume wale waliokuwa na akili sana au wenye vipaji mbalimbali, walikua wakila sana mashavu ya kununuliwa sijui ubuyu, ice cream n.k....
      bila shaka kuvunja ungo kwa wadada, ni wakati vichocheo hushika hatamu kuliko wakati wowote.
      "Ingawa tunatumia AVATARS na USERNAMES ambazo ni FAKE, bado haibadilishi uhalisia wa MIOYO YETU"



    15. #13
      ndyoko's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd November 2010
      Posts : 4,505
      Rep Power : 1705
      Likes Received
      1199
      Likes Given
      1916

      Default Re: Nilipovunja ungo!

      Kuishi na mtoto wa kike ni mtihani mwingine sawa na ule wa kuishi na mke!!!!!!!!! Teteteeeeeeee!
      Kongosho likes this.
      “If you can not get what you love, then love what you have”

    16. #14
      ney kush's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 16th February 2012
      Posts : 597
      Rep Power : 485
      Likes Received
      97
      Likes Given
      31

      Default Re: Nilipovunja ungo!

      duh! kweli umepita mapito mazuri

    17. #15
      The Infamous's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th May 2009
      Posts : 653
      Rep Power : 641
      Likes Received
      80
      Likes Given
      112

      Default Re: Nilipovunja ungo!

      changamoto za ujana...nilikoswa na mshale na baba mwenye nyuma aliponikuta na mtoto wake...never forget aisee ujana huu

    18. #16
      Kongosho's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st March 2011
      Location : Location loading...
      Posts : 25,141
      Rep Power : 13061
      Likes Received
      14087
      Likes Given
      14889

      Default Re: Nilipovunja ungo!

      On point.

      Ila nafasi ya mama yaweza punguza maruhani wengi

      Quote By ndyoko
      Kuishi na mtoto wa kike ni mtihani mwingine sawa na ule wa kuishi na mke!!!!!!!!! Teteteeeeeeee!
      No matter how hot your anger is, it can not cook yams-Nigeria

    19. #17
      Mwenyeminazi's Avatar
      Member Array
      Join Date : 24th May 2012
      Location : JAMBIANI- ZANZIBAR
      Posts : 59
      Rep Power : 363
      Likes Received
      15
      Likes Given
      23

      Default Re: Nilipovunja ungo!

      Eeeeh nimesoma na nimekuelewa saaana. kweli umri huo huwa na mambo yake. Naomba utupe PART 2 YA STORY YAKO IKIHUSU UTOKAJI WA BIKIRA na wenyewe ulikuaje? Tiririkaa mama mkubwa!!!

    20. #18
      Nabii suleiman's Avatar
      Member Array
      Join Date : 17th January 2012
      Posts : 93
      Rep Power : 388
      Likes Received
      22
      Likes Given
      9

      Default Re: Nilipovunja ungo!

      nakuunga mkono ndugu yangu Mwenyeminazi amalizie part 2 chaap..

    21. #19
      PetCash's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th March 2012
      Location : searching....
      Posts : 640
      Rep Power : 557
      Likes Received
      351
      Likes Given
      104

      Default Re: Nilipovunja ungo!

      Something to take note of
      You are what you eat

    22. #20
      felinda's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 23rd June 2012
      Location : mwanza
      Posts : 272
      Rep Power : 402
      Likes Received
      55
      Likes Given
      45

      Default Re: Nilipovunja ungo!

      ni wazazi wachache sana wanaoweza kukaa chn na mabinti zao na kuwaelezea kuhusu mabadiliko ya mwili.,we unabahati sana ya kupata mzazi wa kukueleza kila ki2 lkn kutokana na kipind hcho cha mpito mabinti hwa na dharau na kujifanya wanajua kila ki2 na ndio chanzo cha wao kushndwa kumaliza shule.

    Page 1 of 2 12 LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...